Riwaya; taaluma iliyopotea

Riwaya; taaluma iliyopotea

ni fupi sana ila ni tamuu, lini mwendekezo
 
RIWAYA: TAALUMA ILIYOPOTEA
MTUNZI: FRANK MUSHI
SEHEMU YA TANO
“Maisha ni kama Shamba, wapo ambao wazazi wao walifanikiwa
kununua shamba hili na wao kwa juhudi wazijuazo wao walifanikiwa
kung’oa visiki, kulima, kupanda mbegu na kupalilia na kisha sasa
mazao yanamea na wao wananyweshea,,watoto au vijana wenye
wazazi wa namna hii huwa hawana kazi sana,wao huwapokea wazazi
wao mpira wa maji na kuanza kumwagilia. Wapo wale ambao wazazi
wao walifanikiwa kununua shamba lakini walishindwa kulihudumia na
sasa wao ndio huenda kuanza upya, kazi yao huwa ngumu sana kwani
hutakiwa kuanza mwanzo, hawa ni wale waliobahatika tu kupata elimu
lakini kwao hakuna uwezo. Ewe ambaye kwenu mmefanikiwa
usikatishe ndoto ya mwenzio kwa uwezo wa mzazi wako,,,USITUMIE
PESA KAMA FIMBO YA KUMCHAPIA MWENZIO” HII NI SEHEMU YA
TANO….ANDIKA HIVI
**BEATRICE ANASIMULIA**
“hapana mimi si muhalifu niacheni jamani” Frank alizidi kujitetea
wakati wale maaskari wakizidi kumkunja pale chini , sikujali hilo
kwakuwa bado sikutaka kumuona duniani.
“ni muongo huyo mkamateni na mumtoe ili abiria wengine waendelee
na safari yao” niliendelea kuwasihi wale maaskari ili wamkamate Frank
na walifanikiwa kumchukua pale kisha tulishuka kwenye ile ndege na
muda mfupi mbele ndege iliondoka, Frank alikuwa bado pale chini
akilia lakini sikuwa na huruma naye;
“Beatrice nipe muda nikuelezee ukweli wa kila kitu tafadhali, ni bado
mapema sasa wewe kuujua ukweli, mimi si kama unavyodhani, mimi
si muhalifu, historia ya maisha yang undo iliyonileta hapa nilipo”
aliendelea kuongea na mimi lakini sikutaka kusikia tena uongo wake,
nilichukua simu yangu na kumpigia baba yangu nikamtaarifu kuwa
tayari nilikuwa niko na Frank pale na juhudi zake za kutoroka zilikuwa
zimegonga mwamba. Nilimtazama Frank usoni alionekana kuchoka
sana lakini swali kubwa kichwani ni alikuwa anatoroka kwenda wapi.
“Beatrice” aliniita na mimi nilimsogelea mpaka pale alipokuwa huku
nikimtazama kwa uso uliojaa chuki, sikumpenda tena Frank hasa
baada ya kugundua kuwa hata jina lake alinificha toka mwanzo, nikiri
leo kuwa ingawaje Frank alikuwa ni mfanyakazi wa ndani nyumbani
kwetu ambaye kiuhalisia alikuwa hana hata hadhi ya kuwa rafiki yangu
wa karibu lakini nilianza kuwa na hisia nae na niliuahidi moyo wangu
kuwa ningembadilisha na kumfanya mwanaume mwenye mwonekano
wa hadhi yangu, alikuwa ni kijana mzuri sema shida pengine ndo
ziliukumbatia uzuri na utanashati wake na kumuachia muonekano wa
kizee wenye kutoa taswira halisi ya kazi yake na muonekano wake,
nilianza kumpenda Frank kwa jinsi alivyonifariji na kunifanya nisahau
machungu niliyopewa na mchumba wangu, ni Frank ndiye aliyekuwa
na mimi mda wote na kunifanya nione kila kitu kama ni kawaida, mara
zote aliponiambia kuwa nisilie sana pengine mungu amenipangia mtu
mwema ajaye atakaye nijali na kunifariji siku zote za maisha yangu
basi moyoni nilikuwa nasema natamani angekuwa yeye. Ni
mwanaume ambaye kwa kumsikiliza anayoyaongea na jinsi
anavyopangilia yale atakayo kusema au jinsi anavyochambua mambo
yake utajua kabisa ni kichwa.
“Beatrice” aliita tena na sasa nilimuitikia.
“unasemaje” nilimuitikia na wakati wote huu bado alikuwa pale chini
ya ulinzi mkali wa polisi wa pale uwanja wa ndege.
“kwanini unanifanyia hivi?” aliuliza na sikutaka kumjibu, nilijua
nikimsikiliza nitamuonea huruma, niliamua kuondoka lakini nikiwa
kama hatua kumi mbele nilimsikia tena akinisemesha nikasimama.
“hukusoma barua niliyokutumia??” aliniuliza kwa sauti ya upole,
kiukweli sikuwahi kuona barua yake na sikuwa na la kumjibu
niliendelea kuondoka kuelekea upande wa pili wa pale uwanjani ili
kuchukua gari langu.
“ile barua ilikuwa inaeleza kila kitu,,kaisome ili ujiepushe na dhambi hii
unayoifanya kwasasa, kasome ile barua tafadhali,,nenda kaisome
usiipuuzie” alizidi kupaza sauti huku akilia, niliendelea kutembea huku
nikijiuliza barua gani anayoongelea lakini sikujali kitu nilikwenda
mpaka nilipopaki gari yangu na wakati nageuza gari niliona baba
yangu akiingia pale na Cadillac nyeusi na niliweza kuitambua na
kumuwashia taa kisha alinifata nyuma na wote tulielekea mpaka kule
Frank alipokuwepo.
Vijana wanne walimshika na kumuingiza ndani ya gari kisha tuliwapa
wale askari dola 1400 kila mmoja na walikaa kimya kisha tuliondoka
pale uwanjani. Tulitembea kwa mwendo wa dakika kumi kisha
tulikamata njia ya Lalana Dok na kuelekea Victoria Planete iliyopo
upande wa kusini mwa pale uwanja wa ndege,,kama mwendo wa
dakika 20 tulishuka na sasa tuliingia kwenye gari nyingine nyeusi aina
ya hiace na sasa tulizidi kutokomea ambapo hata mimi sikupajua,
kilomita moja mbele tulipita Vision Valley School na kuingia njia ya
vumbi kisha tulikwenda mpaka hospitali ya Lutherani ya Ambohibao
na hapo tulisimama kisha mzee alishuka na kuingia kule hospitali na
baada ya dakika tano nilimoana akitoka nje na mzungu mmoja
aliyekuwa amebeba begi, walisogea mpaka tulipokuwa na kuingia
kwenye gari kisha tulianza tena safari , usiku ulikuwa umeshaingia na
kama nusu saa niliona bango kubwa lililokuwa limeandikwa Futura
Park nikagundua tulikuwa Andranomena, tulifika pale getini
tukafunguliwa na kuingia ndani ya mbuga, hofu ilianza kunijia na mimi
juu ya kilichokuwa kinaenda kutokea, tulienda mpaka tukatokomea
kwenye pori na huko tulikuta nyumba yenye geti kubwa na
tulifunguliwa.
Tulipofika ndani Frank alitolewa kwenye gari na kupelekwa mpaka pale
sebuleni kisha mimi niliambiwa nitoke nje, nilitoka nje na kuchungulia
kwa pale dirishani, wakati huo Frank alikuwa ameshakaukiwa sauti,
walimvua nguo zote na kumfunga kamba kisha walimning’iniza juu,
nikiwa pale bado nikiendelea kuchungulia kilichokuwa kikiendelea
niliona yule mzungu akimfata huku ameshikilia dawa ya kupuliza aina
ya GV na wembe mdogo unaotumika mahospitalini kwenye upasuaji;
“unamjuaje Mzee Ripson Odiego” aliulizwa swali la kwanza, na kwa
mbali nilimsikia akijibu kuwa hamfahamu, baada ya kujibu vile wembe
ule ulipitishwa kifuani kwake na kunifanya nisikie kutapika, damu
zilianza kumtoka na kelele zilizidi pale walipompulizia ile dawa,
nilianza kumuonea huruma na kuzidi kulia kichinichini nilikiwa pale nje,
nilitoka mpaka mbele kidogo palipokuwa na bomba la maji nikaketi
chini na kufungua maji kisha nilinawa uso wangu, sikujua kwanini
nilimuonea Frank huruma wakati mimi ndiye niliyeenda kumkamata
kule uwanja wa ndege baada ya kupewa taarifa na rafiki yangu kuwa
amemwona mfanyakazi wetu pale uwanja wa ndege.
Baada ya kupumzika kwa dakika tatu nilirudi tena kuchungulia pale,
nikaona tena wakimsogelea huku yule mzungu akiwa amevaa ‘gloves’
mikononi.
“Ulitumwa kufanya nini nyumbani kwa huyu mzee” aliulizwa.
“nilikuja kutafuta kazi pale,, mimi ni mtanzania nilikimbia nchini
kwangu baada ya….” Kabla hajamaliza kusema chochote alipitishiwa
wembe tena na kupuliziwa ile dawa, nilizidi kulia kila alipolia lakini
nilichohitaji ni ukweli tu auseme ambao hata hivyo hakuwa tayari
kusema kabisa, kila mara alisisitiza kuwa yeye ni mtu mwema lakini
hakuna aliyemsikiliza, baada ya kuulizwa kwa muda mrefu bila kujibu,
yule jamaa alichukua kisu na kumuuliza swali tena kuwa ni taarifa
gani alizifata nyumbani kwetu lakini alizidi kujitetea na kuomba apewe
muda wa kujieleza,,hiyo haikumpendeza yule mtesaji na kumfanya
amchome kisu kwenye paja, kisha alianza kumuuliza maswali huku
akimkata kama vile alikuwa anakata mkate,,Frank alilia na mimi
uvumilivu wa kuangalia akiteseka ulikuwa umekaribia kufika mwisho,
zoezi hili halikufanikiwa kwani Frank aliendelea kusema kuwa yeye sio
huyo wanaomtafuta, yule jamaa alirudi nyuma na kuangalia tena kisu
kingine kidogo na aliporudi alimuuliza tena swali lilelile lakini majibu
yalibaki kuwa yaleyale na hapo alishika uume wa Frank ka kutaka
kuukata nilipiga kelele pale nje na kufungua ule mlango kwa haraka
kisha niliingia ndani;
“Inatosha, angekuwa ni mtu mbaya angesema ukweli baada ya
mateso yote haya, muacheni jamani” niliongea huku nikizidi kulia,
nilimfata baba yangu na kumpigia magoti wamuache kwakuwa
pengine asemayo Frank ni kweli. Walimshusha na kumvalisha zile
nguo, Frank bado alikuwa pale chini akilia na hali yake ilikuwa mbaya
sana kwakuwa alikuwa akitetemeka, nilisikia tena kwa mbali akiniita
na mimi nilimfata pale;
“unasemaje Frank, unasemaje mpenzi” nilijikuta nikianza kumuita
mpenzi na sikujua ilikuwaje lakini kwa hayo machache nilianza
kumuamini.
“nenda kasome ile barua” aliniambia kwa sauti ya chini sana.
“barua gani?” nilizidi kumuuliza huku nikilia, sikujua ni barua gani
anayoizungumzia.
“barua uliyoletewa na yule binti wiki chache zilizopita, nenda kasome”
bado maneno yake yalinichanganya na sikujua anazungumzia nini.
****
Tulikuwa tumeshakubaliana kumpeleka Frank hospitali ili akatibiwe
majeraha yote yaliyokuwa yamempata, yule mzungu alikusanya vitu
vyake na kwenda kuviweka kwenye gari, kisha alirudi pale ndani,
nilisikia akimwambia kijana wake asafishe lakini kabla sijaelewa
maneno yale yalimaanisha nini, baba alinifata pale na kuniambia;
“mwanangu wema huzaa dhambi, ukimpiga nyoka ukamkosa basi
huwa na hasira sana, na akirudi huwa hatari kuliko mwanzo na
hazuiliki” alinisemesha huku akiniangalia usoni
“unamaana gari” nilimuuliza lakini alinigeuza uso kule alikokuwa
Frank.
“Muage” aliniambia maneno hayo na hapo niliona yule kijana akikoki
bastola yake na kuachia risasi iliyopenya kwenye kichwa chake.
“Nooooooo” nilipaza sauti hapo NILISHTUKA. Niliangalia huku na
huku sikuona mtu yoyote nilipotazama nje niliona jua likichomoza
kwa mbali huku ndege wakipiga kelele kuashiria ujio wa siku mpya,
nilisikia mlango wangu ukigongwa na hapo ndipo niligundua kuwa
NILIKUWA NAOTA.
****
Nilinyanyuka na kuanza kutafakari yale niliyoyaota na hapo
nilikumbuka juu ya ile barua aliyokuwa akiniambia ndotoni, nilienda
kuoga na nilipotoka baada ya kunywa chai kazi ilikuwa ni moja tu,
kutafuta ile barua, nilipangua vitu vyangu vyote lakini haikuonekana,
nilikumbuka kuna siku iyo niliweka bahasha ile kwenye mkoba wangu
niliouacha kwakina Lucrecia rafiki yangu aliyekuwa akiishi Anktaso,
nilitoka nje nikakutana na baba, nilisalimia kisha nikaingia kwenye
gari;
“unaelekea wapi na mbona umevaa hivyo” aliniuliza wakati nikigeuza
gari.
“naenda Anktaso” nilimjibu kwa kifupi.
“kuna nini” aliuliza tena,,maswali yake niliona kama yalikuwa
yakinichelewesha.
“kuna mkoba wangu niliuacha kwa Lucrecia ndo nataka nikaufate,
kuna kitu muhimu ndani yake nataka nikisome” nilimueleza hayo na
kisha aliingiza mkono mfukoni na kutoa fedha kisha alinipatia bila
kusema ni za nini, nilipokea na kuanza safari ya kuelekea Anktaso,
lakini baada ya mwendo wa kama dakika 15 nilikuwa nimefika Rabary,
niliona gari ya Lucrecia ikiwa imeegeshwa sehemu, nilikwenda mpaka
pale alipoegesha gari yake kisha nilishuka na kutazama ndani lakini
sikuona mtu, nilisubiri kama dakika moja hivi na yeye alitokea;
“mambo Lucrecia” nilimsalimu huku nikimkumbatia.
“salama, unaenda wapi mbona mapema sana” aliniuliza huku
akinishika nywele zangu.
“nilikuwa nakuja kwako kuchukua mkoba wangu” nilimjibu kiuchovu.
“mh!ndo uje asubuhi hivi?” aliniuliza tena.
Nilimuhadithia Lucrecia kila kitu nilichokiota usiku ule, na baada ya
hapo wote tuliondoka kuelekea kwao, nikiwa kwenye gari mda wote
nilikuwa nikiwaza ni nini kimeandikwa kwenye hiyo barua, niliwaza
sana juu ya ile ndoto lakini sikupata jibu ila kila nilipomuwaza Frank
nilihisi mwili wangu unaishiwa nguvu.
Tulifika nyumani kwa kina Lucrecia na nilichukua mkoba wangu na
kuufungua lakini sikubahatika kuona ile barua, nakumbuka kabisa
nilipewa ile barua lakini sikumbuki nilipoiweka. Akili yangu ilivurugika
na hapohapo sikukaa sana niliamua kuondoka, njia nzima nilikuwa
nikiipekua akili yangu kujua ni wapi niliweka ile bahasha lakini
sikukumbuka kitu, machozi yalikuwa yananitoka mfulululizo kila
nilipoikumbuka ile ndoto.
“ninampenda Frank?” nilijiuliza moyoni lakini sikuwa na la kujijibu,
hisia zangu zilikuwa dhahiri, lakini nilikuwa nimeshachelewa kwakuwa
Frank alikuwa amefariki tena mimi nikiwa mmoja wa watu
waliosababisha kifo chake.
Nilifika nyumbani na kuanza kutoa tena vitu vyangu kimoja baada ya
kingine, nilitoa kila kitu na kuvirudisha lakini sikuona kitu, nilikaa pale
chumbani kama kichaa nikilia.
“unalia nini” nilishtuka na kufuta machozi haraka, kisha niligeuka
kuangalia ni nani nikakuta ni baba.
“jana nimeota ndoto mbaya” nilimueleza hivyo tu nikawa kama ndo
nimemualika pale chumbani, aliingia na kuketi kisha alianza kunihoji.
“umeota nini binti yangu” aliuliza na mimi nilimuhadithia kila kitu lakini
kabla sijamaliza kuhadithia nilikumbuka mahali ambapo ile barua
inaweza kuwepo, nilitoka pale na kukimbia mpaka nje na kwenda
kwenye lile ndoo lakuwekea takataka, lakini bahati mbaya sikukuta
kitu, nilimfata dada wa kazi pale nyumbani na yeye aliniambia gari
lakubeba takataka lilipita pale na kubeba uchafu wote asubuhi ya leo.
Niliwasha gari na kuondoka pale mpaka kwenye jaa kuu la taka
lililokuwa mjini, nilipofika pale ndo walikuwa wanajiandaa kuchoma
takataka zote, niliwaomba nitazame kitu muhimu kilichokuwa kwenye
zile takataka pale lakini hawakuniruhusu, walimwagia mafuta na zile
takataka zilianza kuwaka moto kwa kasi kisha wao waliondoka,,nil
itoka pale na kuingia mtaani kisha niliwaita vijana niliowaahidi
nitawalipa na hasa nilipowatajia mimi ni mtoto wa nani walikuwa
tayari kunifanyia kazi yangu, tulifika mpaka pale jalalani na kuanza
kuuzima ule moto kisha kuanza kupekua kila sehem na hapo
nilibahatika kuiona ile bahasha. Niliwapakia wale vijana mpaka
kwenye benki iliyokuwa pale karibu a kutoa fedha kisha niliwapa na
tukaachana,,niliendesha haraka na nilipofika nyumbani nilianza
kuisoma ile barua kwa undani,,machozi yalinitoka kila nilipoisoma
mstari kwa mstari, barua yenyewe ilisomeka hivi;
Mpendwa Beatrice,
Natangulisha shukrani zangu kwako kwa mema na faraja ulizonipatia
kwakipindi chote nikiwa naishi hapo kwenu, ulikuwa msaada mkubwa
sana kwangu kwakuwa nilipokuwa na huzuni wewe ulikuwa furaha
yangu, nilikupenda na kukuheshimu si kama mtoto wa bosi wangu
bali nilikupenda na kukuheshimu kama ndugu yangu. Mengi
yametokea na yametokea kwa haraka sana, wewe ni mwanasheria
tambua katika maisha yako hakuna haki kubwa kwa unayemtuhumu
kama haki ya kumsikiliza. Kama ungenipa haki ya kunisikiliza leo hii
usingejisikia mwenye hatia. Mimi si mpelelezi wala mimi si mtu wa
aina uliyodhani, ningekuwa na ujasiri wa kuja tena kwenu leo
ningekuomba unitazame machoni kisha uniambie kama naweza kuwa
mtu mwenye nia mbaya na familia yenu. Nenda chumba nilichokuwa
nalala mimi tazama nyuma ya kabati utaona ‘flash’ ifungue utakuta
hadithi ndefu inayoitwa THE LOST PROFESSION hiyo ndiyo historia ya
maisha yangu mpaka nilipofika hapo kwenu. Beatrice kwangu wewe
ulikuwa wa thamani kubwa sana na mpaka leo nakupenda na
kukuthamini licha ya yote yaliyotokea, naelewa kuwa hukufahamu
ndio mana na pengine kama ungejua basi usingekubali hayo yanitokee
mimi, maisha yangu yamekuwa magumu toka zamani, sikuwahi
kupata ahueni ya maisha toka nimalize masomo yangu nchini
Tanzania, lakini baada ya kufika kwenu nilihisi huo ulikuwa mwanzo
mpya japo haikuwa hivyo. Sijutii kukufahamu wala baba yako, wewe
kwangu bado nakupa uzito uleule kama mwanzo. Zingatia masomo
yako, kuwa makini katika maisha, mimi sikufa, msamaria mwema
aliyeniokota kule msituni alinisaidia na nimebahatika kusihi tena, lakini
nategemea kuondoka kwenda Tanzania wiki moja ijayo, nimeona ni
bora nirudi nikafie huko kuliko kufia ugenini, umasikini wangu
umekuwa shida sana kwa uhai wangu. Mikono ya matajiri
imeninyang’anya utu wangu na dhuluma yao imeukaba uhai wangu,
niko tayari kufa ili nikapumzike na familia yangu huko waliko, siko
tayari tena kuishi kama mkimbizi, narudi nyumbani Beatrice. Usijute
ila jifunze, mimi nimekusamehe kwa moyo mmoja na sasa hata nikifa,
hicho kitabu kitakuwa ni zawadi yangu kwako. Msalimie sana mzee
mwambie mimi nimemsamehe, ila yale mateso mliyonipa yaishie
kwangu, msimfanyie mtu mwingine kwakuwa si mazuri hata kidogo.
Kwaheri Beatrice, nakutakia kila lenye heri katika maisha yako, soma
sana na umtegemee mungu.
Ni mimi Fisherman.
Nilimaliza kuisoma hii barua na kugundua kuwa blauzi niliyokuwa
nimevaa ilikuwa imelowa kwa machozi,kamasi na jasho.
Nilinyanyuka haraka na kwenda kuangalia kwenye ile kabati nikakuta
ile flash, niliwasha ngamizi yangu na kuichomeka kisha nilifanikiwa
kuiona ile hadithi, niliisoma kwa muda wa masaa miwili na nusu na
nilikuwa nimemaliza, nililia sana na hapo nilimfata baba nakumpa ile
barua na ile hadith asome, wote tulijuta lakini hatukuwa na la kufanya.
“baba nataka nimfate Fisherman huko aliko, naamini atapatwa na
jambo baya” nilimuambia mzee wangu lakini alikataa kabisa kusikia
jambo hilo,,nililia usiku na mchana lakini hakukubali, niliandika kisirisiri
barua ya kuahirisha mwaka mzima wa chuo na niliruhusiwa, nilirudi na
kumtishia baba kuwa ningejiua kama asingeniruhusu na yeye ikabidi
akubali. Nilisoma katika ile hadithi maeneo matatu ya Tandale,Kimara
na Kibaha, niliingia kwenye ‘google map’ nikachukua ramani izo, baba
alinisaidia kuwasiliana na rafiki yake ambaye alikuwepo nchini Kenya
na huyo rafiki yake alisema anamtoto wake wa kike ambaye yuko
Tanzania hivyo angenipokea na ningekaa kwake.
BAADA YA WIKI MOJA
.
Asubuhi na mapema nilikuwa nimeshafika Ivato International airport
kwaajili ya safari yangu ya kwenda nchini Tanzania kumfata
Fisherman, nilikuwa sielewi ningempataje hasa ukizingatia kuwa
ilikuwa ni nchi kubwa lakini nilikuwa na uhakika wa kumpata,,Saa
12:00 kwa saa za Madagascar ndege ya British airways iliondoka
uwanja wa ndege na kuanza kushika anga tayari kwa safari ya
kuelekea Misri na baadaye Afrika ya kusini kisha Tungepanda ndege
ya shirika la Emirates kwa kuelekea Tanzania.
JE ITAKUWAJE,,,?? tuwemo

Mzn....bila shaka wewe ni shabiki wa bwana Frank Mushi....lakini ingekua vyema zaidi kama ungewasiliana nae kisha u post hii hadithi huku
 
RIWAYA: TAALUMA ILIYOPOTEA
MTUNZI: FRANK MUSHI
SEHEMU YA NNE
“Mapenzi ya kweli hudumu milele,,hila na chuki za kupandikizwa
huweza kumfanya mtu adhani kuwa hawezi kabisa kupenda
tena,,lakini mambo huwa tofauti, ukimpenda mtu kweli, haitajalisha
umepata maumivu kiasi gani kwa kutoelewa kwake, utaendelea
kumpenda huku ukimwomba mungu amfumbue macho. Kuna watu
tunakutana nao katika maisha yetu na hutokea kuwa wathamani
kwetu kwakuwa wanajali sana furaha yetu kuliko waliotufahamu
kabla,,furaha zetu hurudi tena pale faraja ya kweli inapoambatana na
moyo wa uvumilivu unaokumbatia matatizo yetu na kuyaficha
tusiyaone..” KILA MTU NI WA MUHIMU KWAKO,,LISHA MBWA WOTE
CHAKULA SAWA KWAKUWA HUJUI YUPI ATAKUOKOA SIKU
YAKIKUFIKA”…HII NI SEHEMU YA NNE,,,,ANDIKA HIVI.
….Nilitafuta vyeti vyangu pale nilipoviweka lakini sikuviona hata nakala
moja wala picha wala kitu chochote,,nilimpiga simu ya Natasha lakini
iliita bila kupokelewa. Sikujua nielekee wapi na wala sikujua nifanye
nini, nilitoka mpaka kilabu cha pombe kilichokuwa karibu na pale
nyumbani na kuanza kunywa pombe, yote ni kuamini kuwa
ningeondoa mawazo lakini haikuwa hivyo, nilikuwa nimeahirisha
mawazo kwa muda tu na nilipoamka kesho yake asubuhi hakika bado
mawazo yalinisonga,,,nilitoa kila kitu nje ya kile chumba lakini sikuona
hata karatasi moja iliyokuwa na dalili hata ya nakala ya cheti changu.
Niliondoka pale nyumbani na kwenda kituo cha mabasi cha ubungo
nikakata tiketi ya kwenda morogoro, nilipanda gari majira ya saa nne
na ndani ya masaa mawili nilifika kituo cha basi cha msamvu pale
morogoro, wakati na shuka nilifanikiwa kukutana na Abdulaziz kijana
wa kipemba niliyesoma nae darasa moja,;
“Bora nimekuona Abdul,,za masiku kaka?” nilimuuliza huku kabisa
nikionekana kuwa sikuwa sawa.
“Salama kijana,,mbona unaonekana umechoka sana na mkanda
hujavaa, uko sawa kweli” aliniuliza huku akinitazama huku na huku”
“Siko sawa Abdu, nina matatizo makubwa sana ambayo si rahisi
kuyaelezea” nilimueleza na hivyo na kumvuta pembeni,,kabla
sijamuambia chochote nilijikuta machozi yakinitoka,,dhuluma
ninayofanyiwa haikuwa sahihi kabisa, ni umafia na si kitu kingine,,nilili
a kwakuwa nilihangaika sana mpaka kupata elimu niliyokuwa nayo
ambayo kwasasa sina ushahidi nayo, nililia sana kwasababu pamoja
na kuwa nilimpenda mtoto wa kigogo lakini mapenzi yangu kwake
hayakuwa kwasababu ya hadhi aliyokuwa nayo baba yake,,na kuwa
kwenye mahusiano na mwanae halikuwa kosa kubwa lililostahili mimi
kunyang’anywa elimu niliyoisumbukia siku zote za uhai wangu,
halikuwa kosa kubwa namna ile.
“Najua hauko sawa” nilishtushwa na kauli hiyo ya Abdu na kujikuta
nikitoka kwenye kuwaza na kurudi tena duniani.
“unamaana gani?” nilimuuliza Abdu kwa shauku.
“najua kuhusu taarifa iliyoandikwa kwenye gazeti,,lakini najua pia
kuwa huna elimu ya chuo kikuu” aliongea yale maneno na kuonekana
kama vile aliujua mpango wote.
“Abdu unaelewa nini kuhusu hili?” nilimuuliza tena.
“Najua kwa hapo tu nilipokuambia,,ujue Frank maisha si sawa na
ambavyo unaweza ukadhani, kuambiwa sisi sote ni sawa usidhani ni
sawa hapa duniani,,hapana, sisi ni sawa mbinguni, hapa duniani
tunatakiwa tuishi tukiifahamu sheria tu na si haki yetu, uifahamu
sheria inakupa wajibu gani na si sheria inakupa haki gani, huo ndo
msingi wa maisha ya binadamu. Unaweza kuwa una elimu kubwa
sana, lakini elimu yako si kitu kwa mtu mwenye nguvu na madaraka,
nchi hii inaongozwa na wenye nguvu sio wenye elimu,,mwenye elimu
ni kibaraka tu wa mwenye nguvu hivyo jitahidi sikuzote kufata misingi
ya mfumo mpya na si mfumo wa zamani, mapenzi yasizidi yakaharibu
misingi ya sheria na wajibu wako kwa wenye nguvu, fedha haiendi
pachafu, usafi wa nafsi haukutoshi wewe kujitwika taji la ufalme wa
nyika ambayo si hadhi yako. Wahenga walikuwa na busara na utashi
wa kiundani, ila walitahadharisha haya yanayokutokea
waliposema,,kubali matatizo yakutafute ila si wewe uyatafute.
Mchuma janga hula na wa kwao. Pole sana” hizo zilikuwa ngonjera tu
kwangu, sikuelewa lolote alilolisema,,niliinama chini nikiwaza na
kuwazua lakini nikaona ninaota, nilinyanyua kichwa ili kumuomba
ushauri lakini sikumona pale nilipotazama mbele niliona akiwa ndani
ya Land Rover Discovery huku akinipungia kuashiria kuwa alikuwa
akiondoka.
Nilipanda daladala pale msamvu na kushika njia kuelekea Mzumbe,
muda wote kwenye gari nilikuwa nikiyatafakari maneno aliyoniambia
Abdu, baada ya mwendo wa kilomita 20 tulikuwa tumefika Mzumbe,
nilishuka na moja kwa moja nilielekea ofisi ya msajili na kuulizia
taarifa zangu lakini walisema kuwa sitambuliki,,nilienda kutafuta
walimu walionifundisha kipindi kile lakini sikumpata hata mmoja,
nikaingia kwenye ofisi ya mkuu wa chuo na huko ndiko nilikokatishwa
tama baada ya kuambiwa kuwa hawajawahi kuwa na mwanafunzi
kama mimi pale chuoni. Nilitoka nje nakuhisi kama dunia sasa
imenitenga,,sikuwa na la kusema licha tu ya la kufanya. Ilikuwa
imeshafika majira ya saa tisa mchana, nilitafuta simu yangu ili niweze
kumtafuta tena Natasha lakini haikuwepo, nilipofikiri zaidi niligundua
kuwa nilikuwa nimeisahau nyumbani, nilipanda daladala pale na
kuondoka tena mpaka msamvu kisha nilichukua basi na kurudi Dar,
kwenye majira ya saa nne usiku nilikuwa nimeshafika nyumbani, akili
ilinijia kichwani nitafute muhuri wangu,,ooh nilichoka nilipoukosa,,yani
walikuwa wamechukua kila kitu.
Nilikaa pale ndani nikiwa sina ramani yoyote ya maisha,,hakuna
mahali ningeweza kwenda na nikasikilizwa, haki yangu haikutambulika
popote tena na sasa nilibakiwa na hatia tu,,ikumbukwe kuwa hapa
pamoja na mambo mengine bado nilifunguliwa kesi mahakamani ya
kudanganya na kufanya kazi kwa taaluma nisiyokuwa nayo.
Niliitafuta simu yangu nilipokuwa nimeiweka na kisha nilibahatika
kuiona, nilikuta Natasha amepiga simu mara tisa na mwisho aliamua
kutuma ujumbe uliosomeka ‘una matatizo gani?’, nilifarijika sana
kukuta ujumbe ule kutoka kwa Natasha,,niliipiga namba yake lakini
haikuwa inapatikana,,niliketi pale chini nikitafakari mpaka kulipokucha,
sikuwa na usingizi wala njaa, kulipopambazuka niliamua kuondoka na
kwenda wizara ya mambo ya nje ya nchi, nilipofika nilimuulizia
Natasha na nikaelekezwa ofisini kwake. Baada ya kufika pale nilionana
na katibu muktasi wake na kuniruhusu niingie ndani, nilipofungua tu
mlango pamoja na kwamba pale ndani kulikuwa na mtu ambaye
sikumfahamu ila nilimshuhudia Natasha akiacha alichokuwa
akikifanya na kuja kunikumbatia,,nilifarijika sana na ile hali lakini
haikuchukua muda nilinywea kama majani mbele ya jua, mlango
ulikuwa umefunguliwa na aliingia baba yake pale ofisini.
Nilipomtazama Natasha alionekana kumuogopa sana baba yake
ingawaje alikuwa ni msichana mkubwa mwenye uwezo wa kujiamulia
mambo yake. Nilimsalimia yule mzee na aliitika vizuri kama hakuna
lililokuwa linaendelea, niliwapisha ofisini pale na muda kutoka nje,
lakini cha kushangaza nilipotoka nje ya ile ofisi tu walifika maaskari
pale na kunikamata;
“uko chini ya ulinzi kwa kosa la kujihusisha na uuzaji wa madawa ya
kulevya na kosa la kujaribu kumdhuru Natasha Rweikaza, una haki ya
kunyamaza kimya na lolote utakaloongea litatumika dhidi yako
mahakamani” hayo yalikuwa ni maneno machache tu waliyoongea
wale maaskari na kunifunga pingu, nilibaki mdomo wazi na sikuelewa
nini cha kusema, ghafla nikiwa pale nilimuona Natasha akitoka na
baba yake huku machozi yakimtoka, alifika pale nilipo na kunipiga
kofi;
“haya ndo malipo ya wema wangu kwako Frank?” aliniuliza huku
akiendelea kulia, nilikosa cha kujibu, yani kila kitu pale kilikuwa
kinakwenda haraka na sikujua nijibu nini.
“Natasha sio….”nilikatishwa na kofi linguine toka kwa Natasha.
“Shut the *** up, do you think am that idiot?huh, I spent my money,
my love and my carreer just to make a better life with you but today
you want to kill me?”(nyamaza, unadhani mimi ni chizi, nimetumia
zangu, mapenzi yangu, na kazi yangu ili kutengeneza maisha mazuri
na wewwe ila leo unataka kuniua). Aliniambia maneno yaliyonishtua
lakini kabla sijajibu nilianza kupekuliwa na wale maaskari na huku
Natasha akitazama kwa makini, nilipopekuliwa nilikutwa na bomba la
sindano lenye dawa, nilianza kupiga kelele kuwa silitambui ilo bomba
lakini hakuna aliyenisikiliza, si Natasha wala si mtu mwingine yeyote
pale, Natasha alizidi kulia na baadaye aliondoka na mimi nilipakiwa
kwenye gari ya polisi tayari kwa kuelekea kituo cha polisi ambapo
jalada la kupanga kuua lilifunguliwa na kisha nilipakiwa kwenye gari
hilohilo na kwenda kwangu kupekuliwa ambapo ilikutwa chupa ndogo
mbili za sumu, bastola moja yenye risasi nane, kadi za ATM ambazo
sikujua zimefikaje pamoja na madawa ya kulevya gramu 250 na pesa
bandia laki 7, nilichoka kwakweli, sijawahi kuwa na hivyo vitu lakini pia
viliwekwa kiustadi mkubwa sana na hakuna aliyeamini kuwa haikuwa
kweli, majirani zangu pale wote walishtushwa na walianza kurusha
mawe juu ya bati wakisema mtoeni huyo mwizi tumuue,,nilikuwa
nikilia tu hasa ukizingatia nilikuwa nimeshapigwa na maaskari na mwili
wangu ulitapakaa damu lakini sikujua nilichokuwa nikikifikiria, sikuwa
na la kusema,,ilikuwa kama ndoto lakini kiuhalisia ilikuwa kweli kabisa,
baada ya hayo yote nilipelekwa mahabusu na kesho yake nilifikishwa
mahakamani, ambapo nilisomewa mashtaka nane, 1. Kujaribu
kuua,,2. Kukutwa na silaha kinyume cha sheria,,3. Kukutwa na
madawa a kulevya,,4. Kukutwa na fedha bandia,,5. Kuvamia ofisi ya
mfanyakazi wa wizara ya mambo ya ndani,,6. Kufanya kazi za sheria
wakat sikuwa na kibali cha kufanya hivyo,,7. Kujipatia fedha kwa njia
za udanganyifu na 8 ni kadi za benk kinyume na taratibu. Haya yote
yalikuwa ni makosa yangu na sikuruhusiwa kujibu chochote mpaka
uchunguzi utakapo kamilika,,,wakati natolewa nje ya mahakama na
nilipoingizwa kwenye defender ya polisi nilimuona Natasha akija pale
na akaruhusiwa kuongea na mimi..macho yake yalikuwa mekundu
sana;
“kama niliwahi kukuambia nakupenda na niko tayari kufanya lolote
kwaajili yako basi leo hii nikuambie tu kuwa nakuchukia sana na niko
tayari kufanya lolote kuhakikisha unaishi kwa mateso sana hapa
duniani kama si kufa,,,ulikosa nini kwangu mpaka ukatumike na
wanasiasa kupanga kumuumiza baba yangu kwa kuniua mimi,,
nilikupa fedha ukasome kumbe hukuwa unasoma, nilidhani ulikuwa
mwanasheria kweli kumbe tapeli tu,,nakuambia utajuta kwa hili”
aliongea huku machozi yakizidi kumtoka.
“Natasha sikiliza mpenzi” nilijaribu kujitetea lakini haikuwa hivyo
kwani alikuwa ameshafunga ule mlango na kuondoka na baadaye
nilirudishwa mahabusu,,wiki mbili mbele nilipelekwa pale mahakamani
lakini kama vile naota nilisikia mwendesha mashtaka wa serikali
aliamua kufuta mashtaka yale na niliachiwa huru, sikujua kuachiwa
kwangu huru ulikuwa ni mchezo wa kiufundi uliokuwa unachezwa ili
kumuonyesha Natasha kuwa kweli nilikuwa nikitumia na watu
waliokuwa na nguvu sawa na baba yake. Baada ya kurudi nyumbani
sikuiyo usiku niliamua kubeba vitu vyangu na kuhama kabisa eneo lile,
nikaenda kuishi Kibaha kwenye kibanda cha udongo kilichokuwa
kwenye shamba la marehemu babu yangu,,lakini mambo hayakuishia
pale,,nilijitahidi kumtafuta Natasha ili nimueleweshe lakini sikufanikiwa
kabisa, baada ya siku tatu nikiwa kwenye kibanda change nilisikia gari
zikiegeshwa nje nilichomoka mbio lakini sikufika mbali nilisikia kitu
kikipenya kwenye mguu wangu na kunifanya nikae chini, baada ya
kutizama na kupata fahamu kuwa kuna mlio mkubwa nimeusikia
nikagundua ilikuwa ni risasi, wakaja vijana watatu wakaanza kunipiga
sana mpaka nikalegea kabisa kisha walinisogeza karibu na ile gari na
hapo nikamuona Natasha;
“nilikuahidi mateso kwa ulichonifanyia na sasa hayo ndo uyapatayo,
umeniumiza sana, ulikuwa masikini wa kutupwa lakini nilijitolea
kukupenda kumbe wewe una ajenda yako ya siri ya kuniangamiza,
nilikupa kila kitu,,nilikuachia mwili wangu na kila nilichonacho, kila kitu
kwangu ulipata,,ni bora ningekukuta na mwanamke mwingine lakini si
wewe kupanga kuniua mimi” nilisikia akinisemesha,,nilijitahidi sana
kujitetea lakini sikupewa nafasi, walimaliza kunipiga na kuniacha pale
chini nikiwa nimelala bila msaada wowote,, nilianza kujivuta taratibu
nikarudi tena mpaka kwenye kile kibanda change nikajilaza,,,asubuhi
na mapemba niligundua kuwa siwezi kunyanyuka kwakuwa mbavu
zilikuwa zinauma,,nilikaa bila kula kwa muda mrefu ila baadae nilianza
kujivuta hadi nje,,nikasogea karibu na shina la muhogo na kuanza
kuushimba taratibu, nilifanikiwa kupata kipande kimoja na kukipeleka
mdomoni japo kilikuwa kichungu sana.
Basi nilikaa katika hali hiyo kwa muda wa siku nne na nilianza kupata
nafuu na siku ya tano usiku alikuja mzee Rweikaza na walinipakia
kwenye gari huku wamenifunga kitambaa cheusi usoni, baada ya
mwendo mrefu sana nilihisi nachomwa sindano na hapo sikuamka
tena mpaka baadaye nilianza kusikia tena sauti ya watu wakijadili
jambo Fulani na hapo nilipotaza nje niligundua ilikuwa ni uwanja wa
ndege, wale watu baada ya mazungumzo na kupeana maelekezo hayo
walikuja tena pale nilipokuwa mimi na sasa nilisikia wakiambiana
mchome tena ya masaa 96, nilikaa kimya nikasikia tena sindano
ikiingia mwilini mwangu na hapo mda mfupi mbele sikusikia chochote
mpaka nilipokuja kuamka na kushangaa nikiwa ufukweni mwa bahari,
nilipotazama huku na huku sikuona chochote zaidi ya boksi lililokuwa
limechomekwa kwenye mti nyuma ya pale nilipokuwa kilichokuwa
kimeandikwa kwa lugha ya kingereza iliyomaanisha,,usiongee
Kiswahili kama unataka kuishi kwa Amani, tafuta maisha sahau
ulikokuwa,,karibu Madagascar. Nilishtuka sana na nikaamka pale
nilipokuwa nikaanza kutembea nisipopajua, baada ya mwendo mrefu
nilikuwa tayari nina njaa na sikujua pa kupata chakula,,,nilivua shati
langu na kuzama baharini ambapo nilibahatika kupata samaki mmoja
nilirudi ufukweni na kukuta wavuvi wakisubiri muda wakuingia baharini
ufike, niliomba kibiriti na kupatiwa kisha nikawasha moto na
kumchoma yule samaki kisha nilikula. Kwakuwa sikupajua pale vizuri
ilinibidi kulala kule ufukweni na kuishi huko kama sehemu ya maisha
yangu mpaka nilipokuja kupata rafiki mvuvi ambaye hata hivyo
sijawahi kumweleza chochote kuhusu mimi, nilianza kujifunza kuvua
samaki na nilipoweza basi nilikuwa naingia mwenyewe baharini navua
samaki na kuanza kuetembeza mitaani, hiyo ilikuwa kazi yangu kwa
mda wote wa miaka mitano niliyojikuta nikiwa nchini Madagascar jiji
la Antananarivo, uzoefu wangu na ukarimu wangu ulinifanya
kupendwa na wengi na wakati huo nilikuwa bado nikikaa na kusoma
pale nilipopata muda,,nilikuwa nikiandika kitabu change cha THE LOST
PROFESSION kilichokuwa kinaelezea maisha yangu na kila kilichokuwa
kinanitokea kwa siku za maisha yangu. Baadae nilikuja kupata kazi
nyumbani kwa mzee Aristede Rusovelt na ndipo yaliponikuta mambo
yaliyosababisha majeraha haya niliyoyapata.” Nilimaliza kumuhadithia
Mzee Russel na nilipotazama niliona mkewe na mwanae wakilia.
“msilie, yamepita na nashukuru kwakuwa niko hai” niliwaambia huku
nikitabasamu. Walinipa pole kwa pamoja na maisha mapya yalianza
tena pale msituni, japo nilijua kuwa baba yake na Beatrice hata sita
kunitafuta na kuniua kama atagundua bado nilikuwa hai. Kwakipindi
chote hiki sikuwahi kumsahau au kuacha kumpenda Natasha,
sikumlaumu kwa lolote kwakuwa hakufahamu ukweli bali uongo na
dhuluma ilipandikizwa kwenye kichwa chake na kumfanya auamini,
niliamini ipo siku moja ataujua ukweli na pengine tungeweza kuwa
pamoja tena,,japo sikutegemea tena kurudisha kila nilichokipoteza.
MWEZI MMOJA MBELE
Nimepamis sana nyumbani, hilo lilikuwa wazo la kwanza kunijia
kichwani siku iyo, niliamka na kuketi, mawazo yalinijaa na nilijiuliza
nitakuwa mtumwa hadi lini,,nilisogea mpaka kwenye kioo na
kujitazama vyema, nilikuwa na ndevu ndefu na uso wangu ulikuwa
umebadilika kabisa, sio rahisi kwa mtu yoyote aliyeniona miaka
mitano iliyopita kuweza kunitambua leo,,kutwa nzima mawazo
yalikuwa ni kurudi nyumbani,, niliandika barua ndefu yenye kurasa sita
kwa Beatrice nilimweleza kila kitu kuhusu mimi na kumtaarifu kuwa
narudi Tanzania. Sikutaka kuondoka lakini niliona huu ndo muda wa
kurudi nchini,,nirudi nikayatazame japo makaburi ya wazazi wangu na
lile la mdogo wangu kabla sijafa. Baada ya kuandika ile barua
nilimpatia mtoto wa mzee Russel aipeleke kwa kina Beatrice,
nilimuelekeza kila kitu lakini nilimwambia akifika ampe mlinzi wa geti
na asimwambie imetoka kwa nani, alienda mjini siku hiyo na
alifanikiwa kuifikisha lakini alisema alipokuwa anagonga geti alitoka
msichana Fulani na alimpatia lakini yule msichana hakuuliza
chochote,,kwajinsi alivyonitajia kuhusu huyo msichana nilijua kuwa ni
Beatrice.
Jioni siku iyo baada ya chakula nilimueleza mzee Russell na mkewe
juu ya nia yangu ya kutaka kurudi nchini kwangu na hivyo wao
walianza kuniandalia namna ya kusafiri na baadaye walinipa kiasi cha
pesa ili kinisaidie nitakapofika huku.
***
Ni Septemba ya tarehe13 mwaka 2010 saa 9:45 jioni niliondoka nchini
Madagascar kurejea Tanzania, nikiwa pale uwanja wa ndege wa
Antananarivo ilikuwa huzuni na simanzi kwangu na kwa familia ya
mzee Rusell, hao ni watu walionifanya nijione binadamu tena baada ya
manyanyaso ya muda mrefu ya walimwengu, nilikuwa kwamba mzn....bwana FRANK MUSHI ANAOMBA UWASILIANE NAE KWA NAMBA 0717353606 KABLA YA KUENDELEA KUIPOST KWAKUWA HADITHI HIYO IMESAJILIWA NA INA HATI MILIKI. HIVYO KUENDELEA KUIPOST BILA IDHINI YAKE NI KOSA KISHERIA
 
Mzn....bwana FRANK MUSHI ANAOMBA UWASILIANE NAE KWA NAMBA 0717353606 KABLA YA KUENDELEA KUIPOST KWAKUWA HADITHI HIYO IMESAJILIWA NA INA HATI MILIKI. HIVYO KUENDELEA KUIPOST BILA IDHINI YAKE NI KOSA KISHERIA
 
Habari mwana Jf...mimi naitwa FRANK MUSHI mwenye hadithi uliyoipost hapa. Hadithi iyo nimeisajili na ina namba ya usajili na hati miliki. Si sahihi kuipost bila idhini yangu kwakuwa ni kazi inayolindwa na sheria ya hati miliki. Hivyo nakusihi usiipost tena na pia nitafute kwa namba aliyoiweka mdau hapo juu.
 
Habari mwana Jf...mimi naitwa FRANK MUSHI mwenye hadithi uliyoipost hapa. Hadithi iyo nimeisajili na ina namba ya usajili na hati miliki. Si sahihi kuipost bila idhini yangu kwakuwa ni kazi inayolindwa na sheria ya hati miliki. Hivyo nakusihi usiipost tena na pia nitafute kwa namba aliyoiweka mdau hapo juu.



nadhani promo yenu imefanikiwa.well done frank
 
Sasa tuambieni hicho kitabu nitakipata wapi?
 
Back
Top Bottom