RIWAYA: Sitaisahau Facebook

RIWAYA: Sitaisahau Facebook

SITAISAHAU facebook
MTUNZI: Emmy John P




SEHEMU YA KUMI​




ILIPOISHIA


Nilitaka kumuita jina lake kwa sababu nilihisi ninalijua jina hilo. Hata sura mbona nilikuwa nimewahi kuiona hapo kabla? Lakini kabla sijajua anaitwa nani. Teksi ilipigiwa honi ikapisha njia ikaondoka zake.
"Ah!! Huenda aliwahi kunibeba hapo kabla." Nilijipa moyo.
Nikafungua pochi yangu na kuhifadhi hicho nilichookota.
"Mungu wangu!!!!" nilipiga kelele kwa nguvu sana. Nilikuwa nimesimama wima.
Kwa kuwa halikuwa eneo la watu wengi nilipata sekunde kumi za kuhakikisha nilichokiona.
Hakika kilikuwa chenyewe.
Kilikuwa kitambulisho cha chuo ni heri kingekuwa changu.
Kitambulisho cha John mikononi mwangu. Kitambulisho kinachoaminika kupotea ,msibani huko Iringa , kitambulisho nilichokiona ndotoni.
Kitambulisho cha muuaji!!!
Ewe dunia funguka unimeze!!! Ni sala niliyoiomba kimyakimya.
Nilikuwa nimezizima siwezi kwenda mbele wala kurudi nyuma.
Harufu ya kifo!!!!


***NI jambo juu ya jambo…….ISABELA ISABELA ISABELA.
Lakini je ungekuwa wewe ungefanya nini sasa….John unampenda, John umeota akiwa anaua, kweli mtu kafa. Huyu mtu ni binamu wa John. John anapoteza kitambulisho. Na ndotoni muuaji anadondosha kitambulisho.
John na muuaji wa ndotoni wanafanana….Kabla ya kujua Isabela mimi nilifanya nini…je WEWE UNGEFANYA NINI HAPO.
Pagumu!!!!!


ENDELEA


ITAENDELEA.


Nilisahau ni jambo gani lilikuwa limenipeleka huko mjini. Yale mawazo niliyoamini nimeyapunguza kwa kunywa pombe sasa yalikuwa yamerudi kikamilifu. Tena mara mia zaidi.
Hofu ikatanda. Nikachukua teksi nyingine nikarejea nyumbani kwangu.
Nilikuwa natetemeka, na kila nilipoguswa na kitu nilishtuka. Hata nywele zangu za bandia kichwani ziliponigusa shingoni nilitetereka.
Nilipohakikisha kuwa nimeifunga milango vyema kabisa na ndani nilikuwa peke yangu. Nilifungua mkoba wangu nikakitoa kitambulisho.
Hapakuwa na mabadiliko. Kilikuwa kitambulisho rasmi cha chuo kikuu matakatifu Augustino. Mmiliki akiwa John Joseph.
Mpenzi wangu.
Nililazimisha akili yangu kutafuta kumbukumbu huenda siku moja aliwahi kunipatia kile kitambulisho. Hapana kitu kama hicho.
Au aliweka mwenyewe bahati mbaya akakisahau? Hilo swali walau kidogo liliamsha uhai na kunipunguzia hofu.
Akija nitamuuliza!!! Nilimaliza hivyo. Nikautua mzigo wa mawazo.
Nikaingia maliwatoni nikasafisha mwili wangu kijuu juu. Nikajitupa katika sofa iliyokuwa sebuleni. Ule uchovu wa ulevi jana usiku ukawa unanishawishi kusinzia.
Nikajifikiria kwenda kulala chumbani. Mara mlango ukagongwa.
Nikajikausha!! Ukagongwa tena.
Nikaenda kufungua. Alikuwa ni John.
Alilazimisha tabasamu!! Nami nikatabasamu. Hatukusalimiana.
Tayari kakereka jana sikulala nyumbani!!! Niliwaza, huku nikijiandaa kukabiliana na maswali atakayoniuliza kwa fujo.
Wanaume wana mikwara jamani!!!!
Akafika hadi katika lile sofa nililokuwa nimejilaza awali. Akajitupa hapo. Akazishusha pumzi kwa nguvu sana. Kisha akajishika kichwa. Mimi yangu macho nikawa nasubiri lawama.
"I hate this….." Alisema huku akiwa kama anajisea mwenyewe.
Yaleyale!!! Nikajisemea.
"Uko ok!! John!!" Hatimaye nilimuuliza. Hakunijibu!!
"John jamani…." Nilibembeleza. Bado hakunijibu kitu. Nikaamini kuwa John amekerwa sana na kitendo changu cha kulala nje bila taarifa.
Wazo!!! Wazo likanijia. Nikasimama tena bila kumuaga nikatoweka pale hadi chumbani. Nikazama katika mkoba. Nikachomoa kile kitambulisho.
Nikakisokomeza katika sidiria niliyokuwa nimevaa. Kisha nikarejea sebuleni. Wanaume dawa yao ndogo tu!! Mfanyie kitu anachopenda kwa wakati!! Baaasi hakuna ujanja tena.
John akishaona kitambulisho chake ndo basi tena anasahau kuhusu suala langu la kulala nje. Najua mada itageuka na yatazaliana maswali.
Umekitoa wapi? Ilikuwaje? Dah!! Siamini.
Kwisha mchezo!! Nilijiaminisha.
Sasa nilikuwa mbele ya John. Bado alikuwa kama anayefikiria kitu kabla ya kuzungumza. Nikamsubiri labda atasema kitu hakusema. Nikamuita akaitika kwa kichwa chake kutingishika.
"I hate…my country (naichukia nchi yangu)." Alisema huku akitazama mbele. Nikaurudisha mkono uliokuwa umekamata kile kitambulisho tayari kwa kumshangaza. Nikakirudisha katika sidiria ili nipishe kwanza anachotaka kusema John.
"Nini tena mpenzi wangu jamani." Tayari nilikuwa ubavuni mwake wakati anayasema haya. Hakujibu upesi bali alicheka kwanza. Kicheko cha kujilazimisha.
"Eti kile kitambulisho….kile kitambulisho kile." Alianza kuzungumza, nikafarijika kusikia mada ni juu ya kitambulisho na sio wivu wowote wa kimapenzi. Kisha akamalizia, "kile kitambulisho eti kimeibiwa ama kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Serikali yetu bwana..haya sasa kuna haja gani ya kuipenda?" Alimalizia, bado alikuwa ametazama mbele tu. Akiyang'ata meno yake kukabiliana na pepo la hasira.
Mshtuko!! Nikatoa kelele ya kuogopa, lilikuwa yowe ambalo hata John aliyekuwa anatazama mbele lilimshtua akapata nafasi ya kuniangalia.
Nilikuwa wima!!! Mikono kichwani mara kiunoni, wakati mwingine najiziba uso. Mithili ya mwendawazimu.
John alidhani nasikitika kwa jinsi alivyonitazama lakini sikuwa katika kusikitika, nilikuwa naogopa sana. Kitambulisho kilichoibiwa si ndio hichi katikati ya maziwa yangu ama!!! La haula!!
Ndio hiki kitambulisho cha muuaji. Muuaji mwenyewe si ndio huyu mbele yangu. John ndiye muuaji anayejitafuta mwenyewe.
Mbiombio nikakimbilia chumbani. Sikujiamini tena kuwa mbele ya John. Sikuwa na uwezo wa kumueleza chochote juu ya kitambulisho chake. Kitambulisho kile kilikuwa na utata mkubwa.
Nilipokuwa natimua mbio kwenda chumbani, John naye nyuma akanifuata. Muuaji nyuma yangu, lengo langu nifike chumbani niwahi kujifungia mlango. Maziwa yakaruka kwa fujo wakati nakimbia, kitambulisho kikazidiwa ujanja kikakosa pa kujificha. Upesi kikachoropoka.
Kitambulisho haramu kikadondoka katika marumaru.
Nikasita kuendelea mbele. Sikutaka John akione kile kitambulisho.
Niliweza kusimama nikageuka. John huyo anakuja mbiombio. Macho ya John kwangu. Macho yangu katika kitambulisho kilichokuwa katika marumaru. Kila mmoja na wazo lake.
Kitambulisho sasa kikawa katikati yetu. John na moka zake modeli ya ‘wanchoma kumoyo' akakikanyaga bila kutambua kile kitambulisho wakati ananikimbilia. Kitambulisho ni manira laini sana, kikaisikia kero ya kukanyagwa na bwana John. Zilikuwa zimebaki hatua moja na nusu niweze kukichukua ndipo nikakumbana na wakati mwingine matata ambao nisipousimulia utanilaumu mwisho wa simulizi. Mi sitaki lawama!!!
John akateleza, baada ya kukanyaga kile kitambulisho. Marumaru ikampokea kwa shangwe, kisogo kikatoa mlio kama chuma kilichogongana na chuma kingine. Kitambulisho kikaachana na kile kiatu kikawa mbele yangu.
Shida yangu ilikuwa kukiwahi kitambulisho. Sasa kitambulisho kimetulia na John ametulia tuli sakafuni.
Mamaaaa!!! Niliita tena, mama mwingine nani sasa zaidi ya mwalimu Nchimbi huko Makambako? Atanisikiaje sasa wakati nipo Mwanza. Ujinga!!
Nikimbie!!! Nilijiuliza huku nikitetemeka.
Kwenda wapi sasa?? Ujinga mwingine.
Mara damu nzito nyuma ya kisogo cha John. Macho yamefumbwa kistaarabu. Mdomo wazi.
Nikahisi kuchanganyikiwa sasa. Damu ikazidi kusambaa katika marumaru ile nyeupe.
"Atakufia huyu Isabella shtuka fanya kitu." Sauti ikaniambia. Sasa hapo nikashtuka, nikainama nikakwapua kitambulisho chenye utata. Nikakimbia nje.
Taksiii!! Nikapiga kelele. Ikasimama, ikaanza kurudi nyuma. Macho ya dereva taksi badala ya kunitazama usoni na kunisikiliza shida yangu, yakawa yananitazama huku mapajani. Nilipojitazama, mbio nyingine mpya kurudi ndani. Nilikuwa nimevaa kinguo kifupi sana. Hakina tofauti na chupi. Kanga iliyokuwa inanisitiri ilikuwa imedondoka huko ndani.
Dereva teksi alinisubiri. Nikarejea nikiwa nimeegesha kanga kiunoni.
Nina mgonjwa!! Ni mume wangu. Ameanguka!!! Nilimsihi huku nikimvuta. Akanifuata. Tulipofika ndani bado John alikuwa ametulia tuli vilevile.
"Ameanguka!!." Nilijibu bila kuulizwa. Dereva akafanya jitihada za kumnyanyua John. Wapi haikuwezekana. Kila aliposhikwa ili anyanyuliwe alilegea na kuangukia upande mwingine.
Mimi nilikuwa mtazamaji na nilikuwa namuogopa sana John.
"Hebu ngoja nakuja!!!." Aliniaga dereva. Nikaamini anaenda kuleta msaada zaidi. Nikangoja kwa muda fulani dereva hakurudi!! Nilipotoka nje hapakuwa na dereva wala teksi.
Nilitamani kupiga kelele. Nikahaha huku na huko. Baada ya robo saa nikaona teksi. Ilikuwa inakuja pale kwangu. Iliposimama alikuwa ni yule dereva. Nyuma yake ikafuatia Ambulance.
Wakashuka wataalamu. Wakamtwaa John asiyejitambua.
Bahati nzuri walikuwa wananitambua. Ukarimu ukaongezeka maradufu.
John akafikishwa hospitali. Agha Khan.


Hakuwa amepasuka sana. Ulikuwa ni mpasuko wa kawaida. Akashonwa. Lakini akatakiwa kupumzika. Fahamu zilimrejea baadaye. Hakuwa msumbufu, alielewa upesi nini kinachoendelea.
Siku iliyofuata ndio siku ambayo John alitakiwa kutoka.
Nililazimika kurejea nyumbani kuchukua pesa kwa ajili ya malipo.
Nikiwa katika teksi, niliwaza juu ya kile kitambulisho. Nikahisi kitaniletea matatizo iwapo nitaendelea kukishikilia, tayari kilitaka kuutwaa uhai wa John. Sasa kitazua mengine.
Sasa nimpatie ama vipi? Nilijiuliza. Sikupata majibu.
Ile ndoto ya muuaji anadondosha kitambulisho ilikuwa inanikera maana haikutaka kufutika kabisa. Haikuwa ndoto kama ndoto nyingine maana sasa niliiona sura ya muuaji. Muuaji alikuwa John.
Nguvu ya penzi lake ikanikwamisha kumwambia mtu yeyote ukweli huu. Hata yeye pia sikumwambia.
"Hichi kitambulisho simpatii." Niliamua kusimamia upande huo.


Wazo la kukitia moto lilikuja baada ya kuwa nimefika nyumbani. Dereva teksi alibaki nje akinisubiri.
Nilikiendea kile kitambulisho nikatoka na mafuta ya taa na kiberiti.
Dakika tano baadaye, moshi ulikuwa ukipepea juu, kitambulisho kilikuwa kinateketea. Sikuondoka hadi pale nilipohakikisha natazama na majivu mbele yangu.
Hata hayo majivu, niliyakusanya nayo nikayafukia na mchanga.
Rasmi nikawa nimekizika kitambulisho!!!
Kitambulisho cha muuaji.
Baada ya hapo nilifanya usafi kidogo kuondoa zile damu katika marumaru.


Nikiwa ndani ta gari kurudi hospitali walau nilijisikia kuwa nimeutua mzigo mkubwa uliokuwa unanielemea. Mzigo wa kitambulisho.
Nilifanya malipo kisha teksi ileile ikaturudisha nyumbani. Mimi na John. Sasa alikuwa anajitambua kabisa. Alitakiwa kupumzika. Na hicho ndicho nilichofanya baada ya kufika nyumbani. Nikamwongoza hadi chumbani akaenda kulala.
Mimi nikarejea katika usafi mkubwa sasa sehemu mbalimbali katika nyumba. Redio ilikuwa ikiniliwazana muziki mkubwa niliojaribu kuuimba kwa kukoseakosea.
Na ni redio hiyo hiyo iliyoniziba masikio nisiweze kumsikia mtu amliyeingia ndani bila mimi kujua. Alama za matope katika marumaru zilinishangaza na kujiuliza yametoka wapi.
Hakungoja niumize akili yangu sana akanijibu.
"Haujambo binti."
Sikumwambia chochote, nikawa namshangaa bado. Akatabasamu.
"Haujambo!!!." Akanisalimia tena, sasa alikuwa analazimisha nijibu.,
"We ni nani katika nyumba yangu?." Nilimuuliza.
"Osmani kwani vipi."
Osmani!! Nikaliweka jina katika kumbukumbu kama niliwahi kukutana nalo hapo kabla. Yes!! Niliwahi kukutana nalo. Hata pale chuo tulisoma na akina Osman, wengi tu. Lakini huyu ni Osmani yupi. Nikaendelea kufikiria. Akatabasamu tena kama vile anaisoma akili yangu. Tabasamu lile likanisogeza kwenye jibu, niliwahi kuliona tabasamu hili. Ndotoni!! Hapana.
Hoteli, na nilikuwa nimelewa!!! Ndio siku hiyo nililiona.
Si hapo tu, na siku nyingine tena. Lini?
Huyu alikuwa ni dereva wa teksi aliyekuwa nami siku ya sakata la kitambulisho. Ni huyu aliyenikumbusha kuwa nimedondosha kitambulisho.
"Unataka nini katika nyumba yangu?." Nilimuuliza nikiwa na hofu.
Akatabasamu tena.
"Nina mazungumzo na wewe."
"Nitakupigia kelele za mwizi naomba utoke ndani ya nyumba yangu." Sasa nilifoka. Nikiwa nimesimama wima. Lakini dhahiri nilikuwa katika kutetemeka.
Akatabasamu kama kawaida yake. "Kweli unataka niondoke au unatania. Halafu nirudi saa ngapi. Au usiku ndio itakuwa vyema?." Aliniuliza kwa utulivu kama vile nilikuwa nampa ushirikiano mkubwa kabisa.
Sikumjibu!! Midomo ilikuwa inatetemeka. Sasa wazo la imani za kishirikina likanitawala. Hapa kuna namna.
Hapa kuna namna kweli mamaaa weeeee!!! Nilipiga kelele kubwa, kelele haswa. Yule aliyejiita Osman alikuwa amepotea mbele yangu. Alichoacha ni matope yale aliyoingia nayo.
Riadha kubwa kuelekea chumbani. Mlango ulikuwa umeegeshwa nikasukuma. Nikamrukia John kitandani nikamkumbatia kama vile tunagombana. Naye akiwa katika usingizi wake akatoa yowe kubwa la hofu. Akanisukuma huko. Nikamrukia tena. Hadi alipokuwa sawa ndipo aliniuliza kulikoni.
Limtu John, limtu!! Nililia.
John akanituliza akanishawishi kwamba zile ni ndoto za mchana. Wala sikupoteza muda kukubaliana naye. Ile haikuwa ndoto.
Amesema anarudi baadaye John. Nilimkumbusha.
"Atanikuta mimi hapa na atakoma kuingia katika nyumba hii usiogope." Aliongea kiujasiri John. Mimi nimemkumbatia bado.
Sikumueleza lolote juu ya huyo Osman. Kwamba niliwahi kukutana naye hotelini nikiwa nimelewa na pia aliwahi kunipatia kitambulisho ambacho kimepotea Iringa.
Niliogopa sana kuzua mengine.
Nikajikunyata na siri yangu.


Nilikuwa ninaenda na John kila hatua. Siku hiyo. Iwe jikoni, bafuni, na popote pale. Sikutaka kumwachia. Masaa yakahesabika na uoga ukaanza kukimbia.
Usiku ukafika. Bado ni mimi na John. John mara nyingi alikuwa ananicheka. Alishangazwa na uoga wangu.
Laiti kama angezijua baadhi ya ndoto nilizowahi kuota huenda naye angeogopa ten asana tu!!!.


Hii sasa haikuwa ndoto.
Nilitamani kubaki kumkumbatia John lakini. Nimuheshimu nani sasa John ambaye hata nyumbani sijamtambulisha kama mchumba ama mwalimu Nchimbi. Mama yangu mzazi aliyeniagiza maji ya kunywa. Nikamtazama John nikatamani kumtukana kwa kusababisha nichelewe kuitikia wito. Nikamsukuma huko. Nikajitoa mikononi mwake.
Nikamsonya!! Nikavaa kanga yangu nikafungua mlango nikatoka.
Nikaenda hadi lilipo jokofu, nikachukua maji yaliyokuwa katika kopo dogo. Nikachukua na kikombe nikajongea sebuleni.
Hapo mama atagomba kweli!!! Nilijishauri.
Sasa nilikuwa sebuleni. Mama hayupo.
Mwalimu Nchimbi naye kwa kununa. Hapo keshanuna huyo.
Nikataka kwenda kumuangaza nje. Lakini sikuona maana hiyo nikataka kumuita, mdomo ukawa mzito sana. Nikageuka huku na huko. Hola!! Nikageuka tena. Hakuna kitu.
Nikajisonya!! Kisha nikaguna mwenyewe kuwa ninamtafuta mtu gizani.
Mpuuzi kweli mimi!!! Nikasogea ukutani nikaanza kupapasa. Nikakipata kiwashio, nikabonyeza. Waaa!! Pakapendeza.
Nikageuka. Waaaa!!! Mdomo wazi, mtu anakula chakula.
Pwaaaa!! Nikaachia kikopo na glasi.
Osmani!!!
Osmani anakula chakula nilichopika mimi.
"Kaa hapo sahivi jamaa si amelala au." Aliniambia kwa sauti isiyosikika vizuri, alikuwa na pande la nyama mdomoni.
Puuuu!! Nikaanguka. Lakini fahamu zipo pamoja nami. Namtazama Osmani.


***OSMANI ni nani katika simulizi hii ya kushangaza….simulizi iliyoanzishwa na kukutana na mwanaume facebook…kanitajirisha sasa nipo katika mabalaa.



culbby mlyn Analyse princetx slim5 MUSSOLIN ram Angelicious showtie Ngoami amina mabata Moderator binti kiziwi Nicas Mtei
 
SITAISAHAU facebook
MTUNZI: Emmy John P.




SEHEMU YA KUMI NA MOJA




ILIPOISHIA


Nikataka kwenda kumuangaza nje. Lakini sikuona maana hiyo nikataka kumuita, mdomo ukawa mzito sana. Nikageuka huku na huko. Hola!! Nikageuka tena. Hakuna kitu.
Nikajisonya!! Kisha nikaguna mwenyewe kuwa ninamtafuta mtu gizani.
Mpuuzi kweli mimi!!! Nikasogea ukutani nikaanza kupapasa. Nikakipata kiwashio, nikabonyeza. Waaa!! Pakapendeza.
Nikageuka. Waaaa!!! Mdomo wazi, mtu anakula chakula.
Pwaaaa!! Nikaachia kikopo na glasi.
Osmani!!!
Osmani anakula chakula nilichopika mimi.
"Kaa hapo sahivi jamaa si amelala au." Aliniambia kwa sauti isiyosikika vizuri, alikuwa na pande la nyama mdomoni.
Puuuu!! Nikaanguka. Lakini fahamu zipo pamoja nami. Namtazama Osmani.
***OSMANI ni nani katika simulizi hii ya kushangaza….simulizi iliyoanzishwa na kukutana na mwanaume facebook…kanitajirisha sasa nipo katika mabalaa.


ENDELEA.


"John!!!! John!!!" Nilianza kuita kwa sauti ya juu sana. Osman alinitazama akacheka huku akijiziba mdomo. Nikaita tena. Hakuna John aliyetokea kunisaidia.
"Amelala wewe acha kelele." Alinionya Osman ambaye sasa alikuwa amemaliza kula na alikuwa anakunywa maji. Nikamshangaa. Alikuwa ananijibu bila wasiwasi wowote.
"Unajua nini Isabela. Tulia tuzungumze, mbona haya mambo madogo tu!!." Aliendelea kuzungumza Osmani. Kidogo nikatulia sasa, akafanya tabasamu kisha akaendelea kuongea.
"Nimefuata kitu kimoja tu hapa!! Kimoja tu."
"Nini?." Niliweza kumuuliza sasa. Nikijilazimisha kuwa jasiri.
"Kitambulisho changu." Alinieleza huku akiwa amenikazia macho. Sauti yake ilisikika vyema kabisa. Hakuwa katika kutania hata kidogo.
"Kitambulisho? Kitambulisho gani?." Nilihoji. Bado nilikuwa chini.
"Kile nilichokupa siku ile. Pale wapi sijui. Unapajua wewe."
"Sina kitambulisho cha mtu." Nilijibu kwa jeuri.
Kama vile jibu lile lilikuwa sawa na kumtukana aliruka akanifikia, kiganja chake kikanyooka akanitandika kofi moja. Maumivu yakapenya hadi mahali machozi yalipojihifadhi, yakatoka kwa fujo huku kilio nacho kikisindikiza.
"Sasa nadhani unaweza kuniambia. Kitambulisho kipo wapi."
"Nilikichoma moto." Nilijibu huku kigugumizi kikinitawala na kilio cha kwikwi.
Yule bwana akakodoa macho baada ya kuisikia taarifa hiyo.
"Umefanyaje?" aliniuliza, sikumjibu. Nilikua natetemeka sana, nilianza kumuogopa sana Osmani, kwanza niliwaza kile kitambulisho ni cha John iweje aseme chake? na kwanini siku ile alinipa akasema nilikidondosha? Mhh!! Ushirikina!! Nilianza kuamini kwenye imani hizo ambazo nilikuwa siziamini kabisa hapo kabla.
Wanafunzi wa SAUT wanaanza kuniroga, wananionea wivu!! nilihisi
" Isabella Isabella!!alinishtua John kutoka kwenye mawazo niliyokua nayo, nilipoangalia kwenye kiti alipo kaa Osmani nikapigwa na butwaa! Osman hakuwepo, Kheeee!! Nikashangaa, John akafikiri nimemuitikia yeye akatoka kutoka kwenye mlango wa chumbani alikosimama akanifuata. Uso wake ulikuwa umetawaliwa na uzembe wa usingizini. Bila shaka alikuwa ametoka kuamka.
"Vipi baby mbona upo mezani? nilishangaa chumbani sikuoni, chooni haukuwepo kulikoni mpenzi au njaa"? Aliniuliza John kwa sauti ya kukwaruza kwaruza. Bado nilikuwa nimekaa chini palepale nilipoanguka baada ya kumshuhudia Osmani akiwa ndani ya chumba changu. Nilishindwa nianze kumjibu vipi John.
Mdomo ulikuwa mzito. Pepo la usingizi lililokuwa linamkabili John lilizidi kutwaa nafasi. Akaonekana kushindwa kuvumilia. Akajivutavuta kuelekea chumbani. Mh!! Nibaki peke yangu hapana!!! Nilikata shauri. Hata taa sikukumbuka kuzima nikatimua mbio. Nikamfuata John. Sasa nilikuwa katika wasiwasi mkubwa hii haikuwa ndoto tena!!!
Nilichokiona ni kweli kilikuwa kimetokea.
Nilifika chumbani na kumkuta John naye akimalizia kujifunika shuka. Nikaingia kwenye shuka kwa fujo. Hakuligundua hili vurumai labda kwa sababu ya usingizi mzito. Nikamkumbatia John huku nikitetemeka.
Hayawi hayawi hatimaye yakawa!! Asubuhi ikafika.
John wangu akaamka wa kwanza. Kuamka kwake kukanifanya na mimi kuukatisha usingizi wangu usiokuwa na ladha kabisa.
"Hivi jana ilikuwa ndoto eeh!!." Alianzisha mazungumzo John.
"Umeamkaje mpenzi jamani." Nikamkatisha kwa salamu, maana hatukuwa tumesalimiana. Akanijibu kisha akaendelea kuzungumza.
"Jana si nikaota aisee. Dah!! Ndoto nyingine nazo!! Ila kuota pesa ni dalili za utajiri."
"Ndoto gani tena. Nikamuuliza."
"Eti amekuja mgeni sijui ilikuwa nyumba gani. Umezungumza naye, alipotoka eti akakuachia wewe Cheque mezani sijui milioni ngapi huko. Nilipotokea si wivu ukawa umenizidi. Nikawa mkali. Akawa kama anahairisha kukupatia. Mi nikaondoka, baadaye nikawa nachungulia mh!! Akaiweka sijui chini ya sahani ile. Ulipotoka kumsindikiza nikawahi kufunua nikakuta amekuandikia kiujumbe hata sikukielewa. Sasa nikawa nakusubiri unieleze yule ni nani. Mara kuku wako haoo wakawika kumekucha tayari!!!" Alimalizia kwa kicheko kirefu John. Nami nikaungana naye. Tukacheka.
"Una wivu we mwanaume!!." Nilimweleza.
"Ah!! Ndoto tu hizo." Alifunga mjadala.


Wakati John anaingia kuoga, mimi niliamka na kuanza usafi wa hapa na pale. Nikiisaili nyumba yangu. Sasa nilikuwa sebuleni. Nilipofika pale palikuwa kawaida tu!!
Hivi kumbe jana nilikuwa naota!! Nilijisemea.
Nikaanza kutoa vyombo mezani. Tayari kwa kuviosha na ambavyo havijatumika nivirudishe mahala pake. Ni hapo ndipo nilipopatwa na mshtuko mwingine mkubwa. Chini ya sahani moja palikuwa na karatasi. Karatasi ya rangi ya kijani kibichi. Hili jani ama karatasi? Nilijiuliza. Nikajikaza nikausogeza mkono nikalishika.
Lilikuwa karatasi!! Nikalinyanyua kwa uoga mkubwa. Bado liliendelea kuwa karatasi. Mkono wa pili nao ukajisogeza ukalipakata.
Kisha nikaligeuza.
Maandishi!!! Ya rangi nyeupe. Kiswahili sanifu, maneno machache.
AFE AMA UKUBALIANE NAMI.
Nani sasa? Nikajiuliza.
UTAMFAHAMU HIVI KARIBUNI.. Maandishi yale yalimalizia kama yanayojibu swali langu. Mwisho zikawekwa alama ambazo nilihisi kuwa ni namba za simu. +666666666. Simu ya wapi hii!! Nilitafakari.
Nikahisi wazimu unataka kunipanda. Akili zikasogeleana niliposikia John akiufunga mlango wa bafuni. Nikatwaa kile kikaratasi nikakificha kabatini.
Sikutaka John agundue kitu chochote. Maana kugundua kwake kungesababisha nimueleze pia juu ya kitambulisho, pia juu ya mauaji aliyoyafanya ndotoni na sasa yametokea kweli. Haukuwa wakati muafaka wa kumueleza.


******


Jina langu Isabella lilizidi kukua katika chuo cha mtakatifu Augustino, wasichana wengi walitamani sana wawe kama mimi maana hakuna kitu ambacho nilikua sina, takataka zote za urembo nilikua nazo, cha ajabu mimi Isabella sikuonekana kuwa karibu na msichana yeyote yule, hata rafiki yangu Happy nilimsahau, hela kitu kingine bwana nilisahau mema yote aliyonitendea Happy maana maisha yalivyokua yananipiga mtu wa kwanza kumfuata alikua yeye lakini kwa wakati ule nilimsahau kabisa
Mtu wa jirani yangu alikua John nilisahau kabisa kuwa John aliniacha kwa ajili ya umasikini wangu, sikufikiria kabisa kuwa anaweza kuwa yupo nami kisa ya pesa nilizokua nazimiliki,pesa za kutotolea jasho zaidi ya kuwaelimisha tu watu kidogo. kweli mapenzi ni kipofu


****


Mama weeeeeeeeeeee!!!nilishtuka kutoka kwenye ndoto mbaya, ndoto iliyonitoa jasho jingi nililowa utafikiri nilijimwagia maji, Niliota nimeenda kwetu Makambako, siku hiyo tulienda kupamba ukumbi wa sherehe na mama yangu Mwalimu Nchimbi, tulimaliza saa tano usiku, hatukupata gari la kuturudisha nyumbani tukaanza kutembea kwa mguu, mara tukashangaa nyuma vijana wawili wanatukimbiza. Tuliamini kuwa walikuwa vibaka. Mama akaanza kukimbia na mimi nikafuata nyuma huku tukipiga makelele ya kuomba msaada, hatukupata msaada tukazidi kukimbia kwa juhudi zote na sasa kila mmoja akaanza kuchoka. Mama akasema maneno fulani ya kukata tamaa huku akimkabidhi Mungu madaraka ya kuamua kitakachotokea kwetu. Mimi sikuwa na neno la kuongezea nikiwa nimekata tamaa niligeuka nyuma kutazama vijana haoa watatuua kwa silaha gani. Badala ya kutilia maanani silaha zao kali walizobeba, macho yangu yakatua kwenye sura zao. Osmani!! Alikuwa anatabasamu. John!! Yeye alikuwa amekunja sura kwa ghadhabu. John wangu!!
Niliendelea kutulia nikitegemea maswali kutoka kwa viumbe hawa wasioonyesha huruma hata kidogo. Sikuulizwa swali.
Mara wakagawana majukumu. John akamwendea mama na Osmani akanifata mimi. Alikuwa ameshikilia kitu mfano wa mkia, aliponifikia akanitandika nao mikononi. Maumivu yakapenya nikatokwa na yowe kubwa sana nikaanza kugalagala. Akaniacha pale akamfuata mama. Wakasaidiana na John kumnyanyua mama halafu wakaanza kukimbia naye huku wakimburuza. Nilipiga kelele nikiwasihi wamuache mama yangu. Lakini hakuna walichobadilisha walizidi kukimbilia na kupotelea gizani. Nilipiga mayowe sana lakini hakutokea mtu wa kunisaidia. Nilipoanza kujigalagaza kwa kukata tamaa ndipo nikakutana na ardhi ya ajabu, ardhi inayonesanesa. He!! Ardhi ya wapi hii? Nilijiuliza huku nikijilazimisha kufumbua macho yangu, macho yalikuwa mazito sana kufumbuka. Nikajilazimisha hadi yakafumbuka. Nikakutana na giza nene, nikaanza kupapasa huku na huko, nikakutana na vitu vingine viwili vinabonyea nilipojilazimisha zaidi kuvitazama ndipo nikakutana na mito miwili katika kitanda changu. Na ile ardhi ndio hichi kitanda changu cha sita kwa sita. Ndoto!!!
Nikawasha taa lakini nikahisi maumivu makali katika mikono yangu, Kheee!nikashtuka kukuta mikono yangu imevimba na ina alama ya kama michirizi hivi, hofu ikanitanda mhh!! ina maana ilikua ya kweli ama? Kama ni kweli kwa hiyo John amempeleka wapi mama yangu? Wamempeleka wapi mwalimu Nchimbi!! Nikaendelea kutahamaki. Hali hii sasa ilikuwa ya hatari kupita zote. Gusa popote katika maisha yangu ila chunga usimguse mama yangu.
Kama hii ni kweli John lazima anieleze ni wapi wamempeleka!! Nilijiapiza.
Uwiii!!! simu yangu iko wapi nimpigie mama kama yupo salama, nilijisemesha mwenyewe huku nikiomba kisiwe kimetokea chochote kama ilivyo kwenye ndoto, nikapata simu yangu nikajaribu kumpigia hapatikani!! Nikaogopa kukubaliana na ukweli huo.
Mungu wangu mama hapatikani ana nini jamani? nilijiuliza hivyo huku nikisahau kuwa huo ulikua usiku na inawezekana akawa kazima simu..ilikua kama saa tisa za usiku..nikampigia baba naye akawa hapatikani, hofu ikanizidi nilitamani nipae nifike nyumbani nijue nini kimejili, lakini huo uwezo sikua nao..ghafla nikapitiwa na usingizi.
Bila kujua hatma ya mama!!!


Nilishtuka kutoka usingizini baada ya simu yangu kuita kwa mda mrefu, kuangalia jina ni la mdogo wangu, usingizi wote ukaniisha nikakumbuka ile ndoto ya usiku, hofu ikanitanda nikawaza au mdogo wangu alikua ananipigia kunipa habari za msiba wa mama? mara simu ikakatika.
Nikampigia mdogo wangu!!! Nijue kulikoni, wakati huo natetemeka mwili mzima. Jasho likinitoka. Sikutaka kuamini hii ndoto.
Kwa hili nilichanganyikiwa kuliko vipindi vyote nilivyowahi kuchanganyikiwa!!


*Tumepafikia patamu, Isabella anaapa kuwa kama John amemgusa mama yake lazima adili naye kikamilifu.


Siri imekaribia kufichuka. Unahisi nini kitatokea........
 
mama yake isabella atakuw amekufa na john anamtihan kw isabella mana ndio anamhisi amemuua mama yake.
 
Back
Top Bottom