RIWAYA: Siku ya graduation

RIWAYA: Siku ya graduation

Casuist

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2014
Posts
1,189
Reaction score
2,971
RIWAYA: SIKU YA GRADUATION
MTUNZI: MAUNDU MWINGIZI



SEHEMU YA KWANZA

"Yaani kweli RAMLA Umeamua kunitenda kiasi hiki!!, pamoja na mapenzi yote niliyokupa lakini umeamua kunisaliti!, nimepoteza pesa zangu nyingi kukusomesha chuo nikiamini we ndo utakua mama wa Wanangu Leo wema wangu umegeuka mkuki wa sumu moyoni mwangu, Ramla Why? Why?!!" Niliendelea kulalama peke yangu huku nikilia kwa uchungu, shuka yote ikiwa imeloana jasho na machozi pale katika kitanda changu..
"Kitendo ulichonifanyia Ramla kinaniua ndani kwa ndani, huu ni zaidi ya ukatili yaani umesahau ahadi zetu zote tulizowekeana!!!.. aaaah" niliendelea kujisemea peke yangu kama Mwehu.


Taarifa hizi za uchungu kua Mchumba wangu Ramla ananisaliti kwa kutoka na na Kigogo maarufu jijini Dar Es Salaam nilizoambiwa na Rafiki yangu Mwl HONDE ziliniumiza sana sikua na sababu ya kupinga sana kwakua nilimuamini sana Rafiki yangu alienipa Ukweli wa Tukio hilo, kwanza Rafiki yangu huyu nimejuana nae siku nyingi tangu nikiwa pale chuo kikuu cha Dar Es Salaam pia Rafiki yangu huyu kwa sasa ni Muhadhiri katika chuo ambacho anasoma Mchumba wangu Ramla hivyo alichoniambia ana uhakika nacho kwa asilimia zote kwa kua nay eye yuko hapo hapo chuoni


Kilichoniuma zaidi ni pale nilipotajiwa na jina la huyo kigogo, Kwanza ni Tajiri, Mfanyabiashara maarufu, anamiliki miradi mingi, ana majumba na magari ya kifahari kila kona, anamiliki Cassino kubwa na maarufu kuliko zote jijini Dar, anahusishwa pia na Biashara haramu ya madawa ya kulevya pamoja na matukio kadhaa ya ujambazi wa magari na nyara za serikali, huyu si mwingine na PABLO MWAKI.

"Hata nikitaka kumfanyizia ubaya huyu Tajiri sitaweza.." Niliendelea kulia kwa uchungu. Basi nikajikaza na kuinuka pale kitandani na kwenda kuoga japo baada ya saa zima nikatoka Bafuni bila ya kujimwagia hata kopo la maji, nilikua nimesimama tu kichwa kikiwa na zaidi ya Kilo mia za mawazo.. nikarudi mpaka chumbani na kupanda kitandani kulala japo usingizi wote uliniruka, Usiku kucha niliwaza na kuwazua nifanye jambo gani ili nimrejeshe mchumba wangu mikononi mwangu na hatimae nikabakiwa na maamuzi ya kupambana na Pablo Mwaki bila ya kuogopa utajiri na ujambazi wake.
*****


Karibu na Posta mpya jijini Dar es salaam kuna Jengo kubwa la kibiashara lililoandikwa MIKINDA BUSSINESS CENTER, Ndani ya Jengo hilo mashuhuri kuna kila aina ya Biashara zinaendelea humo, Spermarket, Slot machine, Bureau De Change, Branch za Benki kadhaa, na pia ndani ya jengo hilo pia kuna Cassino mashuhuri ya kuuza makahaba, mashoga, na wasagaji, kila utakachokihitaji utakapata ndani ya jingo hilo.. Naam mjengo huo na vyote vilivyomo ni mali ya PABLO MWAKI

Pablo Mwaki na Mzee wa makamo japo ukimuona huwezi kudhanai kama ana umri mkubwa kutokana na mazoezi, maisha bora na jinsi tu anavyojiweka, Ni Mweupe, Si mnene wali si mwembamba, anapendelea zaidi kunyoa Kipara.

Mbali na Mjengo huo PABLO MWAKI pia ana miliki miradi mingine kibao zikiwemo kampuni za uchimbaji madini, Kampuni za usafiri wa majini na Angani, pia ana hisa kwenye baadhi ya makampuni makubwa makubwa,Si jambo la ajabu ndani ya Dar es Salaam nyumba kadhaa na maofisi yakihusishwa kumilikiwa na tajiri huyu, Wapo waliomsujudia Pablo kutokana na utajiri wake lakini pia wapo waliomchukia na kumlaani kutokana na kuwaharibia vijana wao kwa kuwatumia katika biashara zake haramu.

Pablo Mwaki alishawahi kuhukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumteka na kumuua kijana Samson Shirima, mfanyabiashara wa madini na kumpora pesa nyingi, Lakini alitumikia kifungo hicho kwa takriban miaka mitano tu kasha akakata rufaa na kushinda kesi hiyo ndipo aliporudi uraiani na kuanza kufanya biashara zake na ghafla kua tajiri mkubwa.
*****

Siku iliyofuata niliwasili ofisini na kuomba Ruhusa kwa Boss wangu Mr Jimmy nlimueleza kua naumwa sana tumbo, japo si kweli. Lengo langu lilikua ni kwenda kuonana na Mwl Honde ambae ni muhadhiri chuoni kwa kina Ramla na ndie alienipa ukweli wa kila kinachoendelea kati ya Ramla na Pablo.


Kila nilipomuangalia Mr Jimmy ambae ni meneja katika kampuni yetu ya SAJAM MARINE Ltd nilizidi kuumia nafsi kwakua mbali ya kua Boss wangu pia ni Mume wa mama'yake mdogo na Mchumba wangu Ramla Aliechangia mama tu na mama yake na Ramla. Nilopotoka tu ofisini nikaenda moja kwa moja mpaka Chuo cha usimamizi wa fedha(I.F.M) kwa Mwl Honde nilipofika Honde akanipokea vizuri ila hatukua katika ule ucheshi na uchangamfu wetu, nilishindwa kabisa kujizuia na kujikuta nikionesha kabisa hali isiyo ya kawaida usoni mwangu, Baada ya salamu mazungumzo yakendelea

"Nisikilize Naufal mimi nakushauri kama mtu wako wa karibu, kwakua namfahamu vizuri Pablo naamini akikujua tu utakua katika hali ya hatari"
"Kwa hiyo wewe unataka nifanyeje?"
"ukubali matokeo na uachie ngazi, Pablo humuwezi, atakupoteza"
"Yaani Honde badala ya kunishauri tufanyeje ili tuwaachanishe we unataka niachane na Ramla!!"
"Kaa ukijua Pablo Mwaki kaishatangaza Ndoa , na Ramla amelipokea kwa furaha suala hilo, sasa kama unataka kuiweka Roho yako Rehani Endelea"
"Hivi Honde una akili timamu kweli wewe?! unajua me na Ramla tumetoka wapi?, unataka nikubali kirahisi rahisi kuibiwa na ----- huyo kisa ni tajiri, Kwanza wataoana vipi wakati Ramla ni Muislam na huyo Mpumbavu Mwaki ni Mkristo"
"Upo dunia gani kaka? Ramla ameshabadili dini na sasa ni Mkristo"

"Nilichogundua na wewe ni Msaliti tu, utakua umetumwa tu, Sio bure!" nikanyanyuka kwa hasira nikaanza kuondoka bila hata ya kuaga, nilimsikia Honde akijaribu kuniita ila hata sikujisumbua kugeuka nikaenda mpaka barabarani upande wa pili ulipo ukumbi wa Makumbusho ya Taifa nikachukua Boda boda na kutokomea zangu.


Nilipofika Nyumbani nikajipumzisha kwenye kochi huku nikiwa na mawazo mapya kichwa,
"Hivi inakuaje rafiki yangu wa karibu kama Honde anashabikia tukio hili? Tena bila hata ya aibu anasema nimuache Ramla, nimeanza kumshtukia, Haiwezekani, huyu itakua nae katumwa na huyu mjinga mwenzao ili anishawishi tu nimuache Ramla wangu au pengine ni yeye ndie anaemtaka" niliendelea kujifariji huku sasa lawama na hofu zangu zote zikawa ni kwa Honde sasa.

Nikainuka pale kwenye kochi nikaenda bafuni kuoga, nikiwa bafuni nilsikia simu yangu ikiita nilipokwenda kuiangalia alikua ni Honde akinipigia simu nikaiangalia simu ikiita bila kuipokea kisha nikarudi bafuni huku nikijisemea mwenyewe "Akkkh hivi huyu mjinga anafikiri mie hayawani kama yeye" nikiwa bafuni naendelea kuoga simu yangu iliita tena ila wala sikujisumbua kwenda kuiangalia nikijua atakua ni Honde tu huyo. Nilipomaliza kuoga nikaenda kuiangalia simu yangu, kumbe hakua Honde, alikua ni Ramla kipenzi cha moyo wangu, haraka nikajifuta maji mwilini kasha nikachukua simu yangu na kumpigia Ramla..
"Hellow" ilikua ni sauti nyororo ya Ramla
"Hi darl"
"Mzima mume wangu"
"Mie mzima wa afya, habari za chuo?"
"Nzuri tu, Mbona kimya sana tangu jana halafu na leo nimekuona umekuja chuo nikajua utanipigia simu tuonane lakini ukanichunia sio vizuri hivyo"
"Hapana sijakuchunia mpenzi wangu nilikua na haraka sana kuna Laptop yangu alikua nayo Mr Honde ndo nikawa nimeiijia kulikua na kazi ya muhimu sana ofisini"
"Ok Baby, kesho nitakuja kwangu nijipikie mwenyewe, nimechoka na haya mambo hostel kila siku chips tu" Tuliendelea kuzungumza kwa madaha kila mmoja akimhadaa mwenzie, mimi nilimhadaa kwa kujifanya kama hakuna tatizo lolote nililolisikia nae bila shaka alinihadaa mimi kwa kuniita majina mazuri ya baby, mume wangu, nk wakati alijua fika kua kwa sasa ni mali ya Pablo Mwaki.

Baada ya kukata simu ya RAMLA Nikajitupia kitandani nikiwa nimechoka Mwili mpaka akili, mawazo ya kila aina yakizunguka kichwani mwangu. Nilikua nusu naamini kua Ramla amenisaliti, hapo hapo nahisi kua Honde ndie anataka kutugombanisha, hapo hapo natamani nimtafute huyo Pablo Mwaki nimfanyie kitu kibaya japo haikua rahisi, ni matamanio tu yasiyowezekana waswahili wanasema Dua la Kuku.


Nikiwa pale kitandani nilisikia mlango wa Chumbani kwangu ukigongwa nikajinyanyua kwa uchovu mpaka mlangoni, nilipofungua mlango tu akaingia NTAHONDI msichana mrembo, mcheshi na mchangamfu, ni rafiki wa karibu sana na Mchumba wangu Ramla pia wanasoma wote chuoni,
"Karibu"

"Ahsante Shem"
"Mpaka nimeogopa mbona usiku? Kuna usalama kweli?"

"Hah ha usiku gani wa kutisha huu, au hautaki wageni shem?"
"Hapana sio kawaida yako, haya karibu uketi"

"Ok, ahsante" Baada ya kumkaribisha ntahondi nilirudi kwanza kuufunga mlango kasha nikaenda mpaka kwenye Friji ili nimuangalizie japo kinywaji lakini akaniwahi kwa kukataa

"Shem wala usihangaike na kinywaji, mie sio mkaaji, nataka tu tuongee haraka niondoke"
"Acha roho mbaya, hautaki hata kuniwekea Baraka ndani!!"

"Usijali nitakunywa hata siku nyingine" baada ya Ntahondi kukataa kinywaji nikarudi mpaka karibu ya kochi alilokua amekaa na mie nikakaa kwenye kiti cha uvivu, kasha Ntahondi akaanzisha mazungumzon nilijiweka sawasawa kupokea habari iliyoonekana kua ni nzito sana kwa jinsi alivyoonekana usoni Ntahondi.

"Kwanza kabisa naomba unisamehe kwa hili nitakalo kuambia kama nitakukwaza maana sisi binaadamu hatujakamilika, pili hata kama halitokufarahisha naomba libakie kua ndani ya moyo wako kwa kua lengo langu mimi ni kunusuru maisha yako naomba nawe uninusuru kwa kuificha siri hii hata kama hautoipenda" alikua akiongea huku akiniangalia usoni bila hata ya kukpepesa macho, Niliendelea kumsikiliza bila kuongeza neno.

"Kwa kifupi masha yako yako hatarini, muda wowote unaweza kuitwa kwa jina moja tu la Maiti" baada ya kuvuta pumzi akaendelea.

" Na anaekuangamiza na ku kuua ni Mchumba wako RAMLA"
"Ramla" kivipi aniue? Mbona sikuelewi?" nilishtushwa sana taarifa hii japo nilianza kuhisi kua huenda sasa huu ni muendelezo wa ile habari niliyopewa na Honde.

"Tulia na unisikilize kwa umakini, Ramla hivi sasa anakusaliti, amepata mwanaume mwingine anaetoka nae kimapenzi, mtu huyo anaitwa Pablo Mwaki, ni kigogo mmoja maarufu tu na kwasasa wanataka kufunga ndoa"
"Unauhakika Ntahondi?"
"Mpaka nimekuja hapa mimi sio mwehu, mimi nasoma na Ramla na ni rafiki yangu wa karibu, Lake langu na langu lake, kwa kifupi PABLO Ameshapewa taarifa zako kua wewe ndie mchumba wake na Ramla hivyo yupo kwenye mchakato wa kukusaka, akukamate hata ikiwezekana akuteke ili wao wawe huru na mapenzi yao na ndoa yao bia ya bughudha ya mtu yeyote" Ntahondi alisimama na kuniaga.

"Mimi naondoka, ila jitahidi kua makini na Ramla kwa usalama wako anaweza kutumiwa yeye ili wafanikishe mpango wao wa kukuteka"
"Aisee mbona kama nachanganyikiwa Ntahondi, yaani Ramla anaweza kufikia hatua hiyo?"
"Na kwa taarifa yako huyo Boss wako Mr Jimmy ni rafiki wa karibu sana na Pablo Mwaki na kwenye hiyo kampuni yenu

Mwaki ana hisa zake, na pia ujue kua Mke wa Jimmy ambae ni mama yake mdogo na Ramla ndie aliemshawishi Ramla akuache wewe ili awe na Pablo hivyo inawezekana hata huyo Jimmy anaujua mchezo mzima nae kua nae makini" Wakati hu tunaongea habari hizo tulikua tumeshanyanyuka kwenye kiti na tunatembea kidogo kidogo mpaka mlangoni ambako tulikua tumesimama na baada ya maelezo hayo Ntahondi alifungua mlango na kuondoka zake, niliufunga mlango nikarudi mpaka kitandani, nikiwa natetemeka wa hofu na uoga wa hali ya juu ulionivaa mwilini.
******

I T A E N D E L E A
Sukula kelcie culbby Ngoami
 
RIWAYA:SIKU YA GRADUATION
MTUNZI:MAUNDU MWINGIZI



SEHEMUYA PILI

Nilizidikuingiwa na hofu kubwa kufuatia tahadhari alizoniachia Ntahondi,chumba nilikiona kidogo utadhani nimo ndani ya yai, kila nilipojaribukujikazanakuutafuta usingizi ilishindikana, niliendelea kujilaza tu palekitandani na hatimae nilikuja kushtuka ilikua ni saa kumi na mbiliasubuhi, kilichonishtua ni mlio wa simu yangu, nikaamka na kuiangaliasimu yangu ili nijue nani anaenipigia simu asubuhi yote ile, Alikuani Jarufu, kaka yangu aishie mkoani Tabora
"Hallow"
"Ehhza asubuhi"
"Salamatu bro za huko?"
"Ahhnzuri kiasi, pole kwanza na matatizo yako"
"Ahsantenashukuru, mbona umesema nzuri kiasi kuna nini?"
"Mamayuko hoi huku, Presha imepanda hapa tuko Hospitalini Kitete"
"Heejamani, imekuaje?"
"Wesi umempigia na kumueleza hayo mambo ya huko kwako"
"Ndionilimpigia lakini….."
"Sasakwanini ulimpigia na unamjua jinsi alivyo na hamaki!?"
"Lakinimimi sikumpigia kwa nia mbaya, ilikua ni kumfahamisha tu hali ilivyohuku.."
"Sasamwenzio ulivyompigia tu akapandwa na jazba zake akajiandaa na hapohapo akaenda Rufita kwa mama Ramla"
"Jamanienhee ikawaje?"
"Nasikiaalivyofika tu wakaanza kutukanana sana almanusura washikane, nasikiawasamaria wema ndo wakawaamua. Kilichomzidisha hasira zaidi mamaNasikia huyo mama Ramla alikua akitoa maneno machafu sana kuhusuwewe, anasema tunamuonea wivu mwanae kwa kuolewa na Tajiri piaanasema kama mwanamke hakutaki tena ya nini kumng'ang'ania!!"

Yaanimaneno ya Jarufu yalizidi kuniumiza, kila nikikumbuka jinsi huyu Mamaalivyokua akiniheshimu na kunijali kipindi chote nilichokuanikimsomesha na kumuhudumia mwanae, Kumbe ilikua ni geresha tu sasaanamjali tena tajiri ambae hamjui hata kwa sura!! nikiwa badonimeshikilia simu yangu yangu sikioni, kaka alizidi kunivurugakichwa
"Baadaya mama kurudi nyumbani ghafla akaanza kuishiwa nguvu, mara akapotezafahamu nadhani itakua ni Presha, ndo hapa tupo Hospital" Baadaya kumaliza kuniambia maneno hayo alikata simu nikabaki nimeduwaakama Chizi, Siku hiyo kwangu ilikua mbaya iliyojaa hofu na simanzi,Hofu itokanayo na maelezo niliyopewa na Ntahondi kuhusu usalamawangu, nilikua na Simanzi iliyochagizwa na
hasiradhidi ya Ramla na mama yake Mzazi ambao wote wamekula fadhila
zanguza pesa na misaada kadhaa Lakini leo wananiona si chochote si
lolotena kuamua kushirikiana kunisaiti kinyama, Pia nilikua namuwazia mamayangu mzazi alieko Tabora akiwa hoi kitandani kwa ajili yangu. Basinikajiandaa haraka haraka na kwenda kazini, nilipofika kazininilianza kutekeleza majukumu yangu kama kawaida japo nilishangazwa nahali niliyomkuta nayo
Bosswangu Mr Jimmy a. hakua katika hali ya furaha wala uchangamfuniliozoea kumuona nao siku zote, nilianza kuhisi kua hali haikuashwari kabisa kwa maana huyu bwana mkubwa inasemekana ndie anaetumiwana PABLO Mwaki kumuunganishia kwa Ramla. hivyo inawezekana amegunduakua nimeshajua hila zake zote zinazoendelea. Lakini mimi sikujalinikaendelea na shughuli zangu kama kawaida

Nikiwanaendelea kuchapa kazi kwenye Computer yangu pale ofininilipokea
ujumbemfupi wa maandishi kutoka kwa Ntahondi akinilaumu "Nilikuombauwe na Subra pia uwe Msiri lakini sasa Umeshindwa" nikamjibu harakaharaka "Kwani kuna nini tena Ntahondi?"
"kwaniniumemueleza mama yako mambo haya?, Mama yako kaenda
nyumbanikwa Mama yake na Ramla wametukanana sana na sasa Imeshajulikana
kuawewe umegundua mpango wao, kwa sasa Mwaki anamtafuta anaeyevujishasiri hizi sasa UNATAKA NIUAWE?" Sikushtuka sana kwa kua tayarinilikua nimeshajua kua Mama alienda kwa Mama Ramla na
walilumbanasana ila sasa hofu yangu ikawa kwa usalama wa Ntahondi endapoatagundulika kua ndie anaenipa siri zao nyeti, nikiwa bado nawazajambo hili nikaanza kupata picha ya kwanini Mr Jimmy hakunichangamkiawakati naingia ofisini, kitu ambacho si kawaida yake

Niliendeleana kazi katika hali hofu kwa takribani wiki tatu mfululizo bila yakua na Mahusiano mazuri ya kimazungumzo na Boss wangu Mr Jimmy,haikunipa tabu kwa kua nilikua nimeshamjua Vema kua ni miongoni mwawatu hatari katika maisha yangu kwa sasa, Lakini pia katika kipindihiki chote sikuwasiliana na Ramla kitu ambacho si kawaida yetu japohali hii ilizidi kunithbitishia kua sasa taa ya hatari ilikuaimeshamulika. Ila nachoshukuru Mungu ni kua nimeendelea kupokeataarifa za kuimarika kwa hali ya Mama kule nyumbani, pia nami nimekuanikipokea massage za kunifariji na kunipa kuniliwaza kutoka kwa nduguzangu kutokana na matatizo haya, Pia niliendelea kupata taarifa zakiusalama kutoka kwa Ntohondi . japo kwa sasa haikua taarifa Nzitopengine hakua akipata taarifa kutokana umakini mpya kufuatia kuvujakwa siri zao, au pengine alizipata ila hakuniambia kwakua haniaminisana katika utunzaji wa siri hizo..

Sikumoja majira ya saa mbili kasoro(usiku) nilikua nimeenda nyumbani kwaMwl Honde katika maongezi yetu akijaribu kunishauri nini cha kufanyajapo mwanzo alipokua akinidokeza kuhusu
kinachoendeleakati ya Ramla na Pablo Mwaki nilikua nikimuona kama Mchonganishi naFatani wa Penzi letu lakini kwa sasa amekua ndo kimbilio langu,Tukiwa katikati ya mazungumzo Ghafla nilipokea ujumbe mfupi waMaandishi kutoka kwa Ntahondi akinitaka tuonane haraka sana maeneo yaLeaders Club, Ikanibidi sasa haraka haraka nisimame na kumuaga Hondeili nimuwahi Ntahond nikijua tu kuna taarifa za muhimu sananikazipate, nikaondoka moja kwa moja mpaka Leaders japo kulikua nafoleni ndefu ila kwa umahiri wa dereva boda boda niliekua nae ndaniya dk 20 tukawa tumewasili,
nilipofikanikaenda mpaka Kiwanjani pembeni ya Bendi ya Muziki iliyokuaikitumbuiza pale Leaders nikachukua kiti na kuagiza kinywaji, kishanikatoa simu yangu na kumpigia Ntahondi ili nimtaarifu kuanimeshafika, Nilipompigia akapokea na kusema "Nimeshakuona uliponakuja hapo hapo" kisha akakata simu

Baadaya muda kidogo akaja mpaka pale nilipo kisha akaketi na kunisalimu,nae akaagiza kinywaji chake kisha akaniambia kua tungeenda upande wapili kule wanapouza Nyama choma ili tuwe salama zaidi..
Tukaendaule upande wa pili na kisha tukaanza mazungumzo japo mie nikiwa namchecheto zaidi wa kutaka kujua kinachoendelea, nae Ntahondi bilaajizi akaanza kufunguka
"Mambovipi"
"Poatu za tangu jana?"
"Nzurihivyo hivyo, kwanza pole na Mchoko"
"Ahsante"
"Sasanimekuja kukuongezea mchoko mwingine," Maneno haya yalipenya sawiakatika masikio yangu nikawa namsikiliza kwa makini, kishaakaendelea
"Nihivi Mwaki sasa yuko serious anataka kumvisha pete ya uchumba Ramla,na Tendo hilo wamepanga kulifanya hadharani, itakua ni siku yaGraduation yetu, Wakati wa zawadi Mwaki amepanga kumpa Ramla zawadiya Gari ya kifahari na kisha baada ya hapo atamvisha na Pete yauchumba" Akashusha tena pumzi kabla ya kuendelea kufunguka
"Natayari sasa ameshaanza mchakato wa kukusaka ili usije ukaletausumbufu siku hiyo, na kama atakutia mikononi pengine ndo itakuamwisho wa maisha yako, hivyo kua makini ikiwezekana hata kazini kwasasa usiende maana Boss wako Mr Jimmy nae ni mwanamtandao, piaikiwezekana hata pale kwako uhame haraka na ukipata muda ukatoetaarifa Polisi kwa usalama wako" baada ya maelezo hayo mdadaakasimama kisha akaniaga na kunisisitiza niwe makini sana, Wakatitunaondoka akanikumbusha tena jambo jingine
"Piainabidi ubadili namba yako ya simu maana hawa jamaa wana mtandaomkubwa wasije wakatufuatilia wakagundua mambo yetu" tukaagana kishaNtahondi akaondoka zake, nilibaki namshangaa sana sikuamini kamamotto wa kike kama Yule angekua na ujasiri na uelewa wa mambo kwakiwango kile,
Naminikasimama na kuondoka mpaka kituo cha polisi cha Msimbazi ili kutoataarifa ya kila kinachoendelea japo nilikumbana na vikwazo vya hapana pale kutoka kwa ma askari wapenda rushwa ambao wanaijua nguvu yaPABLO MWAKI Lakini hatime nilifanikiwa kufungua kesi kisha nikarudimpaka kwangu nilipofika chumbani nikajilaza kidogo juu ya kochi ilinitafakari pa kwenda kulala tofauti pale Nyumbani kamaalivyonielekeza Ntahondi lakini hapo hapo usingiziukanipitia..
*****

Nikaamkana kwenda kuoga haraka kisha nikarui ndani kuvaa ili niende kwa MwlStephen Honde nikamueleze hali ilipofikia, Pia nikiwa na lengo lakwenda kukata tiketi ya Buss nirudi kwanza nyumbani Tabora nikatulizeakili ili nijipange kupambana na huyu fedhuli, nilipotoka kwangunikatembea mpaka barabarani, ikanibidi nikachukue Tax kiusalama maanasasa sikupaswa kuonekana kwakua tayari nilikua kwenye mtego wa Mwaki,nikamchukua Tax driver ambae hua ananibeba mara kwa mara nakumuelekeza anipeleke Stand ya Ubungo ili nikakate tiketi na kishaanipeleke IFM Kwa Mwl Stephen Honde tukiwa njiani dereva aliniombatupitie Shelly tukaweke mafuta, nikakubali, ila cha ajabu huyu derevaalikua akiendesha huku akiwa bussy na simu yake aki chart kituambacho nilishindwa kuvumulia ikabidi nimlalamikie nae akaniombaradhi, akaendelea kuendesha mpaka Shelly ya mafuta..

Baadaya kujaza mafuta akatoa pesa na kumlipa muhudumu pale shelly, ilakabla hatujaanza kuondoka wakatokea jamaa wawili, watanashati,wakamwambia dereva kua awapeleke Ubungo, dereva akawajibu kua tayariana abiria mwingine japo nae anaenda huko huko ngoja tumuombe kamaatakubali, aliponiomba nikaona acha tu nimsaidie kijana huyu aingizeriziki,nikawakubalia wakaingi ndani ya gari vijana wale kisha wakakaaseat za nyuma na tukaendelea na safari yetu tukiwa ndani ya garighafla huyu kijana aliekaa nyuma yangu nikasikia kanishika begani,nilipogeuka tu nikasikia nimepigwa na kitu kizito kichwani kablasijakaa sawa huyu mwingine aliekua nyuma ya dereva nae akanipigangumi nzito, basi ikawa ni kichapo juu kichapo mpaka nikawa nasikiakizunguzungu, mara mmoja akaniwahi mikono kisha huyu mwingineakanifunga kitambaa cheusi usoni, Wakati haya yakiendelea huyu Derevaalikua katulia kimya akiendelea kuendesha gari taratibu hapo ndonikajua kua alikua anajua kila kitu,

Nikiwanimefungwa kitambaa usoni nilimsikia Yule kijana aliekua nyuma yadereva akimuuliza dereva kua anaielewa vema njia waliyomuelekeza?Dereva nae akajibu kua anaijua vizuri hapo sasa nikajua tayarinimeingi mikononi mwa PABLO MWAKI, Gari ilikua ikitembea kwa kasihuku nikiwa sijui tunaelekea wapi, Nikawa katika majuto ya hali yajuu sana, Lengo langu kwenda Tabora sasa limekufa na hata Mwl Hondendo simuoni tena, Nilijua sasa Kifo kipo mlangoni, Gari ikiwainaendelea kuchuka kasi ghafla meseji ikaingia kwenye simu yangusikujua ni nani lakin, yule kijana aliekua nyuma yangu akaingizamkono kwenye mfuko wa wa suruali yangu na kuitoa simu yangu,Nikasikia akishangaa na kuniuliza
"Wembwa, huyu Ntahondi ndo nani?" nikajua tu itakua ni Ntahondindie amenitumia ujumbe, na kabla sijajibu chochote akaendeleakuongea
"Kumbehuyu ndie anaetoa siri zetu eeh?, tutamshughulikia" Nilizidikuchanganyikiwa na sikujua Ntahondi alikua ameniandikia ujumbe gani,japo mimi tayari nimeshakamatwa ila niliamini kua wa kuniokoa niNtahondi tu kwakua alikua akijua kila kinachoendelea hivyo kamaatawasiliana na watu wa kwetu akawapa maelekezo yote huenda wakamtianguvuni huyo Pablo na hatimae nikapatikana, lakini sasa naekashagunduliwa....

I T A E N D E L E A


culbby mlyn Analyse princetx slim5 MUSSOLIN ram Angelicious showtie Ngoami amina mabata binti kiziwi Nicas Mtei korino Sukula aniceth mzahula Khantwe kelcie chwechinyong ram tabibumtaratibu

 
Last edited by a moderator:
tokaaa na mahadith yenu amabyo huwa hamuyamalizii
 
Inaisha mkuu..

.....mimi nadhani prsp umeichukia riwaya kwa vile ulisoma kwa pupa au ulipapasa kwa macho tu!
kumbuka mpishi anayepika jikoni ndiye anayejua tabu ya moto ulivyomsumbua!
ni riwaya nzuri tu,
isome polepole utaielewa tu!
 
Dah!!uandishi wako ulikuwa nzuri sehemu ya kwanza sasa hii sehemu ya pili mkuu hutenganishi maneno!!!!Iko poa sana hii hadithi twende kazi mkuu sehemu ya tatu....
 
RIWAYA:SIKU YA GRADUATION
MTUNZI:MAUNDU MWINGIZI


SEHEMUYA TATU

Msafara uliendelea huku nikiwa nimefungwa kitambaa cheusi usoni, Majadiliano yaliyokua yakiendelea ndani ya Tax kati ya hawa maharamia na huyu dereva waTaxy aliashiria kua dereva huyu alikua amelipwa kwa ajili ya kufanikisha mpango wa kuniteka, iliniuma sana kwa jinsi nilivyomuamini kijana huyu leo kwa tamaa yake ya pesa tena pesa yenyewe itakua ni kidogo tundo ameamua kushiriki kitendo cha kunitoa uhai wangu. Sikuwa na la kufanya kabisa, Safari ikazidi kuchukua kasi Ilituchukua muda mrefu takribani saa moja na nusu hivi tukiwa njiani tu, mpaka hatimae tukafika Eneo lililokusudiwa

Gari yetu ilisimama kwa muda kama wa dk mbili kisha nikasikia Geti likifunguliwa na kisha gari ikaingia ndani baada ya gari kusimama walishuka vijana wale wawili na mmoja akafungua mlango wa mbele upande niliokua nimekaa mimi akanivuta kama kiroba nikajikuta nimeshuka kama mzigo mpaka chini kisha akanifungua kitambaa usoni. Nilijaribu kuangaza huku na kule lakini sikuelewa tuko wapi! ilikuani ndani ya Fance kubwa iliyozunguka Jengo kubwa sana chakavu mfano wa magodaun ya Tumbaku. Mule ndani kulikua na vijana wengine watatu,woteni warefu, wamejazia misuli yao vilivyo, wawili wametinga miwani myeusi, na mmoja akiwa hana miwani na kavaa Suti nyeusi. Walinichukua na kuniingiza ndani kabisa ya jengo hilo..

Mazingira ya ndani ya Jengo hilo yaliku ni ya kutisha sana maana kulikua na ukimya wa hali ya juu, pia hata hawa jamaa sura zao zilivyokaa kikatili ukiwaangalia tu utahisi harufu ya kifo, nilipo fikishwa mule ndani nikafungwa kamba mikono kisha wakanining'iniza juu mithili ya mbuzi anaesubiri kuchunwa ngozi kisha jamaa hawa wasio na huruma hata chembe walianza kunichapa mijeredi ya nguvu, nililia nakupiga kelele mpaka nikawa naishiwa nguvu,lakini kelele zangu hazikuwazuia hawa jamaa kuendelea kuniadhibu. mwili wote ulikua umevimba vimba kwa alama za Fimbo.. baada ya Muda akaja kijana mmoja akiwa ameshika Msumari uwa moto nadhani ndo ulikua umetoka jikoni, Naam ulikua umewiva kisawasawa akaja mpaka pale niliopokua nimetundikwa akaanza kufanya kama vile anachora maandishi kifuani kwangu, kwenye mapaja,na mgongoni nilisikia maumivu makali sana nililia kwa sauti mpaka nikajihisi sasa kupoteza fahamu..

Ndani ya dakika kama kumi na tano nilizofikishwa mule ndani nilikua nimeshaharibika mwili mzima kwa adhabu na mateso makali niliyokumbana nayo mule. wakati nikiendelea kupewa adhabu za kila aina ghafla akaja yule kijana aliekua amevaa suti, alikua kama amechanganyikiwa na jambo fulani;
"Jamani kuna hali ya hatari kidogo"
wale viajana wote wakamgeukia na kumsikiliza, kisha akaendelea
"Wakati akina Zungu wanamteka huyu Dogo, nasikia walianza kumpiga mule mule ndani ya Tax sasa kuna watu walishuhudia hilo tukio hivyo wamechukua namba ya Tax na wameenda kutoa taarifa Polisi"
Baadaya maelezo hayo kutoka kwa jamaa huyu ambae alionekana kama ndie msimamizi wa kitengo kile cha mateso akadakia kijana mwingine aliekua akiniunguza na Msumali wa moto
"Hili sasa ni tatizo lakini kwa kua huyu Tax Driver hajaondoka me nadhanitumzuie mpaka Soo likitulia huko town ndo tumuache aende..."kabla hajamaliza yule mwenye suti akadakia
"Hapana,hatupaswi kumuachia, akibanwa huyu atasema tu, muingizeni ndanimummalize kimya kimya" Nilishtuka sana niliposikia kua kijanaYule anatakiwa auwawe, hapo ndipo nikajua kua sasa hata mimi siponitena, baada ya maelekezo yale vijana wa kazi wote wakatoka njewakaniacha mie nikiwa pale juu naning'inia

Ndani ya muda mfupi walirudi ndani wakiwa na kijana yule dereva tax japo hawakuingia nae katika chumba nilichokuwepo mie wakaenda nae mpaka chumba cha mbele kisha nikaanza kusikia kelele kali za kilio alichokua akilia kijana huyu, alilia kwa sauti ya hali ya juu kisha akatulia kimya, sikumsikia tena wala sikujua wamemfanya nini, baada ya muda wakaja wale vijana waliokua wakinitesa mimi walipofika pale usawa wangu wakaikata kamba niliyokua nimefungwa nayo pale juu nikaanguka kama kiroba cha taka mpaka chini kisha wakanimwagia maji mengi halafu wakaondoka

Ilipofika jioni nikiwa nimelala pale chini kama mzoga waliingia tena wale vijana na kuniinua kisha wakaniambia niwafuate, nilianza kuwafuata huku nikichechemea kwa taabu kutokana na maumivu niliyoyapata siku nzima, tukafika mpaka kwenye Chumba kilichoandikwa PEPO HURU,sikuelewa maana ya neno hilo nikahisi ndani mule kuna raha japokidogo ila hali ilikua tofauti nilipoingia nilikuta maiti ikiwa imelala juu ya dimbwi la damu, utumbo ukiwa nje ya tumbo. Niliogopa sana hali ile nikajikaza na kusogea eneo lile Kuangalia vizuri 'Tobaa", alikua ni yule kijana dereva wa Tax.. wameamua kumuua ili asiende kutoa siri. na hapo sasa nikazidi kupoteza Bima ya Matumaini kama nitatoka salama mule ndani. Vijana wale wakaniamuru nimnyanyue maiti yule kisha nimpeleke nje halafu nirudi kusafisha damu na uchafu wa maiti yule..

Nilimuonea huruma sana kijana huyu dereva wa Tax kwa kifo cha kinyama kama kile japo niliamini Mungu ameamua kunilipia kwa ushenzi alionifanyia mimi wa kunikamatisha kwa maharamia hawa kwa Tamaa ya pesa kidogo,Nikafika mpaka alipolala kijana huyu ili nimnyanyue, Cha ajabu wakatinikiwa nimeinama naanza kuibeba maiti ile maharamia hawa wakawawananipiga picha, niliogopa kuhoji kuhusu picha hizo nilizokuanikipigwa nikijua nitapewa kiminyo kikali kuliko kile cha awali,nikaibeba maiti ile mpaka nje kabisa nikaicha kisha nikarudi ndanikusafisha lile eneo alilouliwa.. na baada ya hapo nilirudishwa ndanikuendelea na Adhabu,

Ilipitawiki moja nikiendelea kupata mateso makali sana ikiwemo kupigwa nashoti za Umeme, Hali ilikua ngumu sana kwangu, kila siku nilikuanikapata adhabu kali na za kila aina huku nikipewa chakula kidogosana na maji. siku moja nikiwa nimefunguliwa kamba niko nimekaakwenye sakafu napata chakula nakumbuka ilikua ni ugali na dagaaGhafla nlisikia mlango ukifungulia kisha akaangizwa Msichana mmojaakiwa kalainika sana bila shaka ni kwa kichapo alichopewa namafedhuli hawa, Sikumjua kwa haraka ila nilipotuliza machokumuangalia vizuri alikua ni Ntahondi, Shemeji yangu kwa Ramla,ilikua ni vigumu kumtambua kwa urembo wake aliokua nao maana kwa sasaalikua amesawajika, amevuja damu mpaka zimeganda mwili mwake,inaonekana alipigwa sana. nilijisikia majonzi mpaka hamu ya kulailiniisha..

Nilipomsogeleaniligundua kua alikua amepoteza fahamu, Roho iliniuma sana nikiaminikua ni mimi ndie nimemponza mpaka kufikishwa pale, nikiwa nimesimamanisijue cha kufanya likaniijia wazo nikaenda pembeni mwa chumba kilenyuma ya Mashine ya umeme waliyokua wakiitumia kunitesea nikachukuaDumu la maji nikaja nalo mpaka pale alipolala nikammwagia maji mengikichwani na mwilini, baada ya muda sio mrefu alizinduka!!Aliponiangalia alianza kulia kwa uchungu sana, nilijaribukumbembeleza lakini hakunyamaza.. mpaka baadae kabisa alitulia nakuanza kunisimulia yaliyomkuta japo alikua akiongea kwa taabu sanakutokana na maumivu anayoyapata
"Sikuulipotea ghafla tulijitahidi sana kukutafuta bila ya Mafanikio, keshoyake kaka yako wa Tabora alikuja Dar tukaendelea kukutafuta kila konabila ya Mafanikio, Ramla aligoma kushiriki kabisa kukutafuta yeyealikua busy na Mipango yao ya Kuvishana pete, na Mwaki ameamuakugharamia Sherehe yote ya wahitimu Hakuna mwanachuo yeyote kulipagharama za Sherehe" alikaa kimya kwa muda kashaakaendelea
"Kilichotushangazazaidi baada kama ya siku tatu mbele uliokotwa Mwili wa huyo derevaTax akiwa ametumbuliwa tumbo, katobolewa macho nk walipojaribukuupekua vizuri mwili wake wakakuta picha mbili zikikuonesha wewe ndouko nae, na Mpaka sasa vyombo vyote vya habari vimesha riport kuawewe inasemekana ndo umemuua" Maneno ya Ntahondi yalizidikunifanya niwe kama kichaa, nilizidi kuchanganyikiwa, yaani sasamjini mimi Ndo natafutwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji ambayosikushiriki, nilishindwa kujizuia nilianza kulia nikijua sasavyovyote iwavyo Mwisho wangu umefika,

Ntahondialiendelea kunipa habari kua kule mjini Mama yangu amekua akipotezafahamu kila saa kufuati kutoweka kwangu na taarifa za habari kuanatafutwa kwa Tuhuma za Mauaji ya Dereva Tax, Pia akaniambia Mpangouliopo ni kwamba tunatakiwa kuuawa siku hiyo ya Graduation ili Ramlana hawara yake Mwaki waweze kuishi kwa Amani..

PiaNtahond alinieleza kua anaenishughulika zaidi kule mjini ni Jarufu,pamoja na Mwl Honde. nilifarijika kidogo kusikia kua swahiba wanguMwalimu Honde ananishughulika, nilipata matumaini kwa kua najua fikakua Honde amemuoa mdogo wake na Waziri Mkuu wa Nchi yetu hivyoniliamini kua inaweza ikawa ahueni kama Honde ataamua kulifikishasuala hili kwa Mhe Waziri..

Nikiwanaendelea kububujikwa na machozi kutokana na maneno yaliyouchuma nakuuunguza moyo wangu kutoka kwa Ntahondi, nae aliendelea kunipa Storyza kila kinachoendelea kule mjini na mpaka yeye kukamatwa nakufikishwa kule Msituni.
"Nilipopatataarifa kua unatakiwa kukamatwa siku hiyo nikawahi kukutumia ujumbemfupi kwenye simu yako ili uzidi kujihami kumbe tayari ulikuaumeshakamatwa, na baadae nikapokea msg kutoka kwako kua tuonaneMaeneo ya Coco Beach, kumbe walioijibu msg ile walikua ni hawaMajambazi wa Mwaki na hatimae wakanitia nguvuni, wakanipiga sana nakunitesa kinyama, nimeumizwa sana mbaya zaidi nimedhalilishwa kwakuvuliwa nguo zote kisha nikaanza kuchapwa bakoro mwilini mpakanikapoteza fahamu, nazinduka ndo najikuta humu" Alimalizakuongea Ntahondi kisha akanitaka na mimi nimuelezee hali ikoje kwanguna mule ndani kwa ujumla, na vipi tungejikomboa kutoka katika makuchaya Ibilisi huyu

Naminilimueleza mateso niliyopewa mule ndani ila ikabidi baadhi ya matesonimfiche nikihofia kumzidisha hofu na kumkatisha tamaa ya kuishi,lakini Mwisho kabisa nikamwambia sisi ni vijana makini Lazimatupiganie Maisha yetu na yuhakikishe tunatoka humu, wakati nikiongeakwa uchungu maneno haya ya kijasiri ambayo naimani bila shakakichwani mwa Ntahondi ilikua ni Ndoto ya mchana, ni kama kujifunikaTishu kwenye mvua ya Elninino

ITAENDELEA....


culbby mlyn Analyse princetx slim5 MUSSOLIN ram Angelicious showtie Ngoami amina mabata binti kiziwi Nicas Mtei korino Sukula aniceth mzahulaKhantwe kelcie chwechinyong ram tabibumtaratibu Magembeh Emmanuel Thadei Moderator
 
RIWAYA: SIKU YA GRADUATION
MTUNZI: MAUNDU MWINGIZI



SEHEMU YA KWANZA

"Yaani kweli RAMLA Umeamua kunitenda kiasi hiki!!, pamoja na mapenzi yote niliyokupa lakini umeamua kunisaliti!, nimepoteza pesa zangu nyingi kukusomesha chuo nikiamini we ndo utakua mama wa Wanangu Leo wema wangu umegeuka mkuki wa sumu moyoni mwangu, Ramla Why? Why?!!" Niliendelea kulalama peke yangu huku nikilia kwa uchungu, shuka yote ikiwa imeloana jasho na machozi pale katika kitanda changu..
"Kitendo ulichonifanyia Ramla kinaniua ndani kwa ndani, huu ni zaidi ya ukatili yaani umesahau ahadi zetu zote tulizowekeana!!!.. aaaah" niliendelea kujisemea peke yangu kama Mwehu..


Taarifa hizi za uchungu kua Mchumba wangu Ramla ananisaliti kwa kutoka na na Kigogo maarufu jijini Dar Es Salaam nilizoambiwa na Rafiki yangu Mwl HONDE ziliniumiza sana sikua na sababu ya kupinga sana kwakua nilimuamini sana Rafiki yangu alienipa Ukweli wa Tukio hilo, kwanza Rafiki yangu huyu nimejuana nae siku nyingi tangu nikiwa pale chuo kikuu cha Dar Es Salaam pia Rafiki yangu huyu kwa sasa ni Muhadhiri katika chuo ambacho anasoma Mchumba wangu Ramla hivyo alichoniambia ana uhakika nacho kwa asilimia zote kwa kua nay eye yuko hapo hapo chuoni


Kilichoniuma zaidi ni pale nilipotajiwa na jina la huyo kigogo, Kwanza ni Tajiri, Mfanyabiashara maarufu, anamiliki miradi mingi, ana majumba na magari ya kifahari kila kona, anamiliki Cassino kubwa na maarufu kuliko zote jijini Dar, anahusishwa pia na Biashara haramu ya madawa ya kulevya pamoja na matukio kadhaa ya ujambazi wa magari na nyara za serikali, huyu si mwingine na PABLO MWAKI..
"Hata nikitaka kumfanyizia ubaya huyu Tajiri sitaweza.." Niliendelea kulia kwa uchungu. Basi nikajikaza na kuinuka pale kitandani na kwenda kuoga japo baada ya saa zima nikatoka Bafuni bila ya kujimwagia hata kopo la maji, nilikua nimesimama tu kichwa kikiwa na zaidi ya Kilo mia za mawazo.. nikarudi mpaka chumbani na kupanda kitandani kulala japo usingizi wote uliniruka, Usiku kucha niliwaza na kuwazua nifanye jambo gani ili nimrejeshe mchumba wangu mikononi mwangu na hatimae nikabakiwa na maamuzi ya kupambana na Pablo Mwaki bila ya kuogopa utajiri na ujambazi wake..
*****


Karibu na Posta mpya jijini Dar es salaam kuna Jengo kubwa la kibiashara lililoandikwa MIKINDA BUSSINESS CENTER, Ndani ya Jengo hilo mashuhuri kuna kila aina ya Biashara zinaendelea humo, Spermarket, Slot machine, Bureau De Change, Branch za Benki kadhaa, na pia ndani ya jengo hilo pia kuna Cassino mashuhuri ya kuuza makahaba, mashoga, na wasagaji, kila utakachokihitaji utakapata ndani ya jingo hilo.. Naam mjengo huo na vyote vilivyomo ni mali ya PABLO MWAKI


Pablo Mwaki na Mzee wa makamo japo ukimuona huwezi kudhanai kama ana umri mkubwa kutokana na mazoezi, maisha bora na jinsi tu anavyojiweka, Ni Mweupe, Si mnene wali si mwembamba, anapendelea zaidi kunyoa Kipara..


Mbali na Mjengo huo PABLO MWAKI pia ana miliki miradi mingine kibao zikiwemo kampuni za uchimbaji madini, Kampuni za usafiri wa majini na Angani, pia ana hisa kwenye baadhi ya makampuni makubwa makubwa,Si jambo la ajabu ndani ya Dar es Salaam nyumba kadhaa na maofisi yakihusishwa kumilikiwa na tajiri huyu, Wapo waliomsujudia Pablo kutokana na utajiri wake lakini pia wapo waliomchukia na kumlaani kutokana na kuwaharibia vijana wao kwa kuwatumia katika biashara zake haramu..
Pablo Mwaki alishawahi kuhukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumteka na kumuua kijana Samson Shirima, mfanyabiashara wa madini na kumpora pesa nyingi, Lakini alitumikia kifungo hicho kwa takriban miaka mitano tu kasha akakata rufaa na kushinda kesi hiyo ndipo aliporudi uraiani na kuanza kufanya biashara zake na ghafla kua tajiri mkubwa..
*****


Siku iliyofuata niliwasili ofisini na kuomba Ruhusa kwa Boss wangu Mr Jimmy nlimueleza kua naumwa sana tumbo, japo si kweli. Lengo langu lilikua ni kwenda kuonana na Mwl Honde ambae ni muhadhiri chuoni kwa kina Ramla na ndie alienipa ukweli wa kila kinachoendelea kati ya Ramla na Pablo.


Kila nilipomuangalia Mr Jimmy ambae ni meneja katika kampuni yetu ya SAJAM MARINE Ltd nilizidi kuumia nafsi kwakua mbali ya kua Boss wangu pia ni Mume wa mama'yake mdogo na Mchumba wangu Ramla Aliechangia mama tu na mama yake na Ramla. Nilopotoka tu ofisini nikaenda moja kwa moja mpaka Chuo cha usimamizi wa fedha(I.F.M) kwa Mwl Honde nilipofika Honde akanipokea vizuri ila hatukua katika ule ucheshi na uchangamfu wetu, nilishindwa kabisa kujizuia na kujikuta nikionesha kabisa hali isiyo ya kawaida usoni mwangu, Baada ya salamu mazungumzo yakendelea
"Nisikilize Naufal mimi nakushauri kama mtu wako wa karibu, kwakua namfahamu vizuri Pablo naamini akikujua tu utakua katika hali ya hatari"
"Kwa hiyo wewe unataka nifanyeje?"
"ukubali matokeo na uachie ngazi, Pablo humuwezi, atakupoteza"
"Yaani Honde badala ya kunishauri tufanyeje ili tuwaachanishe we unataka niachane na Ramla!!"
"Kaa ukijua Pablo Mwaki kaishatangaza Ndoa , na Ramla amelipokea kwa furaha suala hilo, sasa kama unataka kuiweka Roho yako Rehani Endelea"
"Hivi Honde una akili timamu kweli wewe?! unajua me na Ramla tumetoka wapi?, unataka nikubali kirahisi rahisi kuibiwa na ----- huyo kisa ni tajiri, Kwanza wataoana vipi wakati Ramla ni Muislam na huyo Mpumbavu Mwaki ni Mkristo"
"Upo dunia gani kaka? Ramla ameshabadili dini na sasa ni Mkristo"
"Nilichogundua na wewe ni Msaliti tu, utakua umetumwa tu, Sio bure!" nikanyanyuka kwa hasira nikaanza kuondoka bila hata ya kuaga, nilimsikia Honde akijaribu kuniita ila hata sikujisumbua kugeuka nikaenda mpaka barabarani upande wa pili ulipo ukumbi wa Makumbusho ya Taifa nikachukua Boda boda na kutokomea zangu..


Nilipofika Nyumbani nikajipumzisha kwenye kochi huku nikiwa na mawazo mapya kichwa,
"Hivi inakuaje rafiki yangu wa karibu kama Honde anashabikia tukio hili? Tena bila hata ya aibu anasema nimuache Ramla, nimeanza kumshtukia, Haiwezekani, huyu itakua nae katumwa na huyu mjinga mwenzao ili anishawishi tu nimuache Ramla wangu au pengine ni yeye ndie anaemtaka" niliendelea kujifariji huku sasa lawama na hofu zangu zote zikawa ni kwa Honde sasa. Nikainuka pale kwenye kochi nikaenda bafuni kuoga, nikiwa bafuni nilsikia simu yangu ikiita nilipokwenda kuiangalia alikua ni Honde akinipigia simu nikaiangalia simu ikiita bila kuipokea kisha nikarudi bafuni huku nikijisemea mwenyewe "Akkkh hivi huyu mjinga anafikiri mie hayawani kama yeye" nikiwa bafuni naendelea kuoga simu yangu iliita tena ila wala sikujisumbua kwenda kuiangalia nikijua atakua ni Honde tu huyo. Nilipomaliza kuoga nikaenda kuiangalia simu yangu, kumbe hakua Honde, alikua ni Ramla kipenzi cha moyo wangu, haraka nikajifuta maji mwilini kasha nikachukua simu yangu na kumpigia Ramla..
"Hellow" ilikua ni sauti nyororo ya Ramla
"Hi darl"
"Mzima mume wangu"
"Mie mzima wa afya, habari za chuo?"
"Nzuri tu, Mbona kimya sana tangu jana halafu na leo nimekuona umekuja chuo nikajua utanipigia simu tuonane lakini ukanichunia sio vizuri hivyo"
"Hapana sijakuchunia mpenzi wangu nilikua na haraka sana kuna Laptop yangu alikua nayo Mr Honde ndo nikawa nimeiijia kulikua na kazi ya muhimu sana ofisini"
"Ok Baby, kesho nitakuja kwangu nijipikie mwenyewe, nimechoka na haya mambo hostel kila siku chips tu" Tuliendelea kuzungumza kwa madaha kila mmoja akimhadaa mwenzie, mimi nilimhadaa kwa kujifanya kama hakuna tatizo lolote nililolisikia nae bila shaka alinihadaa mimi kwa kuniita majina mazuri ya baby, mume wangu, nk wakati alijua fika kua kwa sasa ni mali ya Pablo Mwaki.
Baada ya kukata simu ya RAMLA Nikajitupia kitandani nikiwa nimechoka Mwili mpaka akili, mawazo ya kila aina yakizunguka kichwani mwangu. Nilikua nusu naamini kua Ramla amenisaliti, hapo hapo nahisi kua Honde ndie anataka kutugombanisha, hapo hapo natamani nimtafute huyo Pablo Mwaki nimfanyie kitu kibaya japo haikua rahisi, ni matamanio tu yasiyowezekana waswahili wanasema Dua la Kuku..


Nikiwa pale kitandani nilisikia mlango wa Chumbani kwangu ukigongwa nikajinyanyua kwa uchovu mpaka mlangoni, nilipofungua mlango tu akaingia NTAHONDI msichana mrembo, mcheshi na mchangamfu, ni rafiki wa karibu sana na Mchumba wangu Ramla pia wanasoma wote chuoni,
"Karibu"
"Ahsante Shem"
"Mpaka nimeogopa mbona usiku? Kuna usalama kweli?"
"Hah ha usiku gani wa kutisha huu, au hautaki wageni shem?"
"Hapana sio kawaida yako, haya karibu uketi"
"Ok, ahsante" Baada ya kumkaribisha ntahondi nilirudi kwanza kuufunga mlango kasha nikaenda mpaka kwenye Friji ili nimuangalizie japo kinywaji lakini akaniwahi kwa kukataa
"Shem wala usihangaike na kinywaji, mie sio mkaaji, nataka tu tuongee haraka niondoke"
"Acha roho mbaya, hautaki hata kuniwekea Baraka ndani!!"
"Usijali nitakunywa hata siku nyingine" baada ya Ntahondi kukataa kinywaji nikarudi mpaka karibu ya kochi alilokua amekaa na mie nikakaa kwenye kiti cha uvivu, kasha Ntahondi akaanzisha mazungumzon nilijiweka sawasawa kupokea habari iliyoonekana kua ni nzito sana kwa jinsi alivyoonekana usoni Ntahondi
"Kwanza kabisa naomba unisamehe kwa hili nitakalo kuambia kama nitakukwaza maana sisi binaadamu hatujakamilika, pili hata kama halitokufarahisha naomba libakie kua ndani ya moyo wako kwa kua lengo langu mimi ni kunusuru maisha yako naomba nawe uninusuru kwa kuificha siri hii hata kama hautoipenda" alikua akiongea huku akiniangalia usoni bila hata ya kukpepesa macho, Niliendelea kumsikiliza bila kuongeza neno
"Kwa kifupi masha yako yako hatarini, muda wowote unaweza kuitwa kwa jina moja tu la Maiti" baada ya kuvuta pumzi akaendelea
" Na anaekuangamiza na ku kuua ni Mchumba wako RAMLA"
"Ramla" kivipi aniue? Mbona sikuelewi?" nilishtushwa sana taarifa hii japo nilianza kuhisi kua huenda sasa huu ni muendelezo wa ile habari niliyopewa na Honde
"Tulia na unisikilize kwa umakini, Ramla hivi sasa anakusaliti, amepata mwanaume mwingine anaetoka nae kimapenzi, mtu huyo anaitwa Pablo Mwaki, ni kigogo mmoja maarufu tu na kwasasa wanataka kufunga ndoa"
"Unauhakika Ntahondi?"
"Mpaka nimekuja hapa mimi sio mwehu, mimi nasoma na Ramla na ni rafiki yangu wa karibu, Lake langu na langu lake, kwa kifupi PABLO Ameshapewa taarifa zako kua wewe ndie mchumba wake na Ramla hivyo yupo kwenye mchakato wa kukusaka, akukamate hata ikiwezekana akuteke ili wao wawe huru na mapenzi yao na ndoa yao bia ya bughudha ya mtu yeyote" Ntahondi alisimama na kuniaga,
"Mimi naondoka, ila jitahidi kua makini na Ramla kwa usalama wako anaweza kutumiwa yeye ili wafanikishe mpango wao wa kukuteka"
"Aisee mbona kama nachanganyikiwa Ntahondi, yaani Ramla anaweza kufikia hatua hiyo?"
"Na kwa taarifa yako huyo Boss wako Mr Jimmy ni rafiki wa karibu sana na Pablo Mwaki na kwenye hiyo kampuni yenu Mwaki ana hisa zake, na pia ujue kua Mke wa Jimmy ambae ni mama yake mdogo na Ramla ndie aliemshawishi Ramla akuache wewe ili awe na Pablo hivyo inawezekana hata huyo Jimmy anaujua mchezo mzima nae kua nae makini" Wakati hu tunaongea habari hizo tulikua tumeshanyanyuka kwenye kiti na tunatembea kidogo kidogo mpaka mlangoni ambako tulikua tumesimama na baada ya maelezo hayo Ntahondi alifungua mlango na kuondoka zake, niliufunga mlango nikarudi mpaka kitandani, nikiwa natetemeka wa hofu na uoga wa hali ya juu ulionivaa mwilini
******

I T A E N D E L E A
Sukula kelcie culbby Ngoami

Usichelewe na kuwa na hakika kuwa una ni tag!
 
Back
Top Bottom