Riwaya- penzi chungu

mapengo junior

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2011
Posts
1,135
Reaction score
276
SIMULIZI.......PENZI CHUNGU
MWANDISHI... HALFANI SUDY

SEHEMU YA 2

Bruno alikuwa hajielewi. Akili yake ilihama kabisa. Hakuuona kabisa ubaya wa kumshika Suto namna ile. Sasa alikuwa anamuona Suto ni mzuri zaidi ya Cleopatra. Kiuno kilimchanganya sana, alijikuta ghafla amekipenda kiuno cha Suto, hapana, alijikuta anampenda Suto kutokana na kiuno chake kizuri. Sasa waligusana kabisa, Suto akiwa mbele, Bruno akiwa nyuma.
Mikono ya Bruno ilikuwa kifuani kwa Suto, ikichezea maziwa ya Suto, mdomo wa Bruno ulikuwa sikioni kwa Suto. Walikuwa wananesa kutokana na mapigo ya mziki mzuri wa taarabu. Wote wakiwa hoi kwa hamu ya kitu wasichokifahamu. Pale sikioni mdomo wa Bruno ulijikuta ukisema, maneno yalitoka taratibu kwa sauti ya kukatakata mdomoni.

"Dunia mzi-ma ha-ikupe-ndi Suto. Wa-na-ume wote hawa-kup-endi Suto. Ila mi-mi nimegundua wewe ni mwana-mke mzuri sana. Ndio, Dunia nzi-ma inaku-chukia Su-to. Ila mimi naa-hidi ku-kup-enda kua-nz-ia leo, nit-aku-pen-da siku zote za mai-sha ya-ngu Suto,
Ndio, Nakupenda sana Suto !

Ghafla mlango wa sebuleni ulifunguliwa, hakuna aliyeusikia mlango wakati unafunguliwa, hakuna wala aliyesikia mlio wa gari wakati linapaki kule nje. Wote walikuwa wamezama hisiani.
Wazazi wa Bruno walikuwa wamerudi kutoka sokoni.
Baba na mama Bruno walipigwa na butwaa. Kukuta mtoto wao amemkumbatia Suto namna ile. Ilikuwa picha mbaya sana kwao.

" Bruno ! " mama yake aliita kwa ghadhabu.
"Naam "
" Ni nini hiyo ? !"
"Mapenzi mama " Bruno alijibu kwa upole.
"Unasema ! "
"Mapenzi ya kweli Mama"
"Unataka sema, unampenda Suto ?"
"Ndio mama "
"Maajabu haya ! Tangu lini ? "
"Tangu leo Mama "
"Unampenda toka moyoni Suto "
"Nampenda toka moyoni Mama, nataka nimuoe "
"Haiwezekani ! " Baba na mama Bruno walisema kwa pamoja kwa sauti kubwa yenye ghadhabu !

Muda wote huo Suto alikuwa kimya. Alikuwa anasikia kila kitu alichokuwa anasema Bruno. Lakini hakuelewa kabisa. Hakuwahi kumpenda mwanaume tangu azaliwe. Alikuwa anawachukia wanaume wote duniani, sababu kubwa ikiwa ni Simulizi aliyosimuliwa na mama yake, jinsi baba yake akivyomtesa mama yake, kufikia hatua hadi ya kumkataa yeye, mtoto wake. Suto aliwekuwa na kisasi na wanaume wote duniani. Maneno yale ya Bruno yalimtoa Suto machozi.

"Usilie Suto, chozi lako ni la thamani sana kwangu.." Bruno hakumalizia kauli yake.
"Hivi we mtoto umerogwa !" Baba yake alisema kwa sauti ya ukali.
"Nimependa baba " Bruno alisema kwa kujiamini.

Yalikuwa kama maigizo, Bruno mwenyewe hakujua nguvu ya maneno hayo inatoka wapi. Wazazi nao walishikwa na bumbuwazi, Suto alihemewa sana.
Wote hawakujua, mapenzi ni kitu cha ajabu sana, na muda mwengine yanaanza bila sababu maalumu. Bruno hakuwa amerogwa, sasa hakuwa amependa kiuno cha Suto pekee, alimpenda kweli Suto, na dhamira ya dhati toka moyoni mwake alikuwa anataka kumuoa kweli.

ITAENDELEA .....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…