Mungu Mweusi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 1,474
- 1,088
SEHEMU YA KWANZA
Wakati Angel anakimbilia kuwahi ndege, ghafla alijikwaa katika shimo dogo lililokuwa kwenye geti la kuingia uwanja wa ndege na hivyo kusababisha kuumia kifundo cha mguu wa kulia. Nusu saa kabla ya kuingia uwanjani aliwasiliana na hawala yake raia wa Ufilipino, Mr. John ambaye alikuja nchini kwa shughuli ya utengenezaji mifumo ya uendeshaji mitambo ya kiwanda cha nguo cha Sky Shine textile.
Haikuwa rahisi kwa Angel kufanya maamuzi mengine isipokuwa kuwahishwa hospitali ya Amana kwa ajili ya matibabu.
Mume wa ndoa wa Angel Mr. Steven alipokea simu kutoka hospitali akifahamishwa kuhusu kulazwa kwa mke wake hapo bila kuelezwa tatizo la mgonjwa wake zaidi ya kuambiwa awahi haraka hospitali. Ilikuwa jambo gumu kwa Steven kuamini kilichotokea maana aliona kama ameandamwa na mikosi katika familia yake, kwa sababu wiki mbili nyuma mke wake alilazwa hospitali kutokana na kusumbuliwa na ujauzito wake wa miezi mitano.
Hivyo moja kwa moja alihisi huenda tatizo limerejea tena au mimba imeharibika. Steven alienda moja kwa moja kwa Foreman na kumueleza matatizo yaliyomsibu, licha ya kufanya kazi katika kampuni ya BM building and Construction LTD, inayojishughulisha na ujenzi wa majumba na ujenzi wa barabara, maisha ya John yalikuwa ni magumu kuliko ombaomba wa mtaani. John alijiandaa haraka haraka na kuelekea kituo cha basi za mwendo kasi pale Kimara Mwisho ambako siku hiyo walikuwa wamepata tenda ya ujenzi wa Hostel ya shule ya sekondari Dreamland.
Baada ya Dakika Steven alifika wodi ya upasuaji wa mifupa (orthopedic ward) na kuulizia jina la mke wake. “Subiri kidogo, wewe unaambiwa mke wako amepata ajali lakini unakuja kwa kujivutavuta huna hata haya?” Ni maneno yaliyokuwa yakimiminika toka kinywa cha Nurse. Baada ya Steven kujitetea Nurse alimwambia asubirie mapokezi kwa sababu mgonjwa wake yupo theater akifanyiwa upasuaji mdogo.
Wakati hayo yote yakiendelea Steven hakuweza kubaini kama mke wake alikuwa na njama za kutoroka na raia wa kigeni ambaye wameishi naye kama mahawala kwa muda wa mwaka mmoja tangu afike nchini. Japo wakati mwingine walikuwa wakiingia katika migogoro ya hapa na pale lakini hakuweza kuhisi jambo baya. Japo wakati mwingine alishangaa jinsi mke wake alivyokuwa akipendeza kwa nguo nzuri na mapambo mengine muhimu kwa mwanake. Baada ya taratibu za upasuaji kukamilika, Angel alipelekwa wodini kupumzika na kuona na ndugu na jamaa waliofika kumjulia hali. Mume wake alikabidhiwa simu pamoja na mkoba mdogo wa mkononi ambao ulikuwa umehifadhiwa pale mapokezi.
Steven alimuuliza mkewe wake kipenzi jinsi alivyoumia mguu na kwa kujua hali halisi ya tukio, Angel akamdanganya mume wake na kumwambia kwamba alisukumizwa na bodaboda na kuanguka akiwa anatoka sokoni.
Wakati mazungumzo yakiendelea ghafla simu ya Angel iliita, ngriii ngriii, Steven ikabidi ashike mkoba na kutoa simu kwa ajili ya kupokea kwa niamba ya mke wake ambaye alikuwa akiugulia maumivu ya upasuaji. Helloo, unaongea na Inspekta Shibe toka kituo cha polisi JKIA-Julius Kambarage International Airport, baada ya kujitambulisha aliulizwa wewe ni Angel Kawambwa? Steven haraka akajibu hapana mimi ni mume wake kuna nini tafadhari? Inspekta Shibe akamwambia tumeokota begi la nguo lililokuwa limesahaulika katika Kituo cha ukaguzi wa mizigo ya ndani Gate One hapa airport, Inspekta Shibe aliendelea; “ndani ya begi tumekuta kuna nguo za kike, vitambulisho na Dawa ambazo bado hatujafahamu ni za nini mpaka tutakapopata watu wa kitengo cha Drugs kwa ajili ya ukaguzi zaidi hivyo tunaomba mfike kituoni kabla ya saa tatu usiku” akakata simu.
Kwa kuwa Steven alipokelea simu nje ya wodi hakuweza kumshirikisha mke wake kuhusu simu aliyopokea kutoka kituo cha polisi uwanja wa ndege JKIA. Hivyo alimuomba mdogo wake wa kiume waongozane. Baada ya kufika kituoni alijitambulisha na kupokewa na bila mazungumzo zaidi alionyeshwa Begi kubwa ambalo aliweza kulitambua ni la nyumbani kwake. Polisi walimwambia pia kwamba kulikuwa na tiketi ya ndege ya kampuni ya Rwanda Air ambayo ilionyesha alikuwa akisafiri kuelekea Uingereza siku hiyo saa 08:00 mchana. Steven alizidi kuchananyikiwa akiwa halewi maneno aliyokuwa akiambiwa kama yalikuwa kweli au hadithi.
Hivyo polisi walichukua maelezo kutoka
kwa Steven na baadaye kumzuia kuondoka mpaka zile dawa zilizokuwa ndani ya begi zitakapotambuliwa. Kwa akili ya haraka sana ilibidi steven akubali kwamba ni kweli mke wake alikuwa akisafiri kwenda uingereza siku hiyo kwa ajili ya matembezi, lengo la kufanya hivi ilikuwa ni kumalizana na askari ili suala hili liende sasa kifamilia zaidi.
Kikosi cha kinachohusika na dawa kiliweza kutambua dawa hizo zilizokuwa ndani ya mkoba zikiwa zenye maandishi Delavirdine na Nevirapine ambazo kitaalamu waligundua kwamba ni dawa ambazo zinaruhusiwa kwa matumizi ya binadamu, ambazo kazi yake kubwa ni kuongeza kinga ya mwili kwa kuzuia virusi vya UKIMWI kuzaliana. Polisi waliweza kumruhusu Steven achukue vitu vyake bila jibu la dawa zilizokutwa ndani ya begi zilikuwa za nani na zilikuwa na matumizi gani.
Moja kwa moja Steven alichukua begi la mke wake na kuelekea nyumbani, huku akiwa hajitambui kutokana na msongo wa mawazo ya tukio zima la mke wake. Baada ya kufika nyumbani alienda chumbani na kuhifadhi begi na kuchukua zile dawa na tiketi ya ndege kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa suala la mke wake kabla ya maamuzi mengine.
Asubuhi kulipopambazuka Steven aliandaa chai mapema na kuelekea hospitali kwa ajili ya kumjulia hali mke wake. Akilini alijua kabisa kwamba hata kama kuna jambo lolote isingekuwa rahisi kwa mke wake kukubali. Mke wake mara nyingi walipokuwa wakipishana alikuwa akikimbilia kisu au panga kwa ajili ya kumjeruhi mume wake. Kwa kuzingatia mambo hayo ilihitajika umakini mkubwa katika kuweza kugundua ni jambo gani linaendelea katika ndoa yake.
Daktari Daktari!! Samahani kwa usumbufu, unaweza kunisaidia kwamba hiki ni kitu gani?..........
Itaendelea sehemu ya pili