Mdharuba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2011
- 824
- 521
STORY: "SIKUTEGEMEA"
MTUNZI: Mdharuba J.K.
SEHEMU YA KWANZA.
★★★★★★★★★★★
"Ndo huyu huyu.. mi naona dawa yake ni kumpoteza kabisa duniani.." Alisema yule bwana aliyekuwa amevaa koti jeusi na suruali yake ya kijani kibichi, alionekana kabisa kuwa alipania mimi nife kikatili..
Yule mganga akaangalia vizuri kwenye lile dishi la maji na kumgeukia tena yule bwana, "Bwana Mbago hapa umefika, na huyu Kassim mimi ntafanya kama unavyotaka mwenyewe,, labda nikuulize tu kwa mara ya tatu na ya mwisho, "Kipi unakipendelea zaidi achanganyikiwe au tumuue kabisa?" Aliweka nukta hapo kwenye swali kisha akaendlea, "Hiki ni kitendo cha dakika moja tu, ukitoa jibu lako mimi namaliza na huko aliko anakua kama ulivyotaka". Baada ya Maelezo haya ya Mganga yule Maarufu kama "Dr Mwinyi" sikuona sababu ya kusubiri jibu la Mbago wala kuendelea kuwabakiza wawili hao duniani tena, nkaikoki vizuri bastola yangu kisha nikafyatua risasi mbili za haraka nkianzia kwenye kichwa cha Dr Mwinyi kisha nikamaliza na Mbago. Kisha nikarudisha bastola kiunoni na kuondoka haraka eneo lile..
"Kama mbwai mbwai tu, mmenifanyia mengi mabaya na mkanifanya nikateseka sana, kwa hakika hili liliwastahili" Nilijisemea moyoni nikiwasha gari na kugeuka kwa kasi saaana nikielekea nyumbani kwa babu yangu, Bagamoyo kumueleza yaliyojiri..
★★★★★★★★★★★★★★★★
Jina langu ni Kassim Omari Mkomwa, nimezaliwa katika kijiji cha Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga miaka 35 iliyopita. Kutokana na umasikini uliokuwa unaikabili familia yetu, sikubahatika kusoma sana, niliishia darasa la saba tu, kwani baada ya matokeo kutoka na nikawa sijafanikiwa kuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule za serikali, hakuna aliyekua na uwezo wa kuniendeleza kielimu katika familia yetu, maisha yalikua duni sana familia nzima..
Nikawa nipo nipo nyumbani nikijihusisha sana na shughuli za Kilimo cha mahindi, angalau mwisho wa siku nipate walau cha kupeleka mdomoni kisha cha kujazia choo..ndio maisha ya kimasikini yalivyo, kwanza tunajaza tumbo halafu mambo mengine baadaee..
Nilijihusisha na kilimo mpaka nilipofikia umri wa miaka 20. Siku moja ambayo niliamka mapema kuliko kawaida, kwa sababu ya ndoto niliyoota, nilitoka nje nikakaa katika baraza ya pale nyumbani kwetu.. Ilikua ni saa 11 kasoro dakika 3 alfajiri.. Nakumbuka ilikuwa siku ya Jumanne, siku ambayo babu yangu alikua akiniambia kuwa sio siku nzuri..yeye aliita 'siku ya nuksi'. Pamoja na kuwa nilimuhoji sana kuhusiana na siku hii, lakini yeye alikua bado hajataka kunieleza kwa kina sana bali alikua akiniasa tu kuwa nisijihusishe na mambo mengi yanayoweza kuniletea mitafaruku na watu katika siku hii..Kwahiyo babu yangu huyu ambaye alikua akiitwa Mkomwa Omar Mwandeni alinikataza kukopa, kudai, kutongoza na hata kulipa madeni siku hii, yeye akinambia niiheshimu sana siku ya Jumanne kwani sio siku nzuri..
Nilikaa pale nje mpaka asubuhi jua lilipochomoza na watu wote walipoamka walikuwa wakishangaa kuniona pale nje kwani haikua kawaida yangu.
Mpaka alipotoka babu yangu huyu ambaye nilikua napenda sana kumsikiliza nasaha zake, yeye alinipachika jina la utani ambalo ndilo lilikua maarufu sana kipindi hiki..Aliniita Al'wattan..
?Nasikia leo umeamka mapema sana na kukaa hapa nje, imekuaje mjukuu wangu?? Babu, ambaye alikua amekalia kigoda kilichokua pembeni ya kile kigoda changu, aliniuliza huku akinitizama usoni..
?Kuna ndoto nimeota, nilikua nasubiri uamke hapa unieleze maana ya ndoto ile?
?Ndoto gani tena hiyo Al'wattan unayoota usiku wa kuamkia jumanne??
?Babu, nimeota nakula Komamanga lililoonekana kuiva vizuri sana na lilikua limenivutia, Komamanga hili nililetewa na mtoto mdogo ambaye alinambia ameagizwa na dada mmoja ambaye yeye hamfahamu, baada ya kulila, nikagundua kuwa lile komamanga lilikua na mdudu katikati..naye nilimtafuna..nilipogundua nimetafuna mdudu nikatema haraka, ndipo nikashtuka kutoka usingizini..Nikaangalia saa yangu nikagundua tayari ilishaingia alfajiri, nilipata fazaa kwakweli na wewe ulishanambia kuwa ndoto za alfajiri zinakua za kweli.. Ndo maana nikakosa kabisa usingizi?
?Laahaulaaa..mjukuu wangu Al'wattan.. Ndoto asali katika siku shubiri? Babu alishangaa na kuongea kwa mafumbo kama kawaida yake..
?Unamaanisha nini babu unaposema ndoto asali katika siku shubiri?? Nilimuuliza, maana kiukweli sikumuelewa..
?Ndoto hiyo inatafsirika hiviii...? Babu aliamua sasa kunieleza tafsiri ya ndoto, alishapotezea kunipa maana ya maneno "ndoto asali katika siku shubiri" na hii ndio ilikua kawaida yake, alikuwa hanipi maana ya mafumbo yake mara nyingi, nilijitahidi kuzoea lakini babu alikuwa akinipa wakati mgumu sana kusema ukweli..
?Enheee..? Nilifanya 'Verbal following' kama wanavyotutaka wataalamu wa mambo ya communication.
?Wewe umeamka na bahati leo, lakini siku yenyewe ni mbaya, kwahiyo bahati yako itakukuta leo lakini baadae utapata tabu sana kwa bahati hiyo utakayoipata, kama hutokuwa makini unaweza ukajikuta hata umekuwa muuaji.. , natamani sana ningekuwepo kipindi hicho ili nikupe nasaha nzuri usifikie pabaya, kwa sababu ninavyokujua Al'wattan wewe moyo utakushinda?
Babu aliyaeleza haya kwa hisia kubwa sana, akinisihi nisije kufanya ubaya..
?Babu sijakuelewa, ni bahati gani hiyo inayoweza kunipelekea mpaka kuua?? Niliuliza kwa hamaki..sikuwa naelewa kabisa anachokisema babu yangu mzee Mkomwa Omari Mwandeni.
?Al'wattan, nilitamani sana uwe na hekima na busara kama zangu mjukuu wangu, lakini umezaliwa muda ambao umri wangu umeenda sana.. Utashindwa kujifunza mengi? Babu alianza tena kunizungusha kama kawaida yake, siku zote hakuwa akienda straight kwenye maelezo yake. Baada ya nukta fupi aliendelea tena babu, mimi nilikua namtizama tu wakati huu..
?Bahati utakayokutana nayo leo ni kubwa sana kwa mujibu wa ndoto yako, na hayo matatizo hayatatokea sasa..ni mpaka hapo utakapokuwa umenufaika na bahati husika tena kwa muda mrefu, hapo ndipo utakaposhawishika kufanya chochote kama mtu yeyote ataingilia kuleta kikwazo? Babu alikuwa amenishika mgongoni muda huu anaponieleza maneno haya..
?Babu, nifanyeje ili nisiingie katika kipindi kigumu, yaani namaanisha nifanyeje ili nisifikie huko kwenye mauaji?? Niliuliza kwa shauku, nilitamani kujua cha kufanya kabla babu hajafa..
?Huwezi kuzuia hayo yasitokee kwa mujibu wa ndoto yako, ila mimi nakuasa tu kuwa UKITAKA KULA HARAMU, BASI KULA VINONO? Babu alinijibu swali langu na kunifanya nibaki mdomo wazi..Maana hapa, hata hili fumbo la mwisho ambalo ndio ushauri wake SIKUELEWA.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Itaendelea...
MDHARUBA J.K pia ni Mtunzi wa Riwaya ya HISTORIA BATILI ambayo kwa sasa ipo kitabuni. Vitabu vitaanza kuuzwa rasmi kuanzia tarehe 1/11/2015.
Wasiliana nami kwa simu 0718274130