Riwaya mpya: Historia batili na JK

Riwaya mpya: Historia batili na JK

Mdharuba

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2011
Posts
824
Reaction score
521
RIWAYA: HISTORIA BATILI(Fake History)
MTUNZI: Jumaa Khatib Mdharuba (Jk)
+255 718 274 130


SEASON 01-EPISODE 01
★★★★★★★★★★★★★★★
"Mume wangu, huendi kazini leo??" Aliongea Sauda Ally ikiwa ni Majira ya saa 3:30 asubuhi, hii ilikua sio kawaida ya bwana Khatib Jumaa kuwa ndani mpaka muda ule.
"Leo sitoki" alijibu kifupi akiwa bado yupo kitandani akiwa busy na simu yake..
"Ok sawa, mi nipo uani nafua kidogo".
"sawa". Alijibu bwana Khatib na kuendelea na ubize wake..
"Haloo Nira Saire..mimi leo sitokuja kazini kabsaa..naomba muendlee na kazi kesho mtanipa ripoti kamili." alisema maneno hayo baada ya simu kupokelewa upande wa pili.
★★★★★★★★★★★★★
Jumaa Khatib Mdharuba, kama alivyofahamika, alikua akijulikana kama kijana aliyekulia katika maisha ya kitajiri sana, mtu ambaye hakuwahi kuonja ladha ya shida katika maisha yake. Kipindi hiki akiwa na umri wa miaka 27 tu alikua akimiliki yard kubwa sana ya magari iliyokuwepo mkoani Morogoro. Alikua akifanya kazi yake kwa ufanisi mkubwa kiasi cha kuwa na wateja wengi wa uhakika kuliko hata wale washindani wake ambao walimiliki yard hizo katika majiji makubwa kama Dar, Arusha, Tanga na Mwanza. Aliuza magari yake kwa bei nafuu na yalikua na warranty ya zaidi ya miaka mitatu. Alimudu kufanya kazi yake vizuri sana, akawa anaishi maisha safi sana. Mpaka sasa alishaweza kutoa ajira kwa vijana 15 ambao walikua wakishiriki ktika shughuli tofaut katika yard ile, wakiongozwa na Nira Saire kama kiongozi msimamizi wa wafanyakazi wa pale. Nira Saire alikua akimuheshimu sana bwana Khatib kwa sababu alikua akiishi nae vizuri na vilevile yeye ndiye aliyekua analipwa mshahara mkubwa zaidi kuliko wafanyakazi wote wa pale. Mara zote Khatib asipokuwepo majukumu ya kusimamia yalibaki kwa Nira.
Nira alijaribu kutengeneza urafiki wa karibu saana na Khatib nje ya kazi, lakini jambo hili linaonekana Khatib hakulipenda saana.. yeye alitaka awe anashirikiana nae zaidi kwenye kazi tu na kutoruhusu saana wazoeane nje ya mazingira ya kazi..Nira alilishtukia hili na akaamua awe mpole tu, kwanza aliamini watu wenye pesa walikuwa na dharau sana..
Sauda Ally, mke wa Khatib, alijitahidi sana kuweka mapenzi ya dhati kwa mumewe ambaye alikua na miaka miwili sasa kwenye ndoa, ingawa Khatib hakuonekana kujali sana. Alikua busy sana na mambo yake na mara nyingi akirudi nyumbani alikua akipanda kitandani na kulala..hakuwa na muda wa kupiga story na mkewe wala kuongelea maisha yao yanaendaje..
Matendo yake yalikua yakishangaza watu wengi saana, na kila mmoja alikua akimtafsiri tofauti. Alijitolea sana kusaidia masikini na yatima na walemavu ila hakutaka chombo chochote cha habari kihusike katika misaada hiyo. Alikua akitoa misaada kimyakimya na akitembelea kituo kimoja anatoa zaidi ya mil.50!! Alifanya hivyo kwa zaidi ya miaka mitano sasa..
★★★★★★★★★★★★★
Maelezo ya utajiri wa Khatib na mambo anayoyafanya yalishangaza watu wengi sana..hakua na dharau wala kiburi kwa mtu yeyote, ila swali kubwa lililokuwa akilini mwa watu wengi ni kuwa "Kwanini anafanya kwa siri sana?"
Mambo yake aliyaendesha kwa siri kubwa,licha ya kumiliki yard ya magari lakin tathmini ya utajiri wake ni zaidi ya hapa.!! hela zingine anatoa wapii?? Na watu wote walijua kuwa alikua akitokea katika familia ya kitajiri akimtambulisha Noor A Mdharuba kama baba yake mdogo na mlezi wake anayeishi naye hapa Tanzania wakati babayake mzazi alkua akiishi nchini Canada akiwa ni Manager wa benk moja ya biashara nchini humo.. Mara nyingi Khatib alikua akisafiri kwenda Canada kuonana na baba yke Mzazi Mzee Jumaa Mdharuba.
Ni Noor ndiye aliyemshawishi Khatib kuoa mapema ili awe na familia yake.
"Ila mimi sina hata mwanamke kwa sasa, ntamuoa nani?" Alihoji bwana Khatib kipindi hcho..
"Kazi ndogo mwanangu, hiyo kazi ntamwachia Bi Nuro Ahmed aniangalizie nani anaweza kuwa mke wa kuolewa na wewe.." Alipangua hoja bwana Noor na kumfanya Khatib akubaliane nae..
Bi Nuro Ahmed ambaye alikua ni mmiliki wa kituo kikubwa cha malezi na shule kwa watoto wadogo, alikuwa na wafanyakazi wote wa kike katika kituo kile. Hivyo alikuwa akiwafaham vizuri tabia zao na misimamo yao katika maisha. Aliweza kufanikisha zoezi na kufanya bwana Khatib amuoe Sauda Ally ambaye Nuro ndiye aliyempendekeza.
★★★★★★★★★★★★★★
"Mama, Khatib yupo huko kwako?" Alikua ni Sauda akiongea baada ya salamu kumuulizia Mama yake Mzazi Khatib ambaye alikua akiishi Mbezi jijini Dar..
"Hapana mwanangu, kwani vipi hajakuaga alipotoka?"
"Aliniaga kuwa anaenda kazini, lakini sio kawaida yke kutorudi mpaka sasa.."
"Ucjali mwanangu, si wajua wanaume tena wanakutana na mengi sana katika kutafuta" Mama Mdharuba Alijaribu kumliwaza mkwe wake licha ya kuwa hakujua Sauda alikua anajickiaje..
Kwa miaka miwili aliyoishi nae alishamfaham vizur Khatib ni mtu wa aina gani, mwanzo ilikua ngumu lakin baadae alizoea tabia ya Khatib kutoka na baadae kupiga simu kuwa yupo sehemu tofaut na aliyoaga.. lakini leo ni tofaut, haijawahi kutokea akatoka na kuchelewa kurudi kias kile na mbaya zaidi simu yake haipatikani!! Sauda alijawa na wasiwasi sana na kupiga simu sehemu zote ambazo mumewe angeweza kupatikana.. lakini hakufanikiwa..chakula cha jioni pia kilimshinda kula..sasa ilikua yapata majira ya saa 6:48 usiku, haelewi nini afanye..!!
Akajaribu kukumbuka matukio ya siku hyo tangu asubuhi, akakumbuka kitu ambacho kilimshtua kidogo!!
Akanyanyuka pale kitandani na kwenda katika meza ndogo iliyokuwepo chumbani mle..akavuta droo yake na kutoa kibunda cha pesa na kuanza kuhesabu.
Akagundua zilikua ni milioni moja na laki moja!! Akatafakari kwa muda na kuishirikisha akili yake katika kufikiri, akajikuta anaangua kilio!!.
★★★★★★★★★★★★★★
Don't Miss Episode 02
 

Attachments

  • 1431906777704.jpg
    1431906777704.jpg
    28 KB · Views: 788
Hamna Mkuu, itakuwa umejichanganya mbona haionekan

Haya soma hii basi nimekuletea hapa:
STORY: Historia Batili(Fake History)
MTUNZI: Jumaa Khatib Mdharuba
+255 718 274 130

Season 01-Episode 02
★★★★★★★★★★★★★★
Kawaida bwana Khatib alikua akimuachia mkewe kila siku hela ya matumizi madogo madogo ya nyumbani sh elf 50, licha ya kuwa kulikua na kila kitu mle ndani, ila hela hizi Khatib alikusudia zinunuliwe vtu vidogo vidogo vya dharura. Na kila siku alikuwa akiziweka pesa katika droo ya meza ndogo ya pale chumbani..Ila leo asubuhi alimshuhudia akiziweka pesa nyingi kuliko alivyozoea.. ingawa haikumstua sana, ila kwa sasa ndo anapata picha nini kilifanyika!! Kwa hesabu za haraka haraka pesa ile ilikua ni ya matumizi ya siku 22!!
"Ina maana Khatib hatokuepo nyumbani kwa siku 22?" Ni swali lililozunguka kichwni mwa Sauda muda huo..
"Na kwa mara ya kwnza leo namshuhudia amefikisha saa 4 bdo yupo nyumbani, na alinambia hatoki!! baadae akaniaga tena kuwa anaenda kazini, imekuajee??" alizidi kupatwa na mawazo mazito bi Sauda.. alishapiga simu ofisini kwa mumewe tangu saa 2 ucku muda ambao ndo ofisi ilikua inafungwa na cm yake ilipokelewa na bwana Nira Saire na kumjibu kuwa boss hakufika kazini siku hiyo..na kua alishampgia simu na kumpa maelekezo muhimu na kumwambia pia kuwa kesho atampa maendleo yalikuaje.
Alibaki akijiuliza maswali mengi saaana..wazo kuu la wakati huu ni kuwa Khatib ameenda kulala na mwanamke mwingine leo!! Mwanamke yeyote lazima angewaza hivi kabla ya yote-wivu ndo mapenzi!! Lakini wazo hli lilijipinga lenyewe kichwani mwake, kwani Khatib hakuwahi kuonesha dalili yoyote ya kuchepuka kabla ya hapo..hata simu yake ilikua free sana kwa mkewe, muda wowote aliojisikia alishika na kufanya atakacho katika simu ile...
Akiwa katika dimbwi hili la mawazo ikiwa ni takriban saa 7 unusu za usiku, alipokea simu kutoka kwa Mama Mdharuba, "Vipi huyo mumeo bado hajarudi?"
"Ndio, hajarudi mama"
"Sasa, naomba nisikilize kwa makini sana mwanangu" Alianza kuongea Mama Mdharuba na kuweka kituo kumruhusu Sauda aitike kidogo..
"Ndio mama nakuckiliza, endelea tu" alijibu Sauda kwa sauti ya upole saaana..
"Khatib, ndo mwanangu wa kwanza baada ya yeye kuna mdogo wake hyu wa kike Hawa, wanangu ni hao wawili tu, na mimi Khatib namtegemea sana.. naomba nikutoe wasiwasi, kama kungekua kuna tatizo lolote linalomuhusu ningekua nimeshapata taarifa mwanangu, hata kama asingenipa yeye mwenyewe lakini mimi taarifa ningepata tu, kwhy ondoa wasiwasi mwanangu, mumeo atakua yu salama tu" Aliweka nukta kubwa Mama Mdharuba na kumfanya Sauda kushusha pumzi ndefu na kuitia kuwa amemuelewa..walitumia takribani dakika 10 kuongea, Mama Mdharuba akijitahidi kumliwaza Sauda alichukulie kuwa lile ni jambo la kawaida.
Na kwa kutumia utu uzima wake, Mama Mdharuba alifanikiwa kumshawishi Sauda alale kwa amani tu bila ya mumewe pembeni..licha ya kuwa ndio ilikua mara yake ya kwnza..
★★★★★★★★★★★★★
Mama Mdharuba, aliijua historia halisi ya mwanawe mpaka kufika hapo alipo, na hakuwa tayari kumwmbia mtu yeyote kuwa mwanae anatembelea HISTORIA BATILI katika ulimwengu huu.. Historia halisi ya maisha ya Khatib aliijua yeye na mwenyewe Khatib tu basi..
Kutokupatikana kwa Khatib hakumpi mawazo kabisaa mama hyu na sababu hiyo tabia alikua nayo kabla hajaoa wala hakusumbuka sana.. Khatib alishapitia kwake mchana na kumwachia hela ya matumizi inayoweza kutumika mwezi mzima, kwhyo alilijua hilo mapema kuwa Khatib hatokuwepo hapo kwa mda kidogo.. Kitu pekee na cha muhimu alichokua akikifanya Mama Mdharuba ni kumliwaza Sauda na kumfanya asijihisi mpweke sana, mpaka Sauda akaanza kupatwa na wasiwasi huenda hyu mama anajua nini mwanawe anafanya na ni kwamba tu anafichwa yeye Sauda..
"Mama, naomba kama unajua mume wangu alipo uniambie plzzz mama, ni wiki ya pili sasa mume wangu hajatokea na sina taarifa yake yoyote..na ww nakuona kama huna wasiwas mama".
Alihoji Sauda machozi yakimtoka akiwa nyumbani kwa mama mkwe wake maeneo ya Mbezi jijini Dar, Morogoro palikua hapakaliki, hakuwa na kampani ya aina yoyote, maana Khatib hakutaka kuwa na housegirl nyumbani kwake..sababu alizijua mwenyewe..ilikua ni siku ya 13 tangu Khatib aondoke pale nyumbani!! Sauda alikua ameanza kukonda tayari, tabasamu lililokua usoni mwake lote lilishapotea, hakuonekana kuyafurahia tena maisha yale ya ndoa, mume wake pekee aliyempenda na ndo mwanaume wake wa kwanza katika maisha yake ndo hyu asiyeeleweka..Alipata kila anachohitaji, lakini bdo amani haikuwepo moyoni mwake.. ukimuona lazima umlilie gere kwa maisha ya kifahari aliyokua anaishi..Lakini kumbe ni kama sumu tu iliyofichwa kwenye vikombe vya dhahabu!! Alikosa amani..
Ndoa yake ilikua na matatizo mengi sana ambayo hayakutaka pesa kuyamaliza..Tukio hili lilimfanya awaze mambo mengi saaanaa..
Kwanza, Khatib hakutaka wapate mtoto kipindi chote cha miaka miwili alichoishi naye, akidai bdo sana, walitakiwa wafurahie ndoa kwanza..
Pili, Khatib alikuwa na ratiba maalum ya kufanya mapenzi na mkewe kwa sababu alizozijua mwenyewe.. na kutokana na sababu ya kwanza, alikua akimkwepa sana mkewe katika siku zote za kipindi cha hatari..hivyo hata kama angetaka bi Sauda ratiba ilikua haibadiliki.
★★★★★★★★★★★★★★
"Haloo dada..mambo??" Aliongea Sarah mdogo wake Sauda ambaye wakati huo alikua akisoma Bachelor degree nchini Canada alikotafutiwa nafasi na shemeji yake Mr.Khatib!!
"Poa, mzima Sarah?" Aliongea bi Sauda lakini kwa sauti ya kinyonge sana..
"Nimemuona shem huku katika Supermarket moja hapa Vancouver" Aliongea Sarah kwa kujiamini akiwa hajui kinachoendlea..
"Wee usinambiee..umemuona huko Canada?"
"Ndio dada, yani mi niko kwenye basi naelekea chuo na yeye nimemuona anaingia Supermarket" Alizidi kusisitiza Sarah na kumfanya Sauda apagawe..
"Sasaa..sijui nisemeje jaman..Sarah..naomba ushuke katika hilo basi uende ukahakikishe kuwa ni yeye kweli!! Na uhakikishe kuwa anajua kuwa umemuona.." Aliongea Sauda akianza kupata matumaini akiwa na wasiwasi mkubwa..kitendo kilichofanya Mama Mdharuba aliyekuwa chumbani wakati huo atoke na kuja mlangoni kwake, na kuweza kuyafuatilia maongezi yale ya Sauda katika simu akajua Sauda anaongea na nani na anataka Sarah afanye nini..!!
"Kwani kuna tatizo lolote dada? Maana nawahi chuo nina presentation leo" Alihoji Sarah akianza kupata wasiwasi..
"Fanya kama nilivyokuagiza..maswali mengine utauliza baadae.."
"Sawa dada" Aliitikia Sarah na kushuka kituo cha mbele na kuanza kurudi kumfuatilia shemeji yake.
★★★★★★★★★★★★★★
Don't Miss Episode 03
 
:thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup:
 
Back
Top Bottom