Riwaya: Mateso yangu

Riwaya: Mateso yangu

MATESO YANGU

SEHEMU YA 027

Nilipogeuka, nikakutana uso kwa uso na Rehema. Alikuwa akiniangalia kwa wasiwasi huku akionyesha Hofu ya wazawazi. Ile kumuona tu nikahisi kitu kikiuchoma Moyo Wangu. Nikashuhudia chozi langu likishuka. Sikutaka kuongea kitu na Rehema. Nilichofanya nikugeuka na kuanza kuondoka zangu. Kukutana pale na Rehema kulirudisha maumivu niliokuwa nayo Moyoni. Nikahisi mwili ukitetemeka kwa hasira. Sikutaka kuendelea kumuangalia kwa kuwa niliogopa kuchukua maamuzi mengine. Nikatembea taratibu nikilizuia Chozi langu kutoka na kuonwa na watu. Hakuna kitu kinachoumiza kama mapenzi. Hakuna maumivu ambayo yanatesa na kukondesha kama ya mapenzi. Sikutaka kuongea tena. Niliendelea kutembea pole pole bila kuongea huku nikiwa na fundo la hasira,. Wakati Nikidhani Rehema asingenifuata kumbe nilijidanganya. Rehema aliendelea kunifuata kwa nyuma huku akiniita na kuniomba nimsikilize, lakini bado sikusimama wala kusikiliza maneno yake. Bado nilikuwa nikitembea kuelekea nyumbani kwetu kigamboni. Sio kwamba sikupenda kusimama, sio kwamba mwili ulikataa. Hapana kila kitu katika mwili na nafsi Yangu kilikuwa tayari nisimame nimsikilize Rehema. Moyo wangu ulikuwa ukinituma nifanye hivy.o. Ulinitaka nisimame na kumsikiliza japo kwa dakika hata moja. Lakini Ibrah sikutaka hata sekunde. Bado kidonda changu kilikuwa kibichi ambacho hakikuwa kimeponeshwa na chochote kitu.. Rehema hakukoma bado aliendelea kunifuatilia, bado hakuacha kuniita huku akinishika bega.

Sikuona tena sababu ya kutokumsikiliza, sikuiona tena sababu ya kumpuuza. Nikasimama pembeni mwa kituo cha daladala posta ili kumsikiliza. Nilikuwa katika kiwango cha juu cha Hasira, licha ya hilo lakini bado nilijipa utulivu wa kumsikiliza Rehema kile ambacho alitaka kunieleza. Zikapita dakika kama mbili hivi tukiangaliana na Rehema. Hakuweza kuongea chochote zaidi ya kuniangalia usoni huku akijisonya na kuyaachia machozi yashuke taratibu na kulowanisha Mashavu Yake. Nikaona hapa tukiendelea kukaa hapa watu watagundua kinachoendelea na kuanza kujisogeza. Nilichokifanya ni kuushike mkono Wa Rehema na Kuondoka naye kuelekea Feri. Muda wote Bado Rehema Hakuinua Kinywa Chake kuongea chochote. Bado aliendelea kukaa kimya bila kuongea kitu. Bado alionekana nafsi yake haikuwa tayari kuongea Chochote.

Nami nikaendelea kukaa kimya, niliendelea kukaa kimya kwa kuwa sikuwa na lakuongea, na hata kama ningekuwa nalo nadhani lingekuwa la kwanza na la mwisho. Tukafika Feri huku tukiwa tumeshikana mikono. Bado nilihisi moto wa mapenzi ukiwaka katika Moyo Wangu. Kule kushikana mikono na Rehema kukaleta msuguano wa mawazo kichwani mwangu. Nilihisi hali yakutokujielewa na kujitambua. Ile hasira ambayo nilitoka nayo kule Chuoni ilianza kuyeyuka pole pole na tabasamu la kukata na shoka lilikuwa limetamalaki Usoni mwangu. Bado tulishikana hata pale tulipoingia kwenye kivuko. Tukaendelea kushikana hata pale tulipopanda ngazi kuelekea juu kabisa ya kivuko. Bado hatukuachana hata pale tulipoketi kwenye mabenchi ya kivuko. Tulikuwa pamoja tena kwa kugusana miili yetu. Ni kweli nilimpenda Rehema Ally, nikweli nilitamani awe Mke wangu, lakini vipi Huyu Gerald Mahundi msomi wa Sheria Katika Chuo kikuu Cha Havard nchini Marekani? Atakubali kuniachia huyu mtoto Mbeach Ili nimkuze Mwenyewe? Kwa nini Rehema Asingekuwa kama Neema Mtobwa msichana mcheshi na mpole kwa watu wote? Kwa nini asimuige Yeye katika kuheshimu na kuthamini Hisia za Mtu.

Kitendo Cha kufikiria Msomi wa Rehema kilinifanya kumbukumbu yote kuhusu kilichotokea kunirudia. Nikamuangalia Rehema kwa makini huku tabasamu lote likipotea. Niliamua kumuonyesha kuwa sikuwa katika furaha kama alivyodhania. Hakuna kitu kinachoumiza kama kuchapiwa mwanamke wako. Bora mtu akupige ngumi lakini sikukuchapia huku ukijua. ''kwa nini Umenisaliti Rehema?'' lilikuwa ni Swali lililonitoka bila kutegemea. Kwanza Rehema hakunijibu Haraka, bali aliinua uso wake na kuniangalia Usoni. Kisha akayaacha macho yake yaniangalie katika namna ambayo sikuwahi kuiona. Uzuri wa macho yake ukanifanya nitulie kwanza. Akataka kuongea kitu lakini nikahisi sauti yake ikikwama na kushindwa kusikika. Akabaki kunitizama kwa muda, punde nikamuona akiruhusu Chozi lake kutoka na kuanza kushuka tena mashavuni mwake. Chozi ambalo liliusonpnesha Moyo Wangu, Chozi ambalo lilinifanya nianze kumuonea Huruma Tena. Sikuliacha lifike Chini, sikuliacha lidondokee kwenye mavazi Yake, nikaliwahi kwa viganja vyangu na Kuanza kulifuta Taaratbu na Kwa Uangalifu. Kila nilipoendelea Kulifuta ndipo uzuri wa Rehema Ulipoongezeka. Sikujua Nini ambacho kilitokea, lakini Wote tulijikuta ndimi zetu zibadilishana Ladha tena Mbele ya Abiria Wengine ndani Ya Kivuko. HAKIKA HII ILIKUWA ZAWADI YA USHINDI KWANGU...

Tuliendelea kudendeka mbele za watu huku macho yakituangalia. Watu wenye midomo wakaanza kulaani na kukemea kile kilichokuwa kikifanyika. HAWAKUJUA, HAWAFAHAMU NA HAWATAJUA. LAITI WANGEJUA? HAKIKA WANGESHANGAA
 
MATESO YANGU

SEHEMU YA 028

Rehema alikuwa ameegemea kifuani kwangu akionyesha majuto makubwa. Majuto juu ya usaliti Aliyonisaliti. Bado hakuamini kama alikuwa kifuani kwangu tena tukinyonyana ndimi mbele ya Umati wa watu. Bado machozi yalikuwa yakimshuka kuonyesha kuwa anajuta na kujilaumu. Sikutaka akumbuke kule alipotoka, sikutaka akumbuke kile alichonifanyia. Nilitaka asahau na kurudi tena kwangu. Nilitaka ajiamini nakutambua kuwa Nampenda na sitamani kumuacha. Nikakipeleka kiganja changu kwa mara ya pili nakutaka kufuta machozi yake. Nikatambua Chozi la Rehema Halina Thamani Ya kufutwa na Kiganja bali Ulimi. Mapenzi ni Upofu, mapenzi hutia ukiziwi, mapenzi huondoa Aibu na kuleta kujiamini. Mbele za watu kwa mara nyingine nilikuwa nikilifuta Chozi La Mwanamke Sahihi katika Maisha Yangu. Mwanamke mpole, mtamu na msikivu. Sikufikiria tena kuhusu usaliti Wake, sikukumbuka kuwa alikuwa anamwanaume tena Msomi Wa Sheria Kutoka Havard. Nilichojali ni mapenzi Yangu kwake. Siku Zote katika Uhusiano wa Kimapenzi ni Lazima Kuwepo na Msamaha. Kwenye mapenzi ya kweli lazima misukosuko iwepo. Ni jukumu lako kusamehe na pia kutoa nafasi na wewe kusamehewa pale ufanyapo makosa.

Nilipoimaliza kazi Ya Kumfuta machozi nikamlaza kifuani na kuanza kumpa matumaini na Maneno matamu. Maneno ambayo yalimpa tumaini jipya. Akainua uso na kunitizama kwa jicho lake tamu na lakuvutia. Alikuwa mzuri, na alikuwa na mvuto. Alikuwa na kila kitu anachotakiwa kuwa nacho mwanadada yoyote. Macho yake bado yalionyesha mapenzi mazito, mapenzi Juu Ya Ibrahim Masimba. Hata pantoni lilipofika upande Wa kigamboni bado tulikuwa Zero Distance. Bado hatukuachiana wala kupeana nafasi. Tukashuka tukiwa pamoja na hata tulipoingia kwenye bajaj tulikuwa pamoja. Tulipofika nyumbani tulishuka wote na kuingia wote ndani. Kuifikia Sebule akakutana na macho ya mama na dada Zangu. Wakapigwa na butwaa kuonyesha hawakuutegemea ule ugeni. Wakainuka wote wakionekana ni Wenye furaha. Furaha ambayo haikuwa kama ninavyowajua.

Sura zao zilionyesha kulikuwa na kitu ndani yake. Sikuwajali wala kuwatizama. Nikaushika mkono wa Rehema na kuelekea Chumbani kwangu. Lakini wakati nakaribia ulipo mlango wa Chumba changu nikashangaa kuviona Viatu Vya Kike. Viatu ambavyo nilivitambua mara moja. Vilikuwa viatu vya Sheila. Kwanza nikasimama nikitaka kurudi nilipotoka kuwauliza Dada zangu. Lakini Rehema aliniambia ni lazima twende. Ni lazima tuingie Chumbani amuone nani ambaye alikuwemo humo. Akili yangu akigoma kufanyakazi kwa muda, kuvikuta viatu vya Sheila Sehemu ile kulinifanya nihisi kutetemeka. Nikakumbuka kuwa Sheila nilimpita Pale Holiday Inn akielekea kama Akiba, sasa nani ambaye atakuwa humu ndani? Kama ni Sheila Je atakuwa amefikaje? Yalikuwa maswali yaliyokosa majibu na hata kama yalikuwa na majibu lakini hayakuwa majibu sahihi.

Nikajivika ujasiri kisha kupiga hatua kuelekea pale mlangoni. Kuufikia mlangoni wa chumba changu nikapokewa na wimbo Wa Celine Dion Uitwao I love You. Wimbo ambao ulinihakikishia kuwa aliye ndani ya Chumba Changu alikuwa Sheila, kutokana na Jinsi anavyoupenda Wimbo huo. Kila hatua niliokuwa nikipiga nilikuwa nikimuangalia Rehema Usoni kama nitagundua Chochote. Lakini bado Rehema alionyesha Utulivu. Utulivu ambao ulizidi kunichanganya. Kwa nini Rehema hana wasiwasi? Kwa nini haonyeshi kuumizwa na muonekana wa Viatu vya mwanamke katika Mlango Wa Chumba Changu. Sikutaka kujiuliza sana, nilichofanya nikushika kitasa Cha mlango kisha nikakinyonga, mlango ukanitii kwa kufunguka.

Nikatangulia kuingia nikifuatiwa na Rehema. Kuingia kwetu tukapokelewa na Mwanamke Mwingine ambaye sikuwahi kuwaza endapo anaweza kufika kwetu. Huyu alikuwa Shamim, Shamim Rafiki wa Sheila. Alikuwa amejilaza kitandani kwangu akiwa katika kigauni kifupi na Chepesi sana. Kigauni ambacho kilionyesha Nusu nzima ya Mwili wake. Sikulitegemea lile. Sikuutegemea ugeni ule nyumbani kwangu. Ingawa sikuwahi kumgegeda Shamim lakini bado nilimchukulia Rehema ndiye mwanamke Sahihi kwangu, kuliko Sheila na hata Shamim. Bado nilisimama sambamba na Rehema. Bado tulishikana mikono na Bado hakuuonyesha wasiwasi wowote.

Kwa mwendo wa mikogo, Dharau pamoja na nyoto nikamuona Shamim akiinuka na Kutufuata pale tuliposimama huku jicho lake likiwa kwa Rehema. Alikuwa akimtizama Rehema mfano wa Mtu anapoangalia kinyesi. Lakini yote hayo bado Rehema alikuwa Kimya akimuangalia Shamim Huku Tabasamu likichanua Usoni kwake. Ibrah nikaendelea kushikwa na Mshangao wa kutokana na kile kinachotokea pale. Punde mlango Wa Chumbani kwangu ukasukumwa. Wakaingia Dada Zangu pamoja na Mama Yangu mzazi. Mkononi Mama alikuwa ameshika Bahasha ambayo ilituna kuonyesha Inakitu ndani. Hakuwa Mama yule mcheshi kwa Rehema. Huyu Alikuwa mama mwenye Chuki na Hasira waziwazi. Akasogea mbele yangu Huku akiifungua Bahasha, alipomaliza kuifungua Akatoa picha kama Nane. Akanikabidhi Mkononi Mwangu Huku akitoa kauli ambayo Ilisababisha Kilio Kwa Rehema. ''SITAKI KUKUONA NA MALAYA HUYU KUANZIA LEO. aliposema Hivyo Akaondoka..
 
MATESO YANGU

SEHEMU YA 029

Hataki kuona naendelea na huyu malaya wangu. Rehema Wangu alikuwa malaya. Rehema wangu alikuwa muuza mwili. Hilo halikuniingia, hilo halikunishtua wala kuniumiza. Nilijua mama yangu amejazwa maneno. Maneno yakumchukia Rehema wangu. Ni mama huyu huyu aliyekuwa akimsifia Rehema na kumponda Sheila. Ni dada zangu hawa hawa waliokuwa wakilazimisha niwe na Uhusiano na Rehema lakini Leo wanamuita Malaya. Sikuwa na muda na hilo neno, bado Rehema alikuwa mikononi mwangu akikilaza kichwa chake kifuani kwangu. Maneno ya mama yakachochea upendo wangu wa dhati kwa Rehema. Upendo ambao ulikuja baada ya kuteseka kwa muda mrefu. Hata pale nilipoifungua Bahasha na kukutana na picha za Rehema akiwa amepiga kimahaba na mwanaume mwingine. Alikuwa amekumbatiwa kwa nyuma huku sehemu ya kitovu Ikiwa wazi. Bado picha hizo hazikunishtua, bado picha hizo hazikuliondoa penzi langu wala kulipunguza. Ndio kwanza nilizidisha kumpenda. Nisingeweza kushtushwa kwa picha zile kwa kuwa nilijua kabla ya kukutana na Mimi, Rehema alikuwa na Mahusiano Yake. Kabla hatujakuta Rehema alikuwa kwenye Mahusiano na Gerald Mahundi. Sasa kwa nini nichukie kwa sababu ya picha. Hapana Nitaendelea kukupenda Rehema hata kama Mama Amekuita Malaya. Nilijikuta nikilopoka kwa sauti. Kitendo ambacho kilizidisha kilio kwa Rehema. Hakuonyesha kuwa ni Malaya, hakuonyesha kuwa ni kicheche. Lakini Mama yangu amemuita kicheche.

Masikini Rehema alikuwa ameinamia Chini akilia. Machozi Yake yalikuwa yakilowesha sakafu. Hakuna nisipopenda kukiona kama kulia kwa Rehema wangu. Nilikuwa tayari kuhama nyumbani na kwenda kuishi mitaani kwa sababu ya kupigania Penzi la mwanamke nimpendaye. Mwanamke aliyeumizwa na Mateso Yangu. Nilikuwa tayari nikateseke mtaani lakini sikumuona mpenzi wangu akinyanyaswa na Mama Yangu ama ndugu. Hayo yalikuwa maamuzi Yangu, Maamuzi ambayo ningeyafikia pale ambapo ningeona bado nafuatiliwa. Nikaondoka na mpenzi wangu mle chumbani na kutokomea zetu mtaani. Niliamua kumuachia Shamim chumba, niliamua nikalale hata Guest lakini sipo tayari kumuona mpenzi Wangu akikashfiwa. Nilifanya hivyo kwa sababu ya Mapenzi, nilifanya hivyo kwa sababu ya Kumpenda Rehema. Nilishasamehe na kuusahau usaliti Wake. Niliamini Atakuwa Wangu wa milele.

****
Zilipita Siku tatu tokea tukio la kuitwa malaya kwa mpenzi wangu litokee. Tulikuwa tumeshaweka kila kitu sawa tukiishi pamoja japo kwa kuibiaibia. Muda wote tulikuwa tukipendana sana. Kila muda tulikuwa pamoja na kila dakika tulikuwa tumegandana. Kila sehemu tulikuwa tukienda pamoja na kila alipokuwepo yeye hata mimi ungenikuta. Kusema kweli lilikuwa penzi tamu sana, lakini licha ya utamu wake bado nilikuwa nikipata Shinikizo kutoka kwa mama hasa kutokana na kuhama kwangu nyumbani. Mama yangu siku zote alikuwa akiniusia kuwa mwanamke ambaye hajakuzaa si wa kumuamini wala kumtegemea. Kwani ipo siku anaweza kukuacha bila kutegemea na ukateseka Sana. Yalikuwa maneno Yenye ukweli lakini sikuweza kuyaamini kwa Muda Ule kutokana na Kukolezwa Na mapenzi kutoka Kwa Mtoto Rehema. Nakumbuka ikafika Siku Moja ambayo kulikuwa na party maalum ya Welcome First Year pale Chuo kikuu cha Dar es salaam.

Ilikuwa pati maalum ya kuwa karibisha wanachuo wapya wanaoanza mwaka wa kwanza. Ilikuwa pati ambayo haikuwa katika Ratiba Zangu kutokana na kuwa na Mishe Zangu Nyingine. Kama kawaida ya penzi letu mimi na Rehema ni Lazima tuombane Ruhusa iwapo mmoja atakuwepo na Mwingine hatokuwepo. Kwa kuwa mimi sikupanga kuwepo kwenye hiyo pati. Nikatoa Ruhusa Kwa Rehema kuhudhuria kwa kuwa pati iliwahusu sana wanafunzi Wa UDSM. Tuliagana vizuri na Rehema ikiwa ni pamoja na kufanya mapenzi tukiwa katika furaha na Upendo Wa Hali ya Juu. Hatimaye Muda wa Saa Moja Rehema akaondoka pale Room kuelekea Mbalamwezi Beach ilipokuwa ikifanyika pati. Sikuwa na wasiwasi Wowote juu yake nikiamini atakuwa salama na ataweza kujichunga mwenyewe. Sikuwa na Wasiwasi katika hilo kutokana na mapenzi ambayo tulikuwa tukionyeshana.

Lakini wakati zimepita Dakika kama kumi hivi aondoke, nikatumiwa Sms na Mshkaji wangu akiniuliza nilipo. Nilipomwambia nipo room, akaniambia amemuona Rehema Yupo Kwenye Gari na Mshkaji mmoja Hivi wakielekea Kibamba. Kupewa Taarifa Hiyo nikahisi Moyo Wangu ukinipiga paa! Nikamuuliza una uhakika kama ni yeye? Akaniambia ni yeye na akataja mpaka Nguo alizovaa. Hapo nikakubali kuwa alikuwa yeye. Kwa haraka nikahisi Kuchanganyikiwa. Nilihisi Kitu kikitaka kutokea kwenye Mahusiano yangu. Nilichokifanya nikuoga na kubadili nguo kisha nikaingia barabarani Kuelekea Mbalamwezi Beach. Kila nilipokuwa nikimfikiria Rehema nilihisi Moyo kuniuma. Sikuwa tayari kuvumilia Maumivu ya Kumfumania Rehema. Niliingia ndani Ya Ukumbi wa Mbalamwezi, nikatafuta Sehemu Nzuri ya Kukaa ambayo ingeniwezesha kumuona kila Mtu anayeingia. Muda uliendelea Kuyoyoma Bila kumuona Rehema Wangu. Nikahisi Chozi la Wivu Likinitoka. Wakati Nikiendelea Kuangalia Huku na huko. Mara Nikamuona Rehema Na Yule Mwanaume Nilimuona Kwa Picha Wakiingia
 
Back
Top Bottom