Riwaya: Mateso yangu

Riwaya: Mateso yangu

MATESO YANGU

SEHEMU YA 013

Alitembea akionyesha dharau zote, uso wake ulisadifu dharau tupu. Hakujisumbua kumsalimia mama yangu, bali alitema mate kuonyesha wote mle wodini tulikuwa tukinuka. Alionyesha umajivuno wa pesa na kila kitu, alionekana kupania kile ambacho alikuwa akikifanya. Mate aliyoyatema na kutua karibu na miguu ya mama yangu mzazi ytaliniumiza sana. Hakuna kitu nisichokipenda kama mama yangu kudharaulika. Nilimuangalia sheila kwa muda sana, nikatamani niinuke nimtandike makofi mawili matatu. Lakini macho Ya mama na yale ya Shamim Yalinifanya nitulie. Sheila akasogea mpaka kitandani nilipolala. Akaniangalia kwa aina ile ya Utizamaji, utizamaji wa kupandishwa na kushushwa. Alifanya kama wanavyofanya watu wanaotizama kinyesi. Kisha kwa Sauti Ile ile ya Dharau na Kejeli Juu Yake akatamka. ''nitakupoteza.'' kisha akageuka na kuondoka akituacha katika mshangao tusioutaraji. Atanipoteza, atanipoteza kwa kipi? Kwa kosa gani? Kuna umuhimu gani wa kuleta vitisho wakati kesi ipo mahakamani? Maneno yake hayo yalinifanya nimpuuze na kumuona kama mjinga. Kilichokuwa kikiniumiza katika Moyo wangu ni kule kumtema mama yangu mzazi kumaanisha alikuwa akinuka. Aliusahau wema wa Mama Yangu Mzazi, alisahau alivyokuwa akitendewa na Mama yangu.

Kilikuwa kitendo ambacho sikukitarajia kutoka kwake. Nilidhani angempa heshima mama yangu kwa wema aliyomfanyia. Lakini ndio kwanza aliamua kumuonyesha Dharau, dharau ya kumfananisha na takataka. Huu ndio wema aliytostahili mama yangu kwa kile alichokitenda kwa Sheila. Nikaamsha macho Yangu kumuangalia Mama Usoni, nikakutana na tabasamu lake ambalo kamwe hutaliona likiondoka Usoni kwake hata kama ana hasira Moyoni. Mama yangu Alipenda kutabasamu, mama Yangu alipenda kufurahi kila wakati. Kwa hiyo huwezi kugundua kama amekasirika ama la! Nilipohamisha macho yangu kumtizama Shamim, nikakutana na jicho lake ambalo kwa kulitizama tu, unaweza kuhisi unatizamana na Jini. Macho yalikuwa mazito sana. Ingawa alikuwa akikwepesha macho yake yasikutane na ya kwangu, lakini kuna kipindi akashindwa. Ikabidi tuangaliane. Kweli tukaangaliana na kutizamana. Macho yetu yalikuwa yakiongea mapenzi lakini nyuso zetu zilionyesha Urafiki. Mioyo Yetu ilikuwa ikiongea mahaba lakini matendo yetu yalikuwa ni ya kiurtafiki.

Kulikuwa na mapenzi katika moyo Wa shamim lakini sikuweza kuwaza hilo. Nilikuwa nikiwaza kesi ya shambulio inayonikabili na Kitendo cha Sheila kumtema mate mama yangu. Shamim bado alionekana kuwa mbali kimawazo. Punde nikamuona akitoka wodini bila kuaga. Nilichofanya ni kumuangalia mama, Mama naye akanitizama, wote tukatabasamu.

******

licha ya kumsaidia sheila lakini leo alikuwa akinilipa ubaya. Sikujua kama yangekuja kunipata haya. Baada ya wiki ya nne nikatolewa hospitali nikiwa na unafuu mkubwa. Nikatakiwa nielekee kituo cha polisi kulipoti. Bado shamim na mama yangu sambamba na marafiki zangu hawakuniacha mwenyewe. Waliongozana nami mpaka kituo cha polisi tabata shule. Huwezi kuamini wakati natolewa pale hospitalini kuelekea kituo cha polisi nilikuwa nikimuwaza kweli Sheila. Nilitamani awe pale nimuombe msamaha ili yaishe.. Nisingeweza kupambana naye kwa kuwa yeye alishika mpini na mimi nilishika makali. Tuliingia kituoni saa tano za asubuhi na kuelekea moja kwa moja mpaka mapokezi. Nikajieleza kwa kirefu, nilipomaliza nikashangaa nikiambiwa nivue mkanda wangu wa suruali, viatu pamoja na vitu vingine nilivyonavyo. Sikutaka kubisa wala kugombana. Niliamua kutii Sheria Bila Shuruti. Nikaingizwa chumba cha mahabusu huku nikiwaacha Matafiki, Mama pamoja na Shamim Wakihangaikia Dhamana Yangu. Licha ya kuhangaika sana kwa siku ile, lakini hawakufanikiwa kunitoa. Ilionekana amri kutoka kwa mkubwa fulani. Kweli nikalala kituoni bila kutolewa. Ulikuwa ni Usiku wa shida sana, Shida ambayo ilinifanya nishindwe kulala. Niling'atwa na Mbu kupindukia. Harufu mbaya na Kinyesi ilitawala chumba kizima.

Asubuhi nikatolewa chumba cha mahabusu na kutakiwa nikasubiri nje. Nilipotoa uso wangu nje nikawaona Sheila na Jamaa yake wakiingia pale kituoni. Walishuka kutoka kwenye gari fulani wakashikana mikono kuelekea polisi. Moyo Wangu Ukashtuka vibaya mno lakini baadae nikaamua kupotezea. Nikapishana nao kama hatujuani. Nilipoangalia kushoto kwangu nikamuona Shamim Wangu akiwa amependeza kupika kiasi. Nikajiambia hapa ni wakati wa kulipa kisasi kwa kumuonyeshea Sheila kuwa UKISEMA CHA NINI WENZAKO WANAJIULIZA WATAKIPATA LINI. nilimfuata pale alipokaa nikiwa kwenye tabasamu la kuumizwa, yeye akaachia tabasamu lenye Ujumbe Usijali Mimi ni Wako. Akainuka Hata kabla Sijafika na kujakunikumbatia bila kujali Watu waliokuwepo pale kituoni. Lilikuwa kumbatio lililonipa faraja, kumbatio lililonifanya nijione kidume haswa. Tulipokuja kuachiana kila mmoja akaangalia chini kwa aibu.. Tulipokuja kuangaliana tena, Tukakumbatiana kwa Mara nyingine... Mapenzi Ya Kazaliwa.
 
MATESO YANGU

SEHEMU YA 014

Lilikuwa penzi ambalo sikuwa na uhakika nalo. Penzi ambalo lilizaliwa katika aina fulani ya ajabu. Bado tulikuwa tumekumbatiana huku nikisahau kuwa shamim alikuwa mwanafunzi. Licha ya hilo kwa kuwa nilitaka nilipe kisasi kwa Sheila bado sikuliona hilo. Bado nilikuwa nimesimama nikimuangalia Shamim, lakini licha ya kufanya hivyo bado macho yangu yalikuwa yakiibia kumwangalia Sheila. Sheila aliyekuwa ameukamatia mkono wa kijana yule. Kwa mbali ndani ya moyo wangu nilihisi mapenzi ya Sheila bado yapo. Bado nilikuwa nikiumizwa na kile ambacho kilikuwa kikiendelea kati yetu. Kila wakati nilikuwa nikimuangalia Sheila na kusahau kuwa nilikuwa nimesimama na Shamim. Nikawa nawaza kwenda kumuomba msamaha, bado niliiona hatari Ikiwa kesi hii ingeendelea. Nilikuwa nikikaribia kifungo cha miaka jela kwa kosa la kuishi kinyumba na Mwanafunzi. Kwa mara ya kwanza nikaanza kumuona sheila kama mkombozi Wangu. Kama ataamua kuniacha katika hili basi nisingekiepuka kifungo cha miaka Thelathini. Lakini Ugumu ukaja katika kumuomba msamaha. Tusi zito alilonitukana pale mabibo Hostel Kuwa Hata mama yangu anajinsia kama yake na anaweza kuwa mke wangu, halikuweza kuondoka katika moyo wangu. Nikaapa kuwa nipo tayati nikafungwe lakini si kumuomba msamaha Sheila.

Mama Yangu alikuwa ni kila kitu, kumtusi mama yangu lilikuwa ni tendo ambalo halisameheki. Kwa mara ya kwanza nikajikuta nikiwa katika wakati mgumu. Nikabaki nikiwaza hili na kuwazua lile. Nikainamia chini nikitafakari, niliogopa sana kupelekwa gerezani, niliogopa sana kukatishiwa ndoto zangu za maisha. Lakini nikiwa katika mawazo hayo, nikahisi nikishtuliwa na Sauti tamu, sauti ambayo ilinifanya niinue kichwa na kuangalia ilipotoka. Nikakutana na Shamim aliyesimama mbele yangu. Kwa macho yalionyesha hofu ya waziwazi nikamtolea jicho la maswali, kisha kwa sauti yenye kutetemeka nikamwambia ''Shamim nadhani kwa hii kesi nitafungwa. Nitafungwa kwa kuwa hii kesi wataunganisha na ile ya kuishi na Sheila baada ya kumsaidia. Shamim lazima nifungwe miaka Isiyopungua Thelathini. Unaonaje unisaidie kuniombea msamaha kwa Sheila?'' niliongea huku woga ukiwa kwenye nafsi Yangu.

Shamim hakunijibu kwa Haraka, kwanza aliniangalia kwa jicho la huruma kisha kwa sauti yake ile ile ya kumtoa Nyoka Shimoni akaniuliza huku akionekana kupoteza furaha. ''Sasa tutafanyaje Ibu Wangu!!?'' likawa swali gumu sana, lakini wakati najiandaa kujibu swali la Shamim wote tukaitwa ndani. Kuisikia sauti ya afande yule nikahisi moyo wangu ukipiga mpaka kuhisi unatoka. Nikawa natetemeka huku nikihisi nguvu kuniishia. Nikatembea huku nikisali kimoyo moyo. Jela sio sehemu sahihi ndugu zangu. Jela sio sehemu ya kwenda kwa binadamu. Miguu iligongana huku mdomoni jina la Mungu likitawala. Tulipoingia ndani tukaambiwa tuelekea ofisi ya mkuu wa kituo. Tukaendelea kutembea huku shamim akiwa nyuma kisha mbele alikuwa Sheila na Jamaa yake. Hapo niliiishiwa kabisa, nikatamani kumuuliza shamim lakini mdomo ulikuwa mzito kufunguka. Tulitembea mpaka ilipoofisi ya mkuu wa kituo. Wakatangulia Sheila na Jamaa yake, kisha Shamim, harafu nikaingia na mimi.

Ndani ya chumba kile kulikuwa na watu watatu. Kwanza alikuwepo Mkuu wa Kituo mwenyewe, wapili alikuwa hakimu aliyenisomea Shitaka la kudhulu mwili kule Hospital na watatu alikuwa ni mwanamama fulani ambaye sikuweza kumtambua. Baada ya kuingia nikashangaa macho ya watu wale watatu wakinitizama mimi, tena walikuwa wakinitizama katika Aina ya Chuki, hasira na Ghadhabu. Nikahisi kutetemeka maradufu. Tukaamriwa wote tukae. Nilikaa huku nikiwa sina imani. Kumkuta hakimu wa kesi Yangu ofisini kwa mkuu wa kituo kulinitia hofu sana. Nikatulia nikiendelea kumuomba Mungu. Punde nikamuona Sheila akiingiza mkono wake ndani Ya Mkoba na kutoa burungutu la pesa na kuliweka juu ya meza ya Mkuu wa kituo. ''Umeamua kweli Kuifuta hii kesi?'' lilikuwa swali lililoingia moja kwa moja katika masikio Yangu. Nikatamani kuruka kwa Furaha. Lakini nilijizuia nisifanye hivyo kitu. Niliendelea kusali huku nikisubiri jibu la Sheila.

''ni kweli nimeamua kuifuta hii kesi kwa kuwa wema aliyonitendea kabla ya matatizo haya ulikuwa mkubwa kuliko huu ubaya ambao nataka kumlipa. Hastahili haya yaliyomtokea. Ndio maana nimeamua kuifuta hii kesi ili kila mmoja aishi kwa amani.'' akajibu Sheila Huku akishindwa kuzuia machozi yasimdondoke: alikuwa akipingana na kitu katika moyo wake. Alikuwa akipingana na Mapenzi, Mapenzi juu ya Ibu. Nikahisi kile kitu kilikuwa ndoto, nilihisi ulikuwa mchezo wa kunizuga, lakini nilipomuona Shamim akiinuka na kwenda kumkumbatia Sheila na kuanza kumfuta Machozi, nikaamini kuwa huu ulikuwa muujiza kwangu. Muujiza uliyonitoa kwenye Kifungo kilichokuwa kikinikabiri. Baada ya Muda wote tukapeana mikono kisha kuruhusiwa Kuondoka pale kituoni Huku nikiwa Huru. Tulipotokea Nje nikashangaa Kumuona Shamim Akiondoka pamoja na Sheila na Yule Jamaa, Wakiniacha pale nje nikishangaa nisijue wapi nielekee.
 
MATESO YANGU

SEHEMU YA 015

Nilibaki nimeshikwa na mshangao nikiangalia kile ambacho kilikuwa kikitokea. Ingawa nilikuwa nimeachiwa huru baada ya Sheila kuifuta kesi, lakini kuondoka kwa shamim sambamba na Sheila kulinifanya niduwae kwa muda. Nikajiuliza ni huyu huyu Shamim kweli? Ni huyu aliyekuwa akinifariji kipindi chote hiki? Kwa ni ni ananiacha sasa? Baada ya kujiuliza maswali hayo na kukosa majibu, nikaamua kuwafuata kwa nyuma huku nikijaribu kumuita Shamim japo anisikilize kwa muda. Shamim hakujisumbua kugeuka, ndio kwanza alikuwa akiingia kwenye gari na kuufunga mlango bila hata kunitizama. Nikaona huu mbona ni Ujinga, Huu ninao uleta mbona ni upumbavu. Kama Shamim hataki kuongea na mimi kwa nini niendelee kujisumbua? Baada ya kuwaza hilo, nilichofanya ni kuondoka pale na kuelekea kituo cha daladala tabata shule. Nikasubiri daladala za posta na ilipofika nikajipakia na kuondoka kuelekea posta na baadae kigamboni. Nilitulia huku nikiwaza kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika maisha yangu mara nilipoanza mahusiano na Sheila. Nilitulia kwa muda nikiwachambua Sheila na Shamim, kila mmoja alikuwa mzuri katika kiwango bora na cha hali ya juu, licha ya uzuri Huo lakini bado Shamim alikuwa bora kuliko Sheila. Lakini mabadiliko ya ghafla baada ya kutoka pale kituoni yaliniacha na maswali mengi sana. Maswali ambayo yalinifanya nipitiwe na usingizi ambao nilikuta nikija kushtuliwa baada ya daladala kufika Posta.

Nilishuka posta na kuchukua daladala jingine lililonifikisha feri. Nikashuka na kupanda pantoni, kila nilipokuwa nikipita kila mmoja alikuwa akinitizama kutokana na jinsi nilivyokuwa nimekonda na bandeji ambazo nilikuwa nazo kichwani. Wachache waliokuwa wakijua waliendelea kunipa pole, huku wale wengine ambao hawakuwa wakijua wakawa wananiuliza.

******

Ilikuwa ni Usiku wa saa tatu baada ya kupita siku mbili tokea kutolewa hospitali na kufutiwa mashtaka. Nilikuwa chumbani kwangu nikiangalia picha nilizopiga na Sheila kipindi tukiwa kwenye mapenzi motomoto. Nilikuwa nimezama katika kuutafakari upendo ule, upendo uliyochipua mithili ya juu la asubuhi na kuzimika mfano wa barafu. Bado sikujua kipi ambacho kilimsibu Sheila mpaka kutokea kunikatili kwa kiasi kama kile. Nilikumbuka nilivyokuwa nikimlisha, nilikumbuka nilivyokuwa nikimbeba na kuzunguka naye Chumba kizima huku tukicheka na kutaniana. Nilikumbuka siku nilipokuwa nikimkanda maji ya moto baada ya kuufungua mlango wake kwa mara ya kwanza. Hapo nikahisi chozi likidondoka katika picha, nilikuwa nikilia bila kujitambua. Nikaitizama picha moja ambayo alikuwa kifua wazi, chuchu zake mfano wa michongoma zikiwa zimesimama kifuani zilinifanya nilie. Nikiwa bado nipo katika maumivu na mateso nikasikia mlango wa chumba changu ukigongwa. Nikajifuta vizuri na kuuficha ukweli kuwa nilikuwa nikilia. Sikutaka mama ajue kuwa nilikuwa nikilia. Hata nilipokwenda kuufungua nikajua ni Mama Yangu. Nikakishika kitasa na kuufungua mlango huku nikiruhusu macho Yangu yatizame mgongaji. Nikashtuka nusura ya kuanguka chini baada ya kumuona mgongaji.

Mgongaji ambaye sikutegemea kumuona pale. Alikuwa Sheila akiwa amesimama katikati ya mlango wa chumba changu. Nikabaki kumtizama nisijue kipi cha kufanya, nisijue nini nimwambie. Kwa mbali nikaanza kushikwa na Hasira. Lakini Sheila hakunipa nafasi, nikashtukia akinitia kikumbo na kuingia chumbani kwangu. Aliongoza mpaka kitandani na kukaa juu yake kisha kuanza kuvua nguo zake moja baada ya nyingine. Nikaamua kutoka nje nikimuacha peke yake Chumbani. Nilikaa nje ya chumba changu mpaka saa saba za Usiku huku nikiona kutokuwepo kwa dalili za kuondoka kwa Sheila. Baada ya kuiona hiyo Hali ngumu, nikaamua nimpigie simu Shamim usiku ule ule kumwambia kile kinachoendelea kwangu. Nikaitafuta namba yake na kuipeleka Simu yangu sikioni. Simu iliita kwa muda lakini ikakatwa, nilipopiga kwa Mara nyingine ikapokelewa na Sauti ya Kiume. Hapo nikahisi maumivu makali sana. Ingawa sikuwa nimewahi kutembea naye lakini kitendo cha simu yake kupokewa na mwanaume kuliniuma sana. ''hivi hawa kweli ni wanafunzi? Wanafunzi gani wana mambo kama ya Aina Hii?'' nilijiuliza maswali yasio na majibu.

Roho iliniuma sana kwa namba ya Shamim kupokewa na mwanaume tena usiku wote ule. Nikiwa bado naweweseka kwa Wivu nikauona ujumbe wa Sms Ukiingia kwenye Simu Yangu ya Mkononi ''Shamim Yupo Hospitali amelazwa.'' ulisomeka Hivyo Ujumbe huo. Nikashangazwa na taarifa ile, nikatamani niondoke usiku ule kuelekea huko, lakini nilipofikiria Sheila kule Chumbani nikaona siwezi kumuacha. Nikaamua nirudi chumbani nikamuulize sheila nini alichokifuata kwangu. Nilipousukuma mlango na kuingia Chumbani, nikakutana na Tukio la kutisha. Sheila alikuwa chali kitandani huku akitoka mapovu mdomoni na Chini Pakiwa na Glass pamoja na Vidonge vichache. Nikajua Sheila Ameshajiua kwa kumeza Idadi kubwa Ya Vidonge. Nikahisi kizunguzungu Huku nikipiga Yowee Kubwa Sana kuwaita Majirani.
 
MATESO YANGU

SEHEMU YA 016

Nilipiga kelele huku nikimtingisha Sheila, lakini bado alikuwa amelegea kama mlenda. Bado hakuonesha kuwa na uhai. Punde majirani wakajaa nyumbani. Wengine wakakimbia nje kutafuta maziwa. Muda wote nilikuwa nikitetemeka kwa woga, nilikuwa nikihisi sheila kutokuwa hai. Muda wote nilikuwa nikimuomba Mungu. Maziwa yakaletwa na kazi ya kuutanua mdomo wa Sheila ikaanza. Meno yalikuwa yamekutana, haikuwa kazi ndogo lakini baada ya muda watu walifanikiwa hivyo kumuwezesha Sheila kunyweshwa Yale maziwa kwa nguvu. Baada ya kunywa maziwa na kuachwa atulie kidogo, Sheila akaanza kutapika, alitapika mpaka nikawa namuonea Huruma. Licha ya kisitani na mabaya yote aliyonitendea lakini ytote nilikuwa nimeshayasahau kutoka na Tukio lile. Nilikuwa karibu na Sheila kila wakati nikiangalia kama anaweza kuwa amerudiwa na fahamu. Kila nilipokuwa nikimuona alivyokuwa anatapika, nilizidi kupatwa na kitu moyoni. Baada ya kuonyesha kumaliza kutapika, tukambeba na kutoka naye nje Tayati kwa safari ya kuelekea Hospitalini.

******

alikuja kurudiwa na ufahamu saa tisa na nusu usiku. Kufumbua kwake macho kulifuatiwa na tukio la kuangaza huku na huko, bado alishangazwa na sehemu alipokuwa amelala. Nami nikaendelea kumwangalia bila kuonyesha tofauti yoyote. Sikutaka kumuita wala kumshtua, nilitaka kumuacha kwanza. Wakati nikilitafakari hilo, akageuza macho yake kutizama kule nilipo. Kukutana kwetu uso kwa macho kukasababisha kitu kingine ambacho hakuna aliyekitegemea. Sheila aliangua kilio kikubwa huku akilalamika kitendo cha kumuokoa. Hakutaka kuokolewa eti, Alihitaji kufa. Akaniangalia kwa macho ya Ghadhabu. Hapo nikahisi akili Yangu Ikihama, hapo nikahisi Hasira, Hasira ambazo sikujua wapi zilipotoka. Kwa nini anilaumu? Kwa nini anikaripie kama mtoto? Huyu Sheila ni Mzima kweli? Si aliniacha kwa kashfa, kwa nini sasa aniwakie kama mtoto? Yalikuwa maswali ambayo yalipishana kichwani mwangu. Nikiwa bado nipo kwenye Pumbazo la Nafsi, nikaisikia Simu Yangu ikiita, nikaitoa Haraka mfukoni ili nicheki namba ya mpigaji. Nilipoitoa na kuangalia, nikashangaa kumuona mpigaji akiwa Shamim. Nikatulia kwanza nikiitizama ile Simu bila kuipokea. Nilikuwa nikiogopa kupokea mbele ya Sheila Kuhofia kuwa Lingetokea Jingine.

Sheila naye kama alishtuka hivi, akanitupia jicho la Hasira Huku akinitaka niipokee simu. Kwanza nilisita, nilipoona anang'ang'ania nikamwambia haina umuhimu.. Nilipomjibu hilo akaniambia nimpe yeye aipokee. Nikahisi fundo likinikaba kooni, nikatamani hata kumtukana au kumwambia yeye ni nani mpaka apokee simu Yangu. Ila nilipokumbuka wema alionitendea kwa kuifuta kesi, nikaamua kupokea simu. Nilikutana na sauti ile ile ya siku zote, Sauti Ya Shamim. Nikashusha pumzi kisha nikamkata jicho Sheila. Nikasikia ''Hallow Baby wangu nikupendaye.'' nikapatwa na furaha ya Ajabu nikajikuta nikitamka NAMBIE MKE WANGU NIKUPENDAYE tena mbele ya Sheila.. Hayakuzidi maneno Zaidi nikamuona Sheila akifanya kitu ambacho kilimshangaza hataa daktari. Sheila alikuwa akichomoa sindano iliyokuwa akiingiza maji mwilini mwake.

Kilikuwa kitendo ambacho sikukitarajia wala kutarajiwa na Daktari pamoja na wauguzi. Ilikuwa patashika kubwa sana pale Hospitalini. Kitendo cha kumuita Shamim mke Wangu mbele yake kilimuuzi sana. Kwa kusaidia na madaktari na wauguzi tulimkamata na kumzuia kufanya kile ambacho alitaka kukifanya. Baada ya kumtuliza madaktari wakamchoma sindano ya usingizi.

Moyo Wangu ulishaanza kushiba penzi la Shamim, moto wa mapenzi ulikuwa ukiwaka ndani ya Moyo wangu. Niliondoka pale Hospitalini huku mawazo juu ya Shamim yakinitawala. Sikuwa namuwaza tena Sheila, nilimuona ni kama msaliti na mwenye majivuno. Wakati natoka nje kabisa nje ya Geti la Hospitalini nikamuona Shamim akija usawa wangu akiwa na kijana fulani hivi mtanashati. Moyo Wangu Ukashtuka na Kupiga paa!! Shamim alikuwa ameshikwa mkono na yule kijana wakiingia pale hospitali. Kama ungebahatika kuwaona kwa mara ya kwanza, lazima Ungedhani kwamba ni wapenzi.

Shamim alinipita na kuingia ndani. Alinipita bila hata kuniangalia, alinipita hata bila salamu. Nikajenga maswali mfululizo kichwani mwangu bila Kupata majibu. Ni dakika tano zimepita tokea nilipoitwa baby na kuambiwa napendwa, lakini muda huu nilikuwa napitwa kama kisiki bila kupewa salama. Hawa vipi hawa? Kuna kitu gani wanakitafuta kutoka kwangu!? Kusema kweli nilikuwa katika wakati ambao sikuujua wala kuutambua. Wakati wa kufanywa mtoto mdogo. Nikaona huu ni upumbavu, kwa nini nisiondoke zangu na kuwapotezea wote? Hilo likawa wazo langu. Nilichokifanya ni kuondoka maeneo yale na kutokomea mtaani. Nikarudi Zangu Nyumbani nikiwa na mawazo nikafikia kujibwaga kitandani mithili ya furushi. Nilikuwa nimechoka kimawazo, kifikra na kiakili. Niliuona mzigo mzito kichwani mwangu.. Mzigo ambao sikuwa na uwezo wa kuutua wala kuutafuta Msaada wa kusaidiwa. LAITI NINGEJUA? NISINGEKUBALI KATU KATU
 
MATESO YANGU

SEHEMU YA 017

Sikuwa nakijua kile kilichokuwa kikiendelea kati ya Shamim na Sheila. Sikuujua mchezo uliyokuwa ukiendelea katikati. Nikashindwa kuamini kama wale walikuwa ni wanafunzi, wanafunzi wa kidato cha tano. Wanafunzi wanaoishi kizungu, wanafunzi wanaofanya matendo kama hawana wazazi. Nikawa najiuliza maswali ambayo asikuwa na majibu. Sikuwa na majibu kwa kuwa bado kilikuwa kizungumkuti. Kingine kilichonifanya nianze kufikitria mengine ni kitendo cha Shamim kufika pale hospitali. Hakuwa na taarifa wala sikumwambia, lakini cha ajabu amekuja hospitalini tena akiwa na mvulana wake. Hapo nikaamua kuufanya uamuzi wangu, uamuzi ambao nikusoma na kukazania katika hilo. Nikaamua kuondoka katika mahusiano. Hakukuwa na sababu ya kuwa katika mahusiano na mwanamke anayekuita mpenzi muda huu, kisha dakika mbili baadae unamuona na mwanaume mwingine. Mapenzi ambayo unaweza kudhani unapendwa kumbe unapotezewa muda. Nikaamua kufunga ukurasa wa mapenzi na kufungua ukurasa wa Masomo. Nikaendelea kufanya kazi zangu huku nikiwatoa mawazoni wasichana hawa.

Nilishinda nyumbani nikiwa peke yangu kutokana na mama kuwa safarini Tanga. Muda mwingi niliutumia nikipiga kitabu na mara nyingine kupiga stori na washkaji. Wakati nikiendelea na hayo ikaingia sms kwenye simu yangu. Nikachomoa simu mfukoni kisha nikaufungua ule ujumbe na kuyapeleka macho Yangu kwenye kioo cha Simu yangu. ''My love najisikia njaa, naomba niletee chakula sijala tokea asubuhi.'' ulikuwa Ujumbe kutoka kwa Sheila. Ujumbe ule ukanitoa katika kile nilichokuwa nimekisahau. Nilishasahau kuwa Sheila alikuwa hospitalini. Nilishasahau kuwa Sheila Alikuwa mgonjwa. Licha ya kuipata Sms ile lakini nikaipuuzia, nikaipuuzia kwa kuwa najua sheila hawezi kukosa chakula. Nilijua Shamim hawezi kushindwa kuwaambia ndugu wa Sheila na wakashindwa kuleta. Lakini nilipojiuliza kwa nini meseji anitumie mimi na sio wengine? Nikajipa jibu kuwa Kuna kitu katika hili. Nikainuka na kuelekea ndani kwetu. Wakati naukaribia mlango nikasikia Ujumbe mwingine ukiingia kwenye Simu Yangu. ''Naomba unipikie Ugali na mlenda pamoja na dagaa. Ugali usiwe mgumu. Nakupenda Ibu wangu.'' ulisomeka ujumbe mwingine kutoka kwa Sheila. Nikauangalia Ujumbe ule zaidi ya mara Tatu bila kupata jibu.

Ameshanigeuza mimi mpishi wake, ameshanigeuza boya kias kwamba ananituma kama mtumwa. Nikaona acha nimpikie kwani inawezekana hajala tokea muda huu. Kiapo changu cha kusoma nikakiweka pembeni kwanza. Nikawasha jiko la mafuta na kuelekea Gengeni kununua mahitaji. Kila nilipokuwa natembea nilikuwa nikijisemea kumbe nami nimekuwa bwege. Lakini bado kuna kitu nilikuwa ninacho katika moyo wangu. Niliunga wale dagaa, kisha kuupika mlenda na baada ya hapo nikaivisha ugali. Muda mfupi nilikuwa kwenye daladala nikiwa na kikapu changu mkononi nikipeleka Chakula Hospitali. Nilikuwa nikionekana kama mwehu, mjinga na punguani. Bado nilikuwa nikizuzuka na Uzuri wa Sheila na Shamim. Katika nafsi yangu kunakitu kilikuwa kikiniambia kuwa ili kuweka Heshima watafune wote harafu anza kuwadharau. Hilo likawa wazo zuri kwangu.

Nilippfika sehemu husika nikashuka na kuongoza moja kwa Moja ndani ya Hospitali. Nilikuwa nikijidharau na kujiona si lolot) si chochote. Kikapu Changu mkononi nikitembea kwa mwendo wa kutokujiamini. Nikauvuka mlango na kupita wodi kadhaa, kabla sijaingia chumba alicholazwa Sheila Macho Yangu yakakutana na macho ya yule kijana mpenzi wa Sheila. Hakuwa yeye pekee bali walikuwa kama watano hivi wawili kati yao wakiwa watu wazima. Nikataka kusimama kwanza na kugeuza ili nirudi nitokapo. Lakini nikaona huu utakuwa Ujinga sana. Yaani nimpikie Chakula, harafu nije mpaka hapa, kisha nirudi nacho hii hapana. Nikausukuma mlango nikaingia nikiwa na kikapu changu mkononi. Nikapokewa na macho ya watu zaidi ya saba waliokuwepo pale. Macho ambayo yalifuatiwa na Vicheko. Vicheko vya Dharau na kejeli. Hata Sheila Alikuwa Akicheka. Ambao hawakuwa wakicheka ni wawili ambao walikuwa mle ndani na walikuwa wageni machoni mwangu. Nikatembea kuelekea pale kitandani huku vicheko vikizidi. Nikatembea huku mapigo Ya Moyo yakinienda kasi. Nikawafikia pale kitandani ambapo walikaa. Nikainama na kukiweka kile kikapu chini. Sikuwa naongea chochote. Moyoni nilikuwa nafundo kubwa.

  • Baada ya kukiweka kikapu nikataka nikitoe Chakula. Lakini mama mmoja kati ya wale wawili akanizuia. ''Mkwe Wangu hawezi kula huu uchafu uliyomletea.'' ilikuwa kauli ya yule mama. Kauli ambayo ilijibiwa kwa vicheko, nilikuwa nikichekwa:. Chakula nilichopika ni Uchafu, Chakula nilichopika ni takataka. Sikujua ilikuwaje lakini nilishtukia Chozi likitoka na Kuanguka kudondoka ndani ya kikapu. Chozi ambalo lilikatisha vile vicheko. Nikainua kikapu changu na kutoka mle wodini Huku nikilia. Kwa nini wanitendee Hiki. Wakati natokea Nje kabisaa nikamuona Shamim akija mbele yangu. Hapo nikaongeza kulia na kulia, kila mmoja aliyekuwa akiona alinionea Huruma. Sheila Aliamua Kunidhalilisha tena.
 
MATESHO YANGU

SEHEMU YA 018

Nilitoka uso ukiwa umenishuka. Nilikuwa nimedhalilishwa vya kutosha. Kikapu nilichokibeba nilikiona ni kizito sana. Nilikuwa bwege kupindukia, licha ya kutendwa na kukashifiwa bado sikukoma. Hakikuwa kitendo kizuri na hakikupendeza. Bado nilikuwa nikijiuliza kosa nililowatendea. Bado nilikuwa nikijiuliza kilichosababisha nidhalilishwe. Ingawa nilitenda vile kwa huruma ya ugonjwa wa Sheila, lakini nilikuwa nimelipwa kile ambacho sikukikusudia. Nilitembea nikiwa na kikapu changu mkononi huku nikilia. Nilikuwa nikilia kwa mengi, nikilia kwa kudhalilishwa. Hata nilipofika nyumbani niliingia chumbani kwangu na kujitupa kitandani. Bado maneno ya kejeli ya yule mama yalikuwa yakizunguka kichwani mwangu. Maneno yasio na staha kutamkwa na mtu mzima umri wa Mama Yangu. Eti chakula nilichopika ni Uchafu. Kila nilipokuwa nikikumbuka hilo nikaongeza Chuki zangu kwao, Sio kwa Sheila wala Shamim. Wote walikuwa ni maadui kwangu. Wote walikuwa watu wasio na shukurani. Niliwaza mengi pale kitandani na kujutia Huruma Yangu. Nikainuka na kwenda mpaka kwenye kabati langu la nguo. Nikatoa mavazi yote ya Sheila, nikachukua picha zake tulizopiga wote. Nikakusanya pamoja na kutoka nje ya nyumba yetu. Nikachukua simu yangu kisha nikaichomoa Laini na kuitupia kwenye lundo la vitu vile. Nichukua mafuta ya taa, nikamwaga juu yake kisha nikachukua kibiriti nikawasha na kuitupia njiti juu yake.

Nikashuhudia vitu vile vikiteketea kwa moto. Sikutaka kuangalia. Nikainuka na kurudi Chumbani kwangu huku nikiwa nimeondosha kumbukumbu zote. Kumbu kumbu zenye kuumiza. Sikuwa hewani tena na hata namba niliokuwa nikitumia iliendelea kuteketea kwa Moto. Nilibaki na Simu tu. Niliendelea kuwaza hili na lile, na hata usingizini ulivyonipitia Sikujua. Nilikuja kushtuka saa mbili Usiku baada ya kusikia mlango Ukigongwa. Niliinuka na kutizama saa ya ukutani, nikakuta ikisomeka ni saa Mbili Usiku. Nikajivuta kivivu vivu Mpaka Mlangoni. Nikanyonga kitasa na kuufungua mlango. Macho Yangu yakakutana na Macho Ya Rafiki Yangu Deo King. Alikuwa mwandishi wa stori na mpenzi sana wa Mpira. Nilimkaribisha ndani Huku nikijaribu kuficha kile ambacho nilikuwa nacho.

Uso wangu bado ulikuwa katika msawajiko. Huzuni ilikuwa imetamalaki katika uso Wangu. Licha ya kitu hicho, lakini bado niliendelea kuongea na Deo. Bado nilijitahidi Kuficha kile ambacho kilikuwa Kikinisumbua. Tukaingia ndani huku nikiendelea kuonyesha Uchangamfu ili kutomuonyesha deo. Baada ya kuongea na Deo Kwa Muda mrtefu na baadae Deo kuondoka. Nikaamua kukitoa kile chakula kilichoitwa takataka na yule mama kule hospitali, kisha nikaanza kula.

*****
niliendelea na Masomo Yangu vizuri huku nikiendelea kuwasahau Sheila na Shamim. Muda wote nilikuwa shule nikisoma kwa umakini wa hali ya juu kwa kuwa mitihani ilikuwa karibu na pia sikutaka kufeli katika masomo Yangu. Kila wakati nilikuwa nikiwaza kuhusu maisha na kuhusu mawazo ya kimapenzi sikuwa nayo kabisa.

*****
ilikuwa Jioni Tulivu yenye kijua cha mbali. Nilikuwa nimesimama Posta mpya nikisubiri Gari la kivukoni. Wakati nimesimama pale akatokea mtoto mmoja wa kike mzuri sana. Alikuwa mzuri kwa macho na mzuri kwa kumtizama. Kila alipokuwa akipiga hatua ndivyo mwili wake ulivyokuwa ukitingishika na kusababisha mgongani katika mioyo ya wanaume kadhaa waliokuwa wakimtupia macho. Kama kuna watu walipendelewa kuumbwa Huyu Binti Alikuwa ameumbwa. Kama ni Mungu kupoteza muda katika kuumba, basi hata ilipoteza muda mwingi sana. Mguu ni mguu kweli, Jicho ni jicho kweli, tabasamu lenye uwezo wa kumnyamazisha mwanaume yoyote mwenye mdomo na Bahili. Kama walivyokuwa wakimshangaa watu wengine, basi hata na mimi niliendelea kumshangaa hivyo hivyo. Lakini Mshangao wangu ukazidi zaidi pale yule msichana alipoonyesha kuniangalia Huku akitabasamu na kilichonichanya ni ile kuonyesha kuja uelekeo ambao nilikuwepo miye. Nikahisi mapigo ya moyo yakibadili gia angani kama Chadema na mwenyekiti wao. Nikakodoa jicho kutizama mwendo mujarabu, mwendo matata kama ule wa Mwanadada Happyness Wa Swagger. Nikatulia kama maji mtungini. Nikatulia kama nipo kwenye kitanzi nikisubiri Kunyongwa. Wakati nikiendelea kulituliza Jicho langu nikasikia mtu akinishika bega huku akisema NILIKUWA NAKUTAFUTA..
 
MATESO YANGU

SEHEMU YA 019

Wakati namshangaa yule binti, nikashikwa bega kisha nikasikia mtu akisema kuwa alikuwa akinitafuta mimi. Ilikuwa sauti ngeni masikioni mwangu, sauti ambayo sikuwahi kuisikia popote. Ilikuwa sauti ya mwanaume. Nikageuka nikiwa katika wasiwasi mkubwa sana. Ni nani mwenye kunitafuta? Ni nani huyu na ametoka wapi? Yalikuwa maswali niliyojiuliza. Hata nilipogeuka na kutizamana naye, bado sura yake ilikuwa ngeni machoni mwangu, bado sikuwa namfahamu. Huyu ni nani? Au ananifananisha? Alikuwa jamaa mmoja ambaye sikuwa nikimkumbuka wala kukumbuka ni wapi aliwahi kukutana na mimi. Nikawa namwangalia usoni bila kuongea kitu. Naye alikuwa akinitizama, bila shaka alikuwa akifikiria kipi cha kuniambia ama nadhani alikuwa amenifananisha. Na mimi nikabaki kuwa kimya, kimya kwa kuwa yeye ndiye aliyenifananisha. Anatakiwa kuongea yeye... Nilipomuona bado ameendelea kuwa kimya, nikataka kujisogeza pembeni, lakini bado yule kijana alikuwa ameushika mkono wangu tena safarii akionyesha hakuwa na utani. Nikabaki kumtumbulia macho hasira zikianza kunipanda, nikamwangalia kwa macho makali kwa muda wa dakika moja nzima nikamuona akiniachia mkono na kuniambia kuwa alinifananisha.

Nilimuangalia yule kijana kwa muda mrefu bila kuongea kitu, hata aliponiomba msamaha kwa mara ya pili bado nilikuwa nikimwangalia tu. Niliendelea kusimama pale kituoni kwa muda huku macho yangu yakianza kumtafuta yule mdada. Niligeuza macho huku na Huko nikimtafuta bila mafanikio. Kila nilipokuwa nikitizama sehemu zote, bado sikuweza kumuona. Kimoyomoyo nikawa namlaani yule kijana. Wakati nikitizama huku na huko nikasikia sauti ikitokea Nyuma Yangu ''habari yako kaka?. Ilikuwa sauti ya mwanamke. Sauti iliyonifanya nianze kuwaza mambo mengine. Nikageuka huku nikiitoa mikunjo ya Hasira usoni mwangu. Kugeuka kwangu nikakutana na sura ile ile ya Yule binti niliyekuwa nikimtafuta pale posta baada ya kunipotea. Sasa alikuwa mbele ya macho yangu akitabasamu. Mbele ya uso, kifua na mbele ya macho yangu. Tabasamu na matata sana likiupamba uzuri wake aliotunukiwa na Mungu. Uzuri ambao haukugusa make up wala kipodozi cha aina yoyote. Bado alikuwa natural Skin, bado ngozi asilia ilimpendeza. Rangi ya maji ya kunde ilimfanya ang'aa na kumeremeta.

Nikajikaza kuijibu sauti salamu yake lakini bado nilikuwa katika bumbuwazi. Huyu ni nani? Kwa nini mimi na asiwe mwingine hapa kituoni? Au ni walewale? Bado sikutaka kumuamini, bado sikutaka kuonyesha kuvutika kwake. Kuwapita watu wote kuja kwangu ni wazi kuwa ananifahamu, ananifahamu tena sana. Nikaituliza akili yangu kwanza nisijefanya maamuzi ya kukurupuka. Nikamwangalia tena na tena.. ''naitwa Rehema Ally, nipo Udsm Mwaka wa Pili nikisomea uchumi ngazi ya Degree.'' (BACHELOR DEGREE IN ECONOMICS AND DEVELOPMENT) akajinasibu mrembo yule huku midomo yake ikicheza na macho yake yakinitizama kwa kuibia ibia. Nikashangazwa na hali ile ya kujitambulisha kwangu pasipokuwa na wasiwasi wa Aina Yoyote. Nami nikamwangalia kwa makini huku nami nikijishauri kumwambia ninachokisomea ama nipotezee tu. Kwanza nilipofikiria kozi ninayoisoma na kiwango changu cha kozi ninayoisoma.. Nikajikuta nikinyamaza kwa Muda. Nimfiche ama nimwambie kweli? Nikimficha siku akigundua si ataniona Muongo? Kwa nini nimdanganye? Nilipojiuliza sana na kukosa majibu nikaona acha nimwambie Ukweli.

''Naitwa Ibrahim Masimba, nipo CBE mwaka wa kwanza nikisomea Utawala wa Biashara Ngazi Ya Cheti. (CERTIFICATE IN BUSINESS ADMINISTRATIONS) nilijibu huku nikimtupia macho yule msichana. Bado sikumuamini na bado sikutaka kumuamini. Huwezi kukutana na mtu harafu akuzoee kwa ghafla kiasi hiki. Nilazima pawe pana namna. Nilipojitambulisha akaniangalia kisha kwa sauti ya Taratibu nikasikia ''pole sana!!'' nikajiuliza mwenyewe kimoyo moyo.. Pole? Pole ya nini? Wakati nikizama kwenye lindi la mawazo la kujiuliza maswali juu ya Pole niliopewa, nikasikia tena Chukua mawasiliano yangu haya tutaonana siku nyingine. Nikapokea mawasiliano yake na kuweka mfukoni kwangu. Nikashuhudia mtoto akiondoka akitembea mfano wa kinyonga. Mwendo mardadi wenye kuvutia kutizama bila kuchoka. Hatua kumi mbele pembeni ya Jengo la Benjamin Mkapa Tower nikamuona akichukua Tax na Kuondoka bila hata kuangalia Nyuma. Nikaachwa nikiwa katika butwaa, butwaa la ajabu sana, butwaa la kutokujua kipi kinaendelea. Nilipotizama pembeni nikakutana na macho ya watu waliokuwa wakitufuatilia kwa macho. Sikutaka kusubiri kuangaliwa Zaidi. Nilichofanya ni kuchukua Piki piki na kuondoka eneo lile.

****
niliingia nyumbani saa moja kamili usiku nikionekana ni mwenye mawazo mengi sana. Kile nilichokutana nacho posta kiliichanganya sana Akili Yangu. Kilinifanya nitumie muda mwing kumuwaza mrembo Yule. Wakati nimezama kwenye Dimbwi la Mawazo Simu Yangu Ikatoa sauti kuonyesha Kuna meseji Imeingia. Nikaichukua na Kuifungua. ''HATA UWE KIMYA VIPI TAMBUA NINA MIMBA YAKO'' Ulikuwa Ujumbe kutoka kwa Sheila. Mmhhh! Nikaguna...
 
MATESO YANGU

SEHEMU YA 020

ulikuwa ujumbe kutoka kwa sheila, ujumbe kwamba ana mimba yangu. Kwanza nilipigwa na butwaa mwili mzima. Nikaingiwa na baridi ya ghafla. Baridi ambayo sikuijua wapi ilipotoka. Sheila hakuwa na namba yangu, sijawahi kumpa namba yangu mpya. Kwa nini anitumie sms kupitia namba yangu mpya? Nikawaza na kuwazua kama nishawahi kumpa rafiki yangu namba yangu, lakini kumbukumbu zilinambia sikuwahi kuigawa namba. Mtu pekee mwenye namba yangu alikuwa ni mama yangu mzazi, hata baba yangu sikuwa nimempa namba yangu. Nani amempa Sheila namba yangu? Ina maana mama ameigawa namba yangu. Kama ameigawa inamaana hajui miye na Sheila tukoje? Hajui mimi na sheila tuna mahusiano gani? Lakini kama sio mama, Sheila kaipata wapi namba Yangu? Maswali hayo yakanipa muwashawasha wa kumpigia mama yangu simu. Nikaipeleka simu sikioni, muda mfupi ikaanza kuita.. Punde mama akapokea akiongea kwa sauti ya taratibu. Kutokana na kimuhemuhe nilichokuwa nacho juu ya Ujumbe aliyonitumia Sheila. Nikasahau hata kumsalimia, nilichofanya ni kumuuliza kama yeye ndiye amempa Sheila Namba Yangu. Mama yangu akanijibu kuwa ni yeye aliyempa Sheila namba Yangu. Na alifanya hivyo baada ya Sheila kumtumia ujumbe kuwa alikuwa na mimba Yangu na kwamba amenitafuta bila mafanikio hivyo alitaka kuniambia mapema ili nitambue hilo.

Maneno ya mama yalinivunja nguvu, nikaiona jela ikinijia mbele yangu. Ukapita ukimya wa muda huku nikitafakali chakufanya. Hivi ni kweli Sheila anamimba ama ndio ameamua kunitisha ili kumrudia? Nilibaki kimya huku nikisahau kuwa nilikuwa nimempigia mama yangu. Nikaona huu ni muda wa mapito. Nikaamua kuusimamia msimamo wangu. Niliamua kuupuuzia ujauzito Ule. Nikaamua kuendelea na msimama wangu. Sikutaka kumsikia tena Sheila. Nikaamua kuikata simu na kuizima kabisa. Sikutaka kumjibu wala sikutaka kuwasiliana na Mama kwa kuwa nilijua kipi ambacho atakiongea.. Kwa hiyo nilichoona ni muda muafaka kwa wakati ule ni kuizima simu ili nikipe kichwa changu muda wa kufikiri na kuwazua kuhusu hiki kitu. Kweli niliizima simu kisha nikawa nafanyakazi zangu nyumbani. Lakini licha ya kujitahidi katika kutoliwaza tukio la ujauzito wa sheila, nilishindwa. Nilijikuta Muda wote nikiliwaza kuhusu hili la sheila. Nilikuwa muoga nikiogopa na kuhofia. Nilikiona kifungo kikinijia kwa kasi ya ajabu. Nikaufikiria ukali wa baba wa Sheila hapo nikakosa hamu kabisa. Hapo nikaona niiwashe simu, nilihisi kuizima simu kuna weza kuniletea matatizo. Nikaiwasha na kusikilizia. Mara ujumbe ukaingia kwenye simu. Nilipoangalia namba, nikakuta ilikuwa namba ya Sheila. Nikaifungua Sms Huku nikitetemeka ''Unadhani kuzima simu ndio suluhisho? Nitakupoteza Ibra!!'' ulisomeka Ujumbe ule kutoka kwa Sheila. Wakati bado sijajua kipi cha kufanya, Ujumbe mwingine Ukaingia kwenye Simu Yangu. Huu ujumbe ulikuwa ukitoka kwa Mama.. ''mwanangu naomba kaa chini na mwenzio myaongee hili suala ni kubwa kuliko unavyowaza na kufikiria wewe.'' ulisome ujumbe kutoka kwa mama. Hapo nikachoka na kukiona kichwa changu kikizunguka, kichwa changu kikishindwa kupata majibu sahihi na Njia ya kunitoa katika suala hili. Hivi ni kweli nimrudie Sheila? Ni kweli nikaongee na Sheila? Kashfa na dharau nilizoletewa siku ile, zilinifanya niumie sana.

Nikauona ugumu wa Mimi kumfuata Sheila na kuongea naye. Nilikuwa nimechoka katika suala hili. Nikaufikiria mustakabali wa maisha Yangu. Ndoto za maisha yangu, nikipelekwa gerezani si utakuwa mwisho wa ndoto zangu. Kwani nikiomba msamaha kipi kitaharibika? Kipi nitapungukiwa? Hapa natakiwa kuomba msamaha katika aina zote. Nikaichukua namba ya Sheila Kisha nikaipiga. Iliita kwa Muda mrefu bila kupokelewa mpaka ilipokata yenyewe. Sikuchoka wala sikutaka kuacha. Nikampigia tena kwa mara ya pili, lakini bado hali ilikuwa ile ile. Simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Na hata mara hii Simu ilikata bila kupokelewa. Nikaona huu ni Ujinga. Nikaamua kuacha kabisa. Nikaamua kutokupiga simu tena. Nikaachana naye nikaendelea na mambo yangu.
 
MATESO YANGU

SEHEMU YA 021

Niliamua kukaa kimya na kutokumtafuta tena. Nilikuwa nimejiandaa kwa lolote na kwa chochote. Sikutaka kumbembeleza wala kumnyenyekea. Wakati nikiamua hivyo nikauona mlango ukisukumwa kisha mwanamke kuingia. Aliingia na kuongoza mpaka niliposimama kisha kitendo bila kutarajia akapiga magoti huku akiishika miguu yangu. Alikuwa Sheila akiniomba msamaha kwa kupiga magoti. Nikashangazwa na kupumbazwa na kitendo kile. Maswali yakatiririka kichwani mwangu. Sheila ananipigia magoti? Sheila leo anaomba msamaha kwa kunipigia magoti? Hii kwangu ilikuwa ni zaidi ya tamthiliya ya kikorea, hii ni zaidi ya Tamthiliya za kifilipino. Hii ilikuwa ni drama kubwa kuwahi kutokea. Sheila aliamua kuigiza sinema katika mahusiano yetu. Alikuwa ni mfano wa filamu za Bongo Movie. Filamu ambazo hazieleweki wala kuelezeka. Nikaendelea kuangalia maigizo yake nikiwa nimenyamaza kimya. Nilikuwa nikimuangalia kwa macho. Nilishindwa kuamini na hata nilipoituliza akili yangu ili niamini bado nilikuwa katika kitendawili kikubwa. Kitendawili ambacho ilibidi nikitengue katika wakati ule. Nikatamani kumuinua pale chini, lakini nilipokumbuka kashfa na matusi niliopewa kule hospitali hakika moyo Wangu Uliingia baridi kabisa. Nilikumbuka siku ile nilipokuwa nikimpigia magoti pale mabibo mbele za watu, nikakumbuka tusi alilomtukana mama yangu.

Hapo nikainua mdomo wangu na kumuomba ainuke. Lakini bado aliendelea kulia tena machozi yakishuka chini. Sheila alikuwa ni muigizaji Zaidi ya Riyama Ally, alikuwa mtaalam wa kucheza na hisia za Moyo Wa mwanaume. Bado hakuinuka na bado hakuniangalia. Nilichofanya ni kuinama na kumshika mikono ili kumuinua. Kitendo bila kuchelewa nikajikuta Sheila akiwa kifuani kwangu na Ulimi wake ukitafuta Hifadhi katika Kinywa Changu. Sikuweza kuukataa ulimi ule wala kuugomea. Niliupa hifadhi Huku mikono Yangu iliyokosa adamu akivinjali ndani ya kisketi alichovaa. Nilikuwa nikigusa hapa na kuachia pale, nikanyonya hapa na kuachia pale. Punde kidogo Sheila alikuwa mlenda wa bamia kitandani macho yakikosa nuru katika kutizama. Sikukurupuka nikataka kumuonyesha kuwa ingawa hanipendi lakini mimi ni nyoko. Nilimpambua nguo zote na kumuacha mtupu akiwa amesawajika kitandani. Nikamuangalia tena safari hii kwa dharau kubwa sana. Nikamtizama jinsi alivyolala. Nikasogea kama nataka kupanda lakini nikatema mate na kumwambia avae nguo zake aondoke ama akaoge.

Yalikuwa maneno yaliyomuinua Sheila Kitandani kwa kasi, kumwambia akaoge lilikuwa tusi kubwa kumaanisha Sheila alikuwa akitoa Harufu. Kuinuka kwake kulifuatia na kitendo cha kuinyanyua chupa Ya Soda Iliyokuwa Mezani na kuirusha usoni kwangu, nikawahi na kuukwepa. Sasa kilichoendelea ilikuwa ni vita kila ambacho alikishika alikuwa akikirusha kwangu. Na hata alipokishika kisu, nikashangaa akikielekeza Tumboni kwake tayari kujichoma. Hilo likanifanya nimuwahi na kuanza kumpokonya. Tukiwa katika ugomvi huo wa kupokonyana kitu Mlango ukasukumwa tena kwa nguvu, wakaingia askari wanne, Shamim, yule mama pamoja na watu wengine ambao sikuwajua.

Cha kushangaza na kusikitisha baada ya sheila kuwaona wale askari akaanza kupiga kelele kuwa nilikuwa nataka kumbaka. Hilo likanifanya niishiwe nguvu na kumuachia. Nikataka kujaribu kuongea lakini kitako cha bunduki kutoka kwa polisi mmoja kikatua usoni kwangu na kunipasua Juu kidogo Ya Jicho. Nikajisikia kizunguzungu na kupepesuka. Kabla sijakaa sawa nikahisi teke likinipiga ubavuni. Lilikuwa Teke Zito sana, teke lililonifanya nihisi maumivu makali sana, maumivu ambayo yalinifanya nipige yowe. Kupiga yowe kwangu lilionekana kuwa kosa kubwa. Nikashtukia kiatu kikitua Usoni kwangu. Nikashindwa kuhimili huku sauti akikata na macho kuingia kiza. Nikanyooka kama mfu nikishindwa kujua kile ambacho kiliendelea pale.

Nilikuja kugutuka saa tisa usiku nikiwa nimelazwa katika Hospitali ya Jiji kule vijibweni kigamboni. Nilikuwa nimetundikiwa drip za damu zikishuka huku na huku. Uso ulikuwa umevimba kupindukia huku nikiwa nimezunguushiwa tena bandeji.

Macho yangu yalikuwa yakiona kwa mbali sana, hayakuwa na uhai wa kufanyakazi kama mwanzo. Kwa nini nafanyiwa hivi? Nimemkosea nini Sheila Miye? Nimemkosea kitu gani mpaka kunionea hivi? Mungu naomba nisaidie baba, nisaidie Mungu wangu. Nateswa bila sababu ya msingi. Naonewa pasipo na kosa lolote. Nilini Mungu nitatoka katika mikono hii. Nikaliona Chozi langu likishuka na kudondoka mashavuni. Nilikuwa katika kiwango cha juu cha uonevu. Kwa nini lakini? Kwa nini sheila lakini? Nini unachokitaka kwangu? Kweli anadiliki kupiga kelele kuwa nilitaka kumbaka. Bila kujua kuwa alikuja kwetu na kunifuata mpaka Chumbani Kwangu. Kipi Nimekukosea Sheila? Kipi kibaya nimekutendea? Niambie basi nije nikuombe Msamaha. Kwa nini UNANITESA HIVI SHEILA? AAAAAH!!!
 
MATESO YANGU

SEHEMU YA 022

Niliona mateso makubwa iwapo nitaendelea na Sheila. Mwili wote ulikuwa ukiniuma. Masikio yangu hayakuwa yanasikia vizuri. Niliendelea kujitizama machozi yakinishuka na kuendelea kunilowanisha. Sikuwahi kuona mapenzi yanayonitesa kama haya. Mapenzi yanayoniliza na kuniumiza mfano huu. Kwa nini mimi? Yalikuwa mateso makali sana kwangu. Niliendelea kulazwa pale hospitalini bila kuwa na msaada wa mtu kwa kuwa mama hakuwepo hapa jijini. Hata kula yangu ilitokana na majirani waliokuwa wakiniletea chakula. Mpaka siku ya tano ndipo mama yangu na baba yangu wakiambatana na dada zangu wakafika. Kitendo cha kunikuta katika hali ile kilionyesha kuwaumiza na kuwatesa dada zangu. Walionekana kupaniki na kuanza kuongea maneno makali juu ya Sheila. Waliapa kumshikisha adabu iwapo atakwenda ama kurudi pale nyumbani. Niliwaangalia tu huku nikiendelea kulia, ni ukweli usiofichika kuhusu kupendwa na dada zangu. Kuwa kwangu mtoto wa mwisho kulinifanya dada zangu wanipende na kutotaka kuonewa na mtu yoyote. Nilikuwa nikiendelea kutoa machozi, maneno ya dada zangu yakanipa hasira kali juu ya Sheila. Nikaapa kuwa nikitoka na nikifanikiwa kumtia mikononi mwangu basi ningekwenda kufungwa kwa Kosa la kuua. Nilikuwa nimekasirika kwa kiwango kikubwa sana.

Wakati dada zangu wakiendelea kuongea kwa jazba, ghafla nikamuona mwanadada yule wa Posta akiingia pale ndani. Huyu alikuwa Rehema Ally. Mwanadada ambaye muda wote alionekana kutabasamu hata pale alipokuwa amechukia. Alikuwa akiingia ndani huku akionesha kushangazwa na maneno kutoka kwa dada Zangu. Hata wote walipomuona na kutizamana na kusalimiana, kila mmoja akanyamaza kumtizama malikia yule akitembea. Hata alipowasalimia hakusimama, bali aliendelea kusogea pale kitandani nilipolazwa mimi. Alionekana ni mwenye huzuni na huruma sana, macho yake mazuri yaliobeba kitu kama mapenzi yakanitizama. Kunitizama kwake kukafuatia na kitendo cha kuliona chozi lake. Chozi lililotoka kwenye macho yake. Alionekana kunionea huruma sana. Ila kwa upande wangu sikuwa namuamini na sikuwa natamani kuwa na mwanamke tena, lakini kule kuonyesha kuguswa na matatizo yangu kulinifanya nimfanye kuwa rafiki badala ya mpenzi. Alinishika hapa na kuniachia, akashika pale na kuachia huku. Dada Zangu wote walikuwa katika mshangao na sura zenye maswali.

Kila mmoja alitaka kumjua Rehema, kila mmoja alitaka kujua alikuwa nani kwangu, alitaka kujua ametokea sayari gani mpaka kufika hapa duniani. Walisubiri majibu kutoka kwangu, hata baba na mama walikuwa kwenye mkumbo ule. Wote walikuwa na maswali vichwani vyao. Kila mmoja alikuwa akijiuliza kuhusu Rehema. Huyu ni nani? Nikaona ni muda wa kuwaambia, nikamuita Rehema kwa sauti ya Chini, akaacha kile alichokua anafanya kisha kunitulizia macho usoni, nikakutana na Neno Mapenzi Katika Macho yake.. Neno ambalo sikutaka kulipa nafasi Moyoni mwangu. ''kutana na mama yangu pamoja na Baba. Huyu ndiye Mrs Masimba na Yule ndiye mr Masimba.''Niliongea huku nikiwaangalia Usoni. Nikarudi Upande wa Dada Zangu nao nikafanya kama nilipofanya mwanzo. Binti akainuka na kusogea pale waliposimama Wazazi Wangu. Akainama kwa Heshima na kutoa Salamu.

Alionesha Heshima ambayo nilimuona Mzee Haji Masimba Akitingisha kichwa na tabasamu kutamalaki usoni kwake. Baada ya kutoka kwa wazazi wangu akawaendea Dada Zangu, alianza na dada Yangu Mkubwa Husna, kisha akaenda kwa salama, harafu akafuatia Kwa Khadija. Huko kote alikuwa akipiga magoti na kuonyesha Heshima ya Hali ya Juu. Baada ya kumaliza utamburisho kwa ndugu ikafuata zamu ya kumtambulisha Rehema Ally Kwa wazazi Wangu na Dada Zangu. ''Baba na Mama Yangu pamoja na dada zangu. Nadhani hapa sio mahala pake katika hiki tunachokifanya. Lakini kwa kuwa mna Hamu na Shauku Ya Kumjua Huyu Msichana hapa, basi sina budi kuwatambulisha. Huyu anaitwa Rehema Ally, ni mwanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam akisomea shahada ya Uchumi na Maendeleo. Ni Rafiki Yangu na Dada Yangu.'' nikamaliza huku nikimtizama kila Mmoja Usoni. Hapo nikakutana na maswali lukuki katika nyuso Za Watu Wote. Kila mmoja alitegemea Utambulisho tofauti na ule. Kila mmoja alitarajia niseme labda ni Mpenzi Wangu. Lakini Haikuwa Hivyo, nilisimamia ukweli mtupu bila kupindisha.

******

zilipita wiki tatu tokea litokee lile tukio la kupigwa na polisi. Na sasa nilikuwa nikienda shule huku nikiwa sina mawasiliano na Sheila pamoja na Shamim. Na Hata polisi sikurudishwa tena wala sikuitwa popote pindi nilipotoka hospitalini. Pia nilikuwa sijaonana na hao watu kwa Muda wote Huo. Nilikuwa nikipiga kitabu kwa raha bila bughuza. Kila jioni Rehema alinipitia Chuoni na kwenda nyumbani kwetu. Muda Wote alionekana ni Mwanamke Mpole, msikivu na Mtaratibu. Muda Wote alikuwa akinishauri na kunishirikisha vitu Vingi sana. Kikafikia kipindi kila Alipo REHEMA basi IBRAHIM nami nilikuwepo.. Lakini Sikujua, Kama Ningejua? Mmmhh...
 
MATESO YANGU

SEHEMU YA 023

Hakika kama ningejua ningemtunza Rehema wangu. Ningempa umalkia katika maisha yangu. Ningempa nafasi ya kumtunza kama mboni ya jicho langu. Lakini nilidanganywa na Sheila, Sheila alinihadaa nikampoteza binti mzuri na msomi. Binti ambaye nadhani alikuja kuutuliza moyo wangu. Kuja kuniponya majeraha yote nilioachiwa na Sheila. Lakini niliamua kumuacha kwa kudanganywa na kupumbazwa na Sheila.

Kila alipo Rehema na Ibrah alikuwa hapo. Hatukuachana hasa kipindi kila mmoja atokapo darasani. Muda wote nilikwenda kwao nayeye alikuja kwetu. Wazazi na dada zangu wakaamini na kunihusia kuwa huyu ndiye mwanamke sahihi wa kumpeleka HANDENI. mwanamke Sahihi wa kunizalia watoto. Licha ya maneno kutoka kwa ndugu lakini bado sikuweza kuunyanyua mdomo wangu na kumwambia Rehema Nakupenda. Bado nilikuwa kimya na sikuwa na Ujasiri Huo. Niliendelea kuogopa kuingia mapenzini kwa mara nyingine. Niliogopa kuumizwa kama mwanzo. Na hata ndani ya kina cha Moyo Wangu nilikili kuwa nilikuwa nikimpenda Rehema lakini nilitaka kumchunguza kwanza. Nilitaka kuhakikisha kama nipo mwenyewe. Kila siku tulikuwa tukikaa sehemu na tukaongea kuhusu maisha, na masomo. Lakini kila nilipokuwa nikimtizama usoni, nilikuwa nikiliona penzi machoni kwa Binti huyu. Penzi ambalo lilikuwa likisubiri liote kisha likue na baadae kuchanua.

Ilikuwa ni siku tulivu ya jumamosi, nilikuwa nikitembea kwa mguu kutoka kivukoni kuelekea posta kukutana na Rehema. Nilikuwa sina hili wala lile nikitembea kwa kujiachia. Wakati nakaribia Kilimanjaro Hotel, nikawaona watu watatu wakija kwa mbele yangu. Walikuwa wasichana wawili na mvulana mmoja. Walikuwa wako umbali wa hatua kama Ishirini hivi. Hawakuwa wengine bali alikuwa Sheila, Shamim na Jamaa mmoja ambaye niliwahi kumuona na Shamim Hospital. Nikahisi moyo Wangu ukipoteza mapigo, jasho jembamba likashuka mwilini mwangu. Miguu ikaanza kutetemeka na kutaka kugongana. Sikuwa Masimba Yule tena, Huyu alikuwa mwingine tena aliyekumbwa na hali ambayo haikuwahi kumtokea. Licha ya kuwaona lakini wao mwanzoni hawa kuwa wameniona, hawakuwa wameniangalia. Lakini Sheila alipokuja kutizama mbele, macho yetu yakakutana. Nikauona mshtuko usoni mwake. Mshtuko ambao ulisababisha wenzake wamtizame.

Hapo ndipo walipotizama mbele, hapo ndipo macho ya wote yaliponitizama. Hakukuwa na mtu aliyeweza kuongea nami. Nikawapita nikiwa bubu, nikiwa kama sikuwaona. Licha ya kuwapita lakini ile hali ya kutetemeka haikuniacha. Sikutaka kugeuka nyuma, nikaendelea kutembea nikimuwahi Rehema Wangu. Kweli punde tu nikamkuta akiwa amesimama posta Mpya pembeni kidogo ya kituo cha Daladala. Alikuwa amependeza sana. Alikuwa aking'aa na kunukia kupita kiasi. Alikuwa ndani ya Kisketi cha Jeans kilicho ukamata mwili wake, juu alikuwa na Kishati kizuri Cheupe kilichomfanya aonekane kama Jokate Mwegelo. Chini alivaa kiatu kimoja matata sana. Kumuona Rehema Wangu kukanifanya nisahau nilichokutana nacho pale kilimanjaro Hotel. Nikaipiga hatua nikipokewa kwa tabasamu pana na macho yenye kuita. Nikapiga hatua kumfuata malikia wangu. Malikia aliyeendelea kuliachia tabasamu lake litamalaki Usoni.

Sekunde mbili nikamuona mtu akiwa mwilini kwangu, akiwa kifuani amejilaza. Hakujali wingi wa watu, hakujali Macho ya watu, hakuiona aibu tena. Alikuwa kifuani akiwa amekilaza kichwa chake. Kila mmoja pale kituoni aliacha anachokifanya na kututupia macho. Rehema Hakujali wala kuogopa bado aliganda kama Sumaku. Manukato aliyojipulizia yaliingia katika matundu ya pua zangu na kunifanya Mzigua Mimi niendelee kuganda. Tulipokuja kuachiana wote tuliingia kwenye daladala na Safari Ya kuelekea mwengi Ikaanza. Sikujua wapi ambapo Tunaelekea. Nilikuwa kimya nikimuangalia Rehema. Alikuwa mpya kwa kila kitu. Alikuwa mzuri, alikuwa mrembo na alikuwa ni mpole na mtaaratibu sana. Hatimaye tukafika Makumbusho hapo tukachukua bajaj iliyotupeleka mpaka maeneo Ya Sinza Kwa Remmy. Bado sikujua wapi ambapo tulikuwa tukielekea. Nilikuwa nikifuata kama kondoo. Safari Yangu na Rehema iliishia kwenye nyumba fulani Hivi nzuri.

Ilikuwa nyumba yenye ukimya wa ajabu. Nyumba ambayo ilionyesha kutokuishi watu. Akaufungua mlango kisha wote tukaingia Ndani. Bado nilikuwa katika kizungumkuti, kizungumkuti cha kushindwa kujua nini kitafuata.. Tukaipita Sebule yenye ukimya wa kutia shaka. Tukaufikia mlango wa chumba kimoja mbele yetu. Nikamuona akiufungua mlango kimya kimya na Kunitaka Niingie Ndani Ya Chumba kile. Nikaingia nikiwa kwenye wasiwasi mkubwa. Kutumbukia kule chumbani nikamuona Rehema Akiufunga mlango kwa ndani kisha kujiegemeza mlangoni. Hakuwa anaongea, hakuwa ananiangalia, muda wote alikuwa akiangalia Chini. Muda wote alikuwa ni Mwenye soni na aibu ya kike. Lakini wakati nikishangazwa na hilo nikamuona akilifanya Jingine. Jingine ambalo ndilo likanifanya nipigwe na butwaa.. Sketi Yake ya Jeans Ilikuwa magotini Ikielekea chini Ya Miguu.. Nikameza Funda la Mate kisha Nikakaa Kimyaaaaa...
 
MATESO YANGU

SEHEMU YA 023

Hakika kama ningejua ningemtunza Rehema wangu. Ningempa umalkia katika maisha yangu. Ningempa nafasi ya kumtunza kama mboni ya jicho langu. Lakini nilidanganywa na Sheila, Sheila alinihadaa nikampoteza binti mzuri na msomi. Binti ambaye nadhani alikuja kuutuliza moyo wangu. Kuja kuniponya majeraha yote nilioachiwa na Sheila. Lakini niliamua kumuacha kwa kudanganywa na kupumbazwa na Sheila.

Kila alipo Rehema na Ibrah alikuwa hapo. Hatukuachana hasa kipindi kila mmoja atokapo darasani. Muda wote nilikwenda kwao nayeye alikuja kwetu. Wazazi na dada zangu wakaamini na kunihusia kuwa huyu ndiye mwanamke sahihi wa kumpeleka HANDENI. mwanamke Sahihi wa kunizalia watoto. Licha ya maneno kutoka kwa ndugu lakini bado sikuweza kuunyanyua mdomo wangu na kumwambia Rehema Nakupenda. Bado nilikuwa kimya na sikuwa na Ujasiri Huo. Niliendelea kuogopa kuingia mapenzini kwa mara nyingine. Niliogopa kuumizwa kama mwanzo. Na hata ndani ya kina cha Moyo Wangu nilikili kuwa nilikuwa nikimpenda Rehema lakini nilitaka kumchunguza kwanza. Nilitaka kuhakikisha kama nipo mwenyewe. Kila siku tulikuwa tukikaa sehemu na tukaongea kuhusu maisha, na masomo. Lakini kila nilipokuwa nikimtizama usoni, nilikuwa nikiliona penzi machoni kwa Binti huyu. Penzi ambalo lilikuwa likisubiri liote kisha likue na baadae kuchanua.

Ilikuwa ni siku tulivu ya jumamosi, nilikuwa nikitembea kwa mguu kutoka kivukoni kuelekea posta kukutana na Rehema. Nilikuwa sina hili wala lile nikitembea kwa kujiachia. Wakati nakaribia Kilimanjaro Hotel, nikawaona watu watatu wakija kwa mbele yangu. Walikuwa wasichana wawili na mvulana mmoja. Walikuwa wako umbali wa hatua kama Ishirini hivi. Hawakuwa wengine bali alikuwa Sheila, Shamim na Jamaa mmoja ambaye niliwahi kumuona na Shamim Hospital. Nikahisi moyo Wangu ukipoteza mapigo, jasho jembamba likashuka mwilini mwangu. Miguu ikaanza kutetemeka na kutaka kugongana. Sikuwa Masimba Yule tena, Huyu alikuwa mwingine tena aliyekumbwa na hali ambayo haikuwahi kumtokea. Licha ya kuwaona lakini wao mwanzoni hawa kuwa wameniona, hawakuwa wameniangalia. Lakini Sheila alipokuja kutizama mbele, macho yetu yakakutana. Nikauona mshtuko usoni mwake. Mshtuko ambao ulisababisha wenzake wamtizame.

Hapo ndipo walipotizama mbele, hapo ndipo macho ya wote yaliponitizama. Hakukuwa na mtu aliyeweza kuongea nami. Nikawapita nikiwa bubu, nikiwa kama sikuwaona. Licha ya kuwapita lakini ile hali ya kutetemeka haikuniacha. Sikutaka kugeuka nyuma, nikaendelea kutembea nikimuwahi Rehema Wangu. Kweli punde tu nikamkuta akiwa amesimama posta Mpya pembeni kidogo ya kituo cha Daladala. Alikuwa amependeza sana. Alikuwa aking'aa na kunukia kupita kiasi. Alikuwa ndani ya Kisketi cha Jeans kilicho ukamata mwili wake, juu alikuwa na Kishati kizuri Cheupe kilichomfanya aonekane kama Jokate Mwegelo. Chini alivaa kiatu kimoja matata sana. Kumuona Rehema Wangu kukanifanya nisahau nilichokutana nacho pale kilimanjaro Hotel. Nikaipiga hatua nikipokewa kwa tabasamu pana na macho yenye kuita. Nikapiga hatua kumfuata malikia wangu. Malikia aliyeendelea kuliachia tabasamu lake litamalaki Usoni.

Sekunde mbili nikamuona mtu akiwa mwilini kwangu, akiwa kifuani amejilaza. Hakujali wingi wa watu, hakujali Macho ya watu, hakuiona aibu tena. Alikuwa kifuani akiwa amekilaza kichwa chake. Kila mmoja pale kituoni aliacha anachokifanya na kututupia macho. Rehema Hakujali wala kuogopa bado aliganda kama Sumaku. Manukato aliyojipulizia yaliingia katika matundu ya pua zangu na kunifanya Mzigua Mimi niendelee kuganda. Tulipokuja kuachiana wote tuliingia kwenye daladala na Safari Ya kuelekea mwengi Ikaanza. Sikujua wapi ambapo Tunaelekea. Nilikuwa kimya nikimuangalia Rehema. Alikuwa mpya kwa kila kitu. Alikuwa mzuri, alikuwa mrembo na alikuwa ni mpole na mtaaratibu sana. Hatimaye tukafika Makumbusho hapo tukachukua bajaj iliyotupeleka mpaka maeneo Ya Sinza Kwa Remmy. Bado sikujua wapi ambapo tulikuwa tukielekea. Nilikuwa nikifuata kama kondoo. Safari Yangu na Rehema iliishia kwenye nyumba fulani Hivi nzuri.

Ilikuwa nyumba yenye ukimya wa ajabu. Nyumba ambayo ilionyesha kutokuishi watu. Akaufungua mlango kisha wote tukaingia Ndani. Bado nilikuwa katika kizungumkuti, kizungumkuti cha kushindwa kujua nini kitafuata.. Tukaipita Sebule yenye ukimya wa kutia shaka. Tukaufikia mlango wa chumba kimoja mbele yetu. Nikamuona akiufungua mlango kimya kimya na Kunitaka Niingie Ndani Ya Chumba kile. Nikaingia nikiwa kwenye wasiwasi mkubwa. Kutumbukia kule chumbani nikamuona Rehema Akiufunga mlango kwa ndani kisha kujiegemeza mlangoni. Hakuwa anaongea, hakuwa ananiangalia, muda wote alikuwa akiangalia Chini. Muda wote alikuwa ni Mwenye soni na aibu ya kike. Lakini wakati nikishangazwa na hilo nikamuona akilifanya Jingine. Jingine ambalo ndilo likanifanya nipigwe na butwaa.. Sketi Yake ya Jeans Ilikuwa magotini Ikielekea chini Ya Miguu.. Nikameza Funda la Mate kisha Nikakaa Kimyaaaaa...
 
MATESO YANGU

SEHEMU YA 024

Nikaliona lile ambalo sikulitarajia hapo mwanzo. Sikulitarajia kama lingetokea ndani ya Chumba kile. Sketi ya Rehema ilikuwa magotini, Ilikuwa ikishushwa taratibu huku jicho zuri legevu likinitizama. Jicho ambalo lilionekana kukosa usingizi kwa Muda mrefu sana. Sketi ikafika chini ya miguu na kuliacha umbo lake nusu likiwa nje. Paja nyeupe zilizonona zilikuwa zikionekana Waziwazi. Nikalimeza fundo la mate pale mkono wa Rehema ulipoishika Kufuli na kuanza kuishusha chini. Kuishusha huku akinitizama kwa jicho lake lile lile. Punde nguo ile ilikuwa chini, chini kabisa ya miguu yake. Macho yangu yakapokewa na nyasi ndogo mbichi mbichi zilizokuwa zikichipua. Hizi hazikuwa za bandia kama zile za uwanja wa Uhuru. Hizi zilikuwa ni nyasi asilia katika uwanja Asilia. Ulikuwa uwanja uliokuwa unavutia kwa kutizama, uwanja ambao kila ambaye angefanikiwa kuutizama alikuwa akiumezea mate. Punde nikamuona akikiondoa kile kishati na kumuacha kama alivyozaliwa. Alikuwa kama alivyokuja Duniani. Umbo lake tambu lilishahabiana na umbo la Mishy, hata Chuchu zake zilikuwa ndogo mfano wa Embe Ng'ongo. Jicho lake lilikuwa zuri kama lile la Trisar Brown ama Mishy wa Tabara. Lilikuwa limelegea kanakwamba hakuwa na uhai. Ibrah nikapigwa na butwaa nisijue nini nifanye. Nilikuwa nimezubaishwa na Uzuri wa Umbo la Rehema. Nikapiga hatua kumfuata pale aliposimama kisha nikamkumbatia. Ulikuwa mkumbatio wenye kuleta faraja ndani yake. Muda mfupi ulimi wangu ulikuwa ukitembea kwenye ncha ya Chuchu zake. Nilikuwa nikiilamba chuchu katika ufundi mtambuka. Mikono ilikuwa akishuka na kupanda katika kuitekenya nyonga. Nikamuona Rehema akishindwa kusimama, akaishiwa nguvu na kutamani kukaa chini.

Sikumpa hiyo nafasi, sikutaka kumfanya ahangaike, nilitaka kumuonyesha ufundi wa kumtoa machozi ya utamu. Bado ulimi wangu uliendelea kushambulia Chuchu za Rehema. Sasa nilikuwa nimeimeza chuchu moja na kuanza kuinyonya. Niliifanya kama mtoto afanyavyo. Punde nikausikia mguno kutoka kWa Rehema. Sikujali hilo, sikulisikia hilo, sasa nilikuwa nimemuinua na kwenda kumlaza katika kitanda kile. Alikuwa amelala kifudifudi akiuacha mgongo Juu. Ibrah nikaanza kukifanya kile ambacho kila mwanamke alihitaji kufanyiwa, nilikuwa nikiutembeza ulimi usawa wa shingo huku nikiufanya kama naupuliza. Kila nilichokuwa nikifanya nilikuwa nikimuona Rehema akipanda juu. Kila nilipokuwa napumua Shingoni na Hata Sikioni bado alikuwa akiweweseka. Alipoteza mawasiliano. Hakuwa anaelewa kile kinachoendelea. Hata nilipomgeuza Hakuwa na Habari. Hakuwa na taarifa kuwa nilikuwa nikitaka kuonja maji ya Chumvi. Nilipogusisha ulimi wangu kisimani nikamuona Rehema akishika mashuka na kuanza kucheza Sebene. Alikuwa akienda kulia na kushoto akifuatia mdundo wa Biti. Nami nilikuwa nikionja maji na wakati mwingine nilikuwa nikinywa kabisa.

Nilipomuona Rehema akinivuta ndipo nami nilipopanda na kuianza safari. Ilikuwa safari salama yenye kuburudisha. Safari ambayo Chombo changu kilipakiwa katika chombo kitulivu. Chombo ambacho kilikuwa kikinibana na kunisababishia joto kali sana. Tukacheka na kufurahi wote, tukashuka bonde kwa taratibu, tulikuwa tukiogopa Ajali, ajali ambayo ingetuharibia. Binti alikuwa akitatarikana kana kwamba kitanda kilikuwa kinasiafu. Alishuka kitandani na kulala chini ya sofa. Tulibadili kila aina ya mitindo. Mpaka Chombo kinafika bandari Ya Zanzibar kila mmoja alikuwa ameifurahia safari kwa kiwango kikubwa sana. Kila mmoja alikuwa alikuwa amelala pembeni akimuangalia mwenzake. ''ahsante'' ilikuwa sauti ya Rehema ambayo ilinifanya nigeuze Shingo kumtizama vizuri. Bado mwili wake ulikuwa Ukiniita, bado mwili wake ulikuwa ukivuta na kunishawishi. Ni kweli ukafanikiwa katika hilo. Muda mfupi baadae Tulikuwa katika safari ya pili. Hii ilikuwa safari ya taratibu katika kupeana nafasi ya kuonyesha ujuzi. Tulikuwa katika burudani timilifu. Kwa Mara Ya kwanza nilikuwa nikimsahau Sheila pamoja na Shamim. Nilihisi Huyu atakuwa mwanamke Wa Maisha Yangu. Macho yalilegea na kiuno alikilegeza. Alikwenda kushoto na hata kulia, alipanda juu na Kushusha. Ulikuwa Mchezo Mtamu, Mchezo ambao ulitufanya tukione kilele kwa pamoja. Nikaapa kuachana na Sheila, nilipanga hata Kuachana na Shamim. Nilitaka kutulia na Rehema Wangu. Sikutaka kumpoteza kwa ujinga wangu. Hakika sikujua. Kama Ningejua nisingejidanganya.
 
MATESO YANGU

SEHEMU YA 025

Nilikuwa nikimpenda Rehema wangu, sikutaka nimpoteze kwa sababu ya mpumbavu mmoja. Mpumbavu ambaye hakupenda kuniona nikiwa katika furaha. Alifanya kila njia niwe katika wakati mgumu. Baada ya kutoka Darasani nikaamua kumtaarifu Mama na dada zangu kuhusu simu niliyopigiwa na mtu aliyeongea nami na sms niliyotumiwa na Rehema. Baada ya maelezo hayo wakaniambia niende kisha chochote nitakacho kiona basi niwataarifu. Niliondoka pale akiba kwa daladala ya mwananyamala kisha nikashuka Palm Beach. Nikachukua Daladala mpaka mwenge nikashuka na kuchua Daladala Ziendazo Ubungo Ambazo hupita pale Mlimani City. Muda wote huo nikipanda gari hili na kushuka hapa, bado kichwa changu hakikuwa kimetulia. Bado kichwa changu kilikuwa kimevurugwa na matendo ya Sheila. Nilikuwa tayari kupambana na chochote kwa sababu ya kupigania penzi langu kwa mtoto Mtamu na Mwenye Mapenzi ya Kweli Kwangu. Nilikuwa nikiwaza kipi natakiwa kufanya kwa Sheila ili aniache na Maisha Yangu. Nikashuka Maeneo Ya Survey na kuivuka barabara nikielekea Mlimani.

Kwa aliyefanikiwa kuniona kwa kipindi kile angehisi labda nilikuwa kwenye matatizo makubwa. Licha ya kutembea pekee yangu, lakini nilikuwa kirusha Mikono kama naongea na watu. Nikalivuka geti na kupitia upande wa parking. Nikaichomoa simu yangu na kuipeleka Sikioni. Sauti tamu ya Upande wa pili ikahanikiza katika ngoma za masikio Yangu. Nikahisi damu kusisimka na mapigo ya Moyo kunienda kasi. Ilikuwa Sauti Tamu ya Rehema Wangu.. ''hellow Beiby'' ni sauti ninayoweza kusema kuwa ilinirudishia Uhai kiasi. Nikamuuliza wapi alipo. Akaniambia wapo kwenye lango la kuingilia. Nikapiga hatua huku simu ikiwa bado sikioni. Nilipenda kuendelea kuisikia Sauti yake. Nilipotokea mbele kidogo nikawaona wamesimama wasichana wanne. Watatu niliwatambua lakini mmoja sikuwa nimemjua pale. Huyu alikuwa mwingine kabisa, lakini wale watatu ni walewale. Sheila, Shamim na Queen of my Heart Rehema Ally. Kumuona tu Rehema nikatabasamu, nikatembea huku tabasamu likitamalaki katika Uso Wangu. Macho Yangu yakagongana na Macho Ya Wote wanne. Wote wakanitizama kwa mitindo tofauti. Huku sheila na Shamy wakiniangalia kwa kunishusha na kupandisha. Kipenzi Changu Rehema alishajitoa pale waliposimama na kuja kujitupa kwenye kifua Changu kwa Mahaba na Pozi Zote. Nikahisi raha na faraja ndani yake. Hatukujali kuangaliwa na Shamim wala SHEILA. bado Rehema alining'ang'ania huku akiipapasa Shingo Yangu. Ingawa nilikuwa nikijisia aibu lakini kule kufanyika Machoni kwa Sheila na Shamy nilijihisi mpya, na mwenye thamani kubwa. Baada ya kuridhika nikamtoa Rehema kifuani kwangu na kuukamata mkono wake nikimuongoza Mpaka pale waliposimama Shamy, sheila na yule msichana mwingine. Bado Sheila alikuwa akiendelea kunipandisha na kunishusha, bado alinitizama kwa dharau zote huku akisonya. Nilichokifanya ni kumtoa Rehema pale na Kuanza kuondoka pale mlangoni. Niliamua kumuonyesha sheila kuwa Hakuwa na nafasi tena katika Moyo na Roho Yangu. Mkono wangu sasa ulikuwa umepita kiunoni kwa Rehema. Ulikuwa umekishika kiuno kizuri mfano Wa Nyigu. Hatukujisumbua kugeuka nyuma, Hatukujisumbua kuwaangalia tena. Nikamuondoa Rehema wangu na Kuchukua Bajaj ambayo ilitupeleka mpaka Chuo kikuu Cha Dar es Salaam. Tuliposhuka tukalipa na kuelekea sehemu ambayo niliona ni nzuri kukaa na Kuongea. Kwa mtu Yoyote ambaye ameshawahi kufika UDSM atakuwa anayajua mazingira na maeneo mengi yakuweza kuongea na hata kumalizana kwa Usiku.

Tulikaa pale na kuanza kuongea mambo yetu lakini kwanza nilitaka kujua ilikuwaje akakutana na Sheila na hatimaye kuombwa nifike pale. Rehema aliniangalia Usoni kisha kwa sauti yake ile ile. ''Unajua Ibrah nakupenda tena sana. Na kama sio utulivu na upole Wangu, basi nadhani ungenikuta Hospitali nimelazwa ama Kituo Cha Polisi. Lakini nilijizuia kwa kuwa nilijua Yule msichana aliyoonyesha kuwa alikuwa Muongo. Kifupi Sikujua namba yangu alipoipata lakini wakati nipo Lecturer Room niliona Ujumbe ukiingia kwenye Simu Yangu. Ulikuwa ujumbe kutoka kwenye namba ngeni. Ujumbe Huo Ulisomeka ''Hi Rehema! Naona umeamua kunipokonya Ibra wangu. Kwa kweli Ujumbe Ule ulinitibua na kunipandisha presha. Mwili Wangu ukazizima na machozi kuanza kutoka. Nikainuka na kutoka lecturer Room na kurudi hostel huku nikilia. Nilikuwa nikikulilia Wewe Ibrah. Nilikuwa nikijua umeniacha Ama Kunisaliti. Wakati bado nikiwa nimechanganyikiwa, Ukaingia Ujumbe mwingine kwamba kama nataka kumuona Mke mwenzangu basi niende pale ulipotukuta. Huwezi Amini Ibrah Wangu, nilitoka kama Mwehu nikiwa tayari kwa Ugomvi na Mapambano. Lakini nilipofika na kumuona Msichana Mwenye nikamtambua kuwa ni Yule ambaye alikutesa kwa kukupigisha Magoti pale Mabibo Hostel na kusababisha upigwe na Askari.'' alimaliza Kuongea Rehema Wangu huku akilala kabisa Miguuni Kwangu. Wakati Tukipiga Stori Huku tukiwa tumesahau kilichotokea, Simu Ya Rehema Ikaingia Ujumbe, Kwa kuwa Simu Niliishika Mimi, Nikaona Niusome ''Baby Nakaribia kutua Airport Muda Mfupi Ujao, njoo nipokee.''
 
MATESO YANGU

SEHEMU YA 026

Ilikuwa meseji iliyouchoma moyo wangu na kunipa kizunguzungu. Mwili wangu ukaanza kutoka jasho kwa wingi. Nikausoma ule ujumbe tena na tena. Nikausoma Ujumbe kama mara kumi huku nikishindwa kuamini kile ambacho nilikuwa nikikishuhudia. Rehema kumbe anabwana? Rehema kumbe anampenzi? Nilijikaza nisitoe machozi lakini nilishindwa. Chozi la kiume likashuka mashavuni mwangu na kudondoka Usoni kwa Rehema. Ni chozi langu lililougeuza uso wa Rehema aliyekuwa amelala miguuni kwangu. Akakutana na uso wangu uliobadilika na kuwa kama mgonjwa. Rehema akahamaki na kutaka kujua kilichonibadilisha na kunifanya nilie. Niliunyoosha mkono wangu niliokuwa nimeishika simu kuikabidhi simu. Rehema akaipokea huku akionekana kutoelewa chochote. Kwani muda wote alikuwa akiniuliza kile ambacho kilikuwa kikinisumbua. Sikuweza kumjibu, sikutaka kumjibu wala kumsikiliza. Nilimpa ishara aangalie kwenye simu yake. Huku akiwa na wasiwasi akaibponyeza simu na Kuusoma Ule Ujumbe. Akainuka akiwa haamini na kuanza kuzunguka akitafuta cha kuniambia. Hakuwa akinitizama usoni bali alikuwa akiangalia chini. Ghafla nikaliona chozi lake likishuka mfano Wa maji. Nikapatwa na kizungumkuti na kuwa na maswali kibao.

Bado machozi ya Rehema hayakunilainisha na kunilegeza. Bado nilikata kujua Gerald Mahundi ni nani. Bado nilitaka kujua kwanini anampenzi harafu aje kunidanganya? Nilihisi kichwa kikiniuma, nikahisi ule upendo kuyeyuka wote ndani ya moyo wangu. Nikataka kuinuka niondoke pale UDSM, lakini Rehema akaniwahi na kunishika mkono. Hakuwa akilia kwa Siri tena bali alikuwa akilia kilio nilichokisikia na kusikiwa na watu wengine. Nikamvuta kwangu na kumkumbatia. Nilimkumbatia nikiwa katika maumivu makali. Maumivu ya kujua kuwa sikuwa peke Yangu. Hilo likaniumiza sana, hilo likanifanya hasira zianze kunijia. Lakini kabla sijaongea chochote nikasikia sauti Ya Rehema ikipenya katika ngoma za masikio Yangu. Maneno yake yalionichanganya na kuuvunja Moyo Wangu. ''Sorry Ibrah nasikitika kuto kukwambia tokea mwanzo. Ni kweli nilikuwa nampenzi na alikuwa masomoni marekani katika chuo cha Havard akifanya Masters Ya Sheria. Naomba Nisamehe Ibrah lakini sina Budi kukuacha. Sina budi Kumfuata Gerald Wangu. Nisamehe sana kwa kukuongezea maumivu. Aliongea Rehema akiwa anamaanisha. Sikusubiri amalizie na kuniaga. Nilijikuta nikiishiwa nguvu na kukaa Chini. Sikuwa hata nguvu. Machozi yakafunika macho Yangu. Yakashuka mashavuni mwangu huku nikishuhudia Rehema akiniacha. Nikishuhudia Rehema akimfuata mwanaume Wake. Hamkuwepo nyie lakini Mungu Alikuwa ni Shahidi Wangu. Sikuweza kuangalia hili, sikuweza kulivunmilia lile. Nikainuka nikilia na kuanza kumfuata Rehema kwa Nyuma. Kila Mmoja aliniangalia, kila mmoja alikuwa akinitizama. Niliendelea kumfuata nikimuita. Rehema akasimama kisha kugeka nyuma. Macho Yangu na yake Yalipogongana wote tukazidisha kulia. Tulikuwa tukilia kama tumefiwa. Lakini hilo halikumfanya Rehema abatilishe Safari Yake.

Akaondoka machoni mwangu kwa usafiri wa tax. Akaniacha nikipewa pole na watu wachache waliokuwa wakikishudia kile kitendo. Nikatamani kuifukuza Ile tax lakini sikuwa na uwezo huo. Nilikuwa nimebaki mwenyewe. Nikaamua kuondoka mlimani kuelekea Nyumbani. Nilikuwa nimeumia sana.

******
Niliingia chumbani kwangu na kuanza kulia upya. Nililia sana, nililia mpaka nikahisi kichwa kikianza kuuma. Kila nilipokuwa nikivuta taswira ya Rehema akiwa na Gerald Kitandani nilikuwa nikiumia Sana. Rehema aliamua kuniumiza. Kile alichokishuhudia wakati nafanyiwa kule Mabibo Hostel Leo hii alikuwa akinitendea mimi. Kosa langu lilikuwa nikutokusoma Havard. Kosa langu lilikuwa nikusoma CBE tena ngazi ya Cheti. Mwisho nikainua mikono Hewani na kumuachia mwenyezi Mungu. Nikimkabidhi maisha Yangu yote. Kisha nikafuta machozi kwa kunawa maji Usoni harafu nikapanda kitandani kuutafuta Usingizi nikiwa sina hamu ya Chakula Chochote.

*****

niliingia Zangu Chuoni nikiwa ni mwenye huzuni sana. Licha ya kuvumilia na kuchukulia kama ni masuala ya kawaida lakini Sikuweza kuihandle Ile Hali. Nilikuiwa mchovu na nilipoteza uchangamfu wangu wote. Mida wote nilikuwa nimeinama nikisoma. Nilijitahidi sana kusoma nikiamini ni Elimu tu ambayo inaweza kuniepusha na Dharau hii. Niliendelea kusoma huku muda mwingi nikijaribu kupingana na Moyo Wangu. Muda wa kuondoka ulipofika nilitoka zangu Chuo na kuelekea Zangu Nyumbani. Nilitembea Taratibu nikielekea Zangu Posta nikiwa sina Raha wala furaha. Nilipofika Maeneo Ya HOLIDAY INN nikamuona Sheila Akitokea mbele Yangu Akiwa peke Yake. Alionyesha hakuwa ameniona, nami nikazuga kuwa sikumuona. Nikainamia chini na kumpita kama Sijamuona. Nikiwa sina Hilli wala lile nikahisi mtu akinigusa Bega. Nilipogeuka, nikakutana Uso kwa Uso na REHEMA akinitizama kwa Wasiwasi. KESHO JAMANI
 
Back
Top Bottom