Riwaya Kali

Riwaya Kali

Man_Sai

Member
Joined
Aug 24, 2016
Posts
8
Reaction score
8
1472966179382.jpg
RIWAYA: Jina
NA: Frank Masai.
SEHEMU YA 2.
ENDELEA.
Warusha ndege waliingia ndani ya Jet P 112, na kufunga mikanda yao. Na nyuma yao, walikaa Montana na watu wake.
Wakashauriwa nao wavae mikanda pamoja na "mask" zilizokuwa zimeambatana na vidumu vidogo vyenye hewa ya oksijeni. Montana na watu wake wakafanya hivyo na kitendo bila kuchelewa, ndege ile kubwa ya kivita ikangurumishwa na marubani wale spesheli kwa ajili ya kazi hiyo.
P 112, ikaanza kusugua matairi yake pale ilipokuwepo kabla ya kuanza kuingia katika sehemu moja ambayo ilikuwa chini (underground). Huko ndege ile ikakutana na barabara kubwa ambayo ilijengwa maalumu huko chini, usawa wa bahari ili ndege ile ipite na isibugudhi watu kwa sauti pamoja na moshi wake.
Naam, baada ya kukamata barabara ile ya ndege, Jet P 112 ikaanza kujichochea na huku ndani yake wale marubani walikuwa wakiwasiliana na mamlaka ya usafiri wa majini na kuuliza kama kutakuwa na meli katika eneo walilokuwa wanapaswa kuibukia. Wakajibiwa kulikuwa hakuna meli wala mtumbwi.
Hapo marubani wakaichochea zaidi ndege yao, na ghafla kikatokea kitu cha kustajaabisha kwa wale ambao hawakuwahi kuipanda ndege ile. Ndege ilichomoka chap, kama kasi ya risasi ikiyotoka kwenye mdomo wa bastola ya Kamanda Amata. Pale ilipoibuka, ilikuwa imeibukia kwenye bahari ya Hindi na wala haikupunguza mwendo. Kwa kasi ileile, ndege ikapaa hadi anga ya kimataifa na kisha ikatulizwa mzuka kwanza kabla haijaingia tena kazini.
Kitendo cha kutoka FISSA hadi katika anga la kimataifa, ilichukua dakika zisizozidi nne. Na huko angani, Jet P 112 pamoja na marubani wake, walikuwa wametulia na wengine kama Montana kuhema kwa kasi kutokana na kutokuwa wazoefu wa kupaa na mashine ile.
Bado marubani waliendelea kuwasiliana na watu wanaoona kwao ni wa muhimu. Na baada ya dakika tano, ndege ile ikaanza kujichochea na kisha kwa kasi ileile, ikapotea eneo la anga ile.
****
VIETNAM.
Frank Masai alionekana kwenye soko moja dogo lakini lililokuwa limejazana watu mithili ya sukari iliyo ndani ya kiroba. Watu mbalimbali wenye asili ya Kiasia, walionekana wakikatiza huku na huko huku wengine wakifanya biashara zao kama kupiganisha kuku na kuchinja vyura kwa ajili ya kitoweo.
Frank hakuwa akifatilia hayo yote, ni wazi alikuwa kazoea kuona biashara kama hizo zikiendelea maeneo kama yale.
Baada ya pepesa ya hapa na pale, macho ya Frank yalitua kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa imejengwa kwa ustadi kuliko nyumba zote zilizokuwa eneo lile la sokoni.
Katika mlango wa nyumba ile, kwa pale juu yake paliandikwa neno moja kwa lugha ya Kivietnan ambayo hufanana na ya Kichina na neno la pili liliandikwa kiingereza, CASINO.
Frank akashika njia hadi pale kwenye mlango ambapo palikuwa na mlinzi.
"Where are you going? (Unaenda wapi?)" Mlinzi yule mwenye nwili mkubwa kama kifaru mtoto, alimuuliza Frank huku akimwekea mkono kifuani akimaanisha asisogee zaidi ya pale.
Frank badala ya kujibu, akatoa picha fulani ambayo kwa nyuma yake ilikuwa na maelekezo machache kuhusu atakayeionesha picha hiyo.
Licha ya mlinzi yule kusoma maelezo yale ambayo yalieleza kuwa atakayeonesha picha ile, aruhusiwe kupita, lakini bado alikataa kumruhusu Frank apite. Labda ni kutokana na taarifa alizozipata kuhusu mtu anayeonesha picha ile kuwa ni wa hatari kupita maelezo. Sasa mlinzi alipomwangalia Frank, mwili mdogo na hana sura ya kikatili, basi na yeye akaleta dharau kwa sababu ya mwili wake wa toto la faru na sura yake ya ubabe.
"Get out the way (toka njiani)" Sauti ya Frank ilitoka huku akiwa hamwangalii yule mlinzi usoni.
"What to do you say?(Unasemaje?)" Yule mlinzi aliuliza kwa jazba huku akianza kushuka ngazi mbili alizokuwa kasimama kwa juu yake.
“Am not here for troubles, don't waste my time (sipo hapa kwa ajili ya matatizo. Usinipotezee muda)" Sauti kavu na tulivu ya Frank, ilipenya masikioni mwa mlinzi na kuona kama anadhalilika kwa yale maneno.
Ghafla alirusha ngumi ambayo kamwe alitakiwa kutofanya vile. Kwani Frank aliinyakua juu kwa juu, na kisha kumsukuma yule mwili jumba hadi karibu na mlango wa ile casino. Mlinzi akahisi kuchafukwa roho, akanyanyuka na kuanza kupambana. Hapo ndipo alimjua mtu aliyeambiwa ni hatari.
Wakati anajaribu kurusha teke lake la kwanza, Frank yeye alikanyaga kwa nguvu mguu ambao ulikuwa chini na kisha akamsukuma na kuufanya mguu ule kutaka hata kuvunjika. Mlinzi akazidi kujaa gesi, akanyanyuka haraka na kuanza kumfata kwa kurusha ngumi kama saba mfululizo lakini zote zilipiga hewa kutokana na Frank kuzikwepa.
Ngumi ya mwisho, jamaa yule mlinzi, aliirusha kwa nguvu, Frank akachupa kidogo chini, kisha akafyatua ngumi yake na kumpiga eneo la ubavu. Mlinzi akabweka kama mbweha.
Hajakaa sawa, akashtukia anapigwa teke la kuzunguka ambalo lilimsogeza hadi karibu na mlango. Wakati anajizoazoa, Frank Masai alimrukia kwa teke zito lililoenda sambamba na kuuvunja mlango wa Casino lile. Mlinzi hoi bin taaban lakini Frank alishaacha kumwangalia na badala yake alikuwa akitafuta kitu mle ndani ya casino.
Macho ya waliomo mle ndani ya Casino, yalihamia kwenye uso wa Frank ambaye alikuwa anapepesa macho huku na huko hadi pale yalipotulia kwenye mlango mmoja ulioandikwa Lee Yang. Hakuwa na mawazo juu ya wale watu waliokuwa wanamwangalia. Yeye sura yake ilijaa uso wa kichunguzi zaidi hasa kwenye ule mlango wa Lee Yang.
Muziki wa Casino tayari ulikuwa umezimwa, na wale wadada ambao walikuwa wanajimenyua menyua mbele ya wanaume huku wakiwa wamevaa mavazi yalionesha asilimia kubwa ya miili yao, tayari walikuwa wameambiwa na midume yao wapotee eneo lile.
Frank akapiga hatua moja tayari kwa kuanza kuelekea kwenye ule mlango aliokuwa kautazama. Lakini ghafla alisitishwa na fimbo ya kuchezea pool table. Alipomwangalia yule aliyemnyooshea fimbo ile, alikutana na sura nyingine ambayo nayo ilikuwa inamuangalia kwa kumtamani, naye huyo mtu alikuwa anapigapiga fimbo ya pool table kwenye mkono wake. Hapo wazo likaja haraka kwenye kichwa cha Frank, wazo ambalo alilifanyia kazi muda huohuo. Lilikuwa wazo la kuwaangalia wateja wa mle. Hapo ndipo alikutana na sura zenye uchu na yeye kuliko kitu chochote.
Akiwa na begi lake mgongoni, hakutaka kujishughulisha na macho yale na badala yake akaamua kuitoa ile fimbo aliyooneshewa na mcheza kamali mmoja mle ndani.
Kitendo cha kuitoa fimbo ile na kusogea, likawa kosa mbele ya macho ya wale wajinga. Hapohapo, fimbo ikabadilika na kuwa silaha. Mshika fimbo ile aliirusha kwa mtindo wa kuchapa, na kwa kuwa Frank alishamwona, akapinda kidogo kwenda nyuma. Fimbo ile ikapita hewani lakini kwa mrushaji, ikawa tatizo.
Pale alipoirusha, alijikuta akitumia nguvu nyingi ambazo zilimfanya asogee mbele kidogo ya Frank, na kwa kuwa alimkosa mtu aliyekusudia, basi ikawa adhabu kwake.
Mwanaume baada ya kupinda kwenda nyuma na fimbo ile kupitiliza, alijiinua kwenda mbele huku mguu wake akiurusha kwa nguvu kwenda kwenye kifua cha yule mrusha fimbo. Teke kali likamkuta yule jamaa, na bila kutegemea, hata yule wa nyuma yake ambaye alikuwa kashika fimbo, naye alikumbwa na mwili ukiopigwa teke na Masai.
Hapo wale waenyeji wengine ndipo walipoamua kuinuka huku kila mmoja akitayarisha silaha yake hasa visu na viti. Na bila kuchelewa wakamvamia Frank kwa fujo nyingi, lakini walichokutana nacho, sidhani kama maishani mwao wamekisahau.

Watch Out Part 3
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom