Riwaya: I Was Wrong

Riwaya: I Was Wrong

Lumbi9

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2014
Posts
8,738
Reaction score
12,424
RIWAYA : I WAS WRONG
SEHEMU YA 1
MTUNZI : PATRICK.CK
CONTACT : 0764294499
“ Mabibi na mabwana sasa ni wakati wa
kufungua shampeni.Mbele yetu hapa tuna
chupa tano za shampeni. Shampeni ya
kwanza ni kwa ajili ya wazazi.Chupa ya pili ni
kwa ajili ya maharusi wetu.Shampeni ya tatu
ni kwa ajili ya wanafamilia.Shampeni ya nne
ni kwa ajili ya wanakamati na shampeni ya
tano ni kwa ajili ya wageni waalikwa wote
mliohudhuria sherehe hii ya aina
yake.Ningewaomba sasa wale wote
waliowekwa maalum kwa ajili ya kutufungulia
shampeni hizi wapite mbele mara moja ili
tuweze kulianza zoezi letu” Mshereheshaji
aliyekuwa amevalia nadhifu sana akiwa ndani
ya suti nyeusi iliyomka vyema akawataarifu
wageni waliokuwa wamefurika ukumbini
wakiwa na nyuso zilizojaa tabasamu.
Watu waliokuwa wameandaliwa maalum kwa
ajili ya kufungua shampeni zile wakapita
mbele ya ukumbi na kila mmoja akakamata
chupa yake na kuanza kuzitikisa kwa
manjonjo.
“ Ndugu wageni waalikwa mabibi na mabwana
shampeni yetu ya kwanza inayokwenda
kufunguliwa ni kwa ajili ya wazazi.Tunaomba
mfunguaji wa kwanza atufungulie shampeni
tafadhali” akasema mshereheshaji na
mwanadada mmoja aliyekuwa amevalia gauni
refu lenye kumeremeta akazunguka na chupa
ile huku akicheza kwa manjonjo na mara
ukumbi wote ukalipuka kwa kelele za
kushangilia.Shampeni kwa ajili ya wazazi
ilikuwa imefunguliwa.Wazazi wa pande zote
mbili wa mwanaume na mwanamke
wakamiminiwa shampeni ile na
kugongesheana glasi wakapongezana.
“ Mabibi na mabwana shampeni yetu ya pili ni
kwa ajili ya maharusi wetu.Nawaomba
maharusi wetu msimame toka hapo mahala
mlipo na msogee hapa mbele.” Akasema
mshereheshaji na maharusi wakasimama na
kusonga mbele.
Mwanadada aliyekuwa ameandaliwa maalum
kwa ajili ya kufungua shampeni ya maharusi
akaanza kuitikisa chupa ile huku akicheza
kwa madoido.Ghafla kikasikika kishindo
kikubwa.Ukumbi wote ukashangilia kwa
kudhani shampeni ile ilikuwa imefunguka kwa
kishindo lakini ghafla ukumbi ukawa kimya
kabisa baada ya kusikia sauti kubwa ikipiga
yowe.Ilikuwa ni sauti ya Flaviana jumbo
,mwanamke mrembo ambaye mchana wa siku
hiyo amefunga ndoa na kijana mtanahati
sana Robinson Gregory.Robinson bwana
harusi alikuwa amelala sakafuni akiwa hana
fahamu huku damu nyingi ikimvuja.Pembeni
ya pale alipokuwa amelala Robinson kulikuwa
na vipande vya chupa.Kila mtu alikuwa
anashangaa kilichokuwa kimetokea.Sandra
mwanamke aliyefungua shampeni ya pili kwa
ajili ya maharusi alikuwa amesimama
akitetemeka mwili mzima.Hakuamini kitu
kilichokuwa kimetokea.Hakuelewa ni kwa
namna gani chupa ile ya shampeni iliweza
kumponyoka toka mikononi mwake na kwenda
kumpiga bwana harusi kichwani.Lilikuwa ni
tukio la kushangaza sana,watu walibaki
wanajiuliza namna lilivyotokea lakini hakuna
aliyekuwa na jibu.
Haraka haraka Robinson akapakiwa garini na
kukimbizwa hospitali .Akiwa njiani kueleka
hospitali mara akaona kitu mfano wa jitu
moja kubwa na lakutisha likimjia na kumtaka
amfuate.Robinson akaogopa sana na
kutetemeka.Jitu lile jeusi na lenye sauti nzito
likamsogelea karibu zaidi na kutaka kumshika
mkono lakini Robinson akauvuta mkono wake
kwa nguvu ili jitu lile lisimguse.
Kutokana na kuuvuta mkono wake kwa nguvu
ili usishikwe na lile jitu la kutisha akajikuta
akiubamiza ukutani na mara akastuka.Kumbe
alikuwa ndotoni.Jasho jingi lilikuwa linamtoka
huku akihema kwa nguvu.
“ Ouh my gosh ! it’s a dream ..!! akasema
Robinson.mwili wake ulikuwa unamtetemeka
kwa uoga kutokana na ndoto ile mbaya na ya
kutisha.Kwa takribani dakika tano alikuwa
amekaa kitandani akiitafakari ndoto ile ya
ajabu.
“ Sijawahi kuota ndoto mbaya na ya kutisha
kama hii.” Akasema Robinson .Kelele za
majogoo waliokuwa wakiwika kwa wingi
zikamfanya aitupie jicho saa kubwa ya
ukutani ili kujua mida hiyo ilikuwa ni saa
ngapi.
“ Saa kumi na mbili kasorobo.Kumekucha !!
akasema Robin na kuinuka akingia bafuni
akaoga halafu akarejea chumbani akawasha
runinga ili atazame taarifa ya habari ya
asubuhi wakati akiendelea kujiandaa kwa ajili
ya kuelekea kazini.Habari ya kwanza katika
taarifa ya habari toka shirika la utangazaji la
taifa ilikuwa kuhusiana na kumbu kumbu za
tukio la kigaidi la September 11 lililotokea
mwaka 2001 nchini Marekani.Robin akastuka
“ Kumbe leo ni September 11.Ndiyo maana
nimeota ndoto ile ya ajabu ajabu.Hii huwa ni
siku yangu mbaya sana.” Akawaza halafu
akaketi kitandani.Akazama katika mawazo ya
ghafla.
“ Tarehe kama ya leo miaka mitano iliyopita
mke wangu Flaviana aliniacha.Ni siku
inayonikumbusha machungu mengi sana.Bado
sijaweza kumsahau Flaviana mwanamke
niliyempenda kwa moyo wangu wote na
kujitolea kila nilivyoweza kwa ajili
yake.Nilifanya kila niwezalo ili kumfanya awe
ni mwanamke mwenye furaha lakini badala
yake hakuyakumbuka hayo yote na akaniacha
nisijue la kufanya.” Akawaza Robin halafu
akainamisha kichwa.Akakumbuka maneno
makalio aliyoambiwa na mke wake siku
alipoondoka nyumbani.
 
Don’t fool yourself that I love you Robin.I’ve
never loved you .I married you not for love.I
just wanted to enjoy life but five years with
you its been a hell to me.Robin sijawahi kuwa
na furaha nikiwa nawe hata siku
moja.Hujawahi kunipa furaha zaidi ya karaha”
maneno haya yakamjia Robin kichwani.Akashi
ka kichwa chake.
“ Mpaka leo sielewi Flaviana alitoa wapi
ujasiri wa kunitamkia maneno haya makali
ambayo kila nikiyakumbuka yanakitonesha
kidonda ambacho kimeanza kupona.”
Akawaza Robin
“Robin you are a worthless man I’ve ever seen
in this world.Its better if you die because you
have no any value in this world.Kosa kubwa
nililolifanya ni kukuonyesha utupu
wangu.Hukustahili kabisa kuuona utupu
wangu mtu kama wewe.Nitakijutia kitendo hiki
kwa miaka yangu yote hadi ninaingia
kaburini.Ninakuacha na kwenda zangu na
mara tu nitakapokiacha hiki kibanda chako
naomba usijaribu kunifuatilia .To me you are
dead already so I’ll never think of you”
Maneno haya yakamuumiza mno Robin
akavuta pumzi ndefu halafu akasimama
akaenda dirishani akalifungua na kutazama
nje.
“ Nilimpa Flaviana kila alichokihitaji katika
maisha yake.gari zuri,vito vya thamani
kubwa.Niliwathamini ndugu zake kuliko hata
nilivyowathamini wa kwangu lakini pamoja na
hayo yote bado aliniacha.Wanawake ..!!!..”
akawaza Robin halafu akarejea na kukaa
kitandani akajiangalia kidoleni
“ Kwa muda wa miaka mitano bado nimeivaa
pete hii ya ndoa.nadhani ni wakati muafaka
sasa wa kuivua.Flaviana hataweza kurudi
tena kwangu ,amekwisha nisahau na
hanihitaji tena na mimi pia simuhitaji tena.Ni
wakati sasa wa kuyasahu maisha ya nyuma
na kuuruhusu moyo wangu uanze maisha
mapya.Kwa miaka mitano nimekuwa kifungoni
,natakiwa nijiweke huru sasa.Nimekwisha
msahau Flaviana lakini siwezi kuisahau tarehe
hii.” Akawaza Robin halafu taratibu akaanza
kuilegeza pete ile ya ndoa kidoleni kwake kwa
lengo la kuivua
“ Flaviana.tulivishana pete mbele ya
madhabahu na mashahidi lakini leo hii
ninaivua pete hii nikiwa peke yangu ,ninajuta
kukufahamu na kuanzisha mahusiano
nawe.Umenifanya niishi maisha magumu kwa
kipindi kirefu lakini sasa ni wakati muafaka
wa mimi kukusahau na kuyaanza tena maisha
yangu mapya.Ninapoivua pete hii ninakutoa
katika moyo na akili yangu.Sikutambui tena
kama mke wangu wa ndoa .Kitu pekee
ambacho ninakishukuru toka kwako ni
kunizalia mtoto mrembo ambaye ameteseka
kwa miaka hii yote mitano bila ya kumuona
mama yake mzazi.Mimi nimekuwa ndiye baba
na mama yake.Kwa heri Flaviana…” akasema
Robin huku akiivua pete ile na
kuitazama.Toka walipovishana pete ile
kanisani siku ya ndoa yao hajawahi kuivua
hadi siku hii ya leo.Akaifunga pete ile katika
karatasi na kuitupa katika chombo cha
takataka
“To me you never existed..” akasema Robin
wakati akiitupa pete ile katika chombo cha
taka.Mara mlango wake ukagongwa.Akauf
ungua na kukutana na sura yenye tabasamu
ya mwanae Penny.
“ Hallow Penny” akasema Robin
“ Shikamoo baba” akasema Penny
“ marahaba hujambo Penny?
“ Sijambo baba.Sijakuona mezani nikaogopa
pengine unaumwa nikaona nije nikuangalie”
akasema penny.Robin akatabasamu
“ Ahsante Penny.Mimi siumwi lakini
nimechelewa kidogo kuna kazi nilikuwa
nafanya .Ninakuja mezani sasa hivi” akasema
robin huku akitabasamu
“ Mungu hawezi kukunyima kila kitu.Nimekosa
mke lakini nimebahatika kuwa na mtoto
mwenye akili anayenipenda na kunijali
sana.Nampenda sana mwanangu Penny na
ndiyo maana ninafanya kila niwezalo ili aweze
kusoma sana na vile vile kumjengea msingi
mzuri wa maisha yake.Sifikirii hata kutafuta
mwanamke mwingine ambaye anaweza
akamlea na kumpatia ule upendo wa
mama,lakini toka aliponitenda Flaviana
nimewaogopa sana wanawake.” Akawaza
Robin wakati akivaa koti.Akajitazama katika
kioo na kuhakikisha amependeza vya kutosha
kisha akachukua mkoba wake na kutoka mle
chumbani akaelekea chumba cha chakula
akaungana na binti yake Penny wakapata
kifungua kinywa.Huwa wana kawaida ya
kupata kifungua kinywa pamoja kila asubuhi
kabla ya kuondoka ,Penny akaelekea shuleni
na Robin akaeleka kazini kwake
“ baba leo naomba usije kunichukua katika
ule muda wa kawaida wa kutoka.Nilimuomba
mwalimu Lucy anisaidie kunifundisha hesabu
Fulani ambazo sikuzielewa vizuri na
akaniambia kwamba leo hii baada ya masomo
atanifundisha.Nitakapokuwa tayari
nitamwambia akutaarifu” akasema Penny
“ Usijali Penny.hata hivyo utakuwa
umenisaidia sana kwani leo hii nina kikao na
wageni muhimu sana.Ukimaliza mwambie
mwalimu Lucy anipigie simu na endapo
nitakuwa bado kikaoni nitamtuma dereva aje
akuchukue
“ Baba leo sitaki dereva aje anichukue.nataka
wewe mwenyewe uje unichukue “ akasema
penny.Robin akatabasamu na kusema
“ haya mama ,nitakuja kukuchukua”
Baada ya kifungua kinywa wakaondoka na
kumuacha Sofia mfanyakazi wa ndani
akiendelea na shughuli zake.Robin alimpitisha
kwanza Penny shuleni halafu yeye akaelekea
kazini kwake.baada ya kufika kazini
akasalimiana na wafanyakazi wake na kuingia
moja kwa moja ofisini .Hakujisikia kufanya
kazi yoyote siku hii. Alihisi uchovu na kichwa
chake alikiona kizito sana .Aliegemea kiti
chake huku akichezea kalamu.Alionekana ni
mwingi wa mawazo .
“ Siwezi kuendelea kuteseka namna hii.Maisha
yangu ni mazuri sasa hivi.Nina kampuni
yangu ya utalii na ninajiweza kiuchumi.Nilich
okosa ni kitu kimoja tu.Mwanamke wa maisha
yangu.Naogopa kuanzisha mahusiano kwa
sababu ya mwanangu Penny.Ninawafahamu
wanawake walivyo kwa watoto wa wanawake
wenzao.Sintavumilia kumpata mwanamke
ambaye atamtesa mwanangu.Hili tu ndilo
linanifanya nisite kuingia katika mahusiano
mengine baada yakutengana na Flaviana.”
Akawaza Robin halafu akaiwasha komyuta
yake
“ Lakini nitaendelea na maisha haya hadi lini?
Natakiwa nimpate mtu wa kuniliwaza,ambaye
ana mapenzi ya kweli na ambaye atanipenda
mimi na mwanangu Penny.Mwanamke huyo
nitampata wapi? Sina hakika kama wanawake
wa aina hiyo bado wanaishi katika sayari hii
ya dunia.Wanawake wenye mapenzi ya aina
hiyo ninayoitaka mimi waliishi enzi hizo za
mitume na manabii .Kizazi hiki
kinachoangaliwa ni uwezo wako wa
kiuchumi.Sitaki mwanamke anipende kutokana
na uwezo wangu wa kifedha bali nataka
anipende kwa moyo wake wote na anipende
mimi na si fedha zangu” akawaza Robin na
mara mlango ukafunguliwa akaingia Neema
katibu muhtasi wake
“Bosi wale wageni tayari wamekwisha fika”
akasema neema
“ Ok .wakaribishe katika chumba cha
mikutano ninakuja sasa hivi” akasema
Robin.Neema akatoka.Robin akamuangalia
wakati akitoka mle ofisini akatabasamu
“ Neema ni mwanamke aliyeumbika kiafrika
haswa.Ana adabu na mchapa kazi mzuri.
lakini niliwahi kusikia kwamba ana mabwana
watatu. Huyu naye namuingiza katika kundi
lile lile la akina Flaviana.” Akawaza Robin
huku akiinuka kitini akavaa koti lake na
kwenda kuonana na wageni wake.
********
David Mwauka alikuwa anakatiza katika mitaa
ya jiji la Arusha huku akiwa na tabasamu
usoni.Ni masaa mawili sasa amekuwa
akizunguka na kulifurahia jiji hili lenye uzuri
wa kipekee.Ni September 11 saa tatu za
asubuhi alipomaliza kifungo chake cha miaka
mitatu katika gereza jipya la Oltoreo lililoko
nje kidogo ya jiji la Arusha na kuachiwa
huru.Alifungwa gerezani kwa tuhuma za wizi
wa mamilioni ya fedha.
Alikuwa amevaa suruali ya jeans rangi ya bluu
na shati la rangi nyekundu.Chini alivaa viatu
vya wazi.Alionekana ni kijana wa kawaida
sana.Hakujua aelekee wapi na mfukoni
hakuwa na pesa zaidi ya shilingi elfu moja na
mia tano tu.Japokuwa alikuwa akizunguka na
kulifurahia jiji hili la Arusha na viunga vyake
,moyoni David alikuwa na mawazo mengi
sana akijiuliza nini kitafuata katika maisha
yake.Hakujua angeanzia wapi au angeyaanza
vipi maisha yake.
“ Mimi ni mwanaume nitapambana na
nitaishi.Nitaishi hapa hapa Arusha.Nyumbani
sintarejea kamwe.Nahisi hakuna
anayenikumbuka tena hivi sasa.Itakuwa ni
furaha yao kusikia kwamba nimekwisha fariki
na siko tena duniani.Mungu ni mwema na
bado ana malengo na mimi na atanisaidia
nitayaanza maisha yangu mapya.” Akawaza
David akiwa ameinamisha kichwa na ghafla
akastushwa na kelele za akina mama wawili
waliokuwa wamebeba vikapu vya
ndizi.Akainua kichwa na kuliona gari moja
lenye rangi nyeusi likiyumba na kupoteza
uelekeo likielekea upande wa David.Kwa kasi
david akaruka na kulishikilia tawi la mti na
gari lile likaugonga ule mti .Kwa kuwa
halikuwa katika mwendo mkali mti ule
haukuweza kuvunjika. David akashuka mtini
na kwa hasira huku akitokwa na jasho jingi
akaelekea katika mlango wa gari lile na
kugonga kwa nguvu.Alikuwa na hasira sana
kwa kukoswakoswa kugongwa.Mara mlango
ukafunguliwa na hasira zote alizokuwa nazo
zikayeyuka
“ Ouh my God ! ..akasema David baada ya
kuchungulia ndani ya gari.Mle garini
alikuwemo mzee mmoja wa makamo ambaye
alionekana kuwa mgonjwa sana,.
“ Nis..nisa..ni.sss..saaiiidiiiiieeee…….!!!!!!
akasema kwa taabu yule mzee.Kwa kasi ya
aina yake Dadid akamvuta Yule mzee na
kumuweka katika kiti cha pembeni halafu
akakaa katika kiti cha dereva.Akaufunga
mlango na kulirudisha gari nyuma na
kuondoka eneo lile na kuwaacha watu
waliokuwa wameanza kujaa ili kushuhudia
kilichokuwa kimetokea wakishangaa.
“ Nip..ele.ke..hosp…!! akasema kwa taabu Yule
mzee.
“ Mzee usijali ninakupeleka hospitali.”
Akasema Alois na moja kwa moja
akakumbuka kwamba wakati akikata mita ya
jiji hili aliiona hospitali moja kubwa
inayomilikiwa na watu toka China.Alifika
katika hospitali ile na kwa haraka Yule mzee
akapokelewa na kuanza kupatiwa
matibabu.Baada ya muda David akaitwa
katika chumba cha daktari mkuu
“ habari yako kijana” akasema daktari Yule
ambaye alikifahamu vyema Kiswahili
‘ Nzuri daktari.Anaendeleaje mgonjwa wangu?
Akauliza David
“ Mgonjwa wako anasumbuliwa na shinikizo la
damu lakini tunaendelea kumuhudumia na
usiwe na wasi wasi.Ataendelea kulazwa hapa
akiwa katika uangalizi wa madaktari.Kitu
kinachohitajika kwa sasa chukua hii karatasi
na uende katika dirisha la cashier yeye
atakupigia hesabu ya gharama zote
zinazohitajika za vipimo na dawa na kisha
kulipa utapeleka risiti katika dirisha la dawa
.Kuna dawa na vifaa ambavyo vinatakiwa
vichukuliwe baada ya kulipiwa kwanza”
akasema daktari Yule.David akastuka sana
lakini hakutaka kuonyesha mstuko wake mbele
ya Yule daktari.Kilichomstua zaidi ni wapi
angepata pesa ya kulipa ? mfukoni alikuwa na
shilingi elfu moja na mia tano tu.Akachukua
karatasi ile iliyoandikwa kichina na kueleka
katika dirisha lililoandikwa Cashier.Akaikab
idhi karatasi ile na kupigiwa hesabu .Jumla
alitakiwa kulipa kiasi cha shilingi laki nne na
elfu ishirini na tatu na mia saba.Kijasho
kikamtoka.Akaichukua karatasi ile na kutoka
nje.
“ Nitafanya nini? Nitapata wapi pesa hizi
nyingi? “ akawaza David na kuzama katika
mawazo mengi.Alitamani kuondoka zake na
kumuacha mzee Yule peke yake pale hospitali
lakini kuna sauti ndani yake ilikuwa
inamwambia kwamba asiondoke na kumuacha
mzee Yule peke yake.Akainama na kufikiri kwa
muda kisha akapata wazo Fulani,akainuka na
kuelekea katika gari .Simu ya yule mzee
ilikuwa mle garini na ilikuwa inaita.David
akaichukua na kuishika mkononi.Alipogeuza
shingo Katika kiti cha nyuma kulikuwa na
mkoba.Akauvuta mkoba ule na
kuufungua.Mapigo ya moyo wake yakaanza
kwenda kwa kasi kubwa.Kulikuwa na mabunda
ya noti yaliyopangana.David akahisi
kuchanganyikiwa.Picha mbali mbali za haraka
haraka zikamjia kichwani kuhusiana na fedha
zile nyingi.Hakuwa na fedha na alihitaji fedha
ili aweze kuyaanza maisha yake mapya baada
ya kutoka gerezani.Wazo la kuchuka fedha
zile na kutokomea zake likamjia.Hakumjua
mzee Yule kwa hiyo angeweza kuchukua fedha
zile nyingi na kupotea kabisa na
asingeonekana tena.Akatabasamu baada ya
kulipata wazo lile lakini ghafla akasikia sauti
ndani yake ikimwambia kwamba asifanye
hivyo anavyotaka kufanya.
“ Ouh No ! Siwezi kufanya hivi ninavyofikiria
kufanya.Si vizuri kumfanyia mwanadamu
mwenzangu jambo kama hili.Natakiwa
nitafute fedha kwa jasho langu mwenyewe na
si kwa kukimbia na fedha za watu.Ee Mungu
naomba unisaidie niweze kuwa mwaminifu
kwa mzee huyu.Nataka kuishi maisha mazuri
na ya haki.” Akawaza David halafu akachukua
bunda moja akahesabu noti zile nyekundu
.Bunda lile lilikuwa na shilingi millioni
tano.Akachukua kiasi cha fedha zinazotakiwa
kulipwa akaenda kulipa na kisha akaelekea
katika chumba ambacho alilazwa Yule
mzee.Hakuruhusiwa kuingia mle chumbani
kwa wakati huo bado Yule mzee alikuwa
anaendelea kuhudumiwa.
“ Natakiwa nimsaidie mzee huyu kama baba
yangu.Nadhani ni Mungu aliyemuongoza
kwangu kwani ingekuwa ni mtu mwingine
asingekubali kuyaacha mamilioni yale
.Angetokomea nayo yote.Siwezi kufanya hivyo
.Nimekaa gerezani nimejifunza namna ya
kuwa mtu safi.Nilifungwa bila hatia lakini
pamoja na hayo nimejifunza vitu vingi sana
nikiwa gerezani.” Akawaza David
Akarudi nje na kuichunguza simu ya Yule
mzee.Alikuwa akitafuta namba ya simu ya
mke wake au mtu wake wa karibu ili aweze
kuwataarifu kuhusiana na ugonjwa uliompata
mzee wao.Katika kuyapekua majina katika
simu ile akakutana na jina moja limeandikwa
my princes Pauline.Akatabasamu.
“ Inawezekana huyu akawa ni mtu wa karibu
wa huyu mzee.Ngoja nimpigie nimtaarifu”
akasema David huku akibonyeza kitufe cha
kupigia simu na simu ikaanza kuita.
***************************************
Pauline alikuwa ameketi sofani akitazama
runinga.Siku hii ya leo hakutaka kutoka
kwenda sehemu yoyote.Alikuwa mkimya na
mwenye mawazo mengi.Mara simu yake
ikaanza kuita.Akaangalia mpigaji Alikuwa ni
baba yake
“Nimesahau kuizima simu yangu.Siku kama
ya leo sitakiwi kupokea simu yoyote ile.Hii ni
siku yangu mbaya sana.Kwanza alianza
kufariki mdogo wangu tarehe kama ya leo na
kuniacha nikiwa peke yangu,miaka miwili
baadae siku kama ya leo nilipokea taarifa za
kifo cha mama yangu.Mwaka jana mchumba
wangu niliyempenda sana alipigwa risasi na
majambazi waliotaka kupora benki na
akafariki tarehe kama ya leo.No ! sipokei simu
hii.Tena ngoja niizime kabisa “ akawaza
Pauline na kushika simu yake ambayo bado
iliendelea kuita
“ I’m sorry dady.Leo sintapokea simu yoyote
hata simu yako” akasema Pauline na kupeleka
kidole chake katika kitufe cha kuzimia simu
lakini ghafla akabadili mawazo
“ Inawezekana baba akawa na jambo la
muhimu analotaka kuniambia.Ngoja
nimsikilize” akawaza Pauline halafu
akabonyeza kituife cha kupokelea.
“ Hallow baba” akasema
“ Hallow “ ikasema sauti ya kiume tofauti na
ile aliyoizoea ya baba yake.Pauline akastuka
“Hallow we ni nani? Akauliza Pauline kwa
wasi wasi.Sauti yake ilianza kutetemeka
“ Naongea na Pauline? Ikauliza sauti ile
“ Ndiyo unaongea na Pauline.Wewe ni nani?
Akauliza Pauline huku akitetemeka
“ Mimi naitwa David”
“ Mwenye simu hii yuko wapi? Umeipata wapi
simu yake? Akauliza Pauline
“Naomba unisikilize Pauline.” Akasema David
na kumfanya Pauline azidi kutetemeka
“ Uko wapi mida hii?
“ Niko hapa nyumbani Njiro”
“ Ok.sasa ni hvi naomba uje hapa katika hii
hospitali ya wachina baba yako amelaza hapa
amepatwa na tatizo kidogo.Utanikuta hapa”
akasema David na kukata simu
“ Hallo Dav……!!!.” Akaita Pauline lakini tayari
David alikwisha kata simu.Pauline akahisi
kuchanganyikiwa.
“Ouh Mungu wangu kwa nini kila ikifika tarehe
kama hii kila mwaka lazima niwe ni mtu
mwenye huzuni? Kuna nini katika tarehe hii?
Tafadhali naomba umponye baba yangu.Bado
namuhitaji sana katika maisha yangu.yeye
ndiye mtu pekee na wa muhimu kwangu kwa
sasa.Please Lord save him” akaomba Pauline
huku akiinuka na kuelekea chumbani kwake
akavaa haraka haraka na kutoka kwa
kasi.Alikuwa anatetemeka mwili.Alistushwa
sana na taarifa zile.Akapanda katika gari lake
lakini mikono ilikuwa inamtetemeka bado.
“ I have to do this.I have to drive..!!” akasema
Pauline halafu akavuta pumzi ndefu na
kuliwasha gari akaondoka kuelekea hospitali
SEPTEMBER 11 NI SIKU YA KUMBU KUMBU
MBAYA KWA ROBIN KWANI NDIYO SIKU
ALIYOTENGANA NA MKE WAKE.NINI KISA
CHA KUTENGANA KWAO? DAVID NI NANI?
KWA NINI ALIFUNGWA? JE NINI KITATOKEA
HAPO HOSPITALI? PICHA NDIYO KWANZA
LIMEANZA ENDELEA KUIFUATILIA SIMULIZI HII
BILA KUKOSA.
 
Pauline alifika hospitali na moja kwa moja
akaelekea mapokezi kuulizia kuhusu hali ya
baba yake.Wahudumu waliokuwa mapokezi
wakampa moyo na kwamba asiwe na wasi
wasi baba yake alikuwa anaendelea
vizuri.Pauline akaomba kuonana na daktari
mkuu lakini akaombwa asuburi kwa sababu
kwa muda huo mganga mkuu alikuwa
anamuhudumia mtu mwingine.Akaenda kukaa
katika viti vya kupumzikia huku ameinamisha
kichwa.Kichwa chake kilijaa mawazo
mengi.Alijiona ni mtu mwenye mkosi katika hii
dunia.Aliichukia September 11.Kila mwaka
huwa ni siku mbaya sana kwake.
“ Kuna nini katika tarehe hii? Kwa nini kila
mwaka katika tarehe hii lazima nikumbwe na
jambo baya? Kwanza alikuwa mdogo
wangu,halafu mama yangu ,akafuata
mchumba wangu na mwaka huu ni baba
yangu.Nani atafuata mwaka ujao? Ouh gosh
I’m tired of this..Maisha yangu yamegeuka na
kuwa ya huzuni kubwa kutokana na tarehe
kama ya leo. Lazima kuna jambo ambalo
haliko sawa na ndiyo maana kila ikifika tarehe
kama ya leo lazima kuna jambo baya
linatokea.” Akawaza Pauline mara akahisi
kama mkono wa mtu umeligusa bega
lake.Akainua kichwa na kukutanisha macho
na kijana mmoja mwenye uso uliopauka na
mavazi kuukuu.Hakuwa na kumbu kumbu
kama amewahi kumuona kijana Yule mahala
kokote.Sura yake ilikuwa ngeni kabisa
machoni pake
“nadhani wewe ndiye Pauline? Akauliza Yule
kijana.Huku akisita Pauline akajibu
“ Ndiye mimi.wewe ni nani?
“ Mimi ni David.!!..”
Pauline akastuka na kushangaa .
“ Naomba unifuate huku nje ninahitaji
kuongea nawe” akasema david.pauline
akainuka na kumfuata kijana Yule.
“ Wewe ndiye uliyenipigia simu? Akauliza
Pauline
“ Ndiye mimi” akajibu David
“ baba yangu anaendeleaje? Amepatwa na
tatizo gani?
“ Usihofu Pauline .Baba yako anaendelea
vizuri .Alipatwa na tatizo la shinikizo la damu
akiwa barabarani na kupoteza mwelekeo.Kwa
bahati nzuri hakuwa katika barabara yenye
magari mengi na hakuwa katika mwendo
mkali vinginevyo ingekuwa mbaya sana
kwake.Nilifanikiwa kuliendesha gari lake na
kumkimbiza hapa hospitali ambao
amepokelewa na ameanza kuhudumiwa na
madaktari wanasema kwamba hali yake
inaendelea vizuri.” Akasema david
“ Ouh ahsante sana David.Ni kweli baba
yangu huwa ana tatizo hilo la shinikizo la
damu .Nashukuru sana kwa kumsaidia baba
yangu.Mungu akubariki David “ akasema
Pauline huku akifungua pochi lake na kutoa
noti tatu za shilingi elfu kumi kumi akampatia
David.
“ Ahsante sana Pauline lakini naomba uziweke
fedha hzo utazitumia kwa matumizi
mengine.Nimemsaidia baba yako kama
ambavyo ningeweza kumsaidia mtu mwingine
yeyote bila malipo.” Akasema David ingawa
alizihitaji sana fedha zile ili ziweze kumsaidia
katika wakati huu mgumu ambao anahitaji
sana fedha ili aweze kuyaendesha masha
yake.
“ david tafadhali naomba uzichukue fedha hizi
kama ahsante yangu kwa kitendo chako cha
kumsaidia baba yangu.Umefanya jambo
kubwa sana na hii ni shukrani yangu na si
kwamba ninakulipa.tafadhali naomba upokee
David” Pauline akasisitiza
“ Ahsante sana Pauline lakini sintaweza
kuzipokea fedha hizo.Nimefanya ninalotakiwa
kufanya kama binadamu.” Akasema David na
kumfanya Pauline atabasamu huku
akizirejesha fedha zile katika mkoba wake.
“Pauline mbona uko peke yako? Mama yako
yuko wapi? Ndugu zako wengine wana taarifa
kuhusiana na ugonjwa wa baba yako?
Akauliza david
“Mama mdogo yuko Morgoro na tayari
nimekwisha mfahamisha na hivi sasa
anafanya mipango ya usafiri ili aweze kurejea
mara moja.Anaangalia uwezekano wa kupata
ndege ya haraka.Ndugu wengine nao
nimekwisha wataarifu ingawa wanaishi mbali
na hapa Arusha.” Akasema Pauline na David
akauliza tena
“ mama yako mzazi yuko wapi?
“ mama yangu alikwisha fariki dunia”
akasema Pauline
“ Pole sana Pauline”
“ ahsante david.Haya ndiyo mambo ya dunia
kwa hiyo hatuna budi kuyakubali na
kuyazoea.Kifo ni sehemu ya maisha yetu
wanadamu” akasema Pauline
“ Kwa hiyo hakuna ndugu wengine wa karibu
ambao unaweza ukashirikiana nao katika
kumuuguza baba yako?
“ Kwa hapa arusha baba hana ndugu zaidi ya
marafiki .Ndugu zake wengi wako mikoani
hususani Mbeya na wengine wako Ulaya.”
Akasema Pauline.
“ sawa Pauline.Naomba basi nikukabidhi
ufunguo wa gari la mzee na badhi ya vitu
vyake.Hii ni simu yake na ndani ya gari kuna
mkoba wenye fedha.Sifahamu kuna kiasi gani
cha fedha katika mkoba ule lakini nimetoa
hapo kiasi kilichokuwa kinatakiwa kulipwa
hapa hospitalini na risiti ni hii
hapa.Utanisamehe Pauline kwa kushika vitu
vya baba yako bila ruhusa lakini sikuwa na
namna nyingine kwani zilikuwa zinatakiwa
fedha za haraka na mimi sikuwa na fedha
hizo zilizokuwa zinatakiwa” akasema
David.Pauline akavua miwani na kumuangalia
David usoni.
“ Ni kweli leo baba alikuwa na safari ya
kuelekea benki kupeleka fedha.Ahsante Mungu
kwa kijana huyu wa ajabu kukutana na
baba,wangekuwa ni vijana wengine kwanza
wangeondoka na gari na fedha zote na
kumtelekeza baba,lakini David ameweza
kutunza uaminifu na nina imani hajachukua
hata senti moja katika mamilioni ya fedha
zile.” Akawaza Pauline
“ Pauline ahsante sana nadhani kwa sasa
mimi naweza kuondoka” akasema david
“ nashukuru sana kwa msaada na uaminifu
wako mkubwa David.Watu kama wewe ni
nadra sana kuonekana katika dunia hii ya
sasa.Ningekuomba David uendelee kubaki
hapa hadi baba atakapopata nafuu ili aweze
kumshuhudia kijana huyu wa aina yake
ambaye ameyaokoa maisha yake “ akasema
Pauline
“ Hata mimi ningefurahi sana kama
ningeendelea kukaa hadi baba yako
atakapopata nafuu lakini nasikitika Pauline
nalazimika kuondoka.Kuna mambo ambayo
natakiwa kuyashughulikia “ akasema david
“ david usijali kama ni kazi niko tayari
kukulipa hata fedha ambazo ungepaswa
kulipwa leo .Naomba uendelee kukaa nami
hapa hospitali.Nahitaji mtu wa kunisaidia
kumuuguza baba na kunipa nguvu.Nakuhitaji
David.Tafadhali naomba tuendelee kuwa wote
hapa hospitali.” Akasema Pauline.David
akainama akawaza na kusema
“ Sawa Pauline nimekubali ,nitaendelea kukaa
hapa hospitali.”
“ ahsante sana David.Usijali nitakulipa
gharama zote za siku ya leo.Unafanya kazi
wapi?
“Sina kazi? Akajibu David kwa ufupi.Pauline
hakuonyesha kuridhishwa na jibu lile akauliza
tena
“ Unaishi wapi david?
“ Kwa sasa sina mahala pa kuishi” akajibu
David akiwa ameinamisha kichwa chini
“ Huna mahala pa kuishi? Unamaanisha nini
unaposema hivyo? Pauline akashangaa
“ Pauline naomba nikueleze ukweli kwamba
mimi si mwenyeji wa Arusha . siku hii ya leo
nimemaliza kifungo changu katika gereza la
Oltoreo na nimeachiwa huru.Kwa hivi sasa
sijui nielekee wapi na wala nitaanzaje maisha
yangu.hakuna mtu ninayemjua hapa Arusha
na sijui nielekee wapi ndiyo maana nilihitaji
kwenda kuendelea kutafuta namna
nitakavyoweza kuimaliza siku ya leo .”
akasema David
“ Ouh my gosh !!..akasema Pauline na
kumtumbulia macho David kana kwamba
amekutana na mzuka.
******************************
Kikao na wageni waliokuwa wamemtembelea
kilimalizika ,Robin akaagana nao kisha
akarejea ofisini kwake.Wakati akiufungua
mlango kuingia ofisini ,Neema katibu wake
muhtasi akamfahamisha kwamba wakati
akiwa katika kikao na wageni wake kuna simu
imepigwa toka shuleni kwa Penny wakimtaka
afike mara moja kuna tatizo limetokea.Robin
akastuka sana
“ Kuna tatizo gani? akauliza
“ Sifahamu bosi.Mwalimu aliyepiga amesema
ufike pale mara moja mara baada ya kumaliza
kikao chako”
“ Ouh my God ! Penny anaweza akawa
amepatwa na tatizo gani? akajiuliza Robin na
kwa haraka akaingia ofisini kwake akachukua
mkoba wake na kutoka kwa kasi
“ Neema sitisha miadi yangu yote siku ya
leo.Inawezekana Penny amepatwa na tatizo
kubwa kwa hiyo sitegemei kurudi tena.”
Akasema Robin na kuchomoka kwa kasi hadi
katika gari lake na kuondoka kuelekea shuleni
kwa Penny.
“ Ouh Mungu wangu naoba unisaidie
mwanangu Penny asiwe amepatwa na jambo
baya.nampenda sana mwanangu na sipendi
kumuona akipatwa na matatizo.yeye ndiye kila
kitu kwangu” akawaza Robin
Alifika shuleni anakosoma mwanae na
kuelekea moja kwa moja katika ofisi ya mkuu
wa shule.Jasho lilikuwa linamtiririka.
“ Karibu sana” Robin akakaribishwa na
mwalimu mmoja wa kike mwenye sura nzuri
sana,mrefu mwembamba na mwenye nywele
ndefu.Alikuwa na suati laini sana huyu
mwalimu
“ Ahsante mwalimu.Mimi naitwa Mr Robinson
ni baba mzazi wa mwanafunzi anaitwa
Penny.Nimepata ujumbe kwamba natakiwa
shuleni haraka kuna jambo limetokea.Nomba
unieleze mwalimu,mwanangu Penny
amepatwa na tatizo gani? akauliza Robin kwa
wasi wasi.Yule mwalimu mwenye uzuri wa
kipekee akamuangalia Robin usoni na kusema
“ wewe ndiye baba yake Penny?
“ Ndiye mimi mwalimu.Mwanangu penny
amepatwa na tatizo gani? akauliza Robin kwa
wasi was.mwalimu Yule hakumueleza
chochote akainuka na kumuomba Robin
amfuate.
“ Mwalimu mbona huniambii mwanangu
amepatwa na tatizo gani? akauliza Robin
lakini mwalimu Yule ambaye alikuwa
akitembea kwa haraka hakumjibu
kitu.Wakayavuka majengo ya shule na
kuelekea katika majengo yaliyoonekama kama
nyumba za kuishi.Wakaelekea katika nyumba
moja iliyokuwa na geti kubwa jekundu.Yule
mwalimu akalifungua wakaingia ndani .
“ penny yuko huku? Anaumwa?? Akauliza
Robin.Yule mwalimu hakumjibu kitu
akaufungu mlango mkubwa wa kuingilia
sebuleni wakaingia katika sebule kubwa
“ Surprise..!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!......” Sauti kubwa
ikasikika mara tu Robin alipoingia pale
sebuleni.Akastuka sana.Moyo ulikuwa
unamwenda mbio.Penny mwanae akiwa na
wanafunzi wenzake zaidi ya kumi walikuwa na
nyuso zenye furaha kubwa .Walikuwa
wamesimama wakiwa na maua mikononi.
“ Ouh my gosh ..Penny !!!!!.. akasema Robin
kwa mshangao.Penny akamsogelea
“ Happy birthday dady” akasema Penny
Robin alishindwa kuyazuia machozi kumtoka
.Akainama na kumkumbatia mwanae.Ilikuwa
nisiku yake ya kuzaliwa lakini kutokana na
mawazo mengi aliyokuwa nayo hakukumbuka
kabisa kuhusu siku hii muhimu.
“ Ahsante sana Penny.Ahsante sana
mwanangu” akasema Robin huku wanafunzi
wakipiga makofi.Penny akamshika mkono na
kumuongoza hadi katika meza ilikokuwa
imeandaliwa keki nzuri yenye maandishi
mazuri ya kumtakia yeye Robin heri ya siku
yake ya kuzaliwa.Mishumaa ikawashwa halafu
akaipuliza yote na kuizima ,wanafunzi
wakapiga makofi.Robin alikuwa na furaha
iliyopitiliza.
Wakati wanafunzi wakiwa jikoni wakiandaa
chakula,mwalimu mkuu akamfuata Robin huku
akitabasamu na kusema kwa sauti laini.
“ Happy birthday Mr Robin”
Robin akatabasamu na kushukuru.
“ Penny alinifuata na akaniomba kwamba
anahitaji kumfanyia baba yake kitu muhimu
katika siku yake ya kuzaliwa na akaniomba
msaada wa mawazo nikampa wazo hili la
kukufanyia sherehe ya kustukiza”
Robin akatabasamu na kusema
“ Ouh kumbe lilikuwa ni wazo lako..!
Nashukuru sana mwalimu.Nashukuru
sana.Sikuwa na kumbu kumbu yoyote
kuhusiana na siku yangu ya kuzaliwa”
“ Ni kweli.Watu wengi huwa hawakumbuki siku
zao za kuzaliwa na hasa kutokana na
kutingwa na kazi nyingi au kutokuona
umuhimu wa siku hii” akasema mwalimu
halafu kikapita kimya cha muda ,Robin
akauliza
“ Mwalimu utaniwia radhi kwani nilikuwa
katika wasi wasi mwingi na sikukumbuka hata
kuuliza jina lako.Sijui unaitwa mwalimu nani?
“ Naitwa mwalimu Lucy” akajibu
“ Ouh kumbe wewe ndiye mwalimu Lucy.!!
Penny amekuwa akikutaja kila siku.Ninafurahi
kukufahamu”
“Hata mimi nimefurahi kukufahamu.namp
enda sana Penny ni mwanafunzi wa pekee
kabisa.Ana adabu,ana akili sana darasani,ni
msafi anajituma katika kazi na ni binti
mwenye uelewa wa hali ya juu kabisa.Nilikuwa
natamani sana kukutana na wazazi wake siku
moja kwani tabia hii njema na kila
alichonacho kimetokana na malezi bora ya
wazazi wake.Kwa bahati mbaya Penny
aliniambia kwamba mama yake hayuko nanyi
tena.Napenda kukusifu kwa malezi mazuri
uliyompa mwanao.Si kazi rahisi kuwa baba na
mama kwa wakati mmoja.Lakini wewe
umemudu na kumfanya Penny awe hivi
alivyo.Hongera sana..” Akasema mwalimu
Lucy
“ nashukuru sana mwalimu Lucy.Kuhusu
malezi ya Penny ni kwamba sote tumeshiriki
kumlea na kumfikisha hapa.Sote tumetimiza
wajibu wetu ipasavyo.Kama mzazi na kama
mwalimu.naomba tuendelee kushirikiana
katika malezi ya watotowetu hawa” akasema
Robin.
Ilikuwa ni siku nzuri sana kwa Robin na
mwanae Penny.Alihisi furaha ya aina yake
ambayo aliikosa kwa muda mrefu.Baada ya
sherehe ile ndogo wakaondoka na kurejea
nyumbani kwao.
“ Penny nashukuru sana kwa tukio la
leo.Umeikumbuka siku yangu ya
kuzaliwa.Umenipa furaha sana
Penny.Sikutegemea kabisa kama ungeweza
kunifanyia jambo kama hili” akasema Robin
wakiwa mezani wakipata chakula cha usiku
“ Baba,ni muda mrefu nimekuona huna furaha
hata kidogo na huikumbuki tena siku yako ya
kuzaliwa.Nikaongea na mwalimu Lucy akanipa
wazo la kukufanyia sherehe ile ndogo ya
kustukiza.” Akasema Penny halafu
wakaendela kula kimya kimya
“ baba ,mama unawasiliana naye? Akauliza
Penny na kumstua baba yake.Hakutegemea
swali lile toka kwa mwanae.Ikamchukua muda
kidogo kujibu
“ Hapana Penny.Mama yako toka alipoondoka
sijawahi kuwasiliana naye tena.Kwa nini
umeuliza?
“ Nilitaka tu kufahamu kama una mawasiliano
naye kwa sababu imepita muda mrefu sana
sijawahi kumuona na hata kuisikia sauti
yake.Hatukumbuki tena.Amekwisha tusahau”
akasema Penny.Maneno yale yakamuumiza
sana Robin
“ Penny mwanangu naomba usiwaze mambo
kama hayo.Mimi niko hapa na chochote
utakachokitaka utakipata.Iko siku mama yako
atatukumbuka na atakuja kukutembelea”
akasema Robin.Penny akaacha kula akaweka
kijiko mezani na kuonekana kuzama katika
mawazo
“ Sina hakika kama siku moja atakuja
tena.Ninashangaa sana roho aliyonayo mama
yangu.hanikumbuki hata mimi mtoto wake ,na
hataki hata kujua ninaendeleaje.Baba
simpendi mama yangu na sitaki hata
kumuona” akasema Penny
“ penny usiseme hivyo.Hata kama amekukosea
kiasi gani lakini atabaki kuwa mama
yako.Inakubidi umpende na usimchukie.Kitu
tunachotakiwa kufanya ni kumuombea ili awe
na maisha mazuri huko aliko” akasema
Robin.Penny akainamisha kichwa na kufikiri
kwa muda kisha akainua kichwa chake na
kusema
“ Baba umemuona mwalimu Lucy? Akauliza
Penny. Baba yake akatabasamu
“ ndiyo nimeonana naye leo.Amekumwagia
sifa nyingi kwamba wewe ni mwanafunzi
hodari mwenye bidii na nidhamu.”
“ Nampenda sana mwalimu Lucy.Ni mpole na
mkarimu.Ananipenda sana.aliniomba siku
moja aje afahamu mahala ninakoishi.Nime
mwambia nitawasiliana nawe kwanza ili kama
utakubali basi tumualike aje jumamosi ya wiki
hii” akasema Penny.Baba yake akatabasamu
na kusema
“Nadhani jumamosi ni siku nzuri.Mwambie
tutamkaribisha siku ya jumamosi.” Akasema
Robin na uso wa Penny ukapambwa na
tabasamu pana sana.Sura ya mwalimu Lucy
ikamjia Robin kichwani akatabasamu.
“ She’s so pretty.Ana uzuri wa kipekee
kabisa.anaonekana ni mwenye roho nzuri na
anapenda sana watoto” akawaza Robin huku
akitabasamu na kuvuta pumzi ndefu.
 
ENDELEA…………………………………..
Baada ya kumaliza kula akamuacha mwanae
akiendelea na kujisomea yeye akaelekea
chumbani kwake akajilaza kitandani.Akavuta
pumzi ndefu
“ Siku yangu ilianza vibaya kwa kuota ndoto
mbaya lakini imeisha vizuri sana.Sikutegema
kama siku hii ya leo ingeisha nikiwa na
furaha kubwa namna hii.Penny amenifanya
niwe na furaha.namshukur sana Mungu kwa
kunipa mtoto huyu mwenye akili nyingi .Nina
haki ya kujisifu kwa malezi niliyompa na
kumfanya awe hivi alivyo.Namsikiotikia sana
Flaviana kwa kitendo chake cha ukatili
alichokifanya na kumsahau kabisa
mwanae.Penny ameumizwa sana na kitendo
hiki na kwa sasa anamchukia kabisa mama
yake na hataki hata kumuona tena.Ana haki
ya kumchukia lakini sitaki afanye hivyo.Yule
ni mama yake na ataendela kuwa mma yake
hata kama amemkose akiasiagani.” Akawaza
Robin akiwa amejilaza kitandani.Mara picha
ya mwalimu Lucy ikamjia tena kichwani
akatabasamu
“ Penny na mwalimu Lucy wanapendana
sana.Nilimsikia akimuongela mara nyingi na
sikuwahi kumuona mwalimu Yule,lakini
nilipoonana naye leo nilistujka
kidogo.Japokuwa nmlkuwa na mstuko
kutokana na taarifa zile za kuakiwa kufka kwa
haraka shulenmi lakini nilisisimka kidogo
baada ya kuiona sura yake.Dah ! ni
mwanamke mzuri sana.Ni mzuri wa sura na
umbo na ananekana ni mwanamke mwenye
hekima na busara na anapenda sana
watoto.Ninamshukuru kwa kuwa amekuwa
karibuna Penny na amemsaidia kuupata ule
upendo wa mama ambao ameukosa kw
amiaka mingi.Nadhani anastahiliheshima ya
kipekee kabisa .Itabidi siku hiyo atakapokuja
hapa nyumbani apewe mapokezi ya kipekee
kabisa ili kumuonyesha shukrani zetu na
kumshukur kw akazi kubwa anayoifanyakwa
mwnaangu Penny.” Akawaza Robin halafu
akajgeuza upande wa pili
“Itanibidi nimtafutie na kijizawadi kidogo
kama ahsante yangu kwake.Nitaongea na
Penny aniambie mwalimu wake anapendelea
vitu gani.” akawaza Robin.Sura ya
mwalimuLucy bado iliendelea kumjia
kichwani.Alikumbuka namna alivyokuwa
akitabasamu
“ Naomba nikiri kwmaba nimevutiwa sana na
Yule mwalimu.Sijui imenitokeaje lakini ghafla
tu baada y akumuona nimejikuta nikivutiwa
naye.lakini hata hivyo sitakiwi kuanza
kuumiza kichwa changutena kwani mwanamke
mzuri kama Yule hawezi kukosa mtu
wake.tena inawezekana mwenzi wake akawa
ni mtu mwenye uwezo mkubwa
kiuchumi.Ngoja nijenge kwanza urafiki naye
wa kawaida tu .Sitaki kutafuta matatizo tena
kwa wakatyi huu japokuwa ninahuitaji sasa
kutafuta mwanamke ambaye atanipenda na
kumpenda mwanangu.” Akawaza Robin
****************************
Pauline bado aliendela kumuangalia David
kwa macho makali .
“ Ouh gosh ! siamini kama maneno haya
nayonieleza David ni ya kweli.Ametoka
gerezani? Kwa ninialifungwa? Al;ifanya kosa
gani kijana mwenye roho nzuri kama huyu?
Hanyeshi kama ni kijana mhalifu au
anayeweza kutenda kosa lolote la kijinai.Kuna
kitu nimekigundua kwa kijana huyu .Kuna kitu
kimejificha ndani yake “
“Pauline mbona unaniangalia namna hiyo?
Samahani kama nimekustua kwa kukuambia
ukweli wangu kwmaba nimetoka
kifungoni.Lakinihuo ni ukweli halisi na endapo
haujisikii vizuri au kama umeogopa kwa
kudani labda ninaweza kuwa ni
mhalifu,isikupe shaka mimi nitaondoka na
nitarejea tena kesho kuja kumaugali mzee
wako” akasema David
“ Hapana David ,si hivyo unavyowaza.Sama
hani kwa kukuangali namna hii.Ni kweli
nimestushwa sana na kusikia kwamba ulikuwa
umefungwa na hivi leo umemaliza kifungo
chako.Nilikuwa najiuliza ni kosa gani ambalo
limepelekea kijana mwema kama wewe
ukaenda kule?
David akatabasamu na kusema
“ Umejuaje kama mimi ni mwema?
“Mtu mwema hana alama usoni lakini
anajulikana kutokana na maneno na matendo
yake.Kitendo ulichokifanya leo hii kwa mzee
wangu kinadhihirisha hayo kwamba u kijana
mwema na mweney roho ya ajabu sana.Ni
mfano wa kuigwa”
“ ahsante sana Pauline kwa kulitambua hilo
.Ahsnte kwa kuniamni pia kwa sababu zama iz
ni nadra sana kwa mtu kuaminiwa kwa haraka
namna hii.Siku hiz hata wazazi wanashidwa
kuwaamini watoto wao. Dunia imebadilika
sana.Upendo uaminifu vimetoweka.Ubinafsi
umetawala siku hizi na kila mmoja
anajiangalia yeye pekee.Pamoja na hayo
najaribu kuionyesha jamii kwamba tunahitaji
kurejesha upendo miogoni mwetu.Tuhurumia
ne,tupendane na tusaidiane.” Akasema
David.Pauline akazidi kuvutiwa na maeno
yake
“ David una mneno ya busara sana.Nafurai
kukutana na mtu kama wewe.Hata baba nina
imani atafurahi sana kukuona kijana mwenye
uaminifu wa aina yake kama wewe.Naomba
nichukue nafasi hii kukukaribisha uishi
nyumbani kwetu.Tuna nyumba kubwa tu hapa
Arusha na tunaishi watu wachache,mimi baba
na mama mdogo pamojana mfanyakazi wetu
mmoja.Kwa kuw aka sasa huna sehemu ya
kuihsi naomba ukubali kwenda kuishi
nyumbani kwetu “
“ Paulne nashukru sana lakini naomba nisiwe
mzigo kwa familai yenu kwa msaada huu
niliomsaidia baba yako.”
“ Haoana David.Wewe umetoa msaada kwa
baba yangu na kwa familai yanguna sisi kama
ulivyofanya wewe tunakusaidia wewe.Umekiri
kwamba huna sehemu ya kuishi kwa hiyo
nakukaribisha nyumbani kwetu.Utaishi nasi
pale hadi hapo maisha yako yatakapokua
mazuri .”
“ Pauline familia yako itaweza kunikubali mtu
kama mimi na hasa muonekano wanguna
wakigundua kwamba nimetoka
gerezani,wataniogopa na kudhani kwamba
mimi ni mhalifu kama ilivyojengeka katika
jamii kwamba kila mtu anayefungw agerezani
ni mhalifu.”
“ David naomba unisikilize mimi.Muoneano
wa mtu si tabia ya mtu.Wewe si mhalifu na
ungekuwa na tabia hizo ungeondoka nay ale
mamilioni ya bba yaliyokuw akatika
mkoba.Unajua kulikuwa na kaisi gani katika
ule mkoba? Kulikuwa na shlingi million
themanini na saba.NI pesa nyingi ambazo
ungeweza kwenda kuyaendesha maisha yako
bila matatizo .Hicho ni kithibitisho tosha
kwmaba wewe si mhalifu na kama ulifungwa
basi ni kw amakosa mengne lakini si kwa
uhalifu.Tafadhalinaomba ukubalikuja kuishi
nasi.Usihofu kuhus muonekano.Hiki ni
kituambacho kinawea kubadilishwa ndani ya
dakika mbili.” Akasema Pauline.David
alishindwa kukataa kwani alihitaji sana
sehemu ya kuweza kuishi wkati akiyapanga
maisha yake vizuri.
Kwa kuw amgonjwa ao alikuwa amelala kwa
wakati huo ,Pauline akamuomba David
waende wakapate chakula cha mchana
.Wakaingia katika gari la Pauline na kuelekea
katika hoteli moja kubwa .
“ Pauline umenileta katika hoteli hii ,naomba
nisikutie aibu kutokana na muonekano
wangu” akasema David na kumfanya Pauline
acheke
Waliaguiza chakula na kuanza kula.Pauline
alikuwa anamchunguza David kwa kuibia
namna alivyokuwa anakula.
“ David anaonekana ni kijana ambaye
anafahamu vitu vingi.Muonekano wake na
matendo yake viko tofauti ana.” Akawaza
Pauline
Wakati wakiendela kula mara Pauline
akapigiwa simu akapokea na kuongea na mtu
aliyempigia na alipomaliza akamgeukia David
“ Ni mama mdogo amenitaarifu kwamba
amekosa ndege ya haraka kwa hiyo hataweza
kuja leo .Atakuja kesho” akasema Pauline
halafu akainama na kuzama katika mawazo.
“Pauline kuna tatizo lolote? Akauliza david
“ David ninasikitishwa sana na huyu mama
yangu mdogo kwani amekuwa akimpa baba
wakati mgumu sana.Toka mama yangu
alipofariki dunia na baba akaamua kuoa
mwanamke mwingine akitegemea kuwa na
maisha yenye furaha lakini imekuwa tofauti
sana.Maisha yake hayana furaha hata
kidogo.Huyu mama amekuwa akimpa wakati
mgumu sana” akasema Pauline
“ Matatizo katika ndoa ni kitu cha kawaida
lakini kuna kitu kimoja ambacho unatakiwa
ujiulize kwamba je huyo mama yako mdogo
anampenda baba yako ?
Swali lile likampa Pauline ugumu wa kulijibu
“ Sifahamu David.Siwezi kujua kama
anampenda baba yangu ama vipi lakini
ninachofahamu ni kwamba yeye amekuwa ni
chanzo cha matatizo mengi ya baba.Amekuwa
na utumiaji mbaya sana wa fedha na hivyo
kuifanya baadhi ya miradi ya baba kufungwa
kitu ambacho kimekuwa kikimuumuza sana
baba yangu na kumfanya awe na mawazo
mengi”
David akastuka sana kwa maneno yale ya
Pauline
“ Mbona umestuka Dadid?
“ Its nothing..” akajibu David na kumstua
kidogo Pauline
“ Kumbe David anafahamu kiingereza vizuri !!
Kuna mambo ambayo yamejificha ndani
yake.Kuna haja ya kumfahamu kwa undani
kijana huyu.Lakini itabidi kwenda naye
taratibu kwani anaonekana hapendi
kuyazungumzia maisha yake.” Akawaza
Pauline.
Baba yake Paulne alikuwa anaendelea vizuri
na madaktari wakawaomba Pauline na David
waende wakapumzike na wasiwe na wasi wasi
na afya ya mgonjwa wao kwani maendeleo
yake yalikuwa mazuri.hawakuweza kuongea
naye kwa jioni hiyo kwa kuwa alikuwa
amelala.Wakaondoka pale hospitali na
kuelekea nyumbani kwa akina Pauline maeneo
ya Njiro.David alikuwa akimfuata Pauline
akiendesha gari la baba yake Pauline na
Pauline yeye akiendesha gari lake
Walifika nyumbani kwa akina Pauline David
akakaribishwa ndani .Lilikuwa ni jumba kubwa
na la kifahari.
“ Wow ! I’m back to life again” akawaza David
huku akitabasamu
PICHA YA MWALIMU LUCY INAANZA
KUJENGEKA KICHWANI KWA ROBIN.DAVID
NAYE AMEKARIBISHWA NYUMBANI KWA
AKINA PAULINE..ENDELEA KUFUATILIA
SIMULIZI HII……..
 
ENDELEA………………………………………………..
Ni saa mbili za usiku familia nzima imekaa
sebuleni.Mzee Zakaria amekwisha toka
hospitali baada ya madaktari kuridhika na
maendeleo yake.Pamoja nao sebuleni
alikuwepo pia David ambaye alikuwa kimya
sana.
“ David .! akaita mzee Zakaria na kumtazama
David
“ Naam mzee” akaitika David na kuelekeza
shingo yake alipokuwa amekaa mzee Zakaria
“Napenda kwa niaba ya familia yangu
nikushukuru sana kwa msaada wako
mkubwa.Uliyaokoa maisha yangu.Bila wewe
sijui hivi saa ningekuwa katika hali
gani.Nadhani ilikuwa ni kwa maongozi ya
Mungu nipite njia ile ili nikutane nawe.Nasema
ahsante sana” akasema mzee zakaria
“ Nashukuru mzee.Nilifanya jambo ambalo
linapaswa kufanywa na mtu yeyote mwemye
ubinadamu” akasema David
“ Jambo la pili ambalo nataka nikushukuru ni
kwa uaminifu wako mkubwa.Ulinifikisha
hospitali ukahakikisha nimepata
matibabu,ukawasiliana na familia yangu na
alipokuja Pauline ukamkabidhi kila kitu
ukiwemo mkoba uliokuwa na fedha zaidi ya
shilingi milioni themanini.Ni vigumu sana
kuamini lakini ni kweli ulifanya jambo
hili.Katika dunia ya sasa ni vigumu kuwapata
watu wenye uaminifu kama wako.Nasema
ahsante sana na ninakuomba uendelee na
uaminifu huo si kwangu mimi tu hata kwa
watu wengine .Ungeweza kuondoka na mkoba
ule wenye mamilioni ya fedha pamoja na gari
lakini hukufanya hivyo.Ahsante sana david”
akasema mzee Zakaria na David hakujibu kitu
akatabasamu.Vicky ambaye alikuwa amekaa
pembeni ya mumewe akiwa na glasi iliyoja
mvinyo akaweka glasi mezani na kuuliza
“ David nasikia ulikuwa umefungwa gerezani?
David akawaangalia wote kwa zamu halafu
akasema
“Ni kweli nilikuwa nimefungwa na siku
niliyokutana na mzee ni siku ambayo nilikuwa
nimemaliza adhabu yangu na nikaachiwa
huru” akasema David
“Pole sana david lakini tungependa kufahamu
ulifungwa kwa kosa gani? akauliza tena
Vicky.Mzee Zakaria na Pauline wote
wakamuangalia lakini hakujali akayaelekeza
macho yake kwa David
“Mama ni historia ndefu sana na samahani
wkani sitaki kuyaongelea mambo ambayo
yamepita.” Akasema david
“ jaribu kutueleza hata kidogo ili tupate walau
picha ni kitu gani hasa kilisababisha
ukapelekwa kule gerezani? Akauliza tena
Vicky.David alionyesha kutokupendezwa na
swali ile akainama chini na kuanza kufikiri.
“ Naomba David asiulizwe jambo lolote
linalohusiana na matatizo yaliyomkuta.Nao
mba aachwe atulie na atatueleza yeye
mwenyewe kama akipenda kutueleza pale
atakapokuwa tayari kufanya hivyo”akasema
mzee Zakaria.Mke wake akamtazma usoni na
kuonyesha kutokuridhishwa na kauli ile ya
mume wake
“ Honey ,sijamuuliza kwa ubaya , lengo langu
ni kumfahamu David kiundani ,ametoka
wapi,na nini malengo yake ya usoni baada ya
kutoka kifungoni” akasema Vicky
“ Naomba mjadala kuhusu David ufungwe
rasmi na sitaki kusikia mtu yeyote akimuuliza
kitu chochote kile kuhusiana na maisha yake
au wapi ametoka.Atatueleza pale
atakapokuwa tayari.” Akasema mzee Zakaria
halafu akamgeukia david
“ David utakaa hapa nyumbani kwangu kwa
muda wote utakaouhitaji wewe
mwenyewe.Hapa ni nyumbani kwenu na usiwe
na hofu yoyote.Nitakulea kama mmoja wa
wanafamilia yangu kutokana na msaada wako
mkubwa ulionisaidia.Endapo una tatizo lolote
naomba usisite kunieleza mimi au mama yako
hapa au mweleze Pauline lakini ningependa
kama una tatzio lolote uje unione mimi
mwenyewe.Sihitaji kufahamu umetoka wapi na
ulifanya nini ukafungwa gerezani ila
ninachofahamu nikwamba umenifanyia jambo
ambalo sijawahi kufanyiwa katika maisha
yangu na ambalo sioni kitu ninachoweza
kukufanyia ambacho kinaweza kulingana na
jambo ulilonifanyia.Jisikie amani hapa
nyumbani.” Akasema mzee Zakaria.Vick
akaingilia kati na kusema
“ Baba Pauline sioni kama unafanya
sawa.Huyu ni mtu ambaye umekutana naye
mtaani na hujui ametoka wapi,ndugu zake
wako wapi.Itakuwaje iwapo atapatwa na
matatizo akiwa nyumbani kwetu? Akauliza
Vicky
“Nimekwisha sema kwamba David atakaa
hapa nyumbani kama mwanafamilia na sitaki
maswali juu yake yaendelee kuulizwa.Ndugu
zake ni sisi hapa.Ndugu yake ni mimi hapa
aliyenisaidia na kuniokoa.” Akasema mzee
Zakaria akionyesha kukerwa na tabia ile ya
mke wake.David aliyekuwa akiyashuhudia
mabishano yale kati yam zee zakaria na mke
wake akasimama na kusema
“ Samahani mzee wangu.Nashukuru sana kwa
msaada wako mkubwa na kunisaidia niweze
kuishi hapa nyumbani kwako. Ni kweli
nilipotoka gerezani sikuwa na sehemu ya kula
wala kulala na sikujua ningeelekea
wapi.Sikuwa na mwelekeo wowote wa maisha
lakini mlinipokea katika familia
yenu.Mmenilea kama mwanafamilia
yenu.Pamoja na hayo mzee wangu ningeomba
nisiwe chanzo cha mvurugano katika familia
yako.Ningeomba uniruhusu niondoke
nikaendelee na maisha yangu mahala
pengine.. “ akasema David
“ David nimekwisha sema kwamba wewe ni
mmoja wa wanafamilia hii na utaishi hapa na
kauli yangu ni ya mwisho.Hutakwenda
sehemu yoyote ile.Utakaa hapa hapa”
akasema mzee Zakaria kwa ukali kidogo
halafu akainuka na kuelekea chumbani kwake
na kisha mke wake naye akainuka na
kumfuata
“ Pauline inaonekana mama yako
hajapendezwa kabisa na mimi kuwepo hapa
numbani.Sipendi niwe chanzo cha
matatiz…………….” David hakumaliza sentensi
yake Pauline akamkatisha
“ Shhhhhhhhhhhhhh..!! usiseme chochte
David.Baba amekwisha sema na utaendelea
kukaa hapa hapa kwetu.” Akasema Pauline na
kimya kifupi kikapita halafu akasema
“ David kesho kuna mzigo nitaupokea dukani
kwangu.Ningeomba uambatane nami
ukanisaidie kuupakua” akasema Pauline
“ Pauline unafanya biashara gani? akauliza
David
“ Nina fanya biashara ya nguo.Nina duka la
nguo “ akasema Pauline kisha wakaendelea
kuangalia filamu
**********************************
Saa tatu za asubuhi siku iliyofuata David na
Pauline wakaingia garini na kuelekea katika
ofisi za kampuni moja ya usafirishaji ambayo
walimsafirishia mizigo yake.Baada ya kulipa
pesa aliyokuwa anatakiwa kuilipa,mizigo yake
ikapakiwa katka gari la mizigo na kupelekwa
dukani kwake ikashushwa na kuhifadhiwa
katika chumba cha kuhifadhia mizigo.Baada
ya kumaliza kazi ile ya kuhifadhi mizigo
ile,Pauline akaendelea kuangalia hesabu za
duka lake na baadae wakaelekea katika hoteli
moja nzuri kwa ajili ya kupata chakula cha
mchana.
“ Hongera Pauline,duka lako zuri sana.Lina
nguo nzuri “ akasema David .Pauline
akatabasamu na kusema
“ Ahsante sana David umenisaida mno siku ya
leo.”
Wakaendelea kula kimya kimya halafu Pauline
akauliza
“ David umewahi kufanya biashara?
David akatabasamu kidogo na kusema
“Nina shahada ya biashara na nina uzoefu
katika masuala ya biashara” akasema david
na kumfanya Pauline amshangae
“ kweli? Akauliza Pauilne
“ Kweli Pauline.Nina shahada ya biashara
toka katika chuo kikuu cha dare s salaam na
nina uzoefu katika biashara na masoko.”
akasema David
“Wow ! basi ni maongozi ya Mungu amekuleta
kwetu.Nadhani baba atafurahi sana akisikia
kwamba una elimu ya biashara.Kwa muda
mrefu amekuwa akitafuta mtu
atakayemuamini wa kumsaidia katika
biashara zake.”
“ baba yako anajishughulisha na biashara
gani?
“ ana miradi mingi tu.Ana maduka ,miradi ya
mbao,vituo vya mafuta n.k
“ Ouh kumbe baba yako ni tajiri sana”
akasema David
“ Siwezi kukataa kwamba baba yangu ana
utajiri mkubwa lakini kwa siku za hivi karibuni
ameingia katika mgogoro mkubwa wa kifedha
baada ya kumuoa mama mdogo.Biashara
zake zimekuwa zikiyumba sana na kuna
biashara zake imemlazimu kuzifunga
kutokana na kuendeshwa kihasara.”
“ Nini hasa tatizo la mama yako mdogo?
“ mama mdogo ana matatizo
makubwa.Kwanza si muaminifu na ni mfujaji
sana wa fedha na nina wasi wasi anaficha
fedha kwa siri.Niliwahi kumueleza baba
kuhusu jambo hili lakini likazua matatizo
makubwa na nikaamua kuachana na biashara
za familia nikaanzisha biashara yangu.Toka
wakati huo baba amekosa mtu wa karibu wa
kumuamini.Lakini kwa siku za karibuni
ameanza kukubaliana na maneno yangu
kuhusiana na mama mdogo.” Akasema
Pauline
“Pauline nasikitika sana kwamba sintakubali
kufanya kazi kwa baba yako na kukutana na
mtu mwenye tabia kama za mama yako
mdogo.Sitaki kuingia katika mgogoro
mwingine hasa kwa wakati huu ambao
nahitaji kuyajenga upya maisha yangu”
akasema David
“David tafadhali naomba usikatae.Nitaongea
na baba ili uweze kumsaidia na
utakapomsaidia baba utakuwa umenisaidia na
mimi vile vile.I’m your friend ..right? akasema
Pauline
“ Ndiyo Pauline mimi nawe ni marafiki lakini
najaribu kuyakwepa matatizo hasa kwa wakati
huu ambao ninaanza kuyajenga upya maisha
yangu.”
“ David tafadhali naomba usikatae.Kama
huwezi kufanya kazi kwa baba do it for
me.Nisaidie mimi.Familia yangu inakuhitaji
sana na Mungu amekuelekeza kwetu ili uweze
kutusaidia.Tafadhali naomba usiseme
hapana.Baba kwa sasa anaumwa na anahitaji
mtu wa kuweza kumsaidia katika kazi zake
hasa kwa wakati huu ambao hana imani tena
na mama mdogo kutokana na vitendo vya
ufujaji wa fedha alivyovionyesha.Alinitaka
mimi nirudi kuisimamia miradi ya familia ili
kumpa yeye nafasi ya kupumzika lakini wakati
nikitafakari nitawezaje kufanya hivyo
umetokea wewe .David naomba usikatae
kutusaidia” akasema Pauline.David akainama
akaonekana kuzama katika mawazo mengi.
“ Nataka kujiingiza tena katika matatizo
ambayo ninajaribu kuyakimbia lakini nahisi
kushindwa kukataa kuwasaidia akina Pauline
katika kuisimamia miradi yao.Ni watu wazuri
wenye roho nzuri na moyo wa
ukarimu.Wamenikaribisha nyumbani kwao na
wananitunza kama mmoja wa
wanafamilia.Mzee zakaria ameonyesha
kuniamini lakini tatizo liko kwa mke
wake.Anaonekana kutokufurahishwa na uwepo
wangu pale katika familia yao na ndiyo
maana jana usiku alikuwa akijaribu kutaka
kuyachimba maisha yangu.Endapo mzee
Zakaria ataridhika nami na kuniomba
nimsaidie katika majukumu itanilazimu
kukubali na pengine hii inaweza kuwa ni fursa
yangu ya kuyatengeneza upya maisha yangu
yaliyopoteza mwelekeo.” Akawaza David
halafu akamtazama Pauline wote
wakatabasamu
“ Toka nilipokutana naye niliamini kuna kitu
ambacho kimejificha kwa david.Kumbe bi
kijana msomi na ana shahada ya
biashara !!..Kuna mambo mengi ambayo
yamejificha nyuma yake ambayo hataki
kuyaweka wazi.Kwa nini hataki kuiweka wazi
historia yake? Ametoka wapi na famili yake
iko wapi? Kwa nini alifungwa gerezani?
Amekuwa akiyakwepa kabisa maswali
haya.Kuna haja ya kumfahamu huyu
kijana.Niliwahi kusoma katika simulizi mbali
mbali kwamba kuna watu ambao hujiweka
katika hali kama hii ya David kumbe ni
wapelelezi .Nina wasi wasi sana na huyu
kijana.Kuna nyakati ninaanza kuingiwa na
wasi wasi naye lakini hata hivyo kuna ulazima
wa kumfahamu undani wake na ili
kumfahamu vizuri inabidi kujiwa naye karibu
sana.” Akawaza Pauline
Wakati david na Pauline wakipata chakula cha
mchana,Robin na mfanyakazi wake wa ndani
walikuwa katika pilika pilika za kufanya
manunuzi kwa ajili ya maandalizi ya ujio wa
mwalimu Lucy nyumbani kwao siku
itakayofuata yaani jumamosi.Walifanya
manunuzi ya vitu vingi ambavyo waliona
vingefaa kwa ajili ya siku muhimu kama
ile.Baada ya kuridhika na manunuzi
waliyoyafanya wakarejea nyumbani ambako
maandalizi kabambe yalianza ikiwa ni katika
kuiweka nyumba katika hali ya usafi na
unadhifu wa kipekee kabisa.
***************************************
Vicky alimuaga mumewe mzee Zakaria
kwamba kuna mahala anakwenda na
asingechelewa kurudi.Aliingia katika gari lake
la kifahari na kuondoka na breki ya kwanza
ilikuwa nyumbani kwa rafiki yake kipenzi
Safia.
“Vicky umerudi lini ? si uliniambia umekwenda
Morogoro na Yule kijana Danny? Imekuaje
umerudi mapema namna hii? Akauliza Safia
baada ya Vicky kuingia sebuleni kwake.Vicky
akautupa mkoba wake sofani na kuketi halafu
akavuta pumzi ndefu
“ Ouh Safia mimi sijui nina mkosi gani
jamani..!! akalalama Vicky ambaye
masikio,shingona vidole vyake vilipambwa
kwa vito vya thamani kubwa
“Kwa nini unasema hivyo Vicky? Akauliza
safia huku akimuita mfanyakazi wake wa
ndani na kumuomba awaletee vinywaji
“Nilikuwa na Danny katika hifadhi ya
Udzungwa tukila raha za dunia mara kila kitu
kikatibuka” akasema Vicky
“Ilikuaje Vicky? Nini kilitokea? Akauliza Safia
“Nilipigiwa simu na Pauline akaniambia
kwamba Yule mzee amepatwa na shinikizo la
damu na amelazwa hospitali.Ikanilazimu
niahirishe kila kitu na kurudi mara
moja.Nimerudi jana mchana .Nimechukia
sana Safia kwa kukatishwa katika starehe
zangu.Nilikuwa nikipata raha za dunia na
Danny na sikupanga kama ningerejea mapema
namna hii.Nimemchukia sana Yule
mzee.Hanikuni nitakavyo lakini ninapompata
mtu anayenikuna kisawasa kinaibuka
kikwazo.Naona ingekuwa vyema kama
angekufa tu ili niendelee na maisha yangu ya
starehe.Nimechoshwa na maisha haya ya
kufungwa ndani kama njiwa” akasema Vicky
“ Dah ! pole sana shoga.Kwa hiyo
anaendeleaje mzee? Akauliza Safasi
“ Linaendelea vizuri tu..” akajibu Vicky huku
akibetua midomo yake
“Pole sana shoga yangu.Usisikitike sana
.Jaribu kupanga tena miadi na Danny ili
mkutane tena na muendelee na mambo
yenu.Nafahamu ugumu unaoupata kwa yule
mzee .Jitahidi usije ukazeeka shiga
yangu.wewe bado mtoto mbichi kabisa”
“ Safia sijui kama nitaweza kumpata tena
Danny hivi karibuni.tayari amerudi kazini
kwake Botswana.Alikuja kwa dharura ya wiki
mbili na kumuona tena itachukua muda
mrefu.Sijui nitafanyaje mimi…!! Akalalama
Vicky halafu kimya kikapita
“Ninavyokwambia mimi nina bahati mbaya
,nimerudi kwagu na kumkuta Pauline
amemuokota muhuni mmoja na kumleta aishi
pale nyumbani kwangu.”
“ Muhuni ..!!!? Safia akashangaa
“ Mzee Zakaria anaweza kweli kukubali kuishi
na muhuni kwa ninavyomfahamu mzee Yule
alivyo na sheria kali?
“ hata mimi sielewi imetokeaje.Yaani Yule
mzee humuelezi kitu kuhusu huyo kijana.
Kijana mwenywe ametoka gerezani na
hajulikani hata kwao ni wapi ,ukitaka
kumuuliza ametokea wapi hajibu na mzee
Zakaria anakuwa mkali kama nini.Shoga
yangu nimekereka sana kwa sababu kwa
namna mzee anavyomuamini Yule kijana
kama hirizi yake ,nina wasi wasi akizoea sana
baadhi ya mambo yangu yanaweza yasiende
sawa.”
“ Dah ! hili sasa ni janga “ akasema Safia
“ janga si kidogo shoga ! yaani akili yangu
haifanyi kazi vizuri.Nataka nimalize nyumba
yangu haraka haraka ili ikiwezekana niachane
na Yule marehemu mtarajiwa.Unajua hata
kama akifariki hivi sasa sintakuwa na changu
pale kwa sababu sijazaa mtoto na Yule mzee
na siwezi kuzaa naye mtoto hata iwe vipi”
akasema Vicky
“Kwa hiyo umepanga nini shoga? Akauliza
safia
“ Kuhusu nini safia? Akauliza Vicky
“Kuhusu huyo kijana. Utamuacha aendelee
kukaa hapo nyumbani kwako?
“ Thubutu !!..labda siyo mimi Vicky
madhahabu..” akasema Vicky na kisha wote
kwa pamoja wakacheka kicheko kikubwa na
kugonganisha mikono.
“ namvutia kasi kwanza ili nimsome vizuri
nyendo zake kwa sababu kwanza anaonekana
ni mzubavu na asiyefahamu chochote.Ukimuo
na ni kama aliwahi kuchukuliwa msukule”
akasema Vicky halafu wote wakacheka tena
kicheko kikubwa sana
“ Lakini Vicky mimi nina wazo moja kuhusu
huyo kijana”
“ wazo gani Safia?
“Huyo kijana usimfukuze.anaweza akawa ni
mtaji mkubwa sana kwako.”
“ Kivipi? Akauliza Vicky
“Kama mzee zakaria anamuamini basi
unachotakiwa kukifanya ni kumuweka karibu
yako ili hata kama kuna jambo unalifanya
basi lisimfikie mzee Zakaria au Pauline.Wakati
mwingine wewe ni binadamu na una mahitaji
na hali ya mzee ndiyo kama hivyo
tena,unaweza ukamtumia huyo kijana
akakuliwaza” akasema Safia halafu Vicky
akacheka sana.
“ Ama kweli Safia umenichoka shoga
yangu.Yaani mimi Vicky madhahabu nilale na
Yule kinyago.!!? Hata kama nina hamu ya
namna gani na mwanaume lakini siwezi
kuthubutu kumvulia nguo Yule
kijana.Nakwambia ukimuona utashangaa
utafikiri ni msukule uliotoroka.Hana mbele wa
nyuma.Lakini kuhusu hilo la kwanza
ulilolisema kwamba naweza kuwa naye karibu
nitalifikiria lakini sina hakika kama anaweza
akakubali kushirikiana nami.” akasema Vicky
“ Vicky hakuna kitu kinachoshindikana hapa
duniani.Pesa ndiyo inayowezesha kila
kitu.Ukiwa na pesa utaweza kufanya lolote
unalotaka.Hata huyo kijana endapo ataonja
pesa atakuwa tayari kushirikiana
nawe.Inawezekana huko alikotoka alikuwa
kibaka kwa hiyo endapo ataonja maisha
mazuri na ukampatia fungu la kutosha basi
atakufanyia kila unachokitaka.Kuhusu
kumtumia huyo kijana kingono sikuwa na
maana mbaya na wala sikutaka kukushusha
thamani shoga yangu lakini nilikuwa nakupa
tu wazo kwamba endapo unaweza ukazidiwa
na ukahitaji mtu wa kukupa raha basi
unaweza mara moja moja ukamtumia huyo
kijana tena ukiwa hapo hapo kwako bila hata
ya kwenda mbali .Kuhusu muonekano wake
isikupe shaka.Muonekano ni kitu ambacho
kinaweza kubadilishwa wakati wowote.Huyo
huyo unayemuona leo kama msukule akipata
fedha na kujibadilisha ataitwa mheshimiwa.”
Akasema Safia na Vicky akatabasamu na
kusema
“ Ok Safia tuachane na hayo ya nyumbani
kwangu, vipi kuhusu mafundi waliendelea na
kuweka milango ? akauliza Vicky
“ Ndiyo na hata hivi sasa wako jengoni
wanaendelea na kazi.”
“ Nashukuru sana shoga yangu kwa kunisaidia
kusimamia nyumba yangu.Nataka iende
haraka kwa sababu nina mipango mikubwa
sana ndani ya muda mfupi ujao.” Akasema
Vicky huku akilifungua pochi lake
“Mipango gani Vicky? Mbona hunishirikishi
mimi shoga yako? Akauliza Safia
“ Usihofu safia.Wewe ni mtu wa kwanza
ambaye nitakufahamisha lakini si sasa hivi
hadi hapo kila kitu kitakapokuwa tayari.Kimya
kingi kina mshindo mkuu.Nimekuwa kimya
kwa muda mrefu sasa subiria kusikia mshindo
wake.” Akasema Vicky huku akitabasamu na
kutoa kitita cha dola za marekani na kuanza
kuhesabu kiasi Fulani halafu akampatia Safia
“ kamata hizo shoga zitakusaidia kwa mambo
madogo madogo” akasema Vicky
“Dah ! shoga ama kweli wewe si mwenzetu
tena. Siku hizi hutumii tena haya madafu
yetu.Ni mwendo wa madola tu” akasema Safia
huku akitabasamu
“Toka nimezaliwa nilikuwa natumia
shilingi.Kwa hivi sasa nataka nibadili maisha
yangu na kuanza kutumia dola tu.” Akasema
Vicky huku akiinuka sofani
“ Safia,mimi si mkaaji nimepita tu kukujulia
hali na kukufahamisha kwamba
nimesharudi.Nataka nielekee mjengoni
nikaangale mafundi wanavyoendelea kisha
nirejee nyumbani kwani lile zee lisiponiona
linaweweseka kama linakata roho.Nitawasili
ana nawe baadae shoga yangu” akasema
Vicky huku akipiga hatua kuelekea katika gari
lake akaondoka
“Safia amenipa wazo japo la kijinga lakini
linaweza likawa na msaada kwangu.Natakiwa
kumsoma Yule kijana na kumuweka upande
wangu.Endapo nikimtia mkononi anaweza
akanisaidia sana katika mipango yangu
mbalimbali.Nina hakika atakapoonja fedha
hatakuwa na kauli kwangu na nitampeleka
nitakavyo.Hili ni wazo zuri sana.Lakini hili la
kumtumia kingono Yule kijana mhhhh !
inataka moyo sana.Lakini safia yuko sahihi
Yule kijana anaweza akanisaidia kuikata kiu
yangu pale ninapokuwa na hamu.Nina kila
kitu kwa sasa,maisha mazuri,nina fedha za
kutosha na nilichokosa ni kuridhishwa tu
kimwili na Yule mzee kwa sasa kutokana na
hali yake hawezi akanikuna nitakavyo.Mimi ni
mwanamke wa shoka nahitaji dozi ya maana
ili niridhike kitu ambacho Yule mzee hakiwezi
sasa hivi.Danny ananifikisha nitakapo lakini
naye yuko mbali ,laiti kama angekuwa karibu
ningekuwa nakwenda kwake kila siku kupata
huduma .Natakiwa kutafuta namna ambayo
nitakuwa nikijiridhisha.Ninaweza kumtumia
yule kijana lakini mhh ! “ akawaza Vicky
wakati akielekea mji mdogo wa Usa river
anakojenga jumba lake la ghorofa mbili
“ Kijana mwenyewe mchafu mchafu namna ile
ana thamani kweli ya kuweza kuuona utupu
wangu? Lakini kama alivyosema Safia
ninaweza nikambadili muonekano na akawa ni
kijana nadhifu kabisa.Ngoja nianze kulifanyia
kazi jambo hili.Sitaki mipango yangu
ivurugike.Nitafanya kila niwezalo ili kila kitu
nilichokipanga kiende kinavyotakiwa “
akawaza Vicky
MAMBO YANAZIDI KUKOLEA..DAVID NI NANI
NA KWA NINI HATAKI KUWEKA WAZI KUHUSu
MAISHA YAKE? VICKY ANA MIPANGO GANI?
ATAFANIKIWA LENGO LAKE LA KUMTUMIA
DAVID? TUENDELEE KUWA PAMOJA
 
Msipo like na Ku Comment nitaacha kutupia humu!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom