Riwaya: Hekaheka

mtzmweusi

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
8,698
Reaction score
9,051
HEKAHEKA - 1
Mtunzi: Japhet Nyang’oro
Phone: 0762204166

“Jacob, napenda kuolewa ila haiwezekani” Alisema ilhali mikono yake ikiwa bado inaminya minya misuli ya mwanaume huyu huku pia machozi yakiwa yanamtiririka.

“Kwa nini ishindikane Regina? Wewe ni msichana ambaye unaweza kumvutia kila mwanaume mwenye mpango wa kupata mwenza wa maisha?” Jacob aliuliza huku akihisi ubaridi uliokuwa ukipenya taratibu katika kifua chake kutokana na machozi yaliyokuwa yakitoka kwa wingi machoni kwa Regina.

“Hapana haiwezekani Jacob…” Regina alisisistiza kwa sauti ya chini, iliyokuwa na chembe chembe za huba na wasiwasi kwa wakati mmoja.

“Usiseme hivyo Regina!”
“Hata nisiposema, huo ndio ukweli na hali halisi Jacob”
“Naomba sababu ya huko kutowezekana…” Jacob alizidi kuhoji kwa shahuku.
“Hata nikikuambia huwezi badili hali na ukweli wa mambo”
“Umejuaje kama sitoweza?”
“Uko peke yako, wako jeshi, huwezi washinda wote....ni waovu sana!”

“Nakupenda Regina, niko tayari kufanya lolote ili kurejesha uhuru wako na Amani” maneno hayo ya Jacob ilikuwa kama sauti ya muziki mororo inayopenya kwenye kiza kinene na kuyafikia masikio ya mtu aliyesimama chini ya mti mukubwa baada ya kunyeshewa na na mvua nzito.

“Sijawahi kuwa huru na sijui amani ikoje Jacob” alisema Regina huku akimkazia macho Jacob, kamasi nyembamba na machozi vikiendelea kuchuruzika.

Wakati mahojiano hayo yakiendelea, sauti yake Bella wa Akudo Impact ilikuwa ikivuma ukumbini hapo huku yale mashairi ya wimbo wake ‘yako wapi mapenzi? ilimfanya kila aliyekuwepo kujishughulisha zaidi na mwandani aliyekuwa nae. Kwa kifupi hali ilikuwa ni ya kuvutia na utulivu katika ukumbi wa Miami Hoteli ambayo ni moja kati ya hoteli za kuvutia zilizoko kando kidogo ya jiji la Dar es salaam baada ya kupita mbezi beach.

Ni kawaida kwa Jacob Matata kutoka nyakati za jioni na kwenda katika mojawapo ya maeneo ya burudani katika jiji la Dar es salaam. Ukimuuliza mwenyewe kwa nini alipenda kwenda maeneo hayo, sababu nyingi angekupa. Lakini katika orodha yake asingesita kutaja, upweke, burudani na kusafisha macho. Lakini ana jingine ambalo kamwe usingelisikia akilitaja...........kazi....kazi yake ya upelelezi ilimtaka kuwa jirani na jamii, jamii iliyoko kwenye madaraja yote, daraja la juu, daraja la kati na daraja la chini.

Siku hiyo Jacob Matata alijikuta anavutiwa kwenda Miami hoteli. Alisikia Akudo Impact wanapiga huko, na kwa vile yeye ni mpenzi wa muziki wao akaona ni bora akaishibishe nafsi yake kitu inataka. Binafsi anamiliki magari mawili, lakini hakuwa anapenda kwenda sehemu za starehe akiwa anaendesha, hivyo alimtaarifu Abdul mmoja wa vijana wake ambao hupenda kuwakodisha akiwa kwenye mizunguko yake na wakati akiwa hataki kuendesha. Abdul alimpitia Jacob nyumbani kwake maeneo ya Sinza Mori mida ya saa tatu unusu usiku.

“vipi bosi, naona leo umekaa kiburudani Zaidi?” Abdul alimuambia Jacob ambaye alikuwa amevaa fulana ya blue na suluali ya jeans nyeusi.
“Si unajua wazee wa masauti Akudo wako Miami Hotel, sasa nataka nikakate kiu huko” Jacob alisema.
“Ahhh wale jamaa hata mie nawakubali sana” Abdul alijibu.

Saa nne na robo ilimkuta Jacob ameshatulia kitini katika ukumbi wa hoteli ya Miami. Akudo walikuwa wameshaanza kushambulia jukwaa taratibu. Alitafuta sehemu na kukaa, kabla ya kuagiza aletewe vinywaji. Vinywaji vililetwa na taratibu akaanza kujipigilia huku akiyapa fursa macho yake yaweze kutalii katika ukumbi mpana wa hoteli hiyo...kusafisha macho. Jacob aliamua aweke mbili-tatu ili wakati mambo yakichanganya nae awe kamili.

Tangu alipoingia hotelini hapo, Jacob Matata alionekana kuwa mtulivu, japo utulivu ni hali ya kujifunza tu kwake, asili yake ni mtu mchangamfu sana na mtundu unaweza sema. Hata ukienda mitaa aliyokulia pale Mwanza mjini maeneo ya Kirumba mwaloni, ambapo nyumba ambayo wazazi wake walikuwa wamepanga ilikuwa jirani na msikiti wa Taqwa, siku hizi kuna shule ya sekondari ya kiislamu pale, ukiuliza utaambiwa wakati Jacob anakuwa miaka ile ya 1991, wazazi walikuwa wakiwazuia watoto wao wasicheze pamoja nae. Alikuwa mtundu balaa.

Kadri masaa yalivyokuwa yakizidi kukatika, ndivyo ukumbi huo ulivyokuwa ukipungua watu. Pamoja na kuwa kulikuwa na watu wengi wa umri na maumbile tofauti, lakini macho ya Jacob Matata yaligota kwa msichana mmoja aliyekuwa ametulia tuli juu ya kiti upande wa kulia wa ukumbi huo. Alipozidi kumtazama, Jacob aliweza kubaini uzuri wa msichana huyo. Hivyo mara kwa mara macho yake yakawa yanapendelea kuangalia upande alipokuwa amekaa kiumbe huyo wa kike. Dakika kumi baadae Jacob alitupia macho kwa yule msichana mrembo na kubaini kuwa hakuwepo sehemu ile aliyokuwa amekaa.

Wakati anageuza macho katika jitihada za kujaribu kuangaza ili aweze kuona kama bado msichana huyo alikuwepo ukumbini hapo, ndipo macho yake yalipogongana moja kwa moja na yale ya msichana mrembo akiwa amekaa hatua chache tu kwa nyuma yake. Macho yao yalipogongana, yule msichana aliachia tabasamu la kukaribisha. Kuona hivyo, Jacob aliachia lake la mwitikio kisha akasita kidogo. Aliangalia saa yake ya mkononi na kubaini kuwa tayari ilikuwa inaelekea kuwa saa tano na robo usiku. Jacob alisimama, kabla ya kupiga hatua yoyote alizungusha macho yake huku na huko ili kuona kama kulikuwa na lolote, alipooona hakuna aligeuka na kuanza kuelekea alipokuwa amekaa yule mrembo.

Haikuwachukua muda mrefu wakajikuta wameshatambulishana. Muda si muda wakakubaliana kumalizia muda uliobaki kwa kucheza muziki pamoja. Na wakati huo huo ule wimbo maarufu wa ‘yako wapi mapenzi? ulikuwa ukiimbwa kwa ustadi mkubwa nae Bella. Haikuwa siri kuwa kila mmoja katika watu hawa alikuwa amevutiwa na mwenzie.

Sijui kama ndio ilikuwa kosa au la, pale Jacob alipomuuliza msichana huyu kama alikuwa na mtu yeyote. Jibu alilolipata lilikuwa ni lile ambalo Jacob alikuwa anaombea apewe. Kule kusikia kuwa Regina hakuwa na mtu kulimfurahisha sana Jacob. Hapo ndipo akauliza swali la kichokozi na ambalo hata hivyo ndilo liloleta kizaa zaa kinachoendelea.

Wakati huu walikuwa bado wamekumbatiana katika hali ya mapenzi huku Jacob akiwa anasisitiza kutaka kujua sababu ya mrembo huyu, aliyejitambulisha kama Regina kusema kuwa haiwezekani yeye kuolewa.

“Kweli haitawezekana, hata kitendo cha mimi kukumbatiana na wewe kiasi hiki ni ujasiri tu nilio nao, haikutakiwa mimi nikukumbatie kiasi hiki, nimeshindwa kujizuia Jacob nimeshindwa..........umenivutia, nimekupenda Jacob. Naomba niondoke maana najua kuwa muda wangu wa kukaa hapa umeisha na nahitajika mahali” Regina alisema huku akitaka kujitoa kifuani kwa Jacob, ambaye mpaka hapo alikuwa na hamu ya kujua ni kitu gani kimemsibu binti mrembo kama huyo.

“Hapana Regina kabla haujaondoka naomba unijulishe tatizo lako, kwani siamini kuwa swali langu ndilo lilosababisha wewe utokwe na machozi mengi kiasi hiki, niko tayari kukusaidia kwa namna yoyote ile kama nitakayoweza” Jacob alisema huku akizidi kumvuta Regina ili atulie zaidi katika kifua chake.

“Jacob, nakuonea huruma sana kwani hata hapa tu najua maisha yako yatakuwa mashakani” Alisema Regina huku akiinua Kichwa chake na kuangaza hapa na pale ukumbini hapo.

“Hatarini kivipi Regina? Mbona sikuelewi?”
“Kuna watu Jacob, watu wasiotaka niolewe kwa faida yao. Kama ni kuolewa basi inamaanisha kifo chang………” Kabla Regina hajamalizia, Jacob alishitukia anapigwa na kitu kizito kisogoni na papo hapo akajikuta anapoteza uwezo wa kupambanua mambo, hata mashairi ya wimbo wa ‘safari sio kifo’ wa Akudo Impact akawa anasikia yakipotelea hewani, akapoteza fahamu na hivyo kutojua ni nini kilikuwa kinaendelea.
 
HEKAHEKA - 2
Mtunzi: Japhet Nyang’oro
Phone: 0762204166

“Kuna watu Jacob, watu wasiotaka niolewe kwa faida yao. Kama ni kuolewa basi inamaanisha kifo chang………” Kabla Regina hajamalizia, Jacob alishitukia anapigwa na kitu kizito kisogoni na papo hapo akajikuta anapoteza uwezo wa kupambanua mambo, hata mashairi ya wimbo wa ‘safari sio kifo’ wa Akudo Impact akawa anasikia yakipotelea hewani, akapoteza fahamu na hivyo kutojua ni nini kilikuwa kinaendelea.

* * *
Aliporejewa na fahamu alijikuta amelazwa kwenye kitanda. Pembeni yake alikuwa amekaa msichana mrembo aliyevalia kiuguzi.
“Habari yako binti mrembo?” Jacob alisema kwa sauti dhaifu kidogo.
“Afadhali....aaaaaaaanha!!!!” Alisema msichana huyo huku akishusha pumzi ndefu na mikono yake yote miwili akiwa kaiweka juu. Tendo hili ilikuwa ni ishara tosha kuwa msichana huyu alikuwa anangojea kusikia sauti hii ya Jacob kwa hamu kubwa. Baada ya kutoa ukelele huo wa furaha msichana huyu alisimama na kukisogelea kitanda ambacho Jacob alikuwa amelalia.
Jacob alimuangalia msichana huyo bila kusema neno jingine zaidi ya ile salamu aliyokuwa ameitoa mwanzo. Hapo tena zilipita kama dakika mbili watu hawa wawili ndani ya chumba wakiwa bado wanaangaliana tu bila kusema neno. Jacob alikuwa na hamu ya kumjua msichana huyo ambaye alikuwa ameshindwa kabisa kuficha furaha aliyokuwa nayo kuona Jacob amerejewa na fahamu.
Baadae Jacob akapata wazo la kuangalia saa yake. “saa kumi!!” Jacob alinong’ona kwa sauti ambayo iliweza kuyafikia masikio ya yule msichana.
“Ndio, pole sana kaka yangu” Hatimaye binti huyo alisema huku akipitisha mkono wake kifuani kwa Jacob katika ile hali ya muuguzi kumjulia hali mgonjwa.
“Pole kwa lipi” Jacob aliuliza kana kwamba hakuwa anajua nini kilikuwa kikiendelea.
“Najua huwezi kujua, kwa kifupi ni kuwa jana wakati ulipokuwa ukicheza muziki na msichana fulani, Miami hoteli, alitokea kijana mmoja na kukupiga na kitu kichwani ukaanguka chini. Yule msichana uliyekuwa ukicheza nae alipojaribu kukutetea nae alipigwa kabla ya kubebwa na vijana wengine ambao bila shaka walikuwa na yule aliyekupiga. Watu hao wakatokomea wakiwa wamemchukua yule msichana, na wewe ukiwa umeachwa pale chini bila msaada. Baada ya tukio hilo, hali ndani ya ukumbi haikuwa shwari tena. Watu walianza kukimbia hovyo, hakuna hata mmoja aliyejitokeza kukupa msaada. Mie ni muuguzi, najua kuwa kama ungekaa mazingira yale bila msaada ungeweza kupoteza maisha, hivyo nikaamua kukuchukua. Tangu jana nilipokuleta hapa hujarudiwa na fahamu mpaka sasa hivi” Alimaliza msichana huyo ambaye hakuweza kuficha furaha yake.
“Asante sana kwa kukubali kuwa mkombozi wangu” Jacob alipomuangalia msichana huyo aliona kitu katika macho yake japo hakujua kwa haraka kilikuwa nini. Alijiinua pale kitandani, akaketi. Akatembeza macho katika chumba hicho alichokuwa amelazwa. Jambo moja alitambua ni kuwa chumba hiki kilionekana kuwa maalum kwa kazi kama hii aliyokuwa amefanyiwa.
“Je hapa ni hospitalini?” Hatimaye Jacob alimuuliza yule msichana ambaye alikuwa amekaa pembeni yake kana kwamba anayasoma mawazo yake.
“Hapana” alijibu.
“Kwa hivyo ni wapi hapa?”
“Hapa ni nyumbani kwangu”
“Unataka kuniambia kuwa ulijua kuwa utakutana na mkasa kama huu mpaka ukawa umejiandaa kiasi hiki katika chumba hiki?”
“Hapana ila huwa na…” alisita kabla ya kuendelea “…mimi ni nesi hivyo huwa natunza chumba hiki hapa kwangu kwa ajili ya kuwasaidia ndugu na jamaa pale inapobidi” Alisema msichana huyo katika sauti iliyokuwa na shaka.
“Asante sana” Jacob alisema huku akijaribu kujinyoosha. Alihisi kichwa chake kizito. Hii ilitokana na pigo alilokuwa amelipata.
“Naomba twende nikuoneshe bafu ili uoge kisha upate chochote, maana ni masaa mengi yamepita hivyo nina hakika una njaa” Alisema msichana huyo huku akiwa anaanza kupiga hatua kuelekea mlango wa kutokea katika chumba hicho. Jacob akaanza kumfuata bila wasiwasi wowote.
Walipita vyumba kadhaa kabla ya kutokezea sehemu iliyooneka kuwa ni maalum kwa shughuli za usafi.
“Huo mlango ndio bafu, kuna kila kitu kwa shughuli ya uogaji, naomba ujisikie huru kaka” Alisema huku akiwa amesimamana kumuangalia Jacob akitokomea bafuni.

Baada ya kuoga na kupata huduma nyingine zilizotakiwa baada ya kuoga, tayari kulikuwa kumeshaanza kupambazuka vizuri. Baadaye Jacob alikaribishwa sehemu aliyoambiwa kuwa ilikuwa maalum kwa chakula. “Kama nilivyotangulia kusema jisikie huru na usiwe na wasiwasi” Alisema msichana huyu ambaye mpaka hapo hakuwa anajua Jacob Matata alikuwa ni mtu wa namna gani.
“Nafikiri tutumie fursa hii kwa ajili ya kujuana pia” Jacob alisema wakati wakiwa wameshaanza kupata kifungua kinywa.
“Naona umeniwahi kusema, kwani nami nilikuwa nikiwaza hivyo” alisema msichana huyo ambaye kwa kila namna alionekana kufurahia sana kuwepo kwa Jacob mahali hapo, kisha akaendelea “Mimi kwa jina naitwa Evelyn, wachache wanaonifahamu huniita Eve, ni nesi katika hospitali moja binafsi hapa jijini. Naipenda kazi yangu kwani inanitosheleza na kunifanya niishi hapa mjini. Nadhani mpaka hapo inatosha” Alisema msichana huyo huku akiwa kayatuliza macho yake kwenye mikono yake. Jacob alijikuta yuko katikati kati ya kumuamini na kumuelewa au kumtilia shaka na kutaka kumfahamu zaidi msichana huyu. Hata pale alipoulizwa na Eve juu ya jina lake Jacob alijikuta anapingana na nafsi yake juu ya nini amuambie.
“Aah naitwa Nico Mkenja, ni mfanyabiashara” Jacob alidanganya huku uso wake ukiachia tabasamu lililoonesha kuwa aliyokuwa akisema ni kweli tupu. Eve aliamini na kutikisa kichwa kwa kuashiria kuwa alikuwa amemuelewa mgeni wake huyu.
“Eve nashukuru sana kwa yote uliyonitendea, ni imani yangu kuwa hakuna mtu ajuaye kuwa umenileta hapa, au kuna mtu alikuona au anajua kuwa umenileta mahali hapa?” Jacob aliuliza huku kayakaza macho yake usoni kwa Eve. Kabla ya kujibu Eve alisita na kuonesha kuwa hakutegemea kupata swali kama hilo toka kwa Jacob.
“Hakuna mtu, lakini hata kama kungekuwa na mtu kwani kuna ubaya gani bwana Nico?” Hatimaye Eve alisema katika hali ya kusita kidogo.
“Si unajua tena, wengine mabibi zetu wana wivu sana, wakipelekewa taarifa kuwa bwana wako kachukuliwa na msichana tena msichana mwenyewe mrembo kama wewe basi sidhani kama kutakuwa na amani huko nyumbani” Jacob alisema kwa utani uliokuwa umejaa uongo.
Ukweli ni kuwa Jacob hakuwa na hakika na sababu hasa ya wale watu waliomvizia kumpiga usiku ule kama walikuwa wanamfahamu au la. Alishindwa kuelewa ni nini kiliwafanya wao wakasirike yeye kuongea na yule mrembo Regina. Pia hakujua kwa nini Regina alikuwa kama mtu aliyeko kifingoni ilhali Tanzania ni nchi huru kabisa. Maswali mengi yalifumuka na ambayo mengine yalimpa wasiwasi.
“Nashukuru kwa kuwa hakuna aliyekuona, hivyo nina hakika ndoa yangu ni salama, nafikiri wakati mwingine nikihitaji kuja kukutembelea hutakuwa na kizuizi chochote, maana sasa tu kama ndugu” Jacob alisema huku akiwa amekaa mkao wa kutaka kusimama. “Bila shaka ila mimi na wewe si kama ndugu bali ni marafiki sasa” Eve alijibu huku akicheka, bila shaka kauli ya Jacob ya uhusiano wa udugu hakuiahafiki. “Basi bibie nitakuwa kama rafiki kwako, sasa naomba uniruhusu niende nikaripoti kwa mama watoto juu ya wapi nilikuwa” Alisema akiwa anasimama. Macho ya Eve yalionesha dhahiri kutoridhia na kuondoka kwa Jacob. Bila shaka alitaka kuwa na maongezi nae zaidi, japo hakujua ni nini wangeongea na Jacob. Alivutiwa na jinsi Jacob alivyoonekana kuwa mcheshi na muelewa wa haraka. “Ningependa kujua nyumbani kwako ili wakati mwingine niwe namtembelea mama watoto wako, au unaogopa inaweza kuwa vita?” Eve alisema.
“Mke wangu ana wivu sana, lakini si kiasi cha kuogopa kutembelewa na watu wa jinsia yake, bila shaka atafurahi sana kutembelewa na wewe. Kama ndivyo ipo siku nitakuja kukuchukua ili ukapafahamu nyumbani kwangu, bila shaka itakuwa vizuri” Jacob alisema hayo huku akiwa tayari kwa kuondoka.

* * *

Wiki ilipita tangu pale Jacob alipopata mkasa ule pale hoteli ya Miami. Katika wiki yote hiyo hakuna siku ambayo hakwenda Miami Hoteli kwa lengo la kukutana na msichana Regina. Mara zote ambazo amekuwa akienda hakuna hata siku moja ambayo alifanikiwa kukutana na wala kumuona mrembo Regina. Jambo moja Jacob alilitambua ni kuwa Regina alikuwa na matatizo ambayo bila shaka yalihitaji kusaidiwa. Tatizo ni kuwa hakujua Regina alikuwa akiishi wapi na wala hawakuachiana njia yoyote ya mawasiliano.
Jumamosi hii nayo aliamua aende tena kujaribu bahati yake. Alifika Miami hoteli majira ya saa nne usiku, wakati ambao mambo yalikuwa yameanza kuchanganya sana ndani ya ukumbi wa hoteli. Kama nilivyosema awali, utulivu na umakini ni moja ya tabia ambazo Jacob alikuwa amejifunza. Kwa asili hakuwa amezaliwa hivyo, kwani alikuwa ni mtu mtundu na mdadisi wa kila linalopita mbele yake. Lakini kazi zake hizi za upelelezi zilimfundisha kuwa; utulivu na umakini ni moja ya silaha kali katika fani hii. Hili lilipelekea aanze kutafuta kwa bidii kuwa na tabia hizi. Alifanikiwa, kwa mtu yeyote aliyemfahamu Jacob alikiri kuwa alikuwa ni mtu mtulivu na makini. Hivyo alipoingia ukumbini hapo alitafuta sehemu iliyokuwa japo na utulivu ili aweze kuwaona waingiao na watokao na kusoma nyendo zao.
Alienda sehemu moja ambayo ilikuwa na watu walioonesha kuwa walikuwa wa makamo kidogo kulinganisha na wengi waliokuwa ukumbini hapo. Aliagiza kinywaji laini na kuanza kunywa taratibu huku akijaribu kuangaza macho kama angeweza kumuona mtu wake - Regina.
Ilipofika saa sita kasoro hivi mara macho yake yakagongana na mtu ambaye sura yake haikuwa ngeni kwake. Jacob alimuangalia msichana huyo mpaka pale alipoenda kukaa. Msichana huyo alionekana kuwa peke yake. Alipokuwa amekaa aliagiza kinywaji. Macho ya Jacob hayakumuachia msichana huyo. Wakati fulani msichana huyo aligeuka na kuangalia upande ule aliokuwa amekaa Jacob. Alipomuona Jacob tu, msichana huyo alitabasamu. Ni tabasamu hilo ndilo lilomkumbusha Jacob kuwa msichana huyo alikuwa Eve aliyemuokoa ukumbini hapo siku chache zilizokuwa zimepita. Jacob alikumbuka kuliona tabasamu hilo nyumbani kwa Eve muda mfupi tu mara baada ya yeye kurejewa na fahamu, Eve aliachia tabasamu la furaha kama hilo. Jacob alitabasamu pia kuitikia.

Eve alinyanyuka na kwenda pale alipokuwa amekaa Jacob. “Vipi umekuja na bibi yako” Alisema Eve katika sauti ya kunong’ona mara tu alipofika pale aliokuwa amekaa Jacob. Jacob hakujibu kitu bali alitabasamu tu. Hii ilidhihirisha kuwa Eve alikuwa ameamini asilimia mia kuwa Jacob alikuwa na mke kitu ambacho si kweli. Mpelelezi Jacob Matata hakuwa na mke, bali aliamua kumdanganya tu msichana huyo. “Karibu uketi na usiwe na wasiwasi” Hatimaye Jacob alisema na kumpa nafasi binti huyu aketi.
Jacob mara tu alipomuona Eve ndipo wazo la kumuhoji juu ya watu waliomchukua Regina siku ile ya tukio lilimjia. “Habari za tangu siku ile tulipoachana” Jacob alisaili.
“Nzuri tu hofu kwako mgonjwa wangu, nimekuwa muuguzi mbaya asiyetaka kujua hali ya mgonjwa wake kwa kuacha kuja kukutakia hali” Alisema Eve huku macho yake akiyapepesa kiwizi wizi.
“Nadhani mimi ndio nimekuwa mkosefu zaidi kwa kuacha kuja kukujulia hali wewe mkombozi wangu” Jacob alisema huku akijaribu kuusoma uso wa msichana huyu.
Baada ya salamu na utani wa hapa na pale Jacob na Eve wakajitoma katika kusakata muziki uliokuwa umepamba moto ukimbini hapo. Kila mmoja alijaribu kumuonesha mwenzie kuwa alikuwa zaidi katika fani hiyo. Jacob kwa upande wake alikuwa na la zaidi, akili yake kwa upande mwingine ilikuwa ikimuwaza msichana Regina na mkasa mzima uliokuwa umetokea. Mara kwa mara kwa chati alikuwa akiyazungusha macho yake karibuni ukumbi wote kuona kama angeweza kukutana na sura ya msichana yule aliyetokea kumvutia na wakati huo huo kugundua kuwa ni moja kati ya watu waliokuwa na matatizo. Matatizo yanayohitaji msaada wa mtu kama yeye. Kwa vyovyote vile, watu waliomchukua Regina si wema hata kama wanamfahamu. Ilikuwa wazi kichwani kwa Jacob kuwa ni watu waliokuwa wanamfahamu na kuwa na uhusioano na Regina japo uhusiano wao yaonesha haukuwa wa heri.
Hali ilipozidi kuwa mbaya kichwani, Jacob alimshika mkono Eve na kumvutia pembeni. ‘Samahani Eve kuna swali naomba nikuulize, je waweza kuwa unawafahamu au kuwakumbuka watu walionifanyia uhuni ule siku ile hapa ukumbini?” Jacob alisema kwa sauti ya chini lakini kavu na ya baridi kiasi cha kuzigutua hisia za Eve. “Hapana, ila kama yule aliyekupiga kichwani akiletwa hapa naweza kumkumbuka” Eve alisema huku mikono yake akiipeleka kifuani kwa Jacob. Bila shaka alishahisi kuwa jambo lile bado lilikuwa linamsumbua Jacob. “Lakini maadam u mzima, sioni sababu ya wewe kutaka kuwafuatilia maharamia kama wale, cha msingi ilikuwa ni usalama wako. Kwani unafikiri ni kwa nini walikufanyia hivyo?” Hatimaye Eve aliuliza swali ambalo kwa muda alikuwa akishindwa namna ya kuanza kumuuliza Jacob. “Sijui hasa ni kwa nini, lakini nadhani ni kwa sababu ya yule msichana niliyekuwa nacheza nae” Jacob alisema huku akiziangalia mboni za macho ya Eve. “Ina maana yule msichana alikuwa bibi yao au ni wivu tu” Eve alitaka kujua zaidi.
“Hapo ndipo sina uhakika. Mimi nilikutana nae humu humu ukumbini, nikamuomba tuwe nae, na tucheze pamoja akakubali, japo alionesha kuwa na wasiwasi kidogo” Jacob alijibu.
“Kwa hiyo yawezekana wasiwasi wake ulitokana na kwamba alijua kuwa kucheza na kuwa na wewe ni makosa, kwa vile alikuwa na mtu ukumbini hapa?”
“Hilo sina hakika nalo sana, ila kama ingetokea nikaonana nae angeweza kunieleza vizuri, lakini tangu siku ile wamemchukua ukumbini hapa, sijamuona tena, sijui nini kitakuwa kimemtokea au hajapata nafasi tu ya kuja tena” Jacob alisema huku akiachilia pumzi za kuonesha kuwa jambo hilo lilikuwa likimtatiza.
Mara wote walishituliwa na tangazo la kuwaarifu kuwa muda wa kufunga ukumbi huo ulikuwa umewadia. Ilikuwa inaelekea kuwa saa saba za usiku. “Jacob mie nimekuja na gari yangu, hivyo kwa urahisi wa usafiri unaonaje kama tukaenda kulala nyumabni kwangu? Sasa hivi teksi ni nadra sana na aghali mno, kwa usalama ni vema twende tu ukalale kwangu” Eve alisema huku akijifanya kutengeneza ukosi wa shati la Jacob.
“Hapana Eve, kesho kuna sehemu ninatakiwa kuwahi sana kwa ajili ya biashara zangu, lakini mie pia nimekuja na gari langu” Jacob alikataa huku wakiwa wameanza kutoka ndani ya ukumbi huo. Kila mmoja alielekea alikojua.

* * *

Siku iliyofuata ilionekana kuwa ya ajabu ajabu tu kwa Jacob Matata. Sababu kuu kwa hili zingeweza kuwa nyingi, lakini iliyoonekana kuwa kubwa ni ile ya Kufikiria suala la msichana aliyetokea kumpenda ghafla na ambaye ametoweka ghafla. Amempenda na katoweka ghafla. Alionana na Regina kwa muda mfupi na kutokea kumpenda mara, lakini watu asiowajua walitokea kumshambulia kwa sababu walizozijua wao, kumchukua msichana huyo aliyeoneka kuwa katika hali ya wasiwasi na ufungwa wa aina yake. Ingekuwa afadhali kwake Jacob kama watu hao hata wangemuachia Regina majeruhi kuliko kumchukua katika mzingira tata kama yale. Ilikuwa kama umeme kukatika wakati umeweka muvi uliyoitafuta kwa muda mrefu. Akili ya Jacob ilitaka kujua undani wa Regina, lakini hakukuwa na mtu wa kumpa ukweli huo zaidi ya Regina mwenyewe, ambaye sasa hajui atampata vipi.

Mara nyingine Jacob alitaka kujilaumu kwa kuchelewa kumuuliza Regina alikuwa akiishi wapi. Lakini wazo jingine likampinga kwa kuzingatia kuwa muda ulikuwa mfupi mno na ilikuwa mapema mno kwa hilo. Mara hisia za kupambana zilimjia, zikamjaa, kawa tayari, lakini hakuona wa kupambana nae. Alitafuta pa kuanzia kumtafuta Regina, hakupaona.
Mchana ilimkuta katikati ya jiji la Dar es salaam, hivyo chakula cha mchana akapata Steers. Ni wakati akiwa Steers anapata mlo wa mchana simu yake ya kiganjani iliunguruma, aliingalia kwa kukinaika, lakini alipoona jina la mpigaji kuwa ni Eve, aliinyakuwa mara moja. Eve alimtaka Jacob nyumbani kwake haraka iwezekanavyo.
Jacob alijaribu kutafakari juu ya wito huo, alimuona Eve kama msichana aliyetokea kumpenda tu, kwa hivyo huenda alikuwa anataka aende ili akaongee nae tu. Kwa Jacob kupendwa na wasichana halikuwa jambo geni, kwani hata wakati akiwa shuleni walikuwa wakimgombani, yeye alibaki akiwaangalia tu, maana hakujua walichokuwa wakikiona kwake na kukigombania. Hakuwa msafi, hakuwa na hela, wala hakuwa mzuri kama baadhi ya vijana wengine. Ni kweli alikuwa na akili darasani pamoja na utundu wake, lakini hakudhani kuwa hilo lingeweza kuwa sababu kubwa ya yeye kugombewa na wasichana. Alipofika chuoni, pale chuo cha uhasibu Arusha hali ilkuwa hivyo hivyo, hadi baadi ya wanachuo wenzie wakadhani anatumia mizizi ya kwao Kigoma, Umanyemani. Hakusita kuwapa walichotaka. Lakini kwa Eve alijikuta akisita kuwa karibu nae. Sababu hakuijua, ila wakati wa moja ya mafunzo yake huko nchini China kuna mwalimu wake wa kichina alimuambia kuwa mara nyingine ni muhimu sana kama mpiganaji kuheshimu hisia zako.
Baada ya kujihoji na kujiuliza sana, hatimaye alijikuta akitia gari moto na kulitambaza taratiibu, ikulu, ocean road, daraja la salender huyo akaingia masaki, mtaa wa chake chake jirani na ofisi za Kilimanjaro International akasimamisha gari jirani na ilipokuwa nyumba ya Eve, ilikuwa ni saa nane na ushee mchana. Wakati kama huu jua la Dar es salaam lilikuwa likiwaadhibu wale wenzangu na mie wasiokuwa na namna ya kulidhibiti. Baada ya kuegesha gari eneo hilo alitembea taratiibu kuelekea geti la nyumba ya Eve. Ukubwa na uzuri wa nyumba ya msichana huyu ukilinganisha na kazi yake ya unesi ni moja ya vitu vilivyoacha maswali yasiyo na majibu kichwani mwa Jacob.
Alipofika getini, Jacob hakuchelewa kutambua kuwa kulikuwa na gari lililokuwa limeingia au kutoka mahali hapo muda mfupi uliopita. Alama za mataili na harufu ya mafuta ya gari bado vilikuwepo. Wakati anaiendea kengele ya getini hapo ili kuwajulisha wenyeji juu ya kuwepo kwake, alichungulia ndani na kuiona gari ya Eve ikiwa imeegeshwa. Hii ilionesha kuwa si gari ya Eve iliyokuwa imetoka.

Muda mfupi tu mara baada ya kubonyeza kengele ya kutaka kufunguliwa geti, mlinzi alikuja na baada ya mahojiano alifunguliwa na kuelekezwa sehemu ambayo aliambiwa kuwa Eve alikuwa akimsubiri. Jacob kwa chati aliangaza macho yake hapa na pale hapo nje kabla ya kuingia sehemu aliyokuwa ameelekezwa.
“Ooh asante kwa kuitikia wito wangu, karibu sana” Eve alisema kwa furaha huku akimkimbilia Jacob na kumkumbatia. Jacob hakuwa na namna ya kukataa bali kukubaliana na hali halisi. “Asante sana” alisema akiwa ameshikwa mkono na Eve kupelekwa sehemu ya maongezi.
“Utanisamehe kwa vile hatutakuwa na muda wa kuongea sana, huu ni wakati ambao natakiwa nielekee kazini, lakini jambo lililonifanya nikuite haraka ni juu ya swali moja ulilokuwa umeniuliza jana, kama nilikuwa namfahamu mtu aliyekupiga na kuondoka na yule msichana Regina pale ukumbi wa hoteli ya Miami. Ni kwamba leo alikuja mzee mmoja ambaye tuko ofisi moja, alikuwa amekuja kwa masuala ya kikazi, lakini alikuwa anaendeshwa na dareva mmoja ambaye mara alipoingia tu hapa niliweza kumtambua kuwa ndiye yule kijana aliyekushambulia siku ile na kumchukua Regina kwa kushirikiana na wenzie. Nilimuuliza yule mzee juu ya kijana huyo, akaniambia kuwa ni dereva wa shirika linalomiliki hospitali tunayofanyia kazi. Kweli nilishituka sana nilipomtambua” Macho ya Jacob yalipokuwa yakigongana na yale ya Eve, Jacob alibaini kuwa msichana huyu hakuwa na hata chembe ya hila katika maelezo yake. “Je ulimuambia kuwa umemfananisha na lile tukio?” Jacob alihoji.
“Hapana sikutaka kumshitua haraka kiasi hicho” Eve alijibu.
“Je waweza kuniandalia mazingira ya kuniwezesha kuonana na huyo dereva?”
“Hilo lisikupe shaka, leo hii nikienda kazini nitafanya kila mbinu ili uweze kumjua huyo dereva”
“Ila naomba usijaribu kutaka kumuhoji kwa njia yoyote wala kumchunguza, sana sana ningependa kujua anaishi wapi na namba ya gari analoendesha” Jacob alisema.
“sawa na……..” Kabla Eve hajamaliza alichotaka kusema mlio wa simu ulimzuia. Aliichukua simu yake ya mkononi na kupokea.
“sawa, sasa hivi nakuja” Lilikuwa ni jibu la Eve mara baada ya kusikiliza kilichosemwa na upande wa pili wa simu hiyo. Aliposema hivyo alisimama haraka na kukimbilia chumbani. Alipotoka alikuwa tayari ameshavaa. “Samahani Jacob, kuna sehemu nahitajika haraka sana, nadhani mambo mengine itakuwa kesho, nitakupigia ili uje nikupe nitakapokuwa nimefikia, kwa sasa sina la ziada, labda tu nikupe lifti ili kukusogeza hapo Coco beach hotel, pale waweza kupata usafiri kwa urahisi” Eve alisema huku akielekea chumbani kwake tena. Safari hii alipotoka tayari alikuwa ameshachukua mkoba wake na kuanza kuelekea ulipo mlango wa kutokea nje.
“Salama lakini uko uendako?” hatimaye Jacob aliona aulize mara baada ya kuona uharaka ule. “Salama tu” Eve alijibu huku tayari akiwa nje. Waliingia ndani ya gari, geti likafunguliwa ili kuwaruhusu kutoka. Jacob alijikuta anashindwa kumuambia Eve kuwa alikuwa amekuja na gari lake. Mambo yalifanyika kwa haraka na alitaka ayaone jinsi yaendavyo.
“Kwa hiyo kesho nitakutaarifu nimefikia wapi, ila jiandae tu maana wakati wowote nitakuita” Eve alisema wakati alipokuwa amesimamisha gari ili Jacob ashuke. Tangu watoke nae nyumani kwake, Eve alikuwa na haraka ya kuwahi wito wa bosi wake. Jacob aliposhuka tu, Eve aliondoa gari kwa kasi ili kuwahi alikokuwa ameamuliwa kwenda kukutana na bosi wake.
“Nilikuwa nataka umsindikize mpenzi wako, kisha turudi tukaongee vizuri nyumbani kwako. Geuza gari turudi nyumbani kwako” ghafla sauti ilisikika toka kiti cha nyuma, Eve akataka kugeuka ili aangalie msemaji ni nani lakini shingo yake ilipoguswa na kitu cha baridi alitulia tuli. Hakungoja kuambiwa kuwa kitu kilichomgusa ni bastola. Kwa chati aliyainua macho yake na kumuangalia huyo mtu kupitia kioo cha mbele cha gari aliona kuwa sura ya jamaa huyu haikuwa na heri hata kidogo. Alipoangalia vizuri aliweza kumuona yule dereva ambaye muda si mrefu ametoka kumuambia Jacob kuwa ndiye aliyempiga na kitu kizito kule Miami hoteli, kijana huyo alikuwa ameshikilia bastola mkononi huku tabasamu la dhihaka likiwa usoni.

Nataka nijue wangapi wanafuatilia kisa hiki.
Like au comment.
Asanteni
 
Tupo tunaopenda story kama hizi mkuu tupia madude ushanipa alosto hapa

Sent from my SM-G900I using JamiiForums mobile app
 
HEKAHEKA - 3

Mtunzi: Japhet Nyang’oro

Phone: 0762204166

“Kwa hiyo kesho nitakutaarifu nimefikia wapi, ila jiandae tu maana wakati wowote nitakuita” Eve alisema wakati alipokuwa amesimamisha gari ili Jacob ashuke. Tangu watoke nae nyumani kwake, Eve alikuwa na haraka ya kuwahi wito wa bosi wake. Jacob aliposhuka tu, Eve aliondoa gari kwa kasi ili kuwahi alikokuwa ameamuliwa kwenda kukutana na bosi wake.
“Nilikuwa nataka umsindikize mpenzi wako, kisha turudi tukaongee vizuri nyumbani kwako. Geuza gari turudi nyumbani kwako” ghafla sauti ilisikika toka kiti cha nyuma, Eve akataka kugeuka ili aangalie msemaji ni nani lakini shingo yake ilipoguswa na kitu cha baridi alitulia tuli. Hakungoja kuambiwa kuwa kitu kilichomgusa ni bastola. Kwa chati aliyainua macho yake na kumuangalia huyo mtu kupitia kioo cha mbele cha gari aliona kuwa sura ya jamaa huyu haikuwa na heri hata kidogo. Alipoangalia vizuri aliweza kumuona yule dereva ambaye muda si mrefu ametoka kumuambia Jacob kuwa ndiye aliyempiga na kitu kizito kule Miami hoteli, kijana huyo alikuwa ameshikilia bastola mkononi huku tabasamu la dhihaka likiwa usoni.
Hakuwa na hiari zaidi ya kufanya kama alivyokuwa ameelezwa. Mara moja picha ya msichana Regina ilimjia kichwani mwake, na kuanza kuwaza kuwa yaliyompata Regina yawezekana yakampata na yeye pia. Aliwaza na kuhisi kuwa yawezekana Jacob ana kitu na watu hawa. Alitamani kumpigia simu Jacob lakini alijua fika kuwa asingefanikiwa. Alipofika kwake alikuta gari mbili ndogo zikiwa zinapakia baadhi ya vitu vyake. Alipotaka kuhoji juu ya hilo, alizuiliwa na huyo kijana.
Wakati Eve anataka kuingia ndani, mara, simu yake ya mkononi iliita. “Hallow Nico, niko nyumbani wameni……” kabla hata hajamaliza alichotaka kusema alishitukia ananyang’anywa simu kwa nguvu. “Nani tena huyo jamani, niacheni basi angalau niongee na simu hivi nini hiki mnanifanyia?!!” Eve alilalamika.

* * *

Ni sauti hii ya kulalamika ambayo ilimshitua Mpelelezi Jacob Matata aliyekuwa amepiga simu hiyo ili kumtaarifu Eve kuwa alikuwa amesahau funguo zake pale walipokuwa wamekaa. Sauti hii iliashiria kuwa msichana huyo alikuwa kwenye matatizo. Jacob alibonyeza tena namba za Eve na kupiga, lakini safari hii simu yake ilikuwa tayari imeshazimwa.
Jacob alikuwa ameshafika mjini, hivyo hakuona busara kurudi nyumbani kwa Eve kwa kutumia gari yake. Hivyo alikodisha teksi. “Haraka hebu nipeleke Masaki” Jacob alisema huku akipapasa kiunoni kwake ili kuona kama bastola yake ilikuwepo, alipoiona alitulia tuli na kumuachia dereva kazi yake.
Alipofika nyumbani kwa Eve tayari alikuwa ameshachelewa. ‘Shiit !!!!! Kuna namna tu hapa lazima kuna mchezo unafanyika tu, wameanza na Regina na sasa Eve?” Jacob alijikuta akiropoka mwenyewe, na kumuacha dereva teksi aliyemleta mpaka hapa abaki anashangaa. “Kwani vipi kaka?” hatimaye yule dereva aliuliza.
“Huyu msichana mwenye nyumba hii inayoungua moto namfahamu” Jacob alijibu huku akiwa anatoka ndani ya gari. Nyumba ya Eve ilikuwa iketeketea kwa moto mkubwa na kuacha kundi la watu wakiwa wamejazana kushuhudia tukio hilo.
Baada ya kuuliza majirani hapo walimueleza kuwa inasemekana hakukuwa na mtu kabla ya moto kuzuka.
Hapo Jacob akajua kuwa Eve nae amechukuliwa kama alivyochukuliwa Regina. Hapo tena akataka kuanza kujilaumu kwa kuchelewa kumuuliza Eve alikuwa akifanya kazi wapi. Kila kitu ilikuwa kama harufu tu ibebwayo na upepo na kutoweka nao. Jacob aliachia pumzi ndefu na kujisemea ''kazi ipo!!!!” Akatabasamu.....tabasamu la kukarahika. Ilikuwa yapata saa kumi na nusu jioni wakati Jacob alipoondoka eneo la tukio.

Naona wafuatiliaji ninwachache sana, inanipa uvivu kupost
 
H E K A H E K A - 4

Mtunzi: Japhet Nyang’oro Sudi

Hapo Jacob akajua kuwa Eve nae amechukuliwa kama alivyochukuliwa Regina. Hapo tena akataka kuanza kujilaumu kwa kuchelewa kumuuliza Eve alikuwa akifanya kazi wapi. Kila kitu ilikuwa kama harufu tu ibebwayo na upepo na kutoweka nao. Jacob aliachia pumzi ndefu na kujisemea ''kazi ipo!!!!” Akatabasamu.....tabasamu la kukarahika. Ilikuwa yapata saa kumi na nusu jioni wakati Jacob alipoondoka eneo la tukio.

*********

Ilivyo ni kuwa; wakati Eve na Jacob wanaongea nyumbani kwa Eve, chumba jirani na kile walichokuwa wakitumia kwa maongezi yao kulikuwa na watu wawili wakiwa wametulia tu kama Pusi angojaye Panya atokee. Muda wote akili na Masikio yao vilikuwa vimeelekezwa kwenye maongezi ya Jacob na Eve.

Hawa jamaa walikuwapo muda wote tangu Jacob anaingia ndani mpaka muda ambao alikuwa anatoka. Si Eve wala Jacob Matata aliyekuwa anajua juu ya kuwepo kwa watu hao chumba jirani sana na kile walichokuwa wamekaa wakiongea.

Nyendo na maisha ya msichana Eve vilikuwa na umuhimu mkubwa kwa tajiri wa kizungu Harken Kalm. Harken Kalm ni jina ambalo lilijulikana kila kona ya Tanzania. Licha ya utajiri wake uliopindukia, Harken Kalm alijulikana sana kwa misaada yake kwa jamii, kuwa mzungumzaji katika semina mbalimbali za kuhamasisha masuala ya kimaendeleo. Kwa kifupi Harken Kalm aliheshimika sana ndani na nje ya nchi.



Ilivyo julikana hadharani Harken Kalm alikuwa amejikita katika utafiti wa sababu ya kasi ya ongezeko la watu wenye matatizo ya akili katika bara la Afrika. Pamoja na kuendesha utafiti huo, amekuwa na zahanati kadhaa ambazo hutoa huduma kwa raia kwa bei nafuu sana. Mara zote Eve hujitambulisha na hujulikana kama nesi wa kawida tu, lakini ukweli ni kuwa yeye ni daktari kamili tena aliyehitimu kwenye moja ya nchi zilizoendelea sana katika fani hii ya utabibu. Sehemu kubwa ya elimu yake imegharimiwa na bosi wake huyu mzee Harken Kalm.

Sababu kuu ya mzee Harken Kalm kutaka Eve awe na elimu ya juu ya utabibu ni juu ya biashara siri kuuza mabinti wazuri yaani ‘human trafficking’ na damu ya binadamu. Ukweli ni kuwa utajiri mkubwa alionao mzee huyu unatokana na biashara hii ambayo humuingizia pesa nyingi za kigeni. Kwa mwaka inakadiriwa kuwa, watoto kati ya 150 hadi 350 huuzwa sehemu mbali mbali za dunia kwa ajili ya kufanyishwa biashara ya ngono, masuala ya urembo na shughuli nyinginezo. Pia alikuwa na biashara ya kukusanya damu kwa njia haramu, lita nyingi za damu zikiuzwa nje na hata ndani kwa matajiri ambao ni waathirika wa UKIMWI, ambao kila mwaka hubadilisha damu zao na kuweka nyingine. Pia alikuwa ni msambazaji mkubwa wa damu kwenye vikosi vya majeshi ya nchi mbali mbali ambavyo majeruhi wake wengi huhitaji sana damu.

Eve aliandaliwa maalum ili kuwezesha zoezi la kuwatibu na kuangalia afya za wasichana ambao walikuwa wakitekwa maeneo mbali mbali ya nchi kwa ajili ya kuuzwa. Ilikuwa ni jukumu lake kuwatibu, kuhakikisha wanapata lishe bora na wakishakuwa na mvuto wa kutosha picha zao zilisambazwa kwenye masoko mbali mbali duniani. Uhitaji wa wasichana hao kwenye masoko hayo ya siri ulikuwa ukiongezeka kwa kasi. Kulikuwa na kundi jingine la watu ambao kazi yao ilikuwa ni kulishwa vema na kutolewa damu kwa ajili ya kuuzwa. Mambo yote yalifanyika nje kabisa ya jiji la Dar es salaam ambako Harken Kalm alikuwa amejenga kambi yake ya siri kwa ajili ya shughuli hizo.



Eve ambaye hudai kuwa ni nesi, ndiye kiongozi wa kundi la wataalam wa Harken Kalm, na ni peke yake aliyekuwa ameruhusiwa kuwa anaishi nje ya jumba ambamo kazi hizo chafu hufanyika. Kwa kuzingatia umuhimu wake ndio maana mzee Harken Kalm alimuwekea ulinzi mkali sana. Ulinzi huu hufanyika kwa siri kiasi kuwa hata Eve mwenyewe hakuwa anajua kuwa kila anapoenda na analolifanya huwa linajulikana na mzee Harken Kalm kupitia walinzi wake aliowaweka. Kwa kifupi ni kuwa hakuwa anaishi ndani ya kambi lakini ni kana kwamba aliishi ndani ya jumba hilo bila kujua.

Bob Sepeto na Said Kipipa ni viongozi wa kundi la walinzi wa Mzee Harken Kalm. Said Kipipa ndiye dereva ambaye Eve alikuwa amemsimulia Jacob. Ni kweli kuwa Said Kipipa ndiye aliyekuwa amemshambulia Jacob kule ukumbi wa Miami hoteli. Eve hakuwa anamfahamu Said Kipipa, lakini alikuwa anamfahamu Bob Sepeto. Alimfahamu Bob Sepeto kama mmoja wa viongozi waliokuwa karibu sana na Mzee Harken Kalm. Hakumfahamu kama mmoja wa wakuu wa waliokuwa wakiongoza kundi la walinzi wa mzee Harken Kalm. Hakufahamu kuwa Bob alikuwa anafahamu nyendo zake mpaka uhusiano wake mpya aliokuwa ameuanza na Jacob Matata.

Siku ile tu Eve alipomleta Jacob nyumbani, Bob Sepeto alipata taarifa. Taarifa kuwa Eve alikuwa na mgeni ambaye ni mgonjwa aliyekuwa ameletwa akiwa kazirai, zilitosha kabisa kuibua wasiwasi kichwani mwa Bob. Bob kama kiongozi wa kundi lake alikuwepo Miami hotel, aliona walichofanywa Jacob na Regina. Hakuwa anamjua Jacob na wala hakuwa na sababu. Lakini kitendo cha Eve kuwa na mtu huyo, kilimhusu Bob. Yeye kama mkuu wa usalama alitakiwa kujua kila kinachoendelea ndani ya himaya. Taarifa zilimfikia kupitia kwa mlinzi wa nyumbani kwa Eve. Mlinzi huyu pamoja na kulinda usalama wa nyumba hii na waliomo, lakini pia amewekwa makusudi ili kufuatilia nyendo za msichana Eve.

Jambo moja Bob hakuwa na uhakika nalo, nalo ni juu ya kiini cha urafiki wa Jacob na Eve. Alikuwepo siku Jacob anashambuliwa pale Miami hoteli, lakini hakuwa na wasiwasi kwa kuzingatia kuwa si Jacob wala Eve ambaye angeweza kumjua Said Kipipa. Bob hakuwa anajua Jacob Matata ni nani, hivyo mchana huu aliamua kuja na Said makusudi ili aone kama Eve angeweza kumkumbuka Said Kipipa. Alipoona Eve amemtambua, Bob alitilia wasiwasi juu ya kinachoendelea kati ya Jacob na Eve. Hivyo mara baada ya kutoka kwa Eve, Bob na Said Kipipa walienda kuegesha gari lao sehemu na kurudi kwa miguu hadi walipoingia ndani ya nyumba ya Eve bila yeye mwenyewe kujua. Kama walivyokuwa wametegemea walimsikia Eve wakati akimtaka Jacob afike hapo kwake haraka.

Maongezi kati ya Jacob na Eve yalihitimisha wasiwasi aliokuwa nao Bob Sepeto juu ya Eve. Hata ile simu iliyopigwa na kuonekana kumchanganya Eve ilikuwa imepigwa na Bob akiwa chumba jirani tu na walipokuwa wamekaa Jacob na Eve. Lengo lake ilikuwa ni kumnyima nafasi Jacob asimuhoji Eve zaidi. Kweli alifanikiwa kwani mara baada ya simu hiyo, Eve hakuwa tayari kwa maongezi ya ziada na Jacob.
 
Tupie mkuu tunasoma kimya kimya
 
HEKAHEKA - 5

Mtunzi: Japhet Nyang’oro

Jambo moja Bob hakuwa na uhakika nalo, nalo ni juu ya kiini cha urafiki wa Jacob na Eve. Alikuwepo siku Jacob anashambuliwa pale Miami hoteli, lakini hakuwa na wasiwasi kwa kuzingatia kuwa si Jacob wala Eve ambaye angeweza kumjua Said Kipipa. Bob hakuwa anajua Jacob Matata ni nani, hivyo mchana huu aliamua kuja na Said makusudi ili aone kama Eve angeweza kumkumbuka Said Kipipa. Alipoona Eve amemtambua, Bob alitilia wasiwasi juu ya kinachoendelea kati ya Jacob na Eve. Hivyo mara baada ya kutoka kwa Eve, Bob na Said Kipipa walienda kuegesha gari lao sehemu na kurudi kwa miguu hadi walipoingia ndani ya nyumba ya Eve bila yeye mwenyewe kujua. Kama walivyokuwa wametegemea walimsikia Eve wakati akimtaka Jacob afike hapo kwake haraka.

Maongezi kati ya Jacob na Eve yalihitimisha wasiwasi aliokuwa nao Bob Sepeto juu ya Eve. Hata ile simu iliyopigwa na kuonekana kumchanganya Eve ilikuwa imepigwa na Bob akiwa chumba jirani tu na walipokuwa wamekaa Jacob na Eve. Lengo lake ilikuwa ni kumnyima nafasi Jacob asimuhoji Eve zaidi. Kweli alifanikiwa kwani mara baada ya simu hiyo, Eve hakuwa tayari kwa maongezi ya ziada na Jacob.

* * *

Mara zote akiwa ndani ya jumba hili msichana Regina aliamini kuwa yeye alikuwa ni mtu mwenye mkosi. Alijiona kama alizaliwa ili kama si awe rafiki wa mikosi basi awe chakula cha mikosi. Hii inatokana na jinsi mlolongo wa maisha yake ulivyokuwa ukienda.

Pamoja na kupewa kila kitu ambacho msichana mzuri alistahili kuwa nacho, lakini Regina aliamini kuwa alikuwa amenyimwa kitu kikubwa kuliko vyote ambavyo mtu anastahili kuwa nacho. Alijiona alinyimwa furaha ya kufurahia maisha na uzuri aliokuwa nao.

Wakati mwingine aliuona uzuri alionao kuwa ndio uliokuwa ukimsaliti mara kwa mara na kujikuta akiangukia katika majanga kama hili alilonalo sasa katika jumba hili. Ndani ya jumba hili la mzee Harken Kalm, maisha ni ya kushangaza mbele ya macho ya Regina. Hakuna kazi wala lolote la maendeleo. Kila siku kulikuwa na wasichana wapya ambao walikuwa wakiletwa. Wasichana walioletwa walitawanywa katika makundi matatu kama bidhaa zinavyowekwa kwenye ghala.

Mgawanyiko huu ulifanywa mara baada ya upimaji kufanywa na jopo la wataalamu ambao walikuwa wakiongozwa na Eve. Baada ya upimaji huo wasichana waliganywa katika mafungu. Kulikuwa na kundi la wasichana ambao bado walikuwa bikira, hao walihifadhiwa katika nyumba yao. Kulikuwa na kundi la wasichana ambao waliandaliwa kwa ajili ya uzalishaji wa damu. Na kundi jingine la tatu ilikuwa wasichana ambao pia wangeuzwa ila hawakuwa bikira. Sababu kubwa ya kutenganisha bikira na ambao sio ni kwa vile katika soko bei ya wasichana bikira ilikuwa kubwa sana kulinganisha na ambao hawakuwa nayo.

Kwa hivyo kuna wasichana waliokuwa wakiingia na wasichana waliokuwa wakija kuchukuliwa na wanunuzi ambao mwisho wa siku wangewasafirisha nje ya nchi.

Pamoja na kupewa huduma bora za afya, malazi na chakula lakini hakuna aliyekuwa akijua hatima ya maisha yake na hivyo kufanya kuwa na hali ya huzuni sana katika himaya hivyo. Kwa msichana kama Regina ambaye alilelewa kimaadili katika utoto wake, mambo hayo alikuwa akiyafananisha na sehemu ambayo mama yake alikuwa akimuambia kuwa kuna sehemu inaitwa kuzimu.

“Mwanangu ukiwa mtenda mabaya utaenda kuzimu, sehemu hiyo imejaa mateso makubwa” Alisikika mama Regina akimuasa mwanae mara kwa mara. Maneno haya yalikuwa yakimuingia sana Regina ambaye alipokuwa anacheza na watoto wa rika lake, ilikuwa ni kawaida kumsikia akisema “Mie sipigani nisije kwenda kuzimu”. Maneno kama hayo yalikuwa ni dalili tu kuwa mama yake alikuwa ameanza kufanikiwa kumfanya mwanawe aishi maisha ya maadili.

Hali ilikuja dhihirika pale Regina alipokuwa akiongezeka kimo. Nidhamu na uchaji wake ulimvutia kila aliyemuona na kukaa na mtoto huyo. Lakini mtazamo wa Regina ulianza kubadilika mara baada ya vifo vya ghafla vya mama na baba yake, ambao walikufa kwa wakati mmoja kwa njia ya ajali. Kwa vile wazazi wake hao hawakuwa na ndugu wengine hapo kijijini, Regina alichukuliwa kulelewa na mama mmoja ambaye alionekana kuwa na uwezo kijijini hapo. Regina aliendelea kuwa katika maadili, lakini vifo vya wazazi wake vilikuwa vikimpa mawazo sana. Uzuri wa msichana huyu ulikuja kunogesha hali ya maadili aliyokuwa nayo.

Taratibu Regina akawa kama ua linalochanua katikati ya nyuki wengi, japo kuwa si wote watengeneza asali. Harakati za ndani na nje dhidi yake zikawa zinaongezeka kila kukicha. Mama mlezi akawa anajitahidi kumuelimisha Regina. Lakini mama huyu alikuwa tofauti na mama mzazi ambaye mafundisho yake na maelekezo yalikuwa na msingi katika Mungu. Mama mlezi alikuwa akipenda kutumia vitisho na mafumbo ambayo hata hivyo Regina kwa umri wake akawa havielewi.

Si vijana wa mtaani na shuleni tu ambao ndio walikuwa wamechanganywa na uzuri wa Regina, bali hata baba mlezi. Baba huyu mlezi alianza kuzidisha zawadi na sifa kwa Regina. Alijifanya kuwa karibu nae, kuwa rafiki, hasa baada ya kugundua kuwa Regina alikuwa akimuogopa sana mama yake mlezi. Baba huyo akatumia mwanya huo kujifanya rafiki. Kwa mbinu hizo pamoja na nyingine nyingi hatimaye baba huyo aliuharibu usichana wa Regina. Alipofika kidato cha pili mama mlezi aligundua kilichokuwa kikiendelea kati ya Regina na baba yake mlezi, hivyo akaamua kumfukuza nyumbani. Maisha ya Regina yakazidi kwenda gizani.

Alianza kuhisi huenda ndio yuko kuzimu ambako mama yake alikuwa akimwambia. Maisha yake yalihamia sokoni kariakoo ambako alianza kuwa anafanya kibarua cha kuwasaidia wakinamama wauza nyanya kupanga nyanya pembezoni mwa soko hilo. Mshahara wake ikawa ni chakula cha mchana na usiku. Hakuna aliyemjali kwa mavazi wala mahitaji mengine aliyokuwa nayo kama msichana. Lakini pamoja na yote haya uzuri wa Regina bado ulikuwa unaonekana.

Vijana wengi wabeba mizigo sokoni hapo walikuwa wakirusha ndoano zao, lakini msimamo wa Regina uliwafanya wabaki wanakula kwa macho tu.

Safari yake ya kuja kwenye jengo hili la mzee Harken Kalm, iliwadia miaka kadhaa baadaye. Siku yenyewe alikuwa katika shughuli zake sokoni hapo, pale baba mmoja nadhifu alipokuja sehemu aliyokuwa amepanga mafungu yake ya nyanya. Baada ya kununua nyanya baba huyo hakusita kumsifia Regina kuwa ni mzuri na kumuuliza jina lake. Sifa haikuwa jambo geni kwa Regina, na siku zote hakuwa anaona tashishwi kutaja jina lake pale alipoulizwa. Huo ukawa mwanzo wa baba huyo kuja kununua nyanya kwa Regina.

Taratibu baba huyo akaaanza kuwa anakuja na vijizawadi kama nguo, viatu na mafuta, kumpa Regina. Regina alivipokea kwa hadhali kubwa. Mwaka ulipita huyo baba akifanya hivyo, huku akimuita Regina kama mwanae. Regina alijikuta taratibu akianza kumuamini baba huyo.

Ikatokea wakati Regina aliugua, yule baba alipokuja na kuulizia akaambiwa kuwa Regina anaumwa na kuwa amelala chini ya meza moja sokoni hapo. Baba huyo aliomba aoneshwe alipokuwa Regina, alipofika alimuomba Regina akubali ili ampeleke hospitali. Kwa kuzingatia yote aliyokuwa amefanyiwa kwa mwaka mzima na baba huyo ambaye hakuonesha nia au kiu ya kumtamani kimapenzi kama wafanyavyo wengine, Regina akajikuta amekubali kwenda.

Kweli kituo cha kwanza baada ya kutoka sokoni hapo na Regina, baba huyo alimpeleka Hospitali. Baada ya kupimwa na kupewa dawa, alimuomba Regina waende nae kwake. Uamuzi huo ulikuwa mgumu sana kwa Regina hasa ukizingatia yale ambayo yameshawahi kumkuta huko nyuma. Baada ya mvutano wa muda mrefu hatimaye Regina alikubali kwenda na baba huyo, ambaye ni Bob Sepeto. Hivyo Regina akajikuta amefika kwenye himaya ya Harken Kalm.

Kila mfanyakazi aliyemuona Regina katika jumba hili alitaka awe wake. Jambo moja lilimuokoa Regina ni kuwa, mzee Harken Kalm alikuwa amewaondolea nguvu za kiume sehemu kubwa ya wafanyakazi wake. Hii ilijumuisha walinzi, wapishi na watu wa usafi. Hivyo Regina akawa salama, japo baadae Bob Sepeto alimchukua na kufanya mke wake wa pambo tu, kwani Bob nae alikuwa amehasiwa.

Huyu ndiye Regina ambaye amekuwa na bahati ya kutoka mara kwa mara ndani ya jumba hili kwa kivuli cha kuwa mke wa Bob Sepeto.

Katika maisha yake alikuwa hajawahi kuvutiwa na mwanaume yeyote yule mpaka pale alipokutana na sura ya mpelelezi Jacob Matata pale kwenye ukumbi wa hoteli ya Miami. Hakumbuki ni nini kilimvutia kwa haraka toka kwa Jacob, lakini anachokumbuka ni kuwa mara macho yao yalipokutana tu kulikuwa na mvutano uliomfanya kwa mara ya kwanza akubali kupeleka macho yake chini mbele ya macho ya mwanaume. Alipomuangalia Jacob mara ya pili na kukutana na tabasamu lake, hapo akahisi mwili wote ukimsisimka na kujikuta ameachia tabasamu ambalo hakumbuki kama amewahi kulitoa tangu amezaliwa.

Ni hapo ndipo alipojikuta anavuka miiko ya kutotembea, wala kucheza muziki na mtu yeyote tofauti na watu wa kundi la Bob Sepeto. Jacob alipokuja na kumuomba wawe pamoja na baadaye wacheze, Regina alijua ni kiasi gani ilikuwa hatari, lakini kuna nguvu fulani ambayo alishindwa kuizuia juu ya kijana huyo. Hapo ndipo alipojikuta amemsababishia kijana wa watu kipigo na yeye mwenyewe kutoruhusiwa tena kutoka ndani ya jumba hili.

Aliweza kuona huruma, upendo wa kweli na udadisi viliyokuwa ndani ya macho ya Jacob. Haya yalimfanya amuamini na kuona kana kwamba anaweza kuwa na funguo za matatizo yaliyokuwa yakimkabili.
 
Tatizo lenu mkishaona follower wamekuwa wengi mnaanza mapozi.
Yaani mkifikia katikati ya utamu mnachomoa betri na kuanza kuweka namba za malipo huku speed ya kushusha vitu ikipungua kama si kupotea kabisa so why wasomaji story wa JF wanapungua kila kukicha.
Bora watu wapige kambi kule JF intergence kuliko kuzinguana na Alosto humu
 
HEKAHEKA - 6


Katika maisha yake alikuwa hajawahi kuvutiwa na mwanaume yeyote yule mpaka pale alipokutana na sura ya mpelelezi Jacob Matata pale kwenye ukumbi wa hoteli ya Miami. Hakumbuki ni nini kilimvutia kwa haraka toka kwa Jacob, lakini anachokumbuka ni kuwa mara macho yao yalipokutana tu kulikuwa na mvutano uliomfanya kwa mara ya kwanza akubali kupeleka macho yake chini mbele ya macho ya mwanaume. Alipomuangalia Jacob mara ya pili na kukutana na tabasamu lake, hapo akahisi mwili wote ukimsisimka na kujikuta ameachia tabasamu ambalo hakumbuki kama amewahi kulitoa tangu amezaliwa.

Ni hapo ndipo alipojikuta anavuka miiko ya kutotembea, wala kucheza muziki na mtu yeyote tofauti na watu wa kundi la Bob Sepeto. Jacob alipokuja na kumuomba wawe pamoja na baadaye wacheze, Regina alijua ni kiasi gani ilikuwa hatari, lakini kuna nguvu fulani ambayo alishindwa kuizuia juu ya kijana huyo. Hapo ndipo alipojikuta amemsababishia kijana wa watu kipigo na yeye mwenyewe kutoruhusiwa tena kutoka ndani ya jumba hili.

Aliweza kuona huruma, upendo wa kweli na udadisi viliyokuwa ndani ya macho ya Jacob. Haya yalimfanya amuamini na kuona kana kwamba anaweza kuwa na funguo za matatizo yaliyokuwa yakimkabili.

* * *

Asubuhi hii Jacob Matata alikuwa kwenye harakati, alidhamiria kujibu mapigo. Saa tatu na dakika kumi ilimkuta yuko ofisi ya ramani na majengo ya jiji la Dar. Hapo alikutana na foleni ndefu ya kwenda kumuona mhusika, lakini kwa kutumia marafiki zake hapo aliingizwa mpaka ofisi husika.

“Ndio kijana wangu nikuzaidie nini?” Hatimaye huyu mzee aliuliza baada ya Jacob kujitambulisha.

‘’Mzee nataka kujua kiwanja namba 201381ª, Masaki kinamilikiwa na nani.” Jacob alisema.

“Marietha, hebu nenda kaniletee file namba 201381A - Masaki” Alisema mzee huyo huku akiendelea kuandika kwenye daftari lake lilioneka kuchoka.

Baada ya dakika tano, yule msichana alirejea bila faili.

“Mzee Nasoro, hilo faili halipo mahali pake”

“Unasemaje?” Alihoji mzee Nasoro huku akiinua uso wake kumtazama yule binti

“Faili halipo”

“Haiwezekani, wiki iliyopita nilikuwa napitia Masaki yote hakukuwa na faili lilikosekana” Alisema mzee huyo huku akinyanyuka kwenda chumba cha kuhifadhia mafaili.

Aliporejea uso ulikuwa umemshuka. Faili halikuwepo. Jacob akajua hapo asingeweza kujua mmiliki wa nyumba aliyokuwa anakaa Eve. Alikuwa ameshawahiwa.



Kituo cha pili Jacob kufika siku hiyo ilikuwa ni Miami hoteli.

“Nahitaji kuonana na meneja wa hoteli” Jacob alisema kwa sauti kavu.

“Una miadi nae?”

Hapana ila ukimuambia Jacob Matata, bila shaka ataniruhusu kuonana nae”

“Okay, subiri kidogo,..” alisema binti huyo huku akinyanyua simu. Baada ya kuongea na upande wa pili aliweka simu chini.

“Naona una bahati kweli umeruhusiwa kumuona, maana leo tangu asubuhi hajaonana na mtu” Alisema binti huyo huku akinyanyuka kumpeleka Jacob sehemu ilipokuwa ofisi ya Meneja. Jacob alimuangalia binti huyo wakati akitembea, akameza mate.

“Unaitwa nani binti?”

“Naitwa Rose..”

“Rose?”

“Rose Mzava…”

“Hongera Rose”

“Kwa nini bosi?”

“Aaaaah, usiniambie hujui!!!”

“Namshukuru Mungu maana wengine hawana hata kazi” Rose alisema

“Sikumaanisha hilo, mbona waruka?” Jacob alisema huku akipiga hatua za haraka kuwa jirani zaidi na Rose. Rose aligeuka akamuangalia Jacob usoni. Akatabasamu. Jacob akajua kazi kwisha. Wakati huo walikuwa wameshaufikia mlango ulioandaikwa General Mnager.

“Karibu ndani, hii ndio ofisi ya meneja wa hoteli” Rose alisema huku akitabasamu. Jacob alimuangalia, akaachia tabasamu pia.

“Nilidhani unanikaribisha vingine, kumbe ni kuingia kwa meneja.” Jacob alitania huku akifinya jicho. Kisha wote wakacheka.



“Karibu Bwana Jacob, karibu uketi” Alisema mtu huyo aliyeonekana kuwa wa makamo kidogo.

“Asante sana na samahani kwa kukuingilia bila miadi”

“wala usijali, kazi zetu hizi za kutoa huduma zinatufanya tuwe tayari kukutana na yeyote wakati wowote”

“Nashukuru kwa hilo bwanaa….”

“Ulomi, Godbless Ulomi ndio jina langu”

“Okay asante bwana Ulomi”

“Naitwa Jacob Matata nafanya kazi na serikali kama mpelelezi” Jacob alisema huku akitoa kitambulisho chake.

“Okay, karibu sana bwana Jacob” Ulomi alisema huku akijitahidi kuficha mshituko alioupata.

“Shida yangu ni kupewa nafasi ya kuona rekodi za video kamera yenu hasa inayochukua picha pale kwenye ukumbi wenu” Jacob alisema safari hii sauti yake ikiwa nzito na yenye msisitizo.

“Duuuuuuh, nasikitika bwana Jacob kijana wangu ambaye husimamia chumba chenye hizo taarifa hajafika ofisini leo” Alisema meneja wa hoteli. Na wakati huo huo kitu kama taa nyekundu kikawaka akilini mwa Jacob Matata.

“Kwa nini hajafika?”

“Hatujui kwa kweli, tumejaribu kumpigia simu, haipatikani, nimetuma mtu aende nyumbani kwake, hawakumkuta. Majirani zake wanasema hakuwa amerudi tangu alivyoondoka jana asubuhi” Alieleza meneja huyo kwa sauti ya kukereka kiasi.

“Anaishi wapi?”

“Sinza”

“Sinza ipi?”

“Kumekucha”

“Okay, nipe namba yake ya simu na uniambie nyumba anayoishi, halafu wewe ni meneja huwezi kuniambia kuwa huna ufunguo wa akiba wa kutuwezesha kuingia kwenye hiyo ofisi na kuangalia nachotaka kuangalia!!!”

“Hilo linawezekana Bwana Jacob Matata, ngoja nichukue ufunguo wa akiba.” Baada ya dakika kadhaa walikuwa mlangoni, mlango uliandikwa ‘Control Room’. Meneja aliingiza ufunguo ambao ulifanya kazi yake. Mlango uliitikia, wakaingia ndani.

“Aaaaaaah, ndio nini hiki?!!!!!!” Meneja aling’aka, mkono ukienda kinywani.

“Vipi Ulomi?” Jacob alihoji kwa utulivu.

“Nashangaa hakuna kompyuta hata moja na vifaa vyote vimeondolewa?” Ulomi alilalama.

“Unataka kuniambia na wewe ndio unaona haya yote sasa hivi kwa mara ya kwanza hapa?”

“Kweli kabisa bwana Jacob, huyu mtoto mwanaharamu kweli, unajua vijana wa siku hizi wanataka mafanikio ya haraka haraka sana. Sasa hivi vitu alivyoiba vitamfikisha wapi?” Ulomi alilalamika. Kwa macho ya kidadisi ya Jacob alishaelewa kuwa Ulomi hakuwa anaigiza.

“Bwana Ulomi, nashukuru kwa ushirikiano wako, nitakutembelea tena nikihitaji taarifa Zaidi” Jacob alisema huku akitoka chumbani humo. Alipitia mapokezi, baada ya kuongea machache na Rose, aliondoka hotelini pale.

Kituo cha tatu ilikuwa ni nyumbani kwa mtu ambaye hakuwa amekwenda ofisini bila tarifa, huku simu yake ikiwa haipatikani. Kama ulomi alivyokuwa amesema, mlango wa kijana huyo alikuta umefungwa. Ila yeye hakutaka kuwahoji majirani. Alitumia funguo zake maalum akaingia ndani. Sebule ilikuwa tupu, ikabidi ajikaribishe chumbani. Huko alimkuta mwenyeji wake akiwa amelala kitandani, lakini aliona cha ziada. Aliona dimbwi la damu likiwa limetapakaa sakafuni na mpini wa kisu kikubwa ukiwa unaelea kifuani mwa kijana huyo. Hakutaka kupoteza muda alishajua nini kilifanyia wala hakutaka kukagua chochote, maana kwa vyovyote waliomuua kijana huyo walikuwa wakitaka zile picha za video za matukio ya hotelini hapo. Jacob alikuwa akitafuta hayo pia ili aweze kubaini ni nani akiyemshambulia usiku wa siku ile alipokuwa akicheza na Regina. Lakini pia alitaka picha ya Eve ili aipeleke ofisini kwao kwa ajili ya kupata taarifa binafsi za msichana huyo. Lakini yote hayo, adui yake alishamtangulia hatua moja mbele. Jacob alishangaa kuona jinsi yeyote anayehusika katika mkasa huu alivyokuwa makini kusafisha kila kitu ambacho Jacob angeweza kutumia kupata fununu zake.



Akili ya Jacob Matata ilifanya kazi kwa kasi zaidi. Alitoa simu yake ya kiganjani na kupiga namba kadhaa.

“Andrew, nomba unisaidie jambo kwa haraka kidogo” Jacob alisema bila kusalimia.

“Naomba uniambie namba tatu za mwisho zilizompigia mtu mwenye namba hii, nataka kujua wapigaji walikuwa maeneo gani” Jacob alisema kwa utulivu kana kwamba hakuna jambo baya lilikuwa limetokea. Utulivu, utulivu kwa mpelelzi ni silaha. Ukiwa na pupa waweza jipeleka mikononi mwa kifo wewe mwenyewe. Baada ya dakika tatu alikuwa ameshapewa taarifa aliyoitaka.



Kituo cha nne ilikuwa ni kituo cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo. Kwa mujibu wa taarifa alizokuwa amepewa, simu tatu za mwisho wapigaji wake wote walipiga wakiwa Ubungo kituo cha mabasi. Namba hizo zilikuwa zimesajiliwa kwa ajili ya biashara ya simu na utumaji wa pesa. Jacob alitaka kuwahoji watu hao. Baada ya dakika kumi alikuwa ameshawahoji wote lakini haikuwa rahisi kwao kukumbuka wateja wote waliokuja kupiga simu kwenye vibanda vyao. Jacob akajikuta ameanza kumhusudu yeyote aliye nyuma ya shughuli hiyo. Alikuwa makini na alijua nini cha kufanya. Maana kila alipofika alikutana na nyayo zilizofutika. Kutoweka kwa Regina na Eve ilikuwa bado ni kitendawili.

Jacob afanye nini?
 
HEKAHEKA - 7

Kituo cha nne ilikuwa ni kituo cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo. Kwa mujibu wa taarifa alizokuwa amepewa, simu tatu za mwisho wapigaji wake wote walipiga wakiwa Ubungo kituo cha mabasi. Namba hizo zilikuwa zimesajiliwa kwa ajili ya biashara ya simu na utumaji wa pesa. Jacob alitaka kuwahoji watu hao. Baada ya dakika kumi alikuwa ameshawahoji wote lakini haikuwa rahisi kwao kukumbuka wateja wote waliokuja kupiga simu kwenye vibanda vyao. Jacob akajikuta ameanza kumhusudu yeyote aliye nyuma ya shughuli hiyo. Alikuwa makini na alijua nini cha kufanya. Maana kila alipofika alikutana na nyayo zilizofutika. Kutoweka kwa Regina na Eve ilikuwa bado ni kitendawili.



* * *



Wakati Jacob aliamkia ofisi ya ramani na majengo katikati ya jiji, maeneo ya Mabibo hostel ndani ya jiji hilo hilo, wakati saa tatu na nusu asubuhi ikigota yeye huyu alikuwa bado yupo kitandani. Aliisikia kutokea dirishani sauti ya redio ya jirani ambayo mmiliki wake alikuwa ameiruhusu ioneshe uwezo wake wa kutoa sauti. Kwa uswahilini hilo ni suala la kawaida sana. Unaambiwa kila mtu jali ustaharabu wako. Huyu ataweka choo chake mlangoni kwa mwingine, yule atafungua baa na kuweka spika kwenye dirisha la chumba cha kulala cha huyu. Mwingine ataweka nyimbo za dini, mwingine taarabu, mwininge hip hop, mwingine rege.

Kwa kawaida Mud si mtu wa kuwa kitandani wakati kama huo. Kitanda chake kilishazoea kuukosa uwepo wake kila ifikapo saa kumi alfajiri na kuupata tena uzito wake kati ya mida ya saa nne hadi sita. Asubuhi hii akili yake ilikuwa imechoka kwa mawazo na mwili wake kuzidiwa na uchovu. Mwili ulizidiwa na uchovu kwa vile hakuwa amepata hata lepe la usingizi tangu alipoingia kitandani saa tano usiku siku iliyopita. Akili yake ilikuwa imechoka kwa mawazo kwa vile ilikuwa kwenye mvutano mkubwa na hakuwa amefikia suluhisho la kipi cha kufanya na kipi cha kuacha.

Moyo wa Mud ulimshauri akubaliane na mpango wa Matokeo Makubwa Sasa, mtu aliyeongea nae mchana uliopita aliutaja kama ‘Big Results Now’ (BRN), lakini mwili wake ulilemewa na taarifa alizopata toka nyumbani kwao Kigoma. Hivyo mapaka wakati huo ambapo sauti ya mtangazaji wa ‘Power breakfast’ iliposikika ikisema ni saa tatu unusu ndipo Mud aliposhituka kuwa bado alikuwa kitandani. Alifikiria kwenda kazini kwake, Sokoni kariakoo, lakini mwili ulimnong’oneza kuwa haukuwa tayari kubeba hata nusu gunia siku hiyo. Ulikuwa umechoka kwa vile haukupumzishwa. Alitaka kuendelea kulala, lakini akili ikamuambia kuwa inahitaji suluhisho la majadiliano yaliyoendela kichwani usiku kucha. Alishika simu yake ya mchina iliyokuwa imefungwa fungwa na mipira kuiwezesha kushikamana. Akaiangalia kwa muda kisha akaiweka chini. Akachukua kioo na kujiangalia uso wake lakini kabla hajafanya hivyo, mlio ulisikika kuashiria kuwa ujumbe mfupi wa maneno ulikuwa umengia kwenye simu yake. Aliweka kioo chini, akaichukua simu na kuiangalia katika hali ya uzembe. Wakati anataka kusoma ndipo akatambua kuwa chandarua cha mbu kilichokuwa kikining’inia toka darini kwenda kitandani kilikuwa kimefanya chumba chake kionekane kidogo Zaidi. Hivyo akaona bora akunje chandarua hicho halafu asome ujumbe simuni akiwa amejilaza kitandani. Alichomoa chandarua toka kwenye mbinyo wa godoro na kitanda, alisita kidogo akawaangalia mbu waliokuwa ndani ya chandarua hicho. Wote walikuwa wameshiba na kuruka kwa taabu. Mud akasonya, kisha akaanza kuwaua mbu hao, alipomaliza akakunja chandarua huku damu iliyokuwa mikononi ikijisafisha kwenye chandarua.

Aliposhika simu, ujumbe mwingine uliingia. Akajilaza kitandani na kuanza kusoma hizo meseji. Meseji ya kwanza ilisomeka “Unasemaje kuhusu mpango wangu? Mud, nakuhakikishia kama ukikubali muda si mrefu utaachana na maisha ya shida” Mud hakuwa amendika jina la mtumaji wa ujumbe huo. Hakuwa anamfahamu. Aliingalia simu yake, huku katoa macho katika hali ya sintofahamu. Hakujua kama aite bahati au balaa ilikuwa ikimnyemelea. Mtu huyu alimpigia simu siku iliyopita, hakujitambulisha jina kwa Mud.

“Bila shaka unaitwa Mud, nimepewa namba yako na rafiki yangu akaniambia kuwa u kijana mzuri na muelewa, nimefuatilia maisha yako na kugundua kuwa unaishi maisha ya shida na dhiki kubwa. Nimeamua kukusaidia, ninataka nikufanye uwe mtu wangu wa karibu katika shughuli zetu” Aliongea huyo mtu bila hata kujitambulisha kwa Mud.

“Umeshawahi sikia kitu kinaitwa mpango wa matokeo makubwa sasa?” Aliuliza mtu huyo.

“Sijawahi sikia na siujui” Mud akajikuta akijibu kikondoo.

“Kwenye vyombo vya habari wanausema kama Big Results Now?” Jamaa akafafanua. Jina hilo halikuwa geni masikioni kwa Mud. Alishasikia mara kadhaa maeneo ya Kariakoo ambako hufanyia kazi. Watu wamekuwa wakitaniana kwa jina hilo, ila hakuwa anajua ni nini hasa.

“Hiyo nimewahi sikia, ila sijui maana yake” Mud alisema kwa kusita kidogo.

“Kwa kifupi huo ni mpango ulioanzishwa mahususi ili kuikomboa jamii iliyoko chini. Ni hivi Mud, kwa kuanzia nataka unifanyie kazi moja ndogo tu halafu kwa hiyo kazi nitakupatia hela nyingi sana” Jamaa alizidi kuongea.

“Kazi gani?” Mud alihoji kwa wasiwasi uliochanganyika na bumbuwazi.

“Kuna mtu atakuja kununua mahindi keshokutwa pale Sokoni, najua wewe ni mmoja wa watu wanaobeba mizigo pale Sokoni. Wakati wa kupakia magunia kuna gunia ambalo nataka lazima libebwe na wewe kupakiwa kwenye gari. Kwa kazi hiyo tu mie nitakulipa shilingi milioni kumi” Jamaa alisema kwa sauti tulivu huku akiweka tuo.

“Unasema shilingi ngapi?” Mud alihamaki.

“Umenisikia Mud, sina haja ya kurudia, kwa kuanzia leo hii nakutumia laki tano kwenye simu yako”

“Mmmmmm mbooona, sikuelewi…kwani wewe….” Mud alibabaika.

“Sikiliza bwana Mud, maelezo mengine nitakupa kesho, kwa sasa kapumzike.” Simu ilikatwa.

Mud akabaki kaduwaa. Dakika kumi baadae ujumbe mfupi wa maandishi uliingia kwenye simu yake kutaarifu kuwa alikuwa amepokea shilingi laki tano. Ni kweli alihitaji hela, lakini hii ilikuja kirahisi sana hadi ikamtia shaka. Kwake yeye hata angefanya kazi usiku na mchana asingeweza kukusana kiasi hicho cha pesa.

Hamu na nguvu za kufanya kazi vikatoweka, amani ikatoweka, mawazo yakamjaa. Hiyo ndio ilikuwa simu ya kwanza aliyopokea jana yake.

Simu ya pili ilitoka nyumbani kwao Kigoma.

“Habari za nyumbani?” Mud aliuliza baada ya kuwa amesalimiana na mdogo wake aliyempigia.

“Si nzuri, hivi natokea hospitali!”

“Kuna nini tena dogo?” Mud alihamaki.

“Mama kapata ajali ya kugongwa na gari, hali yake ni mbaya, hivi anatakiwa asafirishwe kuja Dar kwa ajili ya matibabu Zaidi. Nimekupigia kukutaarifu na kukuambia kuwa hela inahitajika kwa ajili hiyo”

“Daaaaah” Ndicho Mud alichoweza jibu.

Akabaki anaiangalia simu yake. Wakati bado anafikiria, ujumbe wa simu uliingia, ulikuwa ni wa yule mdogo wake aliyempigia punde. “Kwa sasa tunahitaji millioni moja kwa ajili ya vifaa na usafiri wa kumleta mgonjwa huko” Ujumbe ulisomeka hivyo.

Hivyo asubuhi hii Mud alitakiwa afanye maamuzi. Alikuwa ameshatuma nyumbani kiasi cha shilling laki nne, ilihitajika laki sita nyingine ili mama yake aletwe Dar kwa matibabu. Wakati huo huo alitakiwa kukutana na mtu aliyekuwa amemuahidi kumpa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa kazi ya kubeba gunia atakaloelekezwa. Kubeba mizigo Sokoni kariakoo ni kazi yake, lakini hakuelewa ni kwa nini mtu huyu alitaka kumlipa milioni kumi kwa kubeba gunia hilo moja atakaloelekezwa. Moyo ulikataa lakini akili ikamnong’oneza “huna hiari, la sivyo mama yako anakufa”

* * *

Siku zote Harken Kalm hujisifia akili zake, huamini kuwa ana akili za kipekee na ziada tofauti na binadamu wengine. Ndivyo alivyokuwa akitaka Mud asiwe na hiari ya ila kushirikiana nae. Alimuweka Mud katikati ya kufanya au kukataa na kumuacha mama yake afe. Ili kutimiza kazi yake hii, Harken Kalm alitaka mtu mwenye moyo wa kweli na mapenzi ya dhati, lakini pia awe fukara kiasi cha kutoweza kutimiza mapenzi ya moyo wake. Ni hapo ndani ya masaa manne tu jina la Mud liliifikia meza yake. Mud alikuwa na sifa hizo. Alikuwa mtoto wa pekee wa kiume kwa mama yake, waliobaki ni wasichana watatu ambao wote ni wadogo kwake. Mud alimpenda sana mama yake, ila hakuwa na uwezo wa kutimiza yote moyo wake ungemuambia kufanya juu ya mama yake.

Alipiga kama simu mbili hivi kwenda maeneo tofauti ndani ya Jiji la Dar, majibu yalipokuja tayari yalikuwa na namba ya simu ya Mud. Ilimchukua dakika kadhaa nyingine kujua wazazi wa Mud wanaishi wapi. Haikumpa shida kupanga ajali ya mama yake na Mud. Angeshindwa vipi huku anayo pesa sabuni ya nafsi.

Alichekelea kisha akasimama, akatembea taratibu kuelekea chumba kingine ndani ya jumba hilo. Alipovuka mlango alijikuta anatazamana na chumba kikubwa kichokuwa kimepangwa kama chumba cha mkutano. Kilikuwa nadhifu sana na kupangwa kwa ustadi mkubwa. Mbele kabisa ambapo ndio unaweza kusema mwenyekiti wa mkutano angekaa kulikuwa na meza kubwa ya kioo. Meza hiyo iliweza kuonesha nini kilikuwa kwenye uvungu wake. Kulikuwa na vyombo vya kisasa vya mawasiliano. Ukutani kwa mbele kulikuwa na kitu kama kioo, hicho ni kioo cha televisheni, kilikuwa chembamba na kilikaa ukutani kama karatasi iliyobandikwa.



Harken Kalm aliangalia saa yake, kisha akaelekea sehemu fulani kwenye kona ya chumba hicho akachukua remote ya televisheni. Baada ya muda mfupi tayari alikuwa kwenye mkutano mzito. Mkutano huo ulijumuisha watu watano, wawili kati yao walikuwa nchini na wengine watatu walikuwa katika mabara tofauti. Lakini chombo hiki kilionesha sura zao na sauti zao zilisikika sawasawa.

“mambo yote yanakwenda kama yalivyopangwa, kufikia jumamosi kila kitu kitakuwa tayari na siku hiyo usiku shughuli itafanyika. Nadhani itakuwa kazi ya kusisimua kuliko zote tulizowahi kufanya, wakati wengine tukicheka, wengine watakuwa wakilia, wengine watakuwa wakijiuzulu, wengine watakuwa wamekazana kuandika habari magazeti, balozi mbali mbali zitakuwa zikitoa misimamo yao. Wanausalama watakuwa wakihaha kila kona” Harken Kalm alieleza kwa utulivu kwa sauti ya majivuno.

“Huoni kama Jumamosi ni karibu sana kwa kila jambo kuwa mahali pake?” Alihoji huyu kutoka Tanzania ambaye peke yake ndio alikuwa mwafrika, wengine wote ni wazungu ikiwa ni pamoja na Harken Kalm.

“Mheshimiwa, ondoa wasiwasi, tumefanya kazi kwa miaka zaidi ya kumi sasa sijawahi kuharibu, nadhani ndio maana kazi hii mmeniachia mie.” Alijibu kwa sauti iliyochanganyika rangi za dharau na kujiamini.

“Kesho tunapeleka, jioni malaika atakuwa njiani kuelekea chimboni, kule nimeshamuandaa mtu wa kumpokea……..”

“Vipi kuhusu Jacob Matata? Maana yule ni hatari kuliko hatari yenyewe….kama hujaweza kupata namna ya kumdhibiti huyu mtu nachelea kukuambia kuwa mpango wetu hautofanikiwa……” Mheshimiwa wa kitanzania alimkatisha Harken Kalm.

“Naomba mnipe nafasi ya kuelezea mpango wangu kwa kifupi, ripoti kamili ya namna nitakavyotekeleza hili nadhani mnaweza rejea kwenye ‘master plan’ niliyowatumia asubuhi ya leo. Najua udhaifu wa Jacob Matata, udhaifu wake mkubwa ni wanawake, na nimeshamuwekea mtego tayari. Tafadhali naomba muwe mnasoma ripoti nazowatumia kuliko kuanza kuulizana maswali ya ajabu ajabu hapa” Harken Kalm alifoka akionesha dhahiri kukerwa na swali la mheshimiwa toka Tanzania.

“Soko liko tayari, na bei imekuwa juu zaidi ya ile tuliyokuwa tumetazamia kuipata” Alisema huyu mjumbe toka China. Kikao cha watu hao watano kiliendelea kwa mikakati mbalimbali.

Itaendeleas
 
HEKAHEKA - 8

“Naomba mnipe nafasi ya kuelezea mpango wangu kwa kifupi, ripoti kamili ya namna nitakavyotekeleza hili nadhani mnaweza rejea kwenye ‘master plan’ niliyowatumia asubuhi ya leo. Najua udhaifu wa Jacob Matata, udhaifu wake mkubwa ni wanawake, na nimeshamuwekea mtego tayari. Tafadhali naomba muwe mnasoma ripoti nazowatumia kuliko kuanza kuulizana maswali ya ajabu ajabu hapa” Harken Kalm alifoka akionesha dhahiri kukerwa na swali la mheshimiwa toka Tanzania.

“Soko liko tayari, na bei imekuwa juu zaidi ya ile tuliyokuwa tumetazamia kuipata” Alisema huyu mjumbe toka China. Kikao cha watu hao watano kiliendelea kwa mikakati

*******

“Dokta mbona waonekana una mawazo tofauti na kawaida yako” Regina aliuliza kwa upole alipokuwa ameingia sehemu ambayo wafanyakazi wa mzee Harken Kalm hutumia kwa kujipatia chakula. Regina aliamua kumuuliza Dokta Eve, baada ya kuona tangu ameletwa hapo siku mbili zilizopita hakuwa katika hali ya kawaida. “Hayakuhusu bibie, kwani hata nikikuambia hutaweza kunisaidia” Eve alisema kwa sauti ya chini lakini iliyoonesha dhahiri hasira aliyokuwa nayo. Jibu hilo lilimfanya Regina atabasamu na kujua kuwa kuna mambo yalikuwa yamempata Dokta Eve.

“Sawa Dokta waweza ona kuwa siwezi kukusaidia lakini wawili si sawa na mmoja” Regina alijaribu tena kwa sauti ya upole zaidi. Hapo Eve aligeuza kichwa na kumuangalia Regina ambaye alikuwa tayari ameshamshika mabegani kwa upendo.

“Nashukuru kwa kujali kwako, lakini sitakuwa tayari kukuambia tatizo langu” Eve alisema huku akiwa anafuta machozi.

“Si mbaya kama umeona kuwa ni vema ukifanya hivyo, lakini nadhani mimi na wewe tuko katika hali moja na isingekuwa vibaya kama tukishirikishana na kushauriana katika matatizo tuliyonayo katika kambi hii na..” kauli ya Regina ilikatishwa na ishara ya Dk. Eve iliyomtaka kunyamaza haraka. Regina alipogeuka, alimuona Bob Sepeto akiwa anakuja pale walipokuwa wamekaa. Alipofika aliwasabahi na kumvuta Regina ambapo waliongea maneno machache na kisha akaondoka na kuwaacha wasichana hao wawili wakiendelea na maongezi yao. Kiumri Eve alikuwa mkubwa kuliko Regina.

Tangu siku hiyo walijikuta wamekuwa marafiki wakubwa sana. Hakuna la Regina ambalo Eve hakulijua na kadhalika siri za Eve, Regina alizijua zote japo urafiki wao waliamua kuufanya kuwa wa siri.

Jambo moja hakuna aliyejua na kuwa tayari kumuambia mwenzie, nalo ni juu ya uhusiano wao kila mmoja na mpelelezi Jacob Matata. Hakuna aliyekuwa tayari kusimulia matukio yaliyomkuta akiwa na Jacob Matata. Kila mmoja alikuwa akimuwaza Jacob kwa mtazamo tofauti. Regina alimchukulia Jacob kama mvulana pekee aliyetokea kumpenda lakini hakuwa na uwezo wa kumuona tena wala kuwasiliana nae. Kadhalika Eve alikuwa na mawazo kama hayo.

Eve hakuwa anajua kuwa Regina ndiye msichana ambaye Jacob alikuwa akimuongelea kuwa amechukuliwa na watu wasiojulikana. Kadhalika Regina hakujua kuwa Eve ndio msichana aliyemuokoa Jacob alipokuwa amepigwa kule Miami hoteli wakati wakicheza muziki pamoja.

Siku moja wakati wakiwa wanapata chakula cha mchana katika moja ya sehemu za kulia chakula za jumba hili, Eve na Regina walikuwa na maongezi ambayo yalionekana kuvuka mpaka siku hiyo.

“Mdogo wangu Regina, hivi ni kitu gani ambacho kwa sasa unakihitaji kuliko vyote?” Eve aliuliza kwa sauti ya kawaida kama kawaida yao wanapokuwa wakiongea. Walifanya hivi ili kuzuia wasisikiwe na walinzi wa jumba hili ambao walikuwa wengi na wenye silaha kali. Kabla ya kujibu swali aliloulizwa, Regina aliyafumba macho yake na kuyafunika kwa viganja viwili vya mikono yake. Ukweli ni kuwa swali hili lilikuwa limegusa sana hisia za Regina.

“ Eve, msichana ni ku..” alisita kidogo na kuangalia kushoto na kulia, kisha akaendelea.

“msichana ni kupenda na kupendwa na kisha kuwa na familia ni jambo ambalo nina kiu nalo sana kwa wakati kama huu, japo kutokea kwake nakuona kama ndoto tu” Regina alisema huku akijifumbata.

“Kwani inamaana hujawahi kupenda Regina?” Eve alizidi kudadisi.

“Mmmh Eve nawe, umeamua kweli leo” Alisema Regina akionesha aibu kidogo.

“Unajua Regina haya ni mambo ambayo yanatukabiri kwa sasa na inabidi tuyaongelee japo hatujui hatima yetu” Alisema Eve huku akikisogeza kiti chake jirani zaidi na alipokuwa amekaa Regina.

“Eve, nimewahi kupenda, tena si siku nyingi sana zimepita tangu pale nilipokutana na mtu ambaye aliuteka moyo wangu kwa ghafla, ila nashi……” Regina alishindwa kuendelea na badala yake akaanza kulia. Kwa vile Eve alikuwa ameshajisogeza karibu na pale alipokuwa Regina, ilibidi amkumbatie na kuanza kumbembeleza ili anyamaze.

“Nyamaza mdogo wangu mpenzi, mbona wataka kunitia machungu zaidi, lengo langu halikuwa kukuumiza bali tufarijiane na kutafuta namna ya kusaidiana” Eve alisema huku akijaribu kushindana na kasi ya machozi yaliyokuwa yakitoka machoni kwa Regina. Baada ya juhudi za kitambo kidogo hatimaye Regina alinyamaza

“Eve, kama wiki moja iliyopita nilikutana na kijana ambaye kwa mara ya kwanza alinifanya nijisikie na nijue kupenda, kweli nilimpenda ghafla na bado yuko ndani ya moyo wangu. Lakini la kusikitisha ni jinsi alivyofanyiwa kijana huyo kwa kule kuwa karibu nami” Alipofika hapo Regina alinyamaza tena na kuangaza huko na huko kana kwamba mtu aliyekuwa akiangalia kama kuna mtu aliyekuwa akifuatilia mazungumzo yao.

“Kwani alifanywa nini” Eve alihoji baada yakuonekana kuingiwa na habari hii ya Regina.

“Alipigwa vibaya sana, akaanguka chini kama hakufa basi. Jambo hilo liliniuma sana, tangu hapo sina raha, sijui ni namna gani nitakutana na kijana yule niliyempenda ghafla nae kuonekana kunipenda” Hapo Regina alionekana kufuta machozi tena.

Baada ya kusikia kisa hicho cha Regina, Eve nae alimsimulia juu ya pendo alilonalo juu ya kijana mmoja aliyemuokota kwenye ukumbi wa Miami Hoteli akiwa amezimia baada ya kuwa amepigwa na kundi la akina Bob Sepeto. Alisimulia mengi kuhusu kijana huyo ambaye yeye alimtaja kama Nico Badala ya Jacob Matata.

“Umesema ulimuokota kwenye ukumbi wa Miami Hoteli, ilikuwa lini hiyo?” Regina alitia shaka na kuuliza.

“Ndio, na ilikuwa siku ya jumamosi wiki ile iliyopita, nilipomuhudumia na kupona tukawa tunatembeleana, tangu hapo nikajikuta nimempenda sana kijana huyo” Eve alieleza.

“Ulipomuuliza alisema ni kwa nini walimpiga?” Regina aliuliza huku tayari akiwa ameshaanza kuhisi kuwa huenda mtu huyo ni Jacob Matata mvulana ambaye amekuwa akimfikiria kila dakika inayopita.

“Anasema alikuwa anacheza muziki na msichana mmoja aliyekutana nae ukumbini hapo, lakini sababu hasa ya wao kumpiga hakuwa anaijua…” Eve alipofika hapo ilibidi akatize maelezo yake pale alipomuona Regina akiwa anasimama na kunyoosha mikono juu.

“Kwani vipi Regina mbona umefurahi hivyo ghafla?” Eve alihoji kufuatia furaha aliyoionesha Regina ghafla.

“Nimegundua kuwa unaemzungumzia ndiye kijana ambaye nilikuwa namuongelea na mimi, namshukuru Mungu kusikia kuwa kijana huyo yu mzima” Tayari Regina alishabaini kuwa anaeongelewa na Eve ni Jacob Matata. “Umesema unayo namba yake ya simu?” Regina alihoji kwa furaha.

“Ndio ila kama ujuavyo kuwa nimenyang’anywa simu yangu na humu ndani ni wachache sana wenye simu, nao ni wale walio karibu sana na mzee Harken Kalm. Hivyo namba hizi haziwezi kutusaidia lolote” Eve alisema huku akiwa anafungua pochi yake na kuanza kupekenyua ndani. Mkono ulipotoka ndani ya pochi hiyo ulikuwa umeshikilia kijikaratasi kidogo.

“Hizi hapa ndio namba zake za simu, japo sijui tutatumia njia gani kuhakikisha tunawasiliana na Nico” Alisema Eve huku akimkabidhi Regina zile namba. Furaha aliyokuwa nayo Regina ni kana kwamba alikuwa amempata Jacob mwenyewe. Waliachana huku kila mmoja akiwa na mawazo yake. Regina aliapa kuwa kwa vyovyote vile angetumia kila njia kuhakikisha kuwa anawasiliana na kumpata. Alijua fika kuwa yeye kuonana na Jacob ingekuwa ngumu, lakini alihitaji kuwa anasikia sauti yake tu.

Eve kwa upande wake alishangaa kutambua kuwa msichana aliyekuwa anamnyima usingizi Jacob huko nje alikuwa ndio huyu Regina waliyekuwa nae ndani ya jumba hili. Kutokana na upendo aliokuwa nao kwa Jacob, Eve akajikuta anaapa kumpata Jacob na kuhakikisha hawi na Regina japo hakujua ni namna gani angeweza kutekeleza hilo. Taratibu ile hali ya urafiki wa kweli aliyokuwa nayo juu ya Regina ikaanza kutoweka
 
HEKAHEKA - 9

Eve kwa upande wake alishangaa kutambua kuwa msichana aliyekuwa anamnyima usingizi Jacob huko nje alikuwa ndio huyu Regina waliyekuwa nae ndani ya jumba hili. Kutokana na upendo aliokuwa nao kwa Jacob, Eve akajikuta anaapa kumpata Jacob na kuhakikisha hawi na Regina japo hakujua ni namna gani angeweza kutekeleza hilo. Taratibu ile hali ya urafiki wa kweli aliyokuwa nayo juu ya Regina ikaanza kutoweka.



* * *



Siku moja Eve akajikuta anaingiwa na wazo la kuyaharibu zaidi maisha ya Regina. Hii ilikuja pale Regina alipomsimulia Eve kuwa alikuwa amefanikiwa kuwasiliana na Jacob. Regina kwa vile alikuwa katika mapenzi ya kulazimishwa na Bob Sepeto mtu ambaye hata hivyo alikuwa hanithi, alitumia nafasi hiyo kutafuta namna ya kuwasiliana na Jacob kwa kutumia simu ya Bob Sepeto. Na kweli siku hiyo Regina alifanikiwa kutumia simu ya Bob Sepeto kuwasiliana na Jacob. Taarifa hii ya Regina kuwasiliana na Jacob haikumfurahisha kabisa, akajikuta chuki juu ya Regina inaanza kukua. Alijua yeye asingekuwa na uwezo wa kuwasiliana na Jacob kwani tangu agundulike kuwa na uhusiano na Jacob na kuhamishiwa ndani ya jumba hili toka uraiani, Eve alinyimwa uhuru ule alikuwa nao mwanzo.



* * *



Simu iliyopigwa na Regina toka ndani ya jumba la mzee Harken Kalm, ilimkuta Mpelelezi Jacob Matata akiwa tayari ameshajipumzisha baada ya mihangaiko ya siku nzima katika kutafuta chanzo cha kutekwa kwa wasichana wale. Alipochukua simu yake ili apokee ilikuwa inagonga saa nane na robo usiku. Muda huo Regina alikuwa ameiiba simu ya Bob Sepeto na kwenda nayo chooni ambapo wakati huu ndio alikuwa amepiga. Bob alikuwa ndani ya usingizi mzito kitandani.

“Nani na nikusaidie nini?” Jacob alipokea simu hiyo kwa kukereka kidogo hasa baada ya kuona namba ya mtu aliyekuwa amepiga simu hiyo hakuwa anamfahamu.

“Mie Regina, sijui kama bado unanikumbuka?” Regina alisema kwa sauti ya wasiwasi chooni humo alimokuwa.

“Oooh Regina, siwezi kukusahamu mtu niliyeondokea kukupenda kama wewe, uko wapi na je ni salama?” Jacob alisema kwa sauti ya mshangao. Hakuwa anatarajia kupata simu kama hiyo wakati huo.

“Jacob mpenzi, nimepiga kukusalimia tu najua hapa nilipo huwezi kuja na wala mimi siwezi kuja huko, nimeona nikisikia sauti yako tu itakuwa ahueni. Nakutakia kila la heri na maisha mema, ila tambua kuwa japo nipo kifungoni na nilinyimwa nafasi ya kusema, nakupenda sana Jacob. Kaa ukijua hilo…” Wakati Regina akiwa bado anabwabwaja maneno huku sauti yake ikisikika wazi kuwa alikuwa analia, Jacob alimkatisha kwa swali. “Kwani umepataje namba yangu na uko wapi Regina?”

“Eve ndiye aliyenipa namba yako na hapa tulipo tuko kwenye jumba moja huku bagamoyo pembezoni mwa baha…..” Kabla hata hajamaliza Regina alikata simu pale aliposikia vishindo vya mtu akija chooni alikokuwa. Haraka aliifutika simu ndani ya nguo yake ya ndani na kufungua mlango wa choo ili atoke.

Upande wa pili Jacob akiwa chumbani kwake alishangazwa na namna simu ya Regina ilivyokoma, alidhani huenda Regina alikuwa ameishiwa na hela kwenye simu yake. Hivyo akaamua kumpigia.

Regina alikuwa ameshatoka chooni, kwa mwendo wa woga alikuwa anaelekea chumbani ambako alikuwa amemuacha Bob Sepeto akiwa kalala. Kabla hata hajafika mbali mara alisikia vile vishindo vya mtu vikizidi kuwa karibu. Mara Bob Sepeto alitokea akiwa kashikilia bastola yake. Hii ni kawaida ya mtu huyu kuwa kila anapoenda huwa na bastola mkononi. Regina alikuwa ameshaizoea hali hii.

“Leo tumekula nini mbona wote chooni namna hii?” Bob aliuliza kwa mzaha wakati walipokaribiana na Regina. “Labda zil…?” Kauli ya Regina ilikatizwa na mlio wa simu uliorindima tokea ndani ya nguo yake ya ndani.

“Mungu wangu sij….?” Regina alijikuta akiropoka, lakini kabla hajamaliza Bob Sepeto alidakia.

“Mshenzi, Mungu kafanya nini?” Weka mikono yako juu na usimame hapo hapo, chukua hiyo simu na muelekeze huyo mtu aje hapa kesho. Kamwe usimuambie kuwa hapa kuna ulinzi wowote” Bob alimuamuru Regina. Regina hakuwa na namna ya kubisha, aliitoa simu huko alikokuwa ameiweka na kuipokea.

“Hallow, eeh Regina umesema mko na Eve?” Jacob aliuliza bila kujua kuwa alikuwa anaongea na mtu aliyekuwa ameelekezewa mdomo wa bastola.

“ Ndi..ndi.. ndio. Ke….ke…kesho njoo utafika tu, ukiwa barabara kuu ya kuja huku Bagamoyo utakuta kibao kikubwa kimeandikwa Complex Store, katisha ha.. ha.. hapo na utafika tu. Jacob…” Regina ambaye sauti yake ilishindwa kuficha hofu aliyokuwa nayo na ambaye alikuwa akilia ilikatika ghafla. Bob aliinyakua simu na kumpa kofi moja kali kabla ya kumfuata na kuanza kumpa vipigo mfululizo. Baada ya hapo alimfunga vizuri na kwenda kumfungia stoo. Tayari Bob alishahisi binti huyu alikuwa hatari kwa usalama wa jumba hilo. Akawa anafikiria adhabu kali ya kumpa.



Jacob Matata hakuchelewa kutambua kuwa sauti ya Regina ilikuwa imebadilika ghafla na kuwa kule kukatika kwa simu mara ya kwanza haikuwa kwa sababu ya hela, bali kuna matatizo yalikuwa yamempata binti huyo. Alishahisi nini kilikuwa kinaendelea huko walikokuwa Regina na Eve. Mara moja alijiona mwenye dhamana ya kwenda kuwaokoa. Baada ya hapo hakupata usingizi tena, akili yake ilikuwa katika mipango mingi.



Kabla ya kupokea simu hiyo ya Regina, Jacob alikuwa ameshahangaika wiki nzima kutafuta ni nani aliyekuwa nyuma ya mpango wa kuwateka wasichana Regina na Eve. Hakuwa anajua undani wowote wa maisha ya wasichana hawa wawili ambao alitokea kukutana nao kwa nyakati tofauti. Sababu kuu yakutojua undani wao ilikuwa ni muda mfupi aliopata kuwa na kila mmoja wa wasichana hao. Hakuwa na muda mrefu wa kuwajua.Tangu waonane mpelelezi Jacob alibahatika kuwa na masaa machache ya kuwa na Regina kabla hajachukuliwa na watu wasiojulikana huku wakimuacha yeye mwenyewe akiwa kazimia kwa kipigo.

Kadhalika alikuwa na siku chache sana za kuwa na msichana Eve kabla nae hajachukuliwa na watu ambao pia hakuwajua. Hii haikumpa nafasi ya kuwajua kwa undani wasichana hao, wala hakujua ni nani aliyekuwa akiwachukua na kwa nini.



* * *



Saa kumi na moja ilimkuta Jacob tayari akiwa yuko mtaani. Begani mwake alikuwa na kibegi kidogo ambacho kilisheheni vifaa ambavyo vilistahili kubebwa na mpelelezi kama yeye. Alipita mitaa kadhaa toka ule aliokuwa akiishi hadi pale alipotokezea kwenye barabara moja kuu. Hapo alisimama kwa kitambo kabla hajapungia mkono teksi moja iliyoonekana kutokuwa na abiria. “Nipeleke kivukoni” Jacob alisema mara baada ya kuwa ameshaingia ndani ya teksi hiyo.

“Shilingi elfu tano” Alisema dereva huyo huku akiwa anaondoa gari.

“Jitahidi kuwahi” Badala ya kujibu Jacob alitoa ilani.

Dereva huyo alijitahidi kuendesha gari hiyo na kwa vile msululu wa magari haukuwa mkubwa kwenye barabara za jiji wakati huo, baada ya dakika kadhaa tayari walikuwa wameshafika kivukoni. “Hebu nisogeze upande ule pale unaoonekana kuwa na boti nyingi nyingi” Jacob alisema. Walipofika sehemu aliyokuwa ameomba, dereva aliegesha na Jacob alishuka huku akiwa tayari kishamlipa ujira wake dereva huyo.

Alitembea taratibu mpaka ufukweni kabisa mwa bahari hiyo ya Hindi. Hapo alianza kuelekea kule zilikokuwa zimeegeshwa boti kadhaa. Alipofika hakuona dalili za kuwa na mtu maeneo hayo, lakini baadaye akatambua kuwa yawezekana manahodha wa boti hizo wamo ndani yake wamelala. Kwa vile zilikuwa ndani ya maji ilimbidi kusubiri kwani hakuwa tayari kuvua nguo na kwenda kuingia ndani ili kuwasiliana na wenye boti. Lakini akiwa katika mawazo hayo mara alisikia sauti toka ndani ya boti moja ikimuuliza kama alikuwa akitaka huduma. Aliitikia kuonesha kuwa kweli alikuwa akiitaji huduma. Mtu huyo alishuka haraka na kuanza kutembea ndani ya maji kuja upande aliokuwa amesimama Jacob Matata.

“Nahitaji boti ya kunipeleka bagamoyo” Jacob alisema.

“Bagamoyo sehemu gani? maana Bagamoyo ni kubwa,” Alihoji jamaa huyo ambaye Jacob alistahili kumuita babu.

“Bagamoyo jirani na ile kambi ya Koboyo, nadhani unapafahamu hapo?” Jacob alijibu huku akiachilia swali.

“Eeh, hapo napafahamu, lakini huwa si sehemu salama sana, kuna jamaa mmoja ana ghala yake huwa hapendi kuona boti zikipita kwa kudhani ni maharamia?” Alisema mzee huyo kwa wasiwasi. Jacob kusikia hivyo nywele zikamsimama.

“Kwani ghala hizo zinahifadhi nini mpaka awe mwoga kiasi hicho?” Jacob alijifanya kuuliza. Mzee huyo hakuonekana kufurahia swali hilo. “Aah bwana ya duniani humu yaache kama yalivyo, hebu tuongelee yanayotuhusu maana hayo hatuyawezi. Utanipa shilingi laki na nusu kwa kazi hiyo” Alisema mzee huyo huku akimuangalia Jacob usoni. “Basi nitakupa shilingi laki mbili, kwani tunaweza kukaa kidogo kabla ya kurudi” Jacob alisema huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa noti kumi na tano nyekundu, ambazo zilikuwa na thamani ya shilingi laki moja na elfu hamsini zilizomfanya mzee huyo meno yote yawe nje.

Baada ya muda tayari walikuwa wakiyakata maji kuelekea Bagamoyo. Walipofika sehemu fulani, Jacob alitoa simu yake na kubonyeza namba kadhaa kisha akasubiri simu hiyo kupokelewa upande wa pili. Iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

Ndani ya jumba au kambi ya mzee Harken Kalm, kwanza watu ndio walikuwa wanaamka. Ndani ya jumba hilo lenye ukubwa wa kambi robo tatu yao wakiwa ni wanawake, kuanzia madktari wanaofanya kazi hiyo haramu mpaka mateka na wafanyakazi wengine wote wanachukia sana mambo yanayofanyika hapo, ila kutokana na ulinzi uliokuwa hapo hakukuwa na namna ya kufanya lolote la kujiokoa. Walinzi wa mzee Harken Kalm, ndio watu pekee ambao walionekana kufurahia kazi yao. Wao walikuwa na uhuru wa kwenda walipotaka. Walikuwa wakipewa chochote walichotaka toka kwa mzee Harken Kalm.

Simu iliyopigwa na Jacob ilifika chumbani alikokuwa amelala Bob Sepeto mkuu wa walinzi wa mzee Harken Kalm. Tangu alipomkuta Regina akiwa na simu hiyo usiku huo na kumuamuru aongee na Jacob, Bob alikuwa ameihifadhi namba hiyo kwa jina la “hatari”. Hivyo simu ilipoita asubuhi hii, Bob alipoichukua na kukuta jina hatari mara moja akili yake ikajua ni yule aliyekuwa akiongea na Regina usiku.

Wakati mpelelezi Jacob akiwa anasubiri simu hiyo ipokelewe, Bob Sepeto alikuwa akikimbia toka chumbani kuelekea alikokuwa amemfungia Regina tangu usiku. Alipofungua mlango na kuingia alimfungua kamba Regina.

“Pokea simu hiyo na umuulize jamaa yako yuko wapi, akikuambia mwambie kuwa leo umepewa ruhusa ya kwenda hospitali kwa hivyo utaenda kumsalimia” Bob Sepeto alimuamuru Regina huku akiwa anaiseti simu hiyo ili pindi wakiongea isikike kwa sauti ambayo nae angeweza kumsikia mtu wa upande wa pili. Alimpa Regina simu hiyo.

Simu ilipopokelewa Jacob alifurahi kusikia sauti ya Regina japo hakuchelewa kutambua kuwa hakuwa huru na alikuwa amesimamiwa wakati akiongea.

“Uko wapi saa hizi Jacob?” Regina aliuliza huku akisikia wazi sauti ya muungurumo wa injini ya boti. Muungurumo huo ulisikika na Bob Sepeto pia ambaye aliutambua.

“Niko kwenye gari nakuja Bagamoyo na nimeshakaribia kabisa na kibao ulichosema” Jacob aliongopa akijua kuwa hakuwa akisikiwa na Regina peke yake. Alijua kuwa Regina alikuwa ameamuliwa amuulize hivyo ili watu hao waweze kujua Jacob yuko wapi na waweze kumpata. Hivyo aliamua kufanya hivyo ili aweze kuwapoteza maboya, na waende kumsubiri barabarani.

“Sawa, sasa leo nimepewa ruhusa ya kwenda hospitali, hivyo ukifika hapo kibaoni nisubiri nitakukuta hapo, nitakuwa peke yangu na dereva tu” Regina alisema maneno hayo kwa uchungu mkubwa huku akiwa kafumba macho yake. Alikuwa kama vile anamuona Jacob na kuyaona macho yake kama yanayomuambia mbona unanisaliti mpenzi.

“Usiwe na hofu, nitakusubiri hapo, kwani kwa mujibu wa dereva ndio tumekaribia kabisa…” Kabla Jacob hajamaliza, Bob alisonya kwa hasira na kuinyang’anya ile simu toka mkononi kwa Regina na kuizima. “Mbwa koko wako huyu anajifanya mjanja sana sio, yuko kwenye boti na anadanganya kuwa yuko kwenye gari anakuja, ila amejimaliza mwenyewe kwani ni kweli anakuja lakini si kwa gari bali kwa boti. Jiandae kwani muda si mrefu mtakuwa nae hapa na mtazeeka pamoja nae hapa, mtazaa nae watoto ambao watakuwa chakula cha viwanda huko ulaya” Maneno hayo yalitamkwa na Bob katika sauti iliyokuwa imejaa ukatili mkubwa.

Kwa upande fulani Regina alifurahishwa na maneno hayo, na upande mwingine yalimuumiza mno. Haikuwa siri kuwa alikuwa anampenda Jacob na alifurahi kusikia kuwa angekuwa nae japo si katika hali ya amani. Lakini kilichomuumiza ni kusikia kuwa wangezaa watoto na Jacob na watoto hao wangekuwa chakula cha viwanda huko ulaya. Kweli alipenda wazae na Jacob, lakini si watoto wa kukaushwa na maiti zao kwenda kuzikwa ulaya.

Baada ya hapo, Bob Sepeto alimchukua Regina na kumfunga tena kamba. Alifunga mlango na kumuacha Regina ndani ya chumba hicho kilichokuwa kimejaa nguo nyingi.

Alipotoka hapo, haraka haraka akatoa amri ya kutaka kukutana na kikosi chake cha walinzi wa majini. Muda si muda, kikosi hicho kikawa tayari kimekusanyika ndani ya chumba maalum ambamo ndimo Bob Sepeto kama mkuu wa ulinzi hutumia kutoa amri na maagizo.

“Kuna binadamu mmoja anakuja hapa kambini, kutokea mjini, hivi ninavyoongea na ninyi yuko ndani ya boti akiwa anakuja. Ninachotaka ni kuwa ndani ya muda mfupi muwe nae hapa akiwa mzima kabisa. Kwa vile hatuijui sura yake, hivyo boti yoyote mtakayokutana nayo katika mwambao huu asubuhi hii hakikisheni mnawachukua watu wake, sitapenda kusikia taarifa nyingine tofauti na hii. Tumieni zana yoyote mnayodhani kuwa itawasaidia katika zoezi hili. Nawatika kazi njema” Alipomaliza tu alifunga mlango na kutokomea huku akiwaacha walinzi hao wa majini wakiwa wanatawanyika kufuata vifaa vyao na baadaye kwenda baharini.

Asante kwa like na comment yako.

Vipi tuendelee au?
 
Shusha vitu mkuu.
Tupo pamoja kiongozi.
 
HEKAHEKA - 10

“Kuna binadamu mmoja anakuja hapa kambini, kutokea mjini, hivi ninavyoongea na ninyi yuko ndani ya boti akiwa anakuja. Ninachotaka ni kuwa ndani ya muda mfupi muwe nae hapa akiwa mzima kabisa. Kwa vile hatuijui sura yake, hivyo boti yoyote mtakayokutana nayo katika mwambao huu asubuhi hii hakikisheni mnawachukua watu wake, sitapenda kusikia taarifa nyingine tofauti na hii. Tumieni zana yoyote mnayodhani kuwa itawasaidia katika zoezi hili. Nawatika kazi njema” Alipomaliza tu alifunga mlango na kutokomea huku akiwaacha walinzi hao wa majini wakiwa wanatawanyika kufuata vifaa vyao na baadaye kwenda baharini.

Bob Sepeto alipomaliza kutoa amri hiyo, alielekea moja kwa moja mpaka kwenye nyumba yake ya kulala. Humo alimchukua Regina na kuondoka nae. Kwa kuwa kambi hiyo ilikuwa kubwa mno, hakuna aliyekuwa akijua Mzee Harken Kalm alikuwa akilala wapi zaidi ya Bob sepeto na Said Kipipa. Alitembea na Regina mpaka walipofika nyumba fulani na kuingia. Ilikuwa ni nyumba ya kifahari ambayo usingedhani kuwa ilikuwa ndani ya kambi hii ambayo wengi waliamini kuwa ilikuwa imejaa bidhaa zisizokuwa na thamani yeyote, kumbe imejaa watu walio katika mateso na vitu vingi vyenye thamani kubwa. Walipofika sehemu iliyoonekana kuwa ni sebuleni, Bob Sepeto alimuamuru Regina asimame sehemu fulani ambayo ilikuwa imechorwa rangi nyeusi. Mwenyewe Bob aliuendea ukuta fulani na kuchukua kitu kilichokuwa mfano wa remoti ya Televisheni. Alikielekeza alipokuwa amesimama Regina, mara sehemu ile aliyokuwa amesimama ilianza kudidimia ardhini. Regina alitaka kupiga kelele, lakini kabla hajawahi kufanya hivyo tayari alijikua ametokezea kwenye chumba kimoja nadhifu sana. Alipoangalia nyuma yake aliona tayari kuna kiti, mbele kulikuwa na Mzee mmoja wa kizungu. Mzee huyu alikuwa wa makamo huku kichwa chake kikiwa kimejaa mvi kama aliyepakwa rangi nyeupe. Alikuwa amekaa kwenye kiti kimoja cha gharama huku mbele yake kukiwa na meza iliyokuwa na kompyuta ndogo, seti ya televisheni, mashine ya faksi, na vitu vingine ambavyo Regina hakujua ni nini. Kwa kifupi kilikua ni chumba cha thamani na cha kisasa kabisa.

“Karibu binti mzuri, keti na jisikie huru” Alisema mzee huyo kwa kiswahili kilichosikika kuwa ni cha kujifunza. Regina alikaa, alipokaa tu mara mbele yake ikatokea meza toka ardhini mbele yake. Wakati bado akiwa anafikiria hilo, mara akatokea binti mmoja mzuri akiwa na sinia lililojaa vitafunwa mbalimbali pamoja na chai nzito y maziwa. Vitu hivyo viliwekwa kwenye meza iliyokuwa imetokea mbele ya Regina nukta chache tu zilizokuwa zimepita. “Karibu kifungua kinywa na nadhani utajisikia vizuri kuongea na mimi” Alisema mzee huyo huku akichukua kitu kama remoti aliyokuwa ametumia Bob kumleta Regina katika chumba hiki. Aliielekeza remoti hiyo kwenye ukuta uliokuwa upande wa kulia wa alipokuwa amekaa mzee huyo. Nukta chache baadaye ukuta ule ulikuwa tayari umeshaachana na kufanya sehemu nyingine ya chumba. Regina hakuyaamini macho yake pale alipoangalia vizuri upande huo alimuona Bob Sepeto na Dokta Eve wakiwa wamekaa. Regina alitaka kupiga kelele na kumuita Dokta Eve, lakini Dokta Eve alimuwahi kwa kumfinyia jicho kuashiria kuwa asifanye hivyo.

“Eeh Bob ulikuwa unasemaje kuhusu binti huyu?” Aliuliza mzee huyo huku akimuangalia Bob. Bob alisimama kwa heshima iliyochanganyikana na woga na kuanza kumuelezea mzee Harken Kalm, kila kitu juu ya msichana Regina. Hii ilijumuisha tangu alipompata msichana huyu sokoni kariakoo, mpaka kitendo alichokifanya usiku uliopita. Alipomaliza kutoa maelezo yake, Bob alitoa ishara ya heshima na kisha akakaa kwenye kiti chake.

Mzee Harken Kalm alimuangalia Regina kwa muda mrefu, bila kumpa hata nafasi ya kupepesa kope. Baada ya dakika kadhaa hatimaye mzee huyo alimuuliza Regina. “ Hebu niambie, huyo jamaa jina lake ni nani na kwa nini unawasiliana nae?” Aliuliza mzee Harken Kalm kwa sauti ya taratibu lakini ambayo ndani yake ilikuwa imejaa uovu usiosemeka. Tangu ameletewa ile chai na vitafunwa Regina hakuwa amepiga hata mikupuo miwili. Swali hili lilikuwa jepesi na gumu kwa upande fulani. Lilikuwa jepesi kwa vile majibu yote alikuwa nayo, na lilikuwa gumu kwa vile lilimtaka kuwa mkweli.

“Huyo kijana anaitwa Jacob Matata, na mimi ni…..” Kauli yake ilikatwa na swali la mshituko la mzee Harken Kalm. “Jacob Matata, yule mpelelezi asiyeshindwa na kitu na mpelelezi hatari kabisa, au unamsema mwingine?” Mzee huyu aliuliza swali hili huku kwa mara ya kwanza uso wake ukionesha kuingiwa na hofu. Jambo hili lilimshangaza sana Bob Sepeto, hakuwahi kuona bosi wake huyu akiwa katika mshangao kama huu. Bob alishawahi kusikia watu wakiliongelea jina la Jacob Matata na kazi zake za hatari, lakini hakudhani kuwa anaweza kuwa hatari kiasi cha kumtisha bosi wake huyu ambaye hajawahi kumuona akiingiwa na hofu.

“Sijui kama ndio huyo, ila sidhani kama anaweza kuwa yeye, maana yeye ni kijana mzuri, nadhifu, na asiyekuwa na dalili zozote za uhatari kama unaoweza kuuhofia wewe, sura yake yaonesha kuwa hajawahi hata kupigana kwa jinsi ilivyo nzuri..” Alisema Regina huku akianza kujisahau kuwa alikuwa mbele ya watu hatari kama hawa. “Shiiit, funga domo lako, mie sijakuambia uanze kutoa sifa za mjinga mwenzio huyo” Alifoka mzee huyo kwa hasira huku akionekana kuchanganyikiwa kusikia jina la mpelelezi Jacob Matata likitajwa katika kambi yake kwa mara ya kwanza. Hii ilikuwa dalili mbaya kabisa kwake, kwani kati ya watu ambao alikuwa anaomba afe bila kukutana nao ni mpelelezi Jacob Matata. Alikuwa anamjua vema kwa sura na vitendo vyake. Lakini hakutegemea kama kwenye kambi yake kungekuja tokea mtu anaemfahamu na kuwa na uhusiano na Jacob Matata.

Mzee Harken Kalm, alisimama na kubonyeza kitufe fulani, mara likatokea kasha fulani. Humo alichambua vitu fulani, kisha akachukua kitu kama sahani bila shaka ilikuwa ni CD kwani alipoiangalia kwa makini alienda nayo mpaka mezani kwake na kukaa kama hapo awali. Hapo aliichukua ile CD na kuiweka kwenye kompyuta iliyokuwa mezani hapo. Baada ya muda picha mbalimbali zikaanza kutokea kwenye sehemu fulani ya ukuta, hii ikiwa ni kazi ya kompyuta iliyokuwa imewashwa. Picha hizo zilikuwa zikija na kutoweka. Ilipofika picha ya Jacob Matata kelele zilisikika sebuleni hapo. “Aaah Jacob Mpenzi nime….” Sauti hiyo iliyotoka kwa Regina ilikatizwa na kofi kali la usoni lililorushwa toka kwa mtu nyuma yake. Aligeuka ili amuone mtu huyo alikutana na ukuta tu. Akabaki anashanga.

Picha hiyo ya Jacob kwa chini yake kulikuwa na maandishi mekundu yaliyosomeka ‘hatari kuliko wote afrika’. Mzee Harken Kalm, kwa kutumia kompyuta hiyo aliikuza ile picha mpaka ikaonekana kama mtu mzima akiwa amesimama. Regina alitabasamu sambamba na Dokta Eve japo yeye alionekana kufanikiwa kuficha furaha yake kwa kuiona picha hiyo ya Jacob. Sasa ilikuwa inaonekana kama Jacob Matata mwenyewe akiwa kasimama ukutani hapo akiwa nadhifu kabisa na tabasamu la mbali usoni kwake.

“Unakubali kuwa mpenzi wako ndio huyu?” Aliuliza mzee Harken Kalm huku macho yake yakiwa yamebadilika na kuwa yanang’ara kwa hasira iliyochanganyika na hofu. “Ndio ni yeye Jacob jamani, hebu muoneni, kweli anaweza kuwa mtu hatari huyu?” Alisema Regina akijaribu kumtetea Jacob Matata.

“Unasikia Bob Sepeto, kama huyu ndiye mtu aneyeongelewa na huyu mshenzi, basi yakubidi sasa hivi uwafuate watu wako na uongeze watu wengine ili kuweza kukabiliana na mtu huyu hatari, huyu ni miongoni mwa wapelelezi ambao Afrika na wapenda haki wake wanajivunia kuwa nae. Nitakupa picha zake, na mimi sitajali kama kama mtamleta hapa akiwa maiti au mzima, ila hakikisha hamumpi nafasi ya kujua siri yangu hii wala mahali hapa akiwa huru. Tafadhali usidanganyike na sura yake hii ya kuvutia, kwani kwa sura hii wengi walimdharau na mwisho wao wote umekuwa mbaya. Ukae ukijua nisingependa kabisa nipambane na mtu kama huyu lakini inanilazimu kwa kuwa sasa kuna kitu anakifuatilia. Amini nakuambia kama tusipomuwahi Jacob atatuwahi sisi, yule ni bianadamu wa ajabu sana”

“Dokta Eve mchukue msichana huyu na umuongeze katika orodha ya watu wa kuuzwa. Hakikisha hapewi nafasi yoyote ya kufanya upuuzi wake?” Alipomaliza kusema hivyo, mzee Harken Kalm alibonyeza kitufe fulani na kupotelea ardhini.

Bob Sepeto aliwaongoza Regina na Dokta Eve kutoka ndani ya jumba hili kwa mtindo uleule aliokuwa amewaleta humo. Wakajikuta tu wako nje. Walipofika eneo lililokuwa na watu na wafanyakazi wengine walishangaa kukuta mzee Harken Kalm akiwa anazungukia maeneo hayo kana kwamba siye waliyekuwa nae sehemu nyingine dakika chache zilizopita
 
HEKAHEKA 11

Bob Sepeto aliwaongoza Regina na Dokta Eve kutoka ndani ya jumba hili kwa mtindo uleule aliokuwa amewaleta humo. Wakajikuta tu wako nje. Walipofika eneo lililokuwa na watu na wafanyakazi wengine walishangaa kukuta mzee Harken Kalm akiwa anazungukia maeneo hayo kana kwamba siye waliyekuwa nae sehemu nyingine dakika chache zilizopita.

* * *

Msonyo alioutoa Bob wakati Jacob anaongea na Regina kwenye simu asubuhi hiyo ulilifikia sikio la mpelelezi Jacob Matata upande wa pili. Jacob alitambua kuwa adui yake alikuwa amefanya namna ambayo angeweza kumsikia wakati wakiongea na Regina, kwa hiyo tayari alikuwa ameshasikia muungurumo wa injini ya boti waliyokuwa wanaitumia. Kule kusonya kulitafsiriwa na Jacob kuwa mtu aliyekuwa amemsimamia Regina wakati akiongea, alikuwa amegundua kuwa Jacob alikuwa anamdanganya Regina kuwa alikuwa akienda kambini hapo kwa usafiri wa gari. Hii ilifanya akili ya Jacob kuchukua uamuzi wa kutoendelea na safari kama alivyokuwa amedhamiria, kwani alishajua kuwa adui zake muda si mrefu wangetanda majini na kuanza kumtafuta.

“Unasikia mzee, naomba ukatie nanga kwenye miti ile pale na uniache hapo wewe urudi” Jacob alisema huku akifungua kibegi chake na kukagua kitu fulani kabla ya kukifunga tena. Mzee yule aliyejitambulisha kwa Jacob kwa jina la Maduka hakuwa na la kupinga. “Kwa nini umeamua kushukia hapo ilhali kambi tuliyokuwa tunaiendea haiko mbali sana toka hapa?” Aliuliza mzee huyo huku akiwa anazungusha usukani wa boti hiyo kuelekea kule alikoomba Jacob waende.

“Kwa hiyo tumekubaliana kuwa utaenda na kuja kunichukua jioni sawa?” Badala ya kujibu swali la mzee Maduka, Jacob aliuliza swali huku wakiwa sasa wanakaribia ufukwe. “Hiyo itakuwa kazi sana, unaonaje kama utaniongezea hela ili nikae hapa nakusubiri mpaka jioni?” Mzee maduka alitoa pendekezo. Jacob hakujibu haraka kana kwamba alikuwa hajasikia. Alikuwa akifanya upembuzi yakinifu juu ya hilo. Sawa, lakini sidhani kama tutaenda wote huko kambini, wewe itabidi ubaki hapa.

Tayari walikuwa wameshafika ufukweni, mzee Maduka alitoa nanga na kuitupa majini. Wote walitelemka. “Kwa vile utakuwa hapa muda mrefu na bahari huwa inabadilika wakati wowote, naona tuivute boti hadi nchi kavu na kisha tuifunike majani kwa usalama wako” Jacob alitoa pendekezo hilo wakati wote wakiwa nchi kavu tayari. Mzee Maduka alijua Jacob anamuonea huruma, lakini Jacob alikuwa ameshahisi kuwa jamaa wangeanza kuzungukia pwani hiyo kwa msako. Hivyo ilitakiwa waifiche boti yao kwa majani ili isionekane kwa urahisi. Kazi hiyo ilifanyika kwa haraka sana mpaka mzee yule akawa anashangaa.

Walipomaliza tu mara walisikia mlio wa boti zikija kwa kasi. “Nenda jifiche kwenye kichaka kile pale, usitoke kwa namna yoyote tafadhali!!!” Jacob aliamuru huku na yeye akienda kujificha kwenye kichaka kingine. Alichukua kibegi chake na kutoa darubini ndogo na kuanza kuangalia boti hizo zilizokuwa zimeenea eneo lote sasa. Darubini hii ilikuwa ndogo lakini ilikuwa ni ya kisasa na yenye uwezo mkubwa sana, pia ilikuwa na uwezo wa kupiga picha pale mtumiaji alipohitaji kutunza kumbukumbu ya matukio anayoyaona kwa mbali sana.

Jacob alijitahidi kadiri alivyoweza kupiga picha za wengi kati ya jamaa hao waliokuwa ndani ya boti hizo ambazo zilikuwa ni aina ya zile ziendazo kwa kasi. Jinsi walivyokuwa wameificha boti yao na namna walivyokuwa wamejificha, ilitosha kabisa kuwafanya wasionekane na watu hawa ambao dhahiri walikuwa tayari kuua. Walikuwa na silaha nzito nzito na za kisasa.

Hali hiyo iliendelea kwa masaa kadhaa mpaka pale hali ilipokuwa shwari kabisa. “Sasa wewe baki hapa ila uwe katika hali ya kujificha mpaka hapo nitakaporudi” Jacob alisema huku akiwa anaweka darubini yake ndani ya kibegi chake. Alienda pembeni kidogo, hapo alitoa bastola mbili, moja aliifutika hapa na nyingine akaifutika kule. Akatoa visu kadhaa na kuvifutika huku na huko na zana kadhaa, darubini na vifaa vingine aliviacha ndani ya kibegi chake hicho. Yote haya aliyafanya sehemu ambayo alijua kuwa Mzee Maduka alikuwa hamuoni. Bila kuaga tena, Jacob huyo akatokomea vichakani.

Sehemu aliyokuwa amekusudia kwenda ni kambi ya Koboyo, hii ilikuwa ni kambi ya uvuvi. Kwa maelekezo aliyokuwa amepewa na Regina juu ya sehemu waliyokuwa wanashikiliwa, Jacob aliamini kuwa kambi hii ingekuwa jirani sana sehemu waliyokuwa wakina Regina. Hivyo alikuwa ameamua kwenda hapo ili akapeleleze machache toka kwa wavuvi kambini hapo kuhusiana na sehemu ambayo Jacob aliamini kuwa ilikuwa ya hatari.



* * *



Baada ya kumtafuta Jacob kwa muda mrefu bila kumuona, wala kuona dalili ya boti eneo lote, Bob Sepeto hakuamini kuwa kweli Jacob hakuwepo maeneo hayo. Aliwaamuru walinzi wengine kurudi kambini huku akituma wapelelezi waende kambi ya Koboyo ili kuangalia kama Jacob alikuwa hapo au angeenda hapo. Baadhi ya walinzi aliwaacha waendelee kuzunguka kando kando ya bahari kuanzia hiyo Bagamoyo mpaka mjini.

Wapelelezi waliokuwa wametumwa na Bob kwenda kambi ya Koboyo walikuwa ni wale askari wake watiifu na aliowaamini katika swala zima la kutumia miili na silaha katika mapambano. Walikuwa wamebeba silaha nyepesi nyepesi tu na hawakuwa katika sare yoyote. Walikuwa wakizunguka kila kona ya kambi hiyo, huku wakijifanya wavuvi au wachuuzi wa kawaida wa samaki.

Mzee huyu na yeye alikuwa amechangamka huku akionekana kuanza kukolewa na pombe. Lakini kwa wenyeji wa eneo hilo siku hiyo walikuwa wakimshangaa kwani hakuwa amelewa katika kiwango walichokuwa wamezoea kumuona akilewa.

Mzee huyo hakuwa ni yule waliyekuwa wakimjua siku zote bali alikuwa ni Jacob Matata ambaye tayari alikuwa ameshajibadirisha sura na kuvaa ya mzee huyu. Alipokuwa ameshafika kambini hapo na kugundua kuwa kulikuwa na walinzi kibao ambao wengi wao walikuwa na sura yake, Jacob alienda nyuma ya choo fulani na kujificha mpaka pale alipokuwa amekuja mzee mmoja. Mzee huyo aliingia chooni ili ajisaidie. Hapo ndipo Jacob Matata akatumia fursa hiyo kumuhadaa na kumpa kipigo bila kufanya makelele yoyote, kipigo hicho kingemchukua mzee huyo masaa kadhaa ili kurudiwa na fahamu.

Kwa kutumia darubini yake Jacob alimpiga picha mzee huyo sehemu ya usoni, kisha huyo akatokomea vichakani tena huku akiwa ameuficha sehemu mwili wa yule mzee. Vichakani huko alitumia dakika kadhaa kabla ya kutoka tayari akiwa ameshajibadirisha sura na kuwa sawa na yule mzee aliyepotewa na fahamu. Alifanya hivyo kwa kutumia vifaa vilivyokuwa kwenye kile kibegi chake kidogo.

Alikaa kambini hapo kwa muda mrefu huku akiwa anauliza hili na lile kwa wenyeji, bila kushukiwa na yeyote. Mara kwa mara alikuwa akigongana na walinzi wa waliokuwa wametumwa na Bob Sepeto, hawakumtambua japo yeye aliwatambua na mara nyingine kufanikiwa kuchukua picha za wengi wao kwa kutumia darubini yake ndogo iliyokuwa na uwezo huo.

Ilipofika jioni tayari alikuwa ameshakamilisha sehemu kubwa ya taarifa alizokuwa akizihitaji. Hakuona sababu ya kuondoka mapema kiasi hicho. Hivyo akaendelea kuwepo hapo ili kuruhusu kigiza kuingia zaidi. Ilipofika saa mbili, Mpelelezi Jacob Matata akaona huo ni wakati muafaka wa yeye kuondoka. Lakini aliona si busara kwake kuondoka hivi hivi.

“Mwanangu naomba ukanisaidie kuvuta mtumbwi wangu, maana nahitaji kwenda kutega nyavu zangu” Jacob alimuambia mmoja wa watu aliokuwa na hakika kuwa alikuwa ametumwa kuja hapo ili kumtafuta. “Na nyie wazee kwa usumbufu, haya twende haraka kwani unaenda kutegea upande gani?” Aliuliza jamaa huyo huku akionesha ishara ya kuwa tayari kwenda kumsaidia mtu aliyedhani kuwa ni mzee kumbe ndiye Jacob Matata ambaye wote walikuwa wakimtafuta.

Jacob aliongozana na jamaa huyo huku akiwa anajiandaa kwa shambulio la ghafla na kali. Alijua kuwa ilitakiwa atoe pigo ambalo halitampa jamaa hata nafasi ya kupiga kelele. Walikuwa tayari wameshafika ufukweni kwenye mtumbwi.

“Haya shika huko na….” Kauli ya jamaa ilikatizwa na pigo kali la kareti toka kwa Jacob. Jamaa hakuwa ametegemea pigo hilo, na kwa kuwa lilipigwa sawasawa toka kwa mtu aliyejua vizuri lilimnyamazisha jamaa huyo milele. Haraka haraka Jacob alimbeba jamaa na kumuingiza ndani ya mtumbwi huo. Humo alimvua nguo zote na kutoa kisu chake. Kwa kutumia kisu hicho, Jacob alimchora jamaa maneno fulani. Baada ya hapo alitoka ndani ya mtumbwi huo na kuanza safari ya kuelekea kule alikomuacha yule mtu aliyekuwa amemkodisha. Saa tatu na nusu ilimkuta Jacob na jamaa yake tayari wakiwa wameshafika kwenye ufukwe ulioko jirani na eneo la kivukoni Dar es salaam.



* * *



“Bob nilikuambia kuwa Jacob Matata si mtu wa kumchukulia mzaha hata kidogo. Ona sasa inaonesha ameshafanya upelelezi wa kutosha hapa kwenye kambi aliyokuwepo bila nyie kujua. Siju watu wako walikuwa wanafanya nini. Sasa ni lazima muongeze ulinzi kwenye ukanda huu, nami nitaongea na marafiki zangu walioko kwenye vyombo vya usalama ili wanisaidie kulinda upande huu” Mzee Harken Kalm aliongea kwa hasira huku ngozi yake ikiwa imebadilika na kuwa nyekundu utadhani nini. Muda huu mzee huyu anaongea na Bob Sepeto mkuu wa walinzi wake, ilikuwa ni saa saba usiku. Hali ndani ya kambi hiyo ilikuwa shwari kabisa. Lakini si kwa upande wa walinzi na wana usalama wote wa kambi hiyo. Kwani dakika chache zilikuwa zimepita tangu pale yule mtu aliyekuwa ameuawa na Jacob na maiti yake kuwekwa kwenye mtumbwi ufukweni mwa bahari ilikuwa imeonekana. Hali hii iliwafanya watu hao wawe katika kutafuta wakidhani Jacob bado alikuwa maeneo hayo. Kilichowatia kiwewe zaidi ni ile salamu waliyoikuta imeandikwa kwenye mwili wa marehemu. Maandishi hayo yalisomeka hivi; ‘Jacob anasema siku zenu zinahesabika’ Kwa kumbukumbu alizokuwa nazo mzee Harken Kalm, hakuwahi kutishiwa na yeyote na wala hakuwa anapenda hiyo itokee. Leo ilikuwa ni mara ya kwaza, tena la kutia aibu ni kutoka kwa mwafrika mwenye umri mdogo, Jacob Matata.

Amri ya kutafutwa Jacob popote pale ilitolewa, huku yeyote ambaye angafanikiwa kumuua iliahidiwa kuwa angezawadiwa kiasi kikubwa cha pesa na mzee Harken Kalm.

Asante kwa kuendelea kufuatilia

Kesho itaendelea
 
Shukran mkuu.
Tuko pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…