RIWAYA FUPI.

RIWAYA FUPI.

Joined
Jul 9, 2016
Posts
62
Reaction score
16
WANDISHI😛AUL BEN MTOBWA.

YEAR:2016

CONTACT:0676-310625

Haki zote zimehifadhiwa hairusiwi kuiga,kunakili au kutumia riwaya hii fupi kwa njia yoyote bila idhini ya heko publishers.

ISNBN 27011992.

SURA YA KWANZA.

John david maganga ni mtoto wa kwanza wa familia ya mzee maganga,alizaliwa kwenye ukoo wa kitajiri na kupewa kila alichihitaji na wazazi wake.kimuonekano john alikuwa ni mzuri wa sura na mcheshi wa tabia hasa kwenye maongezi pia utulivu wake ni moja kati ya sifa ambayo watu wengi waliipenda huku wasichana wakihihuhusudu sana.jonh alipofikisha umri wa miaka kumi na sita aliondokea kuwa na vipaji lukuki ambavyo vilimpa sifa na kutukuzwa sana shuleni na ata mtaani,umbo lake kubwa lililomruhusu kucheza basketball na ata kununuliwa kwa dau kubwa ulaya, wepesi wake na umakini awapo uwanjani ulimfanya ulimfanya aitwe cristiano ronaldo na baadhi ya wasichana.sura na uchangamfu wake ulitosha kabisa kumfanya mwalimu wa sanaa amshawishi kuingia kwenye fani hiyo bila mafanikio.kwenye maukumbi ya harusi napo alishapachoka kwani harusi nyingi aliitwa kama best man kwa malipo mazuri na sifa kemu kemu ambazo alishazichoka.

Baaada ya kufikisha umri wa miaka ishirini na nane john aliingia kwenye ulevi wa bangi,pombe na hasa wanawake na alijua haswaa kuchagua wanawake hao.uzuri wa sura yake na ucheshi uliotosha kumfanya mtuhumiwa yoyote wa kesi ya mauaji asahau kesi hiyo na kucheka siku nzima basi kwake aliutumia vizuri kuwalaghai vimada wa haja.wafanyakazi wa benki,mawakili,wasomi wa vyuo vikuu,madaktari na waigizaji walimpapatikia kwa wingi john.alipofikisha umri wa miaka ishirini na tisa john aligeuka mbogo kwani alibalika kabisa kitabia kutoka kondoo mpaka chui aliondokea kuwa na roho ya kishetania ata wazazi wake wasijue alipoipata alifanya madhambi machafu yasioelezeka katika jamii yupo dada mmoja aliefungua kesi mahakamani kwa madai ya kupigwa picha za utupu na john pindi walipokuwa faragha kisha picha hizo kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, alipoulizwa sababu ya kufanyiwa ivo dada huyo alidai sababu ilikuwa ni kutaka kuachana na john ambaye alikuwa msaliti kwake.kama hio haitoshi john aliwahi kukumbwa kesi yeye pamoja na marafiki zake kwamba walibaka na kulawiti wasichana watatu waliotekwa kwenye jumba la kifahari huko pwani chalinze kesi zote hizo hazikuwa nzito kwa john kwani umaarufu wake ukichanganya na ule wa baba yake ulitosha kumshawishi mpelelezi mwepesi yoyote kupokea hongo na matokeo yake ni ahadi ndefu za tarehe ya kesi hiyo mpaka washtakiwa wakasahau kama waliwahi kuhusishwa na kesi yoyote.
 
Jamani hiyo hadith tangu aug 3 hadi leo du inakatisha tamaa kusoma utafikiri mtu amekuonjesha mchuzi kiganjani
 
Kwa yoyote anmbaye amevutiwa na hii story anitafute watsup,ntampa story yote bila malipo.
 
Back
Top Bottom