princewilly
JF-Expert Member
- Nov 30, 2017
- 259
- 528
- Thread starter
- #21
NYEMO CHILONGANI
BIASHARA YA KIFO
Sehemu ya Kumi
“Nataka twende sehemu.”
“Wapi?”
“Kutembea! Unapenda kukaa hapa tu kwa siku zote tangu umefika?”
“Hapana! Ila sidhani, sijapazoea sana huku.”
“Unaogopa utapotea?”
“Ndiyo!”
Ethan alikuwa akizungumza na Annabel, alitaka kumchukua na kumtoa mtoko huku lengo lake kubwa likiwa ni kutaka kuzungumza naye juu ya kile kilichomfanya kuwa nchini Tanzania. Bado Ethan aliona kulikuwa na ugumu wa msichana huyo kukubaliana naye kwani kila alipojaribu kumchombeza kwa maneno ya haya na yale, ugumu ulionekana dhahiri.
Annabel hakuwa na maamuzi ya maisha yake, alikuwa na umri chini ya miaka kumi na nane, kila kitu kilichotakiwa kuamuliwa maishani mwake kilikuwa chini ya wazazi wake. Japokuwa kipindi hicho wazazi wake hawakuwepo lakini hakutaka kulisahau hilo, hakutaka kuondoka nyumbani hapo.
Bado Ethan alikuwa akimchombeza kwa maneno matamu ya mahaba, alitaka msichana huyo awe mpenzi wake kwanza, alale naye na ndipo ampeleke nchini Marekani kwa ajili ya kucheza filamu ya ngono kama ilivyokuwa imepangwa.
Wanawake wale kumi walikuwa tayari, walijiandaa na wengine kuaga kabisa lakini tatizo likawa kwa Ethan tu. Hakutaka kuondoka nchini Tanzania pasipo Annabel, alimpenda mno msichana huyo na alimhitaji kuliko mtu yeyote yule, kila alipomwangalia, cha zaidi ya yote alihitaji kufanya naye ngono.
“Why are you here?” (Kwa nini upo hapa?) aliuliza askofu Benedicto mara baada ya kufika nyumbani.
“Me?” (Mimi?)
Askofu akakasirika, alijua fika kwamba Ethan alijua kuwa alikuwa akiongea na yeye sasa ilikuwaje aanze tena kumuuliza kama alikuwa akiongea naye. Akaanza kukunja ndita usoni mwake, hakumpenda kijana huyo na alimchukia mno.
“I’m sorry sir, I want to take your daughter out,” (Samahani mkuu, ninataka kumtoa binti yako mtoko) alisema Ethan huku akijivika ujasiri mkubwa.
“Impossible.” (Haiwezekani)
Askofu hakutaka kukaa mahali hapo, moja kwa moja akaelekea chumbani kwake kwa kuamini kwamba mara unapoamua kumuua nyani haukutakiwa kumwangalia usoni. Ethan akanyong’onyea, hakuamini kama baba yake Annabel angekataa kumruhusu binti yake kuondoka naye.
Alimwangalia Annabel usoni, kila alipomwangalia, mapenzi yalizidi kuchomoza moyoni mwake kiasi kwamba kuna wakati alijiona kutokujiweza kwa msichana huyo, aliamua tu kumchukua na kuwa naye huku lile lengo la kutaka kumpeleka nchini Marekani kwa ajili ya kuigiza filamu za ngono aachane nalo.
“Naomba unisamehe,” alisema Ethan.
“Umenifanyia nini kibaya?”
“Hakuna! Ila naomba unisamehe.”
Moyo wa Ethan ulikuwa kwenye maumivu makali mno, kutokana na mapenzi makubwa yaliyougubika moyo wake, hapo ndipo alipogundua kwamba alifanya kosa kubwa kutaka kumchukua Annabel na kumpeleka nchini Marekani kuigiza filamu zile za kikubwa.
Alijiona mkosaji na ndiyo maana wakati huo aliamua kumuomba msamaha msichana huyo kwa kile alichotaka kukifanya japokuwa hakumuweka wazi ni kitu gani.
“Utarudi Marekani?” aliuliza Ethan.
“Kurudi? Mmmh! Sijajua, ila sijui kama nitarudi, nitataka kukaa na wazazi wangu zaidi,” alisema Annabel.
Ethan hakutaka kurudi nchini Marekani peke yake, mtu aliyekuwa akimhitaji kurudi naye alikuwa Annabel tu. Kila siku akawa mtu wa kufika nyumbani hapo kwa ajili ya kumuona msichana huyo na kuzungumza naye mengi.
Japokuwa siku za nyuma askofu alikuwa akimchukia sana Ethan lakini mwisho wa siku akajikuta akimzoea kijana huyo na hatimaye chuki kuanza kupotea moyoni mwake. Wakaanza kukaa chini na kuzungumza mengi huku kila mmoja akijaribu kumficha mwenzake kile kilichokuwa kikiendelea katika maisha yake, yaani askofu akimfichana Ethan kama alikuwa askofu wa Kanisa la Kiroma huku kijana huyo akificha kazi aliyokuwa akiifanya kipindi hicho.
“Ninataka kumfanya Annabel kuwa mwanamke mwenye furaha kuliko wote duniani,” alisema Ethan huku akitoa tabasamu kubwa.
“Nyie vijana wa sasa hivi hamuaminiki kabisa.”
“Kwa nini tusaminike? Yaani hata wewe huniamini?”
“Hahaha! Siwezi kukuamini hivihivi.”
“Unataka nifanye nini ili uniamini?”
“Uanze kwenda kanisani.”
“Hahaha!”
Walizungumza kama marafiki, walizoeana mno na wakati mwingine walitaniana hapa na pale. Ethan alijisahau kabisa, akasahau kama alitumwa kwa ajili ya kuwachukua wanawake na kuwapeleka nchini Marekani, kwake, kile alichokuwa akikifikiria kwa kipindi hicho ni mapenzi tu.
Kutokana na ukaribu na familia hiyo, kila mmoja akamzoea Ethan kiasi kwamba hakukuwa na mtu aliyekuwa na hofu naye tena. Kwa kuwa alizoeleka, hivyo alichokifanya ni kuendelea kumsisitizia Annabel jinsi alivyokuwa akimpenda na kumuhitaji maishani mwake.
Alikataa na kukataa lakini mwisho wa siku akaona kama usumbufu hivyo kukubaliana naye na hivyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi. Ilikuwa ni siri kubwa, wazazi hawakujua chochote kile, walifanyiana mambo ya chumbani kila muda ambao wazazi hao hawakuwepo nyumbani hapo.
Wazazi walipokuwepo, waliishi kama kaka na dada kitu kilichowatia upofu wazazi hao. Japokuwa aliaminika sana lakini Ethan hakuwa mtu wa kulala nyumbani hapo, alikuwa akifika asubuhi na kuondoka usiku, kurudi hotelini na kucheza kamari, mchezo aliopenda sana kuucheza kipindi hicho.
*****
“Ninataka mniletee Ethan mahali hapa!” ilisikika sauti ya mwanaume mmoja kutoka ndani ya nyumba moja ya kifahari.
“Sawa.”
“Ninataka mkamilishe kila kitu, ikiwezekana, mmuue kama tu ataleta ubishi,” alisikika mwanaume huyoi.
“Hakuna tatizo mkuu.”
Yalikuwa ni mangezi baina ya bwana Cook na vijana aliokuwa amewaita ndani ya nyumba yake. Alichanganyikiwa mno, biashara zake zilisimama kwa muda. Uchumi wake mkubwa ulitegemea biashara ya ngozi aliyokuwa akiiifanya, wasichana waliokuwa wakiletwa na kukataa ndiyo haohao ambao ngozi zao zilichunwa na kupelekwa nchini China.
Alichanganyikiwa, alijiona kama akikaribia kufilisika. Kijana wake wa kazi ambaye alimtuma nchini Tanzania, alizamia, kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu hakuwa amerudi nchini Marekani, mbaya zaidi, hakuwa akiwasiliana naye kama alivyofanya wakati alipokuwa akienda katika nchi nyingine.
Alikuwa na hasira mno, alichohisi ni kwamba Ethan alitaka kuachana na biashara hiyo kitu ambacho hakutaka hata kukisikia kwa kuona kwamba ni lazima kijana huyo angekwenda kutoa siri juu ya biashara ile iliyokuwa ikiendelea.
Hakutaka hilo litokee, alikuwa radhi kulizuia kwa nguvu zote. Alichokuwa akikitaka mahali hapo, huyo Ethan aletwe kwake ili afanye uamuzi mmoja, kama kumuua au kumuonya kwa kile alichokuwa akikifanya.
“Kwa hiyo?” aliuliza kijana mmoja.
“Mmuue hukohuko.”
“Sawa mkuu!” alisema kijana mmoja na kuanza kuondoka.
“Subirini kwanza. Au kama vipi mleteni huku nimuue kwa mkono wangu! Wakati wa kuja huku, tumieni meli ya mizigo ya Mediteranian Cargo,” alisema bwana Cook.
“Hakuna tatizo!”
Kila kitu kikaanza kufanyika, vijana wale wakapatiwa dola laki tano kwa ajili ya safari yao ya kwenda nchini Tanzania ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kumtafuta Ethan na kwenda naye nchini Marekani.
Hawakujua wangempata wapi lakini kwa kuwa walijua kwamba Ethan alikuwa miongoni mwa watu waliohusudu sana michezo ya kamari, wakataka kuhakikisha wanatembelea sehemu zote za michezo hiyo na kumkamata.
Hawakutakiwa kurudi nchini Marekani pasipokuwa na Ethan mikononi mwao, walitakiwa kufanya juu chini mpaka mwanaume huyo anapatikana na kupelekwa nchini Marekani katika mikono ya bwana Cook.
Mawasiliano na Meli ya Mediteranian Cargo iliyokuwa Mombasa yakaanza kufanyika, mara baada ya Ethan kutekwa, hakutakiwa kupelekwa Marekani kwa ndege, alitakiwa kubebwa kwenye meli kiusalama zaidi.
Hilo halikuwa tatizo, nahodha alipopewa taarifa hiyo tu, akageuza meli hiyo ya mizigo na safari ya kuelekea nchini jijini Dar es Salaam kuanza. Kwa ujumla, kila kitu kilikamilika, kutokana na fedha nyingi alizokuwa nazo, alifanya chochote alichokitaka, hata baadhi ya viongozi wa serikali ya Marekani walikuwa chini yake.
*****
Hakukuwa na kitu alichokuwa akikipenda katika maisha yake kama kucheza kamari. Hakuanza kipindi hicho, tangu alipokuwa kijana mdogo aliyeishi katika mtaa wa kimasikini wa Manhattan, Ethan alikuwa mtu wa kushinda vijiweni na kucheza kamari tu.
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake, haikujalisha kama alikuwa na fedha au hakuwa nazo, alifilisika au la, kitu alichokuwa akikifanya pasipo kujihukumu moyoni mwake kilikuwa ni kucheza kamari tu.
Kila nchi aliyokwenda, kitu cha kwanza kilikuwa ni kupanga hoteli zilizokuwa na cassino ili humo ndani aweze kucheza kamari kama kawaida yake. Kwenye kamari hizo, alikuwa akila sana lakini kuna wakati mwingine aliliwa mpaka kuhisi kufakufa.
Hapo New Africa hotel alipofikia, kulikuwa na ukumbi mkubwa ambao ulitengwa kwa ajili ya cassino, ndani yake kulikuwa na michezo mbalimbali ya kamari. Alipofika hotelini hapo siku ya kwanza, kitu alichokifanya hata kabla ya kula, ni kwenda cassino na kuangalia ni jinsi gani watu walikuwa wakicheza kamari hasa kwa kutumia karata ambao Wazungu waliuita Pokker.
Alijitahidi kucheza, alionekana kama mmoja wa vijana waliozaliwa na kipaji cha kucheza mchezo huo tu. Alipofika ndani ya ukumbi huo tayari kwa kucheza mchezo huo, aliwashinda wengi na kujikusanyia kiasi kikubwa cha fedha.
Kwa kipindi kifupi tu akajikuta akiwa mtu maarufu ndani ya cassino hiyo hali iliyomfanya kujiona kuwa bingwa wa mabingwa na kubatizwa jina la Mr Pokker. Wacheza kamari wakaanza kupeana taarifa kwamba kulikuwa na mtu mmoja ambaye alikuja katika Hoteli ya New Africa na kisha kuzama katika cassino iliyokuwa mahali hapo na kucheza kamari, alikuwa moto wa kuotea mbali hivyo mabingwa wengi kukusanyika hotelini humo kuona makali ya huyo mtu aliyekuwa gumzo.
“Anajua kucheza sana Pokker, kuna wengi amewashinda,” alisema jamaa mmoja simuni, alikuwa akizungumza na rafiki yake.
“Anajua kweli?”
“Ni hatari aiseee...unamjua Muingereza aliyetutesa yule kwenye kamari, Phillip Walker?”
“Ndiyo!”
“Amemla!”
“Duuh!”
“Unamjua Mc Regard, yule Mzungu kutoka Belgium?”
“Ndiyo!”
“Amemla!”
“Acha bwana!”
“Ni hatari sana.”
“Sasa hawezi kuja Las Vegas akutane na wakali wake?”
“Ngoja, nitazungumza naye.”
Watu waliotajwa hapo juu walikuwa hatari katika mchezo wa kamari, walijua kucheza kamari na kuweka gumzo kwa watu wengi waliokuwa wakienda katika Cassino mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kucheza kamari.
Hawakuwa wakiishi nchini Tanzania, walikuwa mabaharia ambao kila siku walisafiri kwa meli, walipofika nchi yoyote ile, kazi yao ilikuwa ni kucheza kamari kisha mizigo iliposhushwa au kupandishwa, waliendelea na kazi yao.
Waliwala fedha watu wengi, walikuwa Wazungu wenye uwezo mkubwa wa kucheza kamari, walijitengenezea majina na kuonekana hatari miongoni mwa wacheza kamari mbalimbali mpaka wengi kuogopa kucheza nao.
Pamoja na uwezo wao mkubwa wa kucheza kamari, kwa Ethan hawakufua dafu, wote hao walipokea vipigo mfululizo hali iliyowafanya kupoteza zaidi ya dola milioni moja kila mmoja.
Baada ya kucheza sana kamari na kujitengenezea jina kubwa ndani ya wiki mbili hapo ndipo alipoamua kuhama na kuhamia katika Cassino ya Las Vegas ambapo kuliaminika kuwa na wakali wa kucheza kamari.
Alipofika huko, bado moto wake ulikuwa uleule, aliendelea kuwala fedha zao na kujikuta akiwa biashara, yaani kila alipokuwa akicheza, watu walimpandia hela na kusema kwamba angeshinda, kweli alifanya hivyo.
Vijana wa bwana Cook walipofika nchini Tanzania, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kwenda katika kumbi za starehe kwa ajili ya kumtafuta Ethan kwani kwa jinsi walivyojua ilikuwa ni lazima kumkuta huko kwa kuwa ndiye alikuwa miongoni mwa watu waliopenda starehe katika vijana wote wa bwana Cook.
Walitembelea katika hoteli kubwa kwa lengo la kumtafuta lakini hawakuweza kumpata. Ndani ya wiki mbili nzima kazi yao kubwa ilikuwa ni kwenda huku na kule katika kumbi na hoteli kubwa lakini hawakuweza kumpata mwanaume huyo.
Kikafika kipindi wote watatu wakaonekana kukata tamaa, hawakuona kama wangeweza kumpata Ethan aliyekuwa amepotelea nchini Tanzania. Kuna kipindi wakahisi kwamba inawezekana Ethan hakuwepo nchini Tanzania hivyo walijadiliana kwenda sehemu nyingine kumtafuta hasa katika nchi jirani kama Kenya na Uganda.
“Mnaonaje?” aliuliza Thorn, mmoja wa vijana waliokuwa wametumwa.
“Nadhani twendeni Kenya, haiwezekani tukamkosa sehemu za starehe na wakati tunajua jinsi Ethan alivyo,” alisema Stephen.
“Sawa! Haina tatizo! Twendeni huko hata kesho!”
“Hebu subiri kwanza!” aliingilia Bruno.
“Una wazo?”
“Ndiyo! Kwa nini tusiendelee kumtafuta hapahapa?”
“Ila tumemkosa, na wewe umeona!”
“Bado! Kuna sehemu nyingi tunatakiwa kwenda,” alisema Bruno.
“Hatujakuelewa!”
“Kipi tena hamjanielewa hapo? Kwani tumemaliza sehemu zote?”
“Bado ila......”
“Jamani! Wote tunamjua Ethan kwamba alikuwa mtu wa kupenda starehe, si ndiyo?”
“Ndiyo!”
“Ila mnakumbuka kwamba hata kucheza kamari Ethan alikuwa balaa?”
“Ndiyo! Tena umenikumbusha, nahisi tukianza kumtafuta kwa staili hiyo itakuwa safi,” alisema Thorn.
“Hebu tujaribuni!”
Hawakuwa na jinsi, walikubaliana kwamba waendelee kumtafuta Ethan kama mcheza kamari. Walichokifanya ni kuanza kutembelea kumbi mbalimbali hasa kulipokuwa kwa wacheza kamari wengi kwa lengo la kumpata mtu waliyekuwa wakimtafuta.
Mpaka kufikia kipindi hicho, tayari mwezi ulikuwa umepita lakini bado hawakufanikiwa kumpata Ethan jambo lililowakera sana. Waliwasiliana na bwana Cook na kumwambia kile kilichokuwa kikiendelea kwamba walikuwa na wazo la kumtafuta katika kumbi mbalimbali za kamari kwani walijaribu kwenda kwenye kumbi za starehe lakini hawakufanikiwa kumpata.
Bwana Cook akakubaliana nao hivyo kuanza kwenda huko. Haikuwa kazi kubwa, usiku hawakulala, muda wao wa kulala ulikuwa mchana, ulipoingia usiku, walikuwa na kazi ya kumtafuta Ethan tu.
Baada ya kukaa kwa kipindi cha miezi mwezi mmoja ndipo waliposikia kwamba kulikuwa na kumbi mbili tu ambazo zilikuwa na wacheza kamari wakubwa, kulikuwa na ile iliyokuwa New Africa na Las Vegas, hivyo wakaanza kwenda huko kwa kuanzia New Africa.
Kabla ya kuulizia, wakaanza kupita katika kila meza ya wacheza kamari wa mchezo wa Pokker na kuanza kuwaangalia wachezaji. Kila mmoja alikuwa makini kabisa kuwaangalia na katika meza kumi na nane zilizokuwa ndani ya cassino hiyo, Ethan hakuonekana kitu kilichowafanya kuuliza.
“Ethan! Who is he?” (Ethan! Ndiye nani?) aliuliza mwanaume mmoja aliyekuwa ameulizwa kuhusu Ethan.
Hapo ndipo walipoanza kumwambia kuhusu mwanaume huyo, walifafanua sana, jinsi alivyokuwa na utaalamu wake wa kucheza kamari lakini mwisho wa siku mtu huyo aliwaambia kwamba hakuwa akimfahamu kwani hapo kulikuwa na wacheza kamari wengi waliokuwa wakifika, hivyo kumfahamu ilikuwa ngumu.
“Tufanye nini?”
“Hebu tuwaulizeni wengine.”
Hapo ndipo wakaanza kuwauliza watu mbalimbali waliokuwa ndani ya cassino hiyo. Jina walilokuwa wakiuliza lilikuwa Ethan kiasi kwamba ilikuwa ngumu sana kwa wengine kumfahamu.
“Unamuulizia mtaalamu wa kucheza kamari hapa?”
“Ndiyo!”
“Unataka kucheza?”
“Kama yupo mkali!”
“Unaweza nikuwekee dau?”
“Kiasi! Kuna wakali kwanza hapa?”
“Wakali wamepungua, wamehamia Las Vegas, kuna mmoja anaitwa Mr Pokker, huyo ndiyo balaa!” alisema mwanaume huyo.
“Hebu kwanza nianze na hawa, nikiwashinda utanipeleka kwa huyo Mr Pokker,” alisema Thorn na kupelekwa kwenye meza iliyojaa wacheza kamari, akapanda dau la dola elfu kumi kwanza kupima upepo.
Je, nini kitaendelea?
Sent using Jamii Forums mobile app