mng'oa kucha
Senior Member
- Jul 31, 2013
- 150
- 179
Katika zoezi la utoaji pasi mpya za kielektroniki ofisi ya uhamiaji wanaelekeza kuambatanisha vitu kadhaa ikiwemo cheti cha kuzaliwa, kuna mtaalamu mmoja ambaye anahakiki vyeti kwa kuviangalia na ukimpa cheti atakwambia "hii siyo sahihi ya mama Kaisi" kwa hiyo atakuamuru uende RITA ukatafute cheti kingine kama umezaliwa baada ya mwaka 80 ila kama umezaliwa kabla ya mwaka themanini atakuelekeza ukaape kwa mwanasheria.
Swali langu ni hivi vyeti vyote vilipatikana ofisi ya RITA na watu wamekuwa wakivitumia katika maisha yao yotee kumbe kuna afisa ambaye alikuwa anaghushi sahihi ya "mama Kaisi" ambaye hakujulikana kwa miaka yote ofisi za Rita mmechukua hatua gani?