RITA boresheni mfumo wenu wa uhakiki

RITA boresheni mfumo wenu wa uhakiki

jajawajaja

Member
Joined
Jul 3, 2020
Posts
5
Reaction score
104
Kwa sasa inafahamika kuwa wanafunzi wengi waliomaliza masomo yao ya elimu ya kidato cha sita wanatakiwa kuomba mkopo kupitia bodi ya mkopo lakini kabla ya kufanya hivyo unapaswa kuhakiki cheti chako cha kuzaliwa kupitia MFUMO WA RITA.

Hapo ndipo hekaheka inapoanzia, kwanza unapaswa kusubiri siku 10 ndio upate majibu yako ya uhakiki, mbaya zaidi majibu yanaweza kurudi eidha kuna baadhi ya taratibu umekosea unapaswa kutuma tena, hapo tena siku 10 zingine omba Mungu iwe vizuri, ikiwa vibaya una siku 10 zingine sasa tukumbuke bodi ya mkopo wametoa siku 30 tu za kuomba mkopo, huoni hapo unasababisha kukosa mkopo kwa mtoto wa huyu wa masikini.
 
Kama siku ni 10 basi kuna watanzania wengi watakosa haki yao ya mkopo.
 
Kwanini wasifanye kama TCU hata siku moja haipiti...
 
Kwa sasa inafahamika kuwa wanafunzi wengi waliomaliza masomo yao ya elimu ya kidato cha sita wanatakiwa kuomba mkopo kupitia bodi ya mkopo lakini kabla ya kufanya hivyo unapaswa kuhakiki cheti chako cha kuzaliwa kupitia MFUMO WA RITA.

Hapo ndipo hekaheka inapoanzia, kwanza unapaswa kusubiri siku 10 ndio upate majibu yako ya uhakiki, mbaya zaidi majibu yanaweza kurudi eidha kuna baadhi ya taratibu umekosea unapaswa kutuma tena, hapo tena siku 10 zingine omba Mungu iwe vizuri, ikiwa vibaya una siku 10 zingine sasa tukumbuke bodi ya mkopo wametoa siku 30 tu za kuomba mkopo, huoni hapo unasababisha kukosa mkopo kwa mtoto wa huyu wa masikini.
Sio 10 mkuu, hizo wanasema tu uhakika ni 15 kwahiyo wanafunzi wengi watakosa fursa hii kwasababu yao.
 
Back
Top Bottom