VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Katika hali ya sintofahamu,Ripoti mbili zilizotua Makao Makuu ya CCM-Dodoma kutoka Jimbo la Uchaguzi la Kalenga zinakinzana. Taarifa za kiitelijensia kutoka Makao Makuu zinaonesha kuwa kuna Ripoti toka kwa Timu ya Kampeni Jimboni humo na ile ya Timu ya Watafiti wa Kisiasa iliyotumwa Kalenga. Ripoti husika zinakinzana kwa kiasi kikubwa.
Wakati Ripoti ya Timu ya Kampeni ikidai kuwa CCM inakubalika na ushindi unanukia,Ripoti ya Washambuzi inaonesha kuwa hali si ya kuridhisha na hivyo chama kinaombwa kuongeza nguvu Kalenga. Baada ya Ripoti hizo za awali kutua chamani, hali ya taharuki imetanda katika Ofisi za chama hapa Dodoma.
Ili kuujua ukweli,chama kinapanga kutuma Timu Huru kurudi na hali halisi ya huko. Nitawajuza kitakachojiri
Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Dodoma)