..kama mtakumbuka kuna taarifa za askari wetu wawili kupoteza maisha na wengine ishirini na sita kujeruhiwa huko DRC ktk shambulizi la kushtukiza.
..habari za mwanzo ziliekea kuwatuhumu waasi wa ADF kwa shambulizi hilo. Taarifa zilizotolewa na Reuters hivi karibuni zinasema wachunguzi wa UN wametoa ripoti wakidai kwamba askari wetu waliuawa na wanajeshi wa DRC.
..kuna madai kwamba walifanya hivyo baada ya kupewa taarifa kuwa askari wa Tanzania wanashirikiana na waasi wa ADF.
..Taarifa hizi zinachanganya. Askari wetu wametumwa kwenda kuwalinda wananchi wa DRC dhidi ya mashambulizi ya vikundi vya waasi/magaidi. Sasa imekuwaje tena watuhumiwe kushirikiana na kikundi cha waasi/magaidi?
..Pia Tanzania iko kusaidia jeshi la DRC ambalo bila shaka limeelemewa na utitiri wa vikundi vya magaidi. Sasa inakuwaje jeshi tulilokwenda kulisaidia linaua askari wetu? Ni majuzi tu, mamia ya askari wa Congo walihitimu mafunzo yao hapa Tanzania. Sasa leo tumegeuka maadui wao?
..Je, kuna askari wetu wamekosa nidhamu na uzalendo na kwenda kunyime na kile walichotumwa kwenda kufanya DRC. Kama ni hivyo jeshi limechukua hatua gani?
..Je, jeshi la DRC liliwashambulia askari wetu kimakosa? Kama ni hivyo hatua gani zimechukuliwa na jeshi na serikali ya DRC?
..Hivi muda wote mpaka UN wanatoa taarifa, JESHI letu ilikuwa halijafanya uchunguzi wake na kufahamu askari wetu walishambuliwa na nani huko DRC? Kwanini umma wa wa-Tz haujapewa taarifa zozote mpaka tusome kwenye vyombo vya habari vya nje?
cc Moshe Dayan, Nyenyere, Kichuguu, MK254, Echolima, MsemajiUkweli, Pasco, Manyerere Jackton, Ritz, MsemajiUkweli, Nguruvi3