Ripoti ya siri ya kushindwa kwa CCM Arumeru yavuja

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Source mtanzania

*Ni ya kushindwa uchaguzi Arumeru Mashariki
*Yabaini siri ya Sioi kubwagwa, NEC yakerwa
*Yadai alikuwa akitamka majina ya vijiji isivyo
RIPOTI ya siri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhusu sababu za chama hicho kushindwa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha, imevuja.

Ripoti hiyo, iliwasilishwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC), iliyofanyika mjini Dodoma hivi karibuni, lakini baadhi ya wajumbe walipotaka kuichambua, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alikataa.

Pamoja na mambo mengine, ripoti hiyo, imeainisha sababu mbalimbali za kushindwa, ikiwa ni pamoja na utekelezaji hafifu wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho na kuwapo kwa ahadi lukuki zisizotekelezeka.

“Sababu nyingine, ni aliyekuwa mgombea wa CCM katika uchaguzi huo mdogo, Sioi Sumari, kutofahamika kwa wapiga kura wake na alikuwa hafahamu hata majina ya vijiji.

“Sababu nyingine ni suala la ardhi ambalo vijiji vingi vya Arumeru vina migogoro na wawekezaji wanaomiliki mashamba makubwa, huku wananchi wakiwa na uhaba wa ardhi,” ilisema sehemu ya ripoti hiyo

Ripoti hiyo, ilisema licha ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Goodluck Ole Medeye, kufafanua hatua zinazochukuliwa na Serikali, bado wananchi walidai hatua hizo zimechelewa na kuhoji kwa nini maelezo hayo yalitolewa wakati wa uchaguzi.

“Sababu nyingine ni kuhusu kitendo cha Serikali kuchelewa kuingilia kati mgogoro katika shamba lililopo Kata ya Seela Sing’isi, ambako yaliibuka mapambano na kusababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha.

“Wananchi waliendelea kuwa na chuki na Serikali, hali ambayo katika uchaguzi mdogo wa ubunge walipiga kura za hasira dhidi ya CCM.”

Ripoti hiyo, inabainisha sababu za CCM kushindwa katika uchaguzi huo, kuwa ni suala la ardhi, ambalo vijiji vingi vina migogoro na wawekezaji wakubwa, wanaomiliki mashamba, huku wananchi wakiwa na uhaba wa ardhi.

“Hata hivyo pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Goodluck Ole Medeye, kufafanua hatua zinazochukuliwa na Serikali, bado wananchi walidai hatua hizo, zimechelewa na wakihoji kwa nini maelezo hayo yametolewa wakati wa uchaguzi huu.

“Kwa mfano, katika eneo la Kata la Seela Sing’isi, ambako kuna shamba kubwa la mwekezaji, huku wananchi wengi wakikosa maeneo ya kulima hata kusababisha malalamiko na mapambano kati ya mwekezaji wa wananchi.

“Mapambano ambayo baadhi ya wananchi wamepoteza maisha na Serikali haijaingilia kati kikamilifu kutatua mgogoro huo.”

Ripoti hiyo, ilisema: “Wananchi waliendelea kuwa na chuki na Serikali, hali ambayo katika uchaguzi mdogo wa ubunge, walipiga kura za hasira kwa CCM. Kwa tatizo hilo, CCM ilipata kura 792 wakati CHADEMA walipata kura 2,100, zaidi ya kura 1,308 katika kata hiyo.”

Sababu nyingine ni barabara nyingi za vijijini kutopitika kwa urahisi kutokana na ubovu.

Ripoti hiyo, ilibainisha mgawo wa umeme nchini, uliendelea kuathiri shughuli mbalimbali za wananchi. Kipindi chote cha kampeni, umeme ulikuwa unakatika mara kwa mara, ingawa TANESCO haikuwahi kutangaza rasmi kuwa kuna mgawo.

“Katika baadhi ya maeneo wananchi walilalamika kuwa huduma za kijamii, hazitolewi kwa wakati na kwa kiwango isipokuwa tu wakati wa uchaguzi.

“Mfano ni kisima cha majisafi kilichopo Tengeru mjini (Sokoni) ambacho kilikuwa hakitoi huduma ya uhakika, lakini wakati wa kampeni, maji yalifunguliwa na yakaanza kutoka na wananchi kupata maji.

“Vitendo vya wapinzani, hususan CHADEMA waliohamasisha wafuasi wao, hasa vijana kufanya vurugu na kutoa vitisho kwa watu wanaoiunga mkono CCM, ziliwatisha na kuwafanya wananchi wahofie usalama wao na mali zao na hivyo baadhi yao kutojitokeza kwenda kupiga kura.

“Aidha, chama hicho kilitumia helikopta siku ya kupiga kura wakidai wanatembelea vituo vya kupigia kura, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria za uchaguzi, kwa kuwa helikopta ilikuwa na bango lenye picha ya mgombea wake, kama ishara ya uhamasishaji na alama ya chama kushawishi wapiga kura.

“Chama hicho pia kilifanya vitendo vya kununua na kughushi shahada za baadhi ya wapiga kura kwa kuondoa picha ya mhusika na kubandika picha ya mamluki walioletwa kutoka nje ya jimbo na ambao walitumia kupiga kura.

“Kama ilivyokuwa kwa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, uchaguzi huu umebainisha wazi wazi makundi kadhaa makubwa ambayo yako mbali na CCM, kama vile vijana, kundi la wasomi na kundi la baadhi ya madhehebu ya dini.

“Aidha, suala linaloonekana kujirudiarudia katika uchaguzi ni baadhi ya Wafanyakazi wa Serikali kutounga mkono CCM na badala yake kushabikia upinzani.

“Madai yao ni kwamba bado Serikali haiwajali katika stahili zao za kazi. Hili lilionekana pia Arumeru Mashariki kwa watendaji wa Serikali za Mitaa na vijiji, hasa walimu.

“Katika uchaguzi huu kulikuwa na makundi ya wanachama kugawanyika ambayo yaliendelea kuathiri wakati wa kampeni.

“Kundi la kwanza lilitokea kabla ya kura za maoni wakati wagombea walipochukua fomu, walipoona ndugu Sioi Solomon Sumari amechukua fomu walianza kupinga kwa madai kuwa alikuwa na tamaa ya mapema mno, kwani kuchukua kwake fomu kulitafsiriwa kuwa ni kinyume cha desturi za Wameru.

“Walidai kuwa, wakati huo ulikuwa ni wakati mara baada ya kifo cha baba yake mzazi, ambao muda wa kumaliza msiba au matanga ulikuwa bado haujatimia.

“Hii ilisababisha hata wakati wa kampeni, baadhi ya watu hawakufurahishwa, hivyo wakanuna na kutegemea wengine waliochukua fomu ambao ni ndugu William Sarakikya na ndugu Elishilia Kaaya kwamba wangefaa kama wangeteuliwa na chama baada ya kura za maoni.

“Kundi la pili lilitokea baada ya kura za maoni. Mgawanyiko wa kushabikia wagombea walioingia kwenye kura za maoni kuwa kila mwanachama au mpiga kura alimchagua anayempenda.

“Mgawanyiko huu ulisababisha wakati wa kura za maoni kutopata mshindi aliyevuka zaidi ya nusu ya kura za maoni na baadaye kamati kuu ikaamua kurudiwa kura za maoni kwa wagombea wawili.

“Ndugu William Sarakikya na Ndugu Sioi Solomon Sumari, ambaye ndiye aliyeteuliwa. Matokeo hayo yakakuza manung’uniko ndani ya chama na kwa baadhi ya wananchi wakidai kuwa ushindi wake ulitokana na rushwa, kitendo kilichosababisha mashabiki wake wengine kukamatwa na vyombo vya dola kwa vitendo hivyo.

“Yalikuwepo madai mengi ya wananchi kwamba, mgombea wa CCM hakuwa chaguo la wana Arumeru Mashariki, bali lilikuwa chaguo la baadhi ya viongozi wa kitaifa na mkoa.

“Hawakufurahishwa na hilo, kwani wana Arumeru Mashariki wanadai walikuwa na chaguo lao, yaani Elishilia Kaaya au William Sarakikya ambalo halikuzingatiwa katika uteuzi, kuwa kulikuwepo na sababu ya matumizi ya fedha za rushwa kwenye kura za maoni.

“Walisema, nguvu hiyo ya fedha ilitumika sana kwa ndugu Sioi Solomoni kuliko wagombea wenzake. Madiwani wa Kata za Koanrua, Seela Singisi, Maji ya Chai, Poli na Koaranga walionyesha waziwazi wanamuunga mkono na kumtegemea Elishilia Kaaya kama angeteuliwa kugombea.

“Aidha, tegemeo la pili, baada ya kurudia kura za maoni walitegemea kijana wao, William Sarakikya angeshinda na kuteuliwa, lakini akazidiwa pia na nguvu ya fedha za mgombea Sioi Sumari, aliyeteuliwa, vitendo hivyo havikuwapendeza.

“Kitendo cha Elishilia Kaaya kutofika kwenye kampeni, kilitafsiriwa kuwa aliendelea kununa na kutomuunga mkono mgombea huyo wa CCM.

“Kwa William Sarakikya kukosa ushindi kwenye kura za maoni za marudio, alidaiwa alipandikiza ubaguzi wa kisiasa kati ya Meru ya Magharibi na Meru ya Mashariki, kwa maeneo ya Akheri na Nkoaranga.

“Kitendo chake hicho kilileta athari katika matokeo kwenye kata hizo, kwani wapiga kura hawakutoa kura nyingi kwa CCM. Madai zaidi yaliyopo ni kwamba ndugu Sarakikya alipandikiza chuki kwa kina mama kwa kuwaambia kuwa hawana uwezo wa kuzaa kiongozi isipokuwa ukoo wa Sumari.

“Ushawishi huo wa chuki ulifanya wanawake wengi wakaamua kwa hasira wampe kura kijana Joshua Nassari kwa kuwa anatokea maeneo yao.

UDHAIFU WA SIOI SUMARI

Kuhusu udhaifu wa Sumari, ripoti hiyo ilisema: “Mgombea wetu Sioi Sumari alionyesha kuwa na upungufu ufuatao: Kwanza, alikuwa hafahamiki kwa wapiga kura wake, pili alikuwa hafahamu hata majina ya vijiji.

“Katika baadhi ya maeneo alifika na kutamka majina ya maeneo tofauti na mahali husika. Kwa mfano:- alipofika kijiji cha Ngarananyuki yeye alitaja Leguruki, alipofika kijiji cha Kwaugoro, alikitaja Songolo na katika kutaja Wilaya ya Arumeru, alitaja mkoa wa Arumeru.

“Aliendelea hivyo katika vijiji vingine. Tatu, uwezo wake katika kujieleza ulikuwa mdogo, haya yote yalithibitisha lile lililokuwa linasemwa na wananchi kuwa si mwenyeji wa Arumeru na wala haijui Meru.

“Alilalamikiwa pia kuwa katika mikutano mbalimbali alionyesha kutojali hata kupungia mkono wananchi, hata aliposhauriwa na viongozi katika timu ya kampeni kwamba ajitahidi kuyafahamu majina ya maeneo na anapokuwa katika hadhara awapungie mikono wananchi, hakujali wala kuzingatia.

“Pamoja na juhudi zilizofanywa na UVCCM makao makuu ya kuwahamasisha vijana jimboni lakini bado vijana wengi katika Jimbo la Arumeru Mashariki, walionekana kukosa mwelekeo wa kumuunga mkono mgombea wetu, japo alikuwa kijana mwenzao,” ripoti hiyo ilieleza.
 
Duh mkuu una gazeti au ni dondoo za StarTV? Weka habari yote basi hapa
 
CCM wakae wakijua kuwa hiki sio kizazi cha kuwapa fulana na ubwabwa ukupata kura.Watanzania wa leo,wanajua haki zao.
 
Hata hizi sababu wamezichakachua ccm wanadai eti sioi alikuwa hawezi kutaja ipasavyo vijiji vya huko arumeru, nadhani hiyo siyo 7bu hata kidogo ila wangetuambia wananchi wamechoshwa na ahadi zisizotimilika na ugumu wa maisha pia wizi na kukumbatia wezi.....
 
Ni kweli kabisa wanaJF, mi ni mkazi wa arumeru kwa hiyo hizo sababu ni za kweli kabisa. Na pia mgombea wa CCM hakuwa mkazi wa arumeru. Kuna sababu zingine pia nyingi.
 
Source Mtanzania

Moja ya sababu hizo ni

Haadi zisizotekelezeka
Mgombea kutojua maeneo ya jimboni mwake
Matusi ya wagombea

Kwi kwii kwiii eti hizo sababu ni SIRI! Ngoja nirejee KAMUSI yangu ya TUKI maana ya neno SIRI
 
Binadamu ni kiumbe ambaye kwa huruka anapenda kumwamini binadamu mwenzake "trusting creature". Imani hiyo hupotea kabla ya binadamu kuacha kumwamini tena binadamu mwenzake. CCM mliaminiwa bila hata ya jasho, kwa kuzaliwa kwetu na huruka yetu tu tuliwaamini, sasa hatuwaamini tena kwa fedha, tisheti, kanga this time hata mtoe pajama kwa wamama na wababa imani imekwisha. mbaya zaidi it is not renewable imani, it is gone by the wind nobody can run after it, it is gone.
 
Back
Top Bottom