Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
Baada ya Ndugu Bashir Mrindoko kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu nimelazimika kuazima andiko la MwanaJF mmoja alipotaka kutukumbusha jambo. Jambo hilo sio lingine ila ripoti ya Mwakyembe (MB) ambayo naamini kwa kiasi fulani ilisaidia sana yeye kuteuliwa kuwa Naibu Waziri kwani ripoti hiyo pamoja na mamabo mengine ilionyesha ni mtendaji kazi mzuri.
Kinachonishangaza ni pale ambapo maazimio ya ripoti hayo yanapokuwa hayana maana, yanadharaulika, yanakejeliwa na yanaonekana yamesahaulika. Ilianza kwa Hosea ikapita, ameendelea kushikilia nafasi yake. Sasa hivi imekuja kwa Ndugu Mrindoko, amepewa cheo.
Hii ni nini? Huyu bwana kama alionewa na tume ya Mwakyembe amewahi kusafishwa? Kama hakukosea je ni hatua zipi zimechukuliwa kumsafisha au ndio anasafishwa kwa kupewa cheo?
Ina maana ilikuwa lazima sana yeye ndie ashike nafasi hiyo? Hakukuwa na mtu mwingine na hakuna mtu mwingine yeyote msafi zaidi yake, mwenye uwezo zaidi yake ndani ya nchi hii?
Kwa kweli kuna maammuzi yanafanyika unabaki mdomo wazi. Kinachouma zaidi ni pale ambapo hakuna cha kufanya zaidi ya kuumia rohoni. Natamani uteuzi kama huu ungekuwa unathibitishwa na Bunge. Ila napata faraja unaweza kuhojiwa na Bunge kwa sababu ripoti hiyo ilitokana na Bunge. Hii ni dharau na kejeli kwa Bunge.
Namtakia kazi njema Ndugu Mrindoko, Mh. Mwakyembe na Mheshimiwa Raisi
"Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Ibrahim Msabaha (Mb.), na Katibu Mkuu, Ndugu Arthur Mwakapugi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kwa makusudi kwenye Mkataba wa Kampuni ya Mfukoni. Aidha, Kamishna wa Nishati, Ndugu Bashir Mrindoko naye achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu wake mpya kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC ambao ulijulikana dhahiri na Wizara mwaka 2004 kwenye Mradi wa bomba la mafuta. Ndugu Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua Kampuni hiyo kusitisha Mkataba wake na Serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa Zabuni ya umeme wa dharura haujaanza."
Mungu ibariki na uilinde Tanzania.

AZIMIO NAMBA 14: