Akili Unazo!
JF-Expert Member
- Feb 18, 2009
- 3,930
- 4,912
Wakuu,
Ni Juzi tu kama siyo Jana toka Ripoti ya kamati ya awali kuwekwa hadharani kuna watu wanatoa michango mingi, wengine ukiwaangalia wanajaribu kupotosha umma kuwa Rais amevunja sheria na mikataba ya uwekezaji juu ya hii sekta ya madini.
Na kuwa siku hawa wawekezaji watakapo kwenda kuproscuute huko kwenye Mahakama za Kimataifa basi watakaoathirika na gharama husika ni sisi wenyewe Wananchi. Hilo halipingiki, ila tujiulizi, huu uoga wetu unatokana na nini? Ni kweli kuingia mikataba mibaya haiwezi kuwa challenged? Hata kama waliopita walifumbia macho, kwa hiyo hakuna wakuja kuyafumbua na kuyaweka wazi ili hata waliokuwa waoga siku za nyuma wajue tulikuwa tunaibiwa?
Ripoti ya kamati ya pili ya Mh. Rais, itapelekea hata hizo Mahakama za Kimataifa za uwekezaji kupotea, kwa kuwa madhara ya kiuchumi ambayo nchi yetu imepitia kwa kuibeba na kuiogoba hii mikataba itauonyesha umma kuwa ukoloni bado upo.
Tuendelee kuvuta subira japo wabishi hawakosekani lakini huo ndio ukweli, miaka 15 Tumeibiwa sana na hawa wawekezaji hawatakuwa na nguvu tena ya kutushinda.