Ripoti ya FikraPevu ‘yapeleka’ mwalimu mwingine kunusuru kufungwa shule Nyasa

mshumbullah

Member
Jan 29, 2015
35
23
SAA chache baada ya gazeti tando la FikraPevu kuripoti kuhusu shule yenye wanafunzi 195 kufundishwa na mwalimu mmoja, tayari Serikali imetuma mwalimu mwingine.

Kuwasili kwa Mwalimu Charioni Mpombo kutoka Shule ya Msingi Tingi, katika Kata ya Tingi wilayani Nyasa kutainusuru shule ya Matarawe sifungwe kila wakati mwalimu pekee aliyepo anaposafiri ama kuugua.

Alhamisi, Januari 26, 2017 saa 1:00 asubuhi, FikraPevu iliripoti kwamba Shule ya Msingi Matarawe katika Kijiji cha Marungu, Tarafa ya Mpepo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, ilikuwa imefungwa kwa wiki mbili zaidi tangu kufunguliwa kutokana na mwalimu pekee aliyekuwepo, Gaudence Msuha (48), kuwa mafunzoni mjini Songea.

SOMA ZAIDI HAPA
 
Kwa hiyo huyo mmoja aliyeongezwa nalo ni bonge la hatua lililochukuliwa?!! Kweli nchi hii ni ya professional comedian!! Na wazazi wataonekana kwenye kideo wanashangilia kwa kupata mwalimu?!!
 
Na kuna wanasiasa wanatuambia walimu wametosha.... Wanahitaji wa Sayansi tuu , si kwamba hawajui ila wanajua wanataka kutengeneza jamii/ kizazi gani.


Demokrasia kama wimbo wa msiba, haupendwi lakini kama hutouimba utaimbiwa ama utasikia tuu ukiimbwa
 
Kwa nini tusifikirie kulipa posho za kuvutia za "hardship allowances" kwa sehemu kama hizo badala yake tunalipa wabunge na vibopa wengine sitting allowances ambazo ni ngumu kuzihalilisha kwa umma? Inawezekana naota tu!!!! Kuna msingi gani mzuri kwa mtoto kuliko elimu bora na bila mwalimu hakuna elimu bora.
 
Magazeti kama haya ndo ya kuyafungia yanafanya uchochezi!!!!....... Tanzania hatuna shida ya walimu tunao hadi wa akiba!!!!!!...... mwalimu mmoja anafundisha wanafunzi 40!!!!!...... Watakuwa wametumwa hawa na wanataka kutukwamisha!!!!!....., na nani kawaambia watendaji wa chini watoe hizo taarifa!!!!!!.....? Mwenye mamlaka ya kufanya hivo ni mkubwa tu!!!!!..... Vila shaka hiyo itakuwa shule hewa!!!!
 
Back
Top Bottom