Ripoti ya CAG kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2014 yabaini ufisadi wa zaidi ya bilioni 600

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
4,163
787
Wakati nchi ikiwa na deni kubwa na Maisha Magumu, Wakuu wa vitengo wanaiba kwa kwenda mbele.

Siku si nyingi Waziri wa Fedha, Mh Waziri Mkuu na wadau wengine walilifuatilia sakata wizi na Mishahara hewa. Sasa! Marehemu wetu, Wastaafu wetu waonekana kupokea mishahara.

Misamaha ya Kodi Bilioni 22.33, Wastaafu Hewa Nje ya Nchi Milion 5.43, Wakwepa kodi bilioni 800, Waliocha kazi Wanakula 141.4 Milion HEWA. -===== BILION 9 NA Milion 48.16



Chanzo: Mwananchi

This is how your money is being stolen - National
 
Hii kitu haiwezi kuisha na hakuna mtu mwenye nia ya dhati kumaliza hili! Waliofanya uzembe ktk report za nyuma wamechukuliwa atua gani? Kama hakuna kwa nn wasiendelee na ukiangalia watu ni wale wale kila mwaka.
 
CCM sasa wanatimiza slogan ya chama chao, CHUKUA CHAKO MAPEMA
 
Kipi kigeni kinachokufanya udamke asubuhi kuandika hii post? Kwanibhuo wizi wa mishahara umeanza leo? Mbona ni toka enzi za Ludovick uttoh? Riport zake zilionyesha hilo zaidi ya mara mbili, wastaafu kuendelea kupokea mishahara ni issue ya almost muongo mzima wizi katika halmashauri zetu kila mwaka ripory zinasema hivyo hivyo ubadhirifu uliopo katika manunuzi ya umma toka enzi za mkapa na kila mwaka ripot zinaonyesha hilo hadi ikulu mnikulu mkuu amefanya sana hiyo mambo, na habari zinasema hivyo kila riport ikitoka na hakuna anayechukuliwa hatua na trust me hata hili hakuna atakayechukuliwa hatua stahiki na mwakani C.A.G atafanya ukaguzi tena na yataonekana hayo hayo na vichwa vya habari vitasomeka kama vilivyosomeka mwaka huu na hakuna litakalofanyika sababu hii ni serikali ya "BUSSINESS AS USUAL" na maisha yaendelee..
 
Serikali ikubali kuingia hasara kwa kusajili upya wafanyakazi. Ili wajue nani yu hai, nani kafa, nani anaishi wapi
 
CAG wa zamani ndugu LUDOVICK UTUOH alikuwa hana neno. Yeye anaandika ripoti yake kisha hatoi INDIVIDUAL REPORTS za kila idara ya serikali na kuweka wazi ONLINE kama ambavyo huyu CAG mpya anavyofanya. Basically UTUOH alikuwa anatoa ripoti ambazo ziko DILUTED to the public lakini zile zingine alikuwa hataki wananchi wazisome wala kujua nani anaiba nini na nani anafuja pesa. Matokeo yake wizi ulikuwa unaendelea with IMPUNITY.

CAG mpya Professa MUSSA J ASSAD amekuwaja na moto wa ajabu na anatumia visingizio kuwa anatekeleza agizo la bosi wake Professa Kikwete kuwa serikali yake ni TRANSPARENT/WAZI na wanaanchi wanayo haki ya kusoma na kujua KODI zao zinavyotumika na jinsi serikali inavyotumia pesa.

Lakini JK kutaka misifa kuonyesha kuwa anakwenda na wakati na anatekeleza mpango mzima wa OPEN GOVT INITIATIVE/PARTNERSHIP (OGP) utapelekea watu kukosa kazi na kuleta vurugu nchi hii na inawezekana serikali ikaanguka kwa sababu si kawaida ya watanzania kuona serikali ikaweka wazi ripoti za matumizi ya kodi (JAPO SHERIA INAMTAKA CAG AWEKE HIZI RIPOTI WAZI) lakini pia inasemekana kuwa huyu CAG mpya alikuwa na tabia za UNOKO toka alipokuwa anasomesha chuo kikuu cha Dar es salaam.

Sasa cha kujiuliza, Je hizi ripoti za ukaguzi za kila shirika na kila wilaya zitawekwa wazi kama ambavyo serikali WAZI na SIKIVU inavyotaka? Na je tujiandae kuona akina nani wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria kwa ufujaji wa pesa za walalahoi? Je inawezekana haya mambo kuwa wazi ni geresha ya CCM kutaka serikali yao kuonekana wako TRANSPARENT na ACCOUNTABLE kuelekea kwenye uchaguzi?

Au JK kaamuatuuu kuwa LIWALO NA LIWE lakini serikali yake anataka ikumbukwe kama THE MOST TRANSPARENT & ACCOUNTABLE GOVT TANZANIA ever had?

Mwisho zaidi swali ni HOW DO YOU SOLVE A PROBLEM OF CAG MNOKO kama huyu mpya?
 
MAGUFULI kudanganya bunge na nchi kuhusu bilion 262-kwa mujibu wa CAG, WOTE TUNAJUA CAG sio mwanasiasa bali ni mtaalam kwa hiyo kauli yake unauzito wa kipekee
Je mwajua:Magufuri kabla ya kupandisha nauli pale kigamboni hakufanya hata upembuzi yakinifu kuwa vile vivuko na zaidi ya daraja kwa watu wakigamboni. Watu huvuka pale kwenda na kurudi zaidi ya hata mara tano kulingana na shughuli ya mtu. yeye huyu magufuri akalinganisha kivuko cha huko sengerema ambacho msafiri huvuka hata mara moja kwa mwaka ndio iwe kama Kigamboni.

Magufuri huyu nashangaa Ripoti ya CAG imeshingwa kusema chochote kuhusu tabia yake ya kujipendekeza kwa rais na kufikia kununua meli ya DAr - Bagamoyo! wamejenga pale magogoni Feri ghati ya hiyo meli kwa mamilioni ya pesa lakini ile ghati imeshindwa kutumia na sasa wanatumia ile ya Bakhresa. Huku pia kukiwa na tuhuma za kununua meli feki ambayo hutumia masaa 3 badala ya dkk 45 tu! Huyu jamaa kituko!



Huyu ASSAD watu walimmbeza ila kwa tunaomfaham tulifurahia sana uteuzi wake yaaan kama ni Gorrila war huyu ni KAGAME na sio GODOFRED kiongozi mpuuzi aliyetaka kuleta mapinduzi Burundi

kama ni bungeni huyu ni Mnyika, kama ni mziki huyu ni ali-kiba, kama ni soka huyu nemanja MATIC, kama ni spika basi huyu ni SITTA wa miaka ile alipokuwa na akili timamu, kama ni soka la bongo huyu ni Okwi na si TAMBWE AMISSI, kama ni ukuu wa majeshi jamaa ni Abdel Fattah al-Sisi. ANGELIKUWA mwanamkee Miss NINGEMFANANISHA na WEMA sepetu mrembo asiyechuja na sio SITTI MTEVU.

Hivi kulidanganya bunge ingekuwa huko china au KOREA kaskazini.
 
Kwa hiyo wewe hutaki uwazi??Tatizo siyo ufisadi tatizo la nchi hii ni jinsi mafisadi wanavyoshughulikiwa.Makomandoo wa UFISADI Idd Simba,Andrew Chenge pesa zimeingia mfukoni mwao hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa
 
Hayo yote ni ukweli mtupu..watumishi hewa bado wapo na wanalipwa ..marehemu na waastaafu kibao bado wanalipwa mishahara na stahiki mbalimbali...Hongera CAG kwa kutufumbua macho .
 

Chanzo. Mwananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…