Ripoti ya CAG: CHADEMA inaisiaidia CCM kuhujumu Uchambuzi wa ACT-Wazalendo?

mkalamo

JF-Expert Member
Sep 7, 2013
324
347
Salam wakuu,

Nimeingia katika tafakari ya muda baada ya kuona Matukio mawili yakitendeka ghafla ghafla ikiwa ni saa Chache kabla Chama Cha ACT Wazalendo hawajafanya uchambuzi wa ripoti ya CAG.

Katika kufuatilia Jambo hili nimejiridhisha kuwa tokea CAG akabidhi ripoti yake kwa Rais hamu na shauku ya watu wengi ilikuwa ni kumsikiliza Zitto Kabwe au Chama Cha ACT kitasema nini juu ya ripoti hiyo.

Katika kukata kiu hiyo Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter aliahidi watafanya Uchambuzi wa kina kama ilivyo ada yao tokea 2016

Kauli hiyo ndiyo imekuwa kauli pekee ya Chama hicho na hata Zitto mwenyewe, juu ya Ripoti ya CAG huku wakiwaahidi wananchi kuwa watafanya Uchambuzi mzuri na umma utaarifiwa

Katika hilo tayari matangazi mbali mbali yameshazunguka na hata baadhi ya Online Media zimeahidi kurusha Uchambuzi huo ili wananchi wajue, ikimbukwe kwamba Zitto ni miongoni mwa wanasiasa waliojipambanua juu ya Uchambuzi makini wa ripoti mbali mbali za kiuchumi na hata hiyo ya CAG.

Sasa basi wakati joto hilo la Uchambuzi wao ukiwa unaendelea mara Chadema nao wakatangaza kuwa watafanya Uchambuzi siku hiyo hiyo sema wao wametaka wafanye asubuhi kabisa kabla y watu hawajanywa hata chai, hii ikiwa si kawaida yao tokea Chama hicho kilipoanzishwa.

Wakati Chadema wakirangaza nao kufanya uchambuzi kama wafanyazvyo ACT mara Rais nae katumbua watu na kutaka wengine washughulikiwe.

Ukiangia mlilongo wote huo utaona namna wanavyotaka kuzima Uchambuzi wa ACT kwa Matukio hayo.

Swali la kujiuliza tu je haikuwa busara kwa Chadema kusuburi wenzao wafanya na wao watafute siku nzima nyingine badala ya kuwavizia ACT?

JE kinachofanywa sasa si muendelezo wa kutafuta sifa za mitandaoni kuwa hoja hii tulianza sisis kabla ya wao?
 
Akili ya kitoto sana hii ya kutaka kumiliki hoja eti tu kutokana na kisingizio cha mazoea ama historia ya mtu kufanya kitu fulani.

Jambo ambalo lipo kwenye "public domain" na tena ni "burning issue" na lenye maslahi makubwa sana kwa nchi iyetu iweje leo hii liwe "attributed" kwa ajili ya mtu mmoja tu, na kuhitaji kuwaengua wengine, au kuwasubirisha mpaka yeye pekee ndiye aongee kwanza!

Pamoja na kuwa na uhuru wa kutoa maoni, lakini uhuru huu uendane na hoja zenye kufikirisha, na pia zenye kuleta uchokozi wenye mantiki ya kutaka kujibiwa kihoja. Hoja kama hii ni "very low" kwa vigezo vya watu makini.
 
Salam wakuu,

Nimeingia katika tafakari ya muda baada ya kuona Matukio mawili yakitendeka ghafla ghafla ikiwa ni saa Chache kabla Chama Cha ACT Wazalendo hawajafanya uchambuzi wa ripoti ya CAG...
Kwa hiyo wenye haki kuchambua hiyo ripoti ni ACT tu wengine ni haramu kufanya hivyo?
 
Huu ujinga ulitaka kujitokeza wakati wa utawala wa Magufuli, eti ikifika saa 2 usiku vituo vyote vya luninga vijiunge na TBC kupata taarifa ya habari. Maelezo ilikuwa eti watu kusikiliza vituo mbalimbali hawawezi kujua serikali yao imefanya nini.

Sasa mleta uzi naye anakuja na ujinga huo huo kuwa aachwe Zito achambue, kana kwamba watu wote wanasubiri uchambuzi toka kwa Zito.

ACT wachambue kwa muda wao na vyama vingine ikiwemo CDM ichambue kimpango wake, kila mtu atafuata uchambuzi popote atakapo. Hii ni dunia ya soko huria la habari, toa habari yako, kama ina mashiko kuliko wengine itafuatiliwa zaidi.
 
Back
Top Bottom