Ripoti ya Benki ya Dunia: Tanzania ina uchumi unaokua kwa kasi kuliko nchi yoyote Afrika Mashariki

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,229
5,285
Kutokana na ripoti hii ya Benki ya Dunia ya Uchumi toleo la nane (8) kwa Tanzania, inaonyesha kuwa ndani ya miaka 10 iliyopita, Uchumi umekua na kufanya idadi ya watu wanaoishi chini ya Dola moja kufikia milioni 12. Bado uwekezaji mkubwa (wa miundo mbinu na Watendaji) unatakiwa kufanywa ili kuboresha maisha ya Watanzania wanaoishi katika maisha duni.

Ripoti hii (miongoni mwa taarifa nyingine), inatoa msisitizo wa umuhimu wa kuwekeza katika Sekta Binafsi kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi na umuhimu wa Serikali kutambua sekta hiyo.

1. Miradi ya Sekta binafsi inatakiwa kuchaguliwa kwa umakini mkubwa kwa misingi ya kiasi cha pesa kinachopaswa kutumika na mvuto wa mradi huo kwa sekta binafsi.

2. Miradi iliyochaguliwa inatakiwa iwe imeandaliwa vema, ikiwa na matumizi sahihi na watu sahihi wa kuiendesha ikiwa pamoja na ushauri na ushiriki wa Wataalam katika miradi hiyo.

3. Miradi inayotolewa bila ushindani wa wadau na uwazi, ina uwezekano mdogo wa mafanikio. Wahisani wanapaswa kushirikisha wadau wengi ili kujenga ushindani wa kuweza kupata watu bora zaidi kuendesha miradi.

4. Kiwango kikubwa cha ushiriki wa serikali ni chambo kikubwa cha kuhakikisha kufanikiwa kwa miradi ya sekta binafsi. Hata hivyo serikali kuingilia katika maamuzi ya miradi hiyo katika ngazi ya chini inachangia kwa uwezekano mkubwa wa miradi hiyo kutokuwa na mafanikio.

5. Miradi iliyopangiliwa vema, ikiwa na mikakati sahihi pamoja na kampeni za kuifikia jamii juu ya kile ambacho mradi huo unafanya inachangia kujenga ufahamu katika jamii na pia maelewano mazuri katika ya serikali na sekta binafsi.​

Kufuatilia uzinduzi huo wa Uchumi (8th Tanzania Economic Update: The Road Less Travelled - Unleashing Public Private Partnerships in Tanzania) fuatilia live kupitia live stream channel hii - The World Bank: 8th Tanzania Economic Update on Livestream

Pia unaweza kupata updates ya tukio hili kupitia timeline yetu ya Twitter (Jamii Forums (@JamiiForums) | Twitter) au fuatilia hashtag ya #TzEU8 #TZEconomy

IMG-20160520-WA0025.jpg

Mkurugenzi wa World Bank Tanzania, Bi. Bella Bird akitoa Muhtasari na kumkaribisha Mgeni Rasmi Mheshimiwa Samia H. Suluhu
 
Alafu watu muwe mnatumia ubongo mlopewa vyema heko JPM zinatoka wapi hapo? Alafu hakuna cha kupongeza zaidi ya hasara,title iko wazi "The road less travelled" hapa cha kupongezana ni kipi? Inatakiwa kutumia report hiyo kujitathmini ili tufanye vyema.Kama Ivory Coast wameweza kukuza uchumi kwa kutegemea kilimo kwa nini tushindwe? Kama tumeshindwa tukaige na kujifunza mbinu zao
 
Hatujashindwa kama kigezo chako ni Ivory Coast kwa maana sisi ni wa pili baada ya Ivory Coast kwa ukuaji wa Uchumi Afrika nzima hivyo kama hicho ndiyo kigezo chako basi tuko vizuri, tunapaswa kuongeza juhudi zaidi lkn tunakwenda vizuri!
 
Nishauri tu kwamba tupokee ripoti hizi critically rather than passively. Ni dhahiri kwamba hapa tunaandaliwa kuuziwa mkopo. The World Bank core business is to sell loans. Kama huniamini, tizama kitakachofuata baada ya ripoti hii kuzinduliwa.

Walipotoa ripoti kuhusu tourism (The Elephant in the Room: Unlocking the Potential of the Tourism Industry for Tanzanians), kilichofuata tulichukua mkopo. Walipotoa ripoti kuhusu bandari (Opening the Gates: How the port of Dar es Salaam Can Transform Tanzania ), kilichofuata tulichukua mkopo kuboresha bandari ya Dar es Salaam. Sasa wamekuja na ripoti hii (The Road Less Travelled - Unleashing Public Private Partnerships in Tanzania). Kitakachofuata tutachukua mkopo.

Uandishi wa hizi ripoti unafanana: Unlocking the potential of tourism industry, Opening the gates, The Road Less Travelled. Ripoti hizi huandikwa kimkakati ili kutega wakopaji wachukue mkopo. Ripoti zinalenga kuonesha wakopaji kwa nini wachukue mkopo kwa jina la utafiti. Ukiwa mfanyakazi wa the Bank, hiyo ndiyo kazi yako ya kila siku - produce 'knowledge' that will enable selling of loans. Kimsingi, hizi ripoti si tafiti bali ni tools za kuuzia mikopo.

Kama unataka kujifunza zaidi jinsi the Bank inavyozalisha "knowledge", look for this book. Imperial Nature: The World Bank and Struggles for Social Justice in the Age of Globalization by Michael Goldman. See particularly Chapter III: Producing Green Science inside Headquarters.
 
Zungu pule umenifumbua jicho la 3,nadhani kama Taifa tunatakiwa tu stick kwenye vipaombele vyetu kama Taifa na kuzitumia hizi ripoti janja zao kufanya tathmini tu na pale tutakapohitaji mkopo sio lazima iwe kwa wao.Wanataka kutu lock kwenye utumwa wa madeni yenye riba kubwa kwa faida yao,lets be catious with whitemen
 
Hatujashindwa kama kigezo chako ni Ivory Coast kwa maana sisi ni wa pili baada ya Ivory Coast kwa ukuaji wa Uchumi Afrika nzima hivyo kama hicho ndiyo kigezo chako basi tuko vizuri, tunapaswa kuongeza juhudi zaidi lkn tunakwenda vizuri!
 
Well hoja yangu hapa mkuu hadi kuweka mfano wa Cote'de Voire ni kwa vile sekta zinazo engineer economy growth ni zile zenye kuajiri watu wengi kama kilimo,manufacturing na services/bisinneses na kwa mantiki hiyo impacts za ecomic growth are felt positively Unlike sie uchumi unakua kwenye ujenzi,madini na Tourism huku kilimo,viwanda na biashara ndogo ndogo zinasua
 
Taarifa ya worldbank miaka miwili iliyopita ilibainisha wazi kuwa mamilionea wengi duniani watatokea kwenye "agriculture na agribusiness"...hakika kama taifa tukiwekeza kwenye sekta ya kilimo tutapiga hatua kubwa katika kuuondoa umaskini.Tanzania pia inahitaji miundombini ya mawasiliano,usafirishaji na nishati ya uhakika ilikuwezesha kilimo chenye tija,masoko pamoja na ukuaji wa viwanda.
 
Nishauri tu kwamba tupokee ripoti hizi critically rather than passively. Ni dhahiri kwamba hapa tunaandaliwa kuuziwa mkopo. The World Bank core business is to sell loans. Kama huniamini, tizama kitakachofuata baada ya ripoti hii kuzinduliwa.

Walipotoa ripoti kuhusu tourism (The Elephant in the Room: Unlocking the Potential of the Tourism Industry for Tanzanians), kilichofuata tulichukua mkopo. Walipotoa ripoti kuhusu bandari (Opening the Gates: How the port of Dar es Salaam Can Transform Tanzania ), kilichofuata tulichukua mkopo kuboresha bandari ya Dar es Salaam. Sasa wamekuja na ripoti hii (The Road Less Travelled - Unleashing Public Private Partnerships in Tanzania). Kitakachofuata tutachukua mkopo.

Uandishi wa hizi ripoti unafanana: Unlocking the potential of tourism industry, Opening the gates, The Road Less Travelled. Ripoti hizi huandikwa kimkakati ili kutega wakopaji wachukue mkopo. Ripoti zinalenga kuonesha wakopaji kwa nini wachukue mkopo kwa jina la utafiti. Ukiwa mfanyakazi wa the Bank, hiyo ndiyo kazi yako ya kila siku - produce 'knowledge' that will enable selling of loans. Kimsingi, hizi ripoti si tafiti bali ni tools za kuuzia mikopo.

Kama unataka kujifunza zaidi jinsi the Bank inavyozalisha "knowledge", look for this book. Imperial Nature: The World Bank and Struggles for Social Justice in the Age of Globalization by Michael Goldman. See particularly Chapter III: Producing Green Science inside Headquarters.

Couldn't agree with you more! Habari ya Economic Hitmen ndiyo inahusika hapo!
 
Kwenye hili la kupunguza ukiritimba kwa mfano kupitia mamlaka zinazokinzana kama tbs na tfda kudos. Prof. Mkenda amenena vema..
 
Nishauri tu kwamba tupokee ripoti hizi critically rather than passively. Ni dhahiri kwamba hapa tunaandaliwa kuuziwa mkopo. The World Bank core business is to sell loans. Kama huniamini, tizama kitakachofuata baada ya ripoti hii kuzinduliwa.

Walipotoa ripoti kuhusu tourism (The Elephant in the Room: Unlocking the Potential of the Tourism Industry for Tanzanians), kilichofuata tulichukua mkopo. Walipotoa ripoti kuhusu bandari (Opening the Gates: How the port of Dar es Salaam Can Transform Tanzania ), kilichofuata tulichukua mkopo kuboresha bandari ya Dar es Salaam. Sasa wamekuja na ripoti hii (The Road Less Travelled - Unleashing Public Private Partnerships in Tanzania). Kitakachofuata tutachukua mkopo.

Uandishi wa hizi ripoti unafanana: Unlocking the potential of tourism industry, Opening the gates, The Road Less Travelled. Ripoti hizi huandikwa kimkakati ili kutega wakopaji wachukue mkopo. Ripoti zinalenga kuonesha wakopaji kwa nini wachukue mkopo kwa jina la utafiti. Ukiwa mfanyakazi wa the Bank, hiyo ndiyo kazi yako ya kila siku - produce 'knowledge' that will enable selling of loans. Kimsingi, hizi ripoti si tafiti bali ni tools za kuuzia mikopo.

Kama unataka kujifunza zaidi jinsi the Bank inavyozalisha "knowledge", look for this book. Imperial Nature: The World Bank and Struggles for Social Justice in the Age of Globalization by Michael Goldman. See particularly Chapter III: Producing Green Science inside Headquarters.

*Slow Clap....* True Thinker. Also read "50 Yrs is Enough" by Kevin Danaher
 
Zungu Pule has a point, but I do have the following reservations,

Have we at hand, evaluation reports on loans performance taken as a result of influence of "The Elephant in the Room" and "Opening the Gates"? Short of that, we can't reach an informative conclusion as to whether the reports are just dragging us.
Can we do it without loans? Absolutely NO! considering leverage effect, but the quality of loan is what matters.
We do not take these loans at gun point, there is a free consent.

Why skeptical about the reports? They are just free consultancy!
 
Back
Top Bottom