Ripoti: Tanzania iko nyuma kwa furaha duniani

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
Tanzania ni miongoni mwa nchi kumi za mwisho kwa viwango vya furaha kwa mujibu wa Ripoti ya Viwango vya Furaha Duniani ya 2016 ambayo imetolewa leo.

Orodha hiyo iliandaliwa kwa kuangazia pato la mtu kwa kila mwaka, miaka ambayo mtu anatarajiwa kuishi, kuwa na mtu wa kutegemea kwa usaidizi, dhana ya kuwepo uhuru wa kufanya maamuzi maishaji, uhuru kutoka kwa ufisadi, na ukarimu miongoni mwa mengine.

Mataifa yaliyo kwenye kundi la mataifa kumi ya mwisho ni Madagascar, Tanzania, Liberia, Guinea, Rwanda, Benin, Afghanistan, Togo, Syria huku Burundi ikishika mkia.

Tanzania imo nambari 149 kati ya nchi 157 ikiwa na alama 3.695 kati ya alama 10 na Rwanda nambari 152 na alama 3.315.

Uganda imo nambari 146 na alama 3.739, Malawi nambari 132 na alama 4.156, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imo nambari 125 na alama 4.272 na Kenya nambari 122 na alama 4.356.

Somalia imo nambari 76 na alama 5.44.

Ripoti hiyo imetolewa mjini Roma, Italia huku ulimwengu ukijiandaa kuadhimisha Siku ya Furaha Duniani ya Umoja wa Mataifa tarehe 20 Machi.

160316121310_happinesscountries.jpg

Orodha hiyo imetayarishwa na shirika la maendeleo endelevu ya Sustainable Development Solutions Network (SDSN) ambalo lilianzishwa na Umoja wa Mataifa.

Denmark inaongoza kwa viwango vya furaha duniani ikiwa na alama 7.526 ikifuatwa kwa karibu na Uswizi, Iceland na Norway.

Finland, Canada, Uholanz, New Zealand, Australia na Sweden zinafunga kumi bora.

Marekani imo nambari 13 na Uingereza nambari 23.
BBC
 
Hapa ndipo ninapouona uongo mwingi,Hivi kati ya sisi WaTZ na Wacongo watu gani wanaweza kuwa na furaha kuliko wengine,halafu Kigezo kilichotumika hakifai na wala hakiwezi kuleta majibu sahihi.
 
Furaha sio kutokua na vita wewe. Tanzania hakuna vita ila watu wengi tunasononeka nyoyoni kwa ufisad, njaa na vingine haswa kwa watu wa dsm ndo maana tunanuniana tu kwenye daladala
 
Hao watu ni wapumbavu
Kwani furaha yetu na huzuni yetu inawahusu nini. Mbona walitufanya watumwa wao kwa zaidi ya miaka mia moja na kutukosesha furaha. Mtaani kwetu sisi kuna furaha watu wanacheka na kufurahi. Kama wao Wazungu ndo wanafuraha mbona siwaoni mitaa ya Feri wakiwa wanachekacheka kama mazuzu? Wapumb*avu sanaa.
 
Hao watu ni wapumbavu
Kwani furaha yetu na huzuni yetu inawahusu nini. Mbona walitufanya watumwa wao kwa zaidi ya miaka mia moja na kutukosesha furaha. Mtaani kwetu sisi kuna furaha watu wanacheka na kufurahi. Kama wao Wazungu ndo wanafuraha mbona siwaoni mitaa ya Feri wakiwa wanachekacheka kama mazuzu? Wapumb*avu sanaa.

Wewe jamaa ni kiboko, umeshapaka matope hapo juu kwenye 'red'.. huku huku unawatukana wazungu..
 
Back
Top Bottom