Ripoti: Tanzania dhaifu kulinda rasilimali zake

Ripoti: Tanzania dhaifu kulinda rasilimali zake

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,331
Posted Mei25 2013 saa 20:45 PM
MWANANCHI

Kwa ufupi
Ripoti ya taasisi hiyo Revenue Watch Institute, inaeleza kuwa Tanzania iliyo na madini ya shaba, fedha, almasi na gesi asilia, imeshindwa kulinda na kudhibiti rasilimali zake, hivyo kuathiri utendaji katika sekta nyingine.

Dar es Salaam.
Taasisi moja ya masuala ya mapato imetoa ripoti yake ya mwaka 2011/12 kuhusu Utendaji na Utawala katika rasilimali. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa Tanzania ni dhaifu katika usimamizi wa rasilimali zake ikishika nafasi ya 27 kati ya nchi 58 zenye usimamizi mbovu katika sekta hiyo.

Ripoti ya taasisi hiyo Revenue Watch Institute, inaeleza kuwa Tanzania iliyo na madini ya shaba, fedha, almasi na gesi asilia, dhahabu n.k. imeshindwa kulinda na kudhibiti rasilimali zake, hivyo kuathiri utendaji katika sekta nyingine.

Inaeleza kuwa katika masuala ya kisheria kuhusu madini Tanzania imeshika nafasi ya 46 kati ya nchi 58, ambayo ni sawa na asilimia 44 na kufafanua kuwa hali hiyo imetokana wananchi wake kutojua mambo mengi kuhusu rasilimali zao hali inayochangiwa na kutokuwa na sheria huru ya vyombo vya habari.

"Kingine ni Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Mamlaka ya Mapato (TRA), zote kukusanya malipo kutoka katika kampuni za madini. Kampuni hizo pia hufanya baadhi ya malipo moja kwa moja kwa wananchi walioathirika, vinginevyo mapato yote huenda Hazina," inaeleza sehemu ya ripoti hiyo.

Inaeleza kuwa baada ya miaka mingi ya Tanzania hupata mrabaha mdogo kutoka katika kampuni za madini, mwaka 2010 sheria ya madini ilifanyiwa marekebisho na mrabaha kuongezwa, lakini bado mikataba ya kampuni za madini imeendelea kuwa siri.

Inaeleza kuwa kampuni hizo zinatakiwa kueleza athari za mazingira katika migodi, lakini nyingi hazifanyi hivyo na kwamba hali hiyo ni kinyume na matakwa ya leseni zao.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kampuni hizo zinatakiwa kuweka wazi taarifa zake za mapato kwa kuwa mwaka 2012, Tanzania ilitia saini mpango wa uwazi katika shughuli za madini.

Inaeleza kuwa sababu ya Tanzania kuwa na usimamizi mbovu katika sekta ya madini ni pamoja na kushindwa kuchapisha mikataba ya madini wala kuwa na takwimu za kampuni zinazomilikiwa na Serikali, licha ya kuwa inatoa baadhi ya taarifa juu ya uzalishaji na mapato ya madini.

"Wizara ya Fedha huchapisha habari juu ya kiasi cha uzalishaji na thamani ya mauzo ya nje, lakini haitoi maelezo juu ya mapato katika madini," inasema sehemu ya ripoti hiyo na kuongeza;

"Wizara ya Nishati na Madini inachapisha maelezo kuhusu hifadhi, kiasi cha uzalishaji, bei ya kuuza nje, idadi ya kampuni, kodi na mirabaha, lakini haitoi takwimu juu ya ada ya leseni, gawio au mafao."

Inafafanua kuwa licha ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) huchapisha ripoti kila mwaka kuhusu mauzo ya nje na kiasi cha uzalishaji, sheria mpya ya madini haijaondoa mamlaka ya hiari ya Waziri wa Nishati na Madini katika utoaji leseni na mazungumzo ya mkataba.Inaeleza kuwa Tanzania pamoja na kuwa na mazingira mazuri imepata alama za chini katika utawala wa sheria, hali inayotokana na kuwepo kwa vitendo vya rushwa na uwajibikaji mdogo.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa katika usimamizi wa kampuni za madini Tanzania imeshika nafasi ya 31 kati ya nchi 45, ambayo ni sawa na asilimia 33.

Inaeleza kuwa shughuli mbalimbali za usimamizi wa madini hufanywa na Shirika la Madini la Taifa (Stamico), ambalo linaimarishwa na Serikali ili kuboresha utendaji wake, lakini bado kumekuwa na kasoro kubwa katika uchapishaji wa mapato na kampuni zilizokaguliwa kwa mwaka.

Inaeleza kuwa nia ya Serikali ya Tanzania ni kuanzisha mfuko wa maendeleo ya madini, lakini mpango huo bado haujatekelezwa.

Posted Mei25 2013 saa 20:45 PM
MWANANCHI

Kwa ufupi
Ripoti ya taasisi hiyo Revenue Watch Institute, inaeleza kuwa Tanzania iliyo na madini ya shaba, fedha, almasi na gesi asilia, imeshindwa kulinda na kudhibiti rasilimali zake, hivyo kuathiri utendaji katika sekta nyingine.

Dar es Salaam.
Taasisi moja ya masuala ya mapato imetoa ripoti yake ya mwaka 2011/12 kuhusu Utendaji na Utawala katika rasilimali. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa Tanzania ni dhaifu katika usimamizi wa rasilimali zake ikishika nafasi ya 27 kati ya nchi 58 zenye usimamizi mbovu katika sekta hiyo.

Ripoti ya taasisi hiyo Revenue Watch Institute, inaeleza kuwa Tanzania iliyo na madini ya shaba, fedha, almasi na gesi asilia, dhahabu n.k. imeshindwa kulinda na kudhibiti rasilimali zake, hivyo kuathiri utendaji katika sekta nyingine.

Inaeleza kuwa katika masuala ya kisheria kuhusu madini Tanzania imeshika nafasi ya 46 kati ya nchi 58, ambayo ni sawa na asilimia 44 na kufafanua kuwa hali hiyo imetokana wananchi wake kutojua mambo mengi kuhusu rasilimali zao hali inayochangiwa na kutokuwa na sheria huru ya vyombo vya habari.

“Kingine ni Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Mamlaka ya Mapato (TRA), zote kukusanya malipo kutoka katika kampuni za madini. Kampuni hizo pia hufanya baadhi ya malipo moja kwa moja kwa wananchi walioathirika, vinginevyo mapato yote huenda Hazina,” inaeleza sehemu ya ripoti hiyo.

Inaeleza kuwa baada ya miaka mingi ya Tanzania hupata mrabaha mdogo kutoka katika kampuni za madini, mwaka 2010 sheria ya madini ilifanyiwa marekebisho na mrabaha kuongezwa, lakini bado mikataba ya kampuni za madini imeendelea kuwa siri.

Inaeleza kuwa kampuni hizo zinatakiwa kueleza athari za mazingira katika migodi, lakini nyingi hazifanyi hivyo na kwamba hali hiyo ni kinyume na matakwa ya leseni zao.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kampuni hizo zinatakiwa kuweka wazi taarifa zake za mapato kwa kuwa mwaka 2012, Tanzania ilitia saini mpango wa uwazi katika shughuli za madini.

Inaeleza kuwa sababu ya Tanzania kuwa na usimamizi mbovu katika sekta ya madini ni pamoja na kushindwa kuchapisha mikataba ya madini wala kuwa na takwimu za kampuni zinazomilikiwa na Serikali, licha ya kuwa inatoa baadhi ya taarifa juu ya uzalishaji na mapato ya madini.

“Wizara ya Fedha huchapisha habari juu ya kiasi cha uzalishaji na thamani ya mauzo ya nje, lakini haitoi maelezo juu ya mapato katika madini,” inasema sehemu ya ripoti hiyo na kuongeza;

“Wizara ya Nishati na Madini inachapisha maelezo kuhusu hifadhi, kiasi cha uzalishaji, bei ya kuuza nje, idadi ya kampuni, kodi na mirabaha, lakini haitoi takwimu juu ya ada ya leseni, gawio au mafao.”

Inafafanua kuwa licha ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) huchapisha ripoti kila mwaka kuhusu mauzo ya nje na kiasi cha uzalishaji, sheria mpya ya madini haijaondoa mamlaka ya hiari ya Waziri wa Nishati na Madini katika utoaji leseni na mazungumzo ya mkataba.Inaeleza kuwa Tanzania pamoja na kuwa na mazingira mazuri imepata alama za chini katika utawala wa sheria, hali inayotokana na kuwepo kwa vitendo vya rushwa na uwajibikaji mdogo.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa katika usimamizi wa kampuni za madini Tanzania imeshika nafasi ya 31 kati ya nchi 45, ambayo ni sawa na asilimia 33.

Inaeleza kuwa shughuli mbalimbali za usimamizi wa madini hufanywa na Shirika la Madini la Taifa (Stamico), ambalo linaimarishwa na Serikali ili kuboresha utendaji wake, lakini bado kumekuwa na kasoro kubwa katika uchapishaji wa mapato na kampuni zilizokaguliwa kwa mwaka.

Inaeleza kuwa nia ya Serikali ya Tanzania ni kuanzisha mfuko wa maendeleo ya madini, lakini mpango huo bado haujatekelezwa.

Hizi ni porojo za taasisi hiyo zenye lengo la kuwafurahisha wanaowapa fedha. Tanzania ni moja ya nchi zinazofanya vizuri sana kulinda rasilimali zake za madini. Tangu mwaka 2009 ilianzisha Wakala wa Ukaguzi wa Madini, TMAA ambayo ilipewa jukumu la kudhibiti na kukagua shughuli za uzalishaji na mauzo ya madini kwa lengo la kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato stahiki. Pia, TMAA inakagua shughuli za utunzaji wa mazingira migodini. Taasisi hiyo imewezesha migodi mikubwa nchini kuanza kulipa kodi ya mapato, na kulipa in full mapato mengine yote ikiwepo mrabaha. Pia, shughuli za utunzaji wa mazingira migodini zimeimarika sana. Ukitaka taarifa zaidi, angalia annual reports zao za 2012 na 2011 kwenye website yao Tanzania Minerals Audit Agency - TMAA |. Kwa sababu ya utendaji mzuri wa TMAA, imesifika nje na ndani kwa kazi yake nzuri na imekuwa ni role model kwa mataifa mengi ambayo yameanza kuiga ukaguzi kama wa TMAA. Tayari Kenya wameanzisha Minerals Audit Unit, na Zambia pia. Serikali ipo makini sana na rasilimali zake kuliko wanavyotaka kutuaminisha hao vibaraka wa mabeberu. Chunguza, ni nchi gani duniani inayofanya physical audit ya uzalishaji madini migodini? Ni Tanzania pekee kupitia TMAA. Ni nchi gani inayokagua shughuli za mazingira migodini kila robo, yaani ukaguzi wa kina? Tanzania tunafanya hivyo. Nimeona nikumegee hayo machache, maana mimi nilijifunza hayo kwenye maonesho nilipotembelea banda la TMAA nikavutiwa sana na kuipongeza serikali kwa uamuzi wake wa kuanzisha chombo hicho. vIVA serikali.
 
Si kila report zinazotolewa na hizi taasisi ni za kweli. Zingine zinatengenezwa kwa maslahi ya wanaowafadhili. Na si kila kinacho postiwa kwenye net kina mantiki,vingine ni utumbo tu. Cha muhimu simama kwenye u great thinker na tafakari.
 
Wao ndiyo dhaifu, waje kwangu niwaonyeshe namana ambavyo rasilimali zinalindwa.
 
We have vast amount of resources. How positively have these resources helped to improve our life.
 
TMAA endeleeni kukaza buti

IJUMAA, SEPTEMBA 14, 2012 05:34 MHARIRI

Source: TMAA endeleeni kukaza buti

JANA, katika gazeti hili tuliandika taarifa, kwamba Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), umebaini kuwapo kwa udanganyifu katika Kampuni ya Uchenjuaji wa Dhahabu ya Aureus Limited.

Katika taarifa hiyo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, alisema kampuni hiyo imefanikiwa kuiibia Serikali Sh bilioni 11 baada ya kukwepa kulipa kodi.

Kwa mujibu wa Masele, watu watatu ambao ni raia wa kigeni, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kutokana na wizi huo.

Kwa hatua hiyo ambayo imefikiwa na TMAA, sisi MTANZANIA tuna kila sababu ya kuunga mkono taasisi hiyo kwa mafanikio hayo.

Tunasema hivyo kwa sababu ni miaka mingi sasa, sekta ya madini imekuwa ikilalamikiwa, kwamba haiwasaidii Watanzania kwa sababu madini yanayochimbwa mara nyingi yamekuwa yakitoroshwa na kupelekwa nje ya nchi bila kulipiwa kodi.

Pia sekta hiyo imekuwa ikilalamikiwa, kwamba haina msaada kwa wananchi kwa sababu wananchi wanaozunguka migodi, wamekuwa wakiishi maisha ya dhiki licha ya ardhi walioyomo, kujaa mamilioni ya tani za madini ya kila aina.

Katika sekta hiyo hiyo ya madini, ndiko yalikojaa malalamiko yanayotolewa na wananchi, kwamba wamiliki wa migodi wamekuwa wakipewa upendeleo wa wazi na hivyo, kuwa chanzo cha wananchi kunyanyaswa katika nchi yao.

Kwa maana hiyo, tunapenda kuipongeza TMAA kwa ujasiri na uwezo waliouonyesha hadi kufanikisha kukamatwa kwa wageni hao raia wa Uholanzi, Israel na Afrika Kusini.

Pamoja na pongezi hizo, tunaitaka TMAA iongeze kasi kwa kuchunguza migodi yote nchini kwa sababu hata huko kuna madudu mengi yanayoendelea.

Tunaamini huko nako kunatakiwa uchunguzi wa haraka na wa kina ili kuondokana na dhana ya kuigeuza Tanzania kuwa kama Shamba la Bibi ambako wageni wanafika na kuchuma mali watakavyo na kuondoka, huku Watanzania wakiendelea kuwa ombaomba katika nchi zao.

Tunaamini TMAA bado wana nguvu na uwezo mkubwa wa kupekua migodi mingine ambako nako kuna uozo unaotakiwa kujulikana na kuchukuliwa hatua kwa sababu utaalam na uwezo wa kufanya hivyo wanao.

Bado tunaendelea kuamini kwamba, kama TMAA itazidi kuwajibika ipasavyo ili kurudisha heshima iliyoshuka katika sekta ya madini na kuwa chanzo cha Watanzania kunufaika na rasilimali za nchi yao.
 
TMAA sasa yaongeza mapato mrabaha ya uchimbaji, mauzo

Jumapili
Mei 26, 2013

Source: TMAA sasa yaongeza mapato mrabaha ya uchimbaji, mauzo - Biashara - mwananchi.co.tz

WAKALA wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), umeongeza mapato ya mrabaha kwenye uchimbaji na mauzo ya madini ya ujenzi mara 70 kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wakala huyo jijini Dar es Salaam jana, ongezeko hilo la maduhuli limetokana na matumizi ya hati ya mauzo ya madini iliyoanza kutumika Juni 2011.

Pamoja na ongezeko la mapato kutoka wastani wa milioni mbili kwa mwezi kabla ya matumizi ya hati hadi milioni 230 za sasa kwa mwezi, pia kumekuwepo na ongezeko kubwa la wachimbaji halali wa madini ya ujenzi.

TMAA ikishirikiana na Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Mashariki kwa msaada wa polisi, iliendesha operesheni kabambe ya kuondoa uchimbaji haramu wa madini ya ujenzi katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kwa muda wa siku 12 kuanzia Agosti 1 hadi 16, 2012.

"Operesheni hiyo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa na kukidhi malengo yaliyotarajiwa," ilisema taarifa ya wakala kwa vyombo vya habari, ikiongeza kuwa kutokana na operesheni hiyo, idadi kubwa ya wachimbaji wadogo wa madini ya ujenzi wasio na leseni waliwasilisha maombi ya kupewa leseni za uchimbaji kwenye maeneo yaliyotengwa.

Kwa kipindi cha miezi mitano, kuanzia Julai 1 hadi 30 Novemba, 2012 jumla ya leseni 282 za uchimbaji wa madini ya ujenzi katika maeneo yaliyotengwa zilitolewa. Kati ya hizo, leseni 270 ni za mchanga na 12 za kokoto. "Hatua hii inadhihirisha kwamba wachimbaji wengi waliokuwa wakifanya shughuli za uchimbaji bila leseni sasa wamepata mwamko na kutekeleza maagizo ya

Serikali ya kuendesha shughuli hizo kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010," ilisema taarifa na kufafanua kuwa kiasi cha madini ya ujenzi yanayozalishwa kutoka kwenye machimbo haramu imepungua kutoka asilimia 70 hadi kufikia asilimia moja tu ya madini ya ujenzi yanayouzwa sokoni.

Takwimu zinaonyesha pia mauzo ya madini yameongezeka kutoka bilioni 1.5 kabla ya kuanza kwa matumizi ya vocha hadi bilioni 4.3 kwa mwezi kwa sasa.

Pamoja na mafanikio yaliyopatikana, wakala ametahadharisha dhidi ya mbinu chafu zinazotumiwa na baadhi ya wachimbaji wasio waaminifu kukwepa kulipa mrabaha stahiki na kuonya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kukiuka taratibu za uchimbaji na matumizi ya hati za mauzo ya madini ya ujenzi.

Baadhi ya mbinu za ukwepaji kodi ni pamoja na wachimbaji kuuza vitabu vya Hati za Mauzo ya Madini kwa wasafirishaji wasio waaminifu ambao huzitumia hati hizo kusafirisha mchanga kutoka kwenye machimbo yasiyo rasmi, hati kujazwa uzito mdogo kuliko kiasi halisi cha madini yaliyouzwa, lengo likiwa ni kukwepa ulipaji wa kiasi halisi cha mrabaha, na mtindo wa kuwahonga madereva wa malori yasafirishayo madini ya ujenzi ili warudishe hati halisi ya madini ya ujenzi kwa mmiliki ili itumike tena kwa kubadilishwa tarehe ya mauzo, mtindo ambao upo katika machimbo ya kokoto na kifusi maeneo ya Bunju.

TMAA ni Wakala wa Serikali iliyoanzishwa Novemba 2, 2009 chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali, ukiwa na lengo la kuhakikisha kwamba Serikali inapata mapato stahiki kutoka kwenye shughuli za uchimbaji na biashara ya madini nchini.
 
Posted Mei25 2013 saa 20:45 PM
MWANANCHI

Inaeleza kuwa shughuli mbalimbali za usimamizi wa madini hufanywa na Shirika la Madini la Taifa (Stamico), ambalo linaimarishwa na Serikali ili kuboresha utendaji wake, lakini bado kumekuwa na kasoro kubwa katika uchapishaji wa mapato na kampuni zilizokaguliwa kwa mwaka.

Hizo kasoro mwandishi wa hii ripoti uchwara ameziona wapi wakati taarifa na takwimu zinapatikana kwenye mtandao kwa Wananchi wote kuona...!!??

Tanzania Minerals Audit Agency - TMAA | Publication / Report - TMAA Annual Report 2012
 
Siyo siri kwamba Watanzania tulikuwa haturidhishwi na mikataba ya uchimbaji wa madini mbali mbali ikiwemo dhahabu ambayo ilisainiwa Mkapa kwa kuwa ilikuwa haina maslahi na nchi. Hii ndiyo sababu ya Kikwete katika kampeni zake za Urais 2005 katika moja ya ahadi zake aliahidi kuipitia upya mikataba hiyo na kukaa chini na makampuni husika ili ifanyiwe marekebisho na hivyo kuongeza maslahi ya Tanzania na Watanzania. Pamoja na ahadi hizi za Kikwete hakuna chochote kile kilichofanyika zaidi ya kuongeza mrabaha kutoka 3% na kufikia 4%. Ongezeko ambalo bado ni dogo sana hasa ukitilia maanani bado makampuni hayo hayatozwi kodi yoyote nchini kutokana na mapato makubwa wanayoyapata baada ya mauzo ya dhahabu.

Muhongo alitangaza mwaka jana kwamba makampuni yote ambayo yanajishughulisha na uchimbaji wa madini nchini kwa miaka mitano na kuendelea yatatakiwa kulipa kodi ya 30% ili kuongeza mapato ya madini kwa Tanzania na kama hayataki kufanya hivyo basi yafungashe virago.

Energy and minerals minister Sospeter Muhongo as telling parliament that Tanzania's gold export earnings rose 31% last year to US$1.879 billion from US$1.436 billion a year earlier on higher world prices for the commodity.
The minister said the government wanted to earn higher revenues from mining companies due to the rising gold price, and added that it had ordered audits of all large-scale gold mines in the country to ensure that they started paying corporate taxes after recovering their costs of production.
"I am instructing all mining companies that have been in operation for more than five years to start paying corporate tax without any excuses," he added. "If they claim they are still making losses and can't contribute to the national economy through taxes, they should shut down their mines and leave because minerals do not rot."

www.miningreview.com | Tanzania introduces 30% corporate tax

****************************************************************

Baada ya Muhongo kutangaza hili la kuanza kuyalipisha makampuni ya uchimbaji wa madini nchini kutangazwa, kampuni ya Barrick ikatangaza kwamba inataka kuuza almost 75% ya hisa zake kwa kampuni ya China kwa visingizio mbali mbali ikiwemo gharama kubwa za umeme. Hili halikuwa halina ukweli wowote bali walikuwa hawako tayari kulipa kodi ya 30% ambayo ingepunguza faida yao ya kila mwaka. Kimya kimya kodi hiyo iliyotangazwa na Muhongo ikapigwa chini na Barrick wakasitisha nia yao ya kutaka kuuza 75% ya hisa zao kwa Wachina.

Barrick eyes Africa sale as problems mount - The Globe and Mail

****************************************************************************

Mapato ya nchi kupitia madini kwa miaka 13 kuanzia 1998 to 2011 yakiwa ni $445.2 million (3.9%) ukilinganisha na mapato ya makampuni hayo ya uchimbaji wa madini katika miaka hiyo 13 mapato ya $11.13 billion huu ni WIZI WA MCHANA KWEUPE na hili halina ubishi.

According to the chairman of the Public Organisations Accounts Committee (Poac), Mr Zitto Kabwe, Tanzania has only received minimal gains from mining.

Delivering a lecture at the National Defence College in the city last week on challenges and prospects of the mining sector in Tanzania, he said:

"Despite Tanzania having abundant wealth of minerals, the sector which has been growing on an average rate of 10.2 per cent since 2000, only contributes 3.3 per cent to the GDP in 2011 and employs just about one per cent of the total labour force."

He added that between 1998 and 2011, the total value of minerals exported from Tanzania was $11.13 billion. But in the same period the total Foreign Direct Investments (FDI) into the mining sector was only $3 billion while the total government revenue from the sector was $445.2 million.(peanuts)

https://www.jamiiforums.com/busines...ommercial-gold-mine-winds-up.html#post5314166

*********************************************************************

Hii annual report ya TMAA uliyoweka hapa sijui hata kama ulipata nafasi ya kuisoma vinginevyo ungeona jinsi wizi wa rasilimali za Watanzania unavyofanywa . Hapa chini ni mapato kama yalivyoonyeshwa na ripoti hiyo ya mwaka 2012 ya TMAA:
Mapato ya madini ya dhahabu katika migodi iliyotajwa ilikuwa ni $2,100,000, 000
Mapato ya madini ya shaba katika migodi hiyo ilikuwa ni $42,220,000
Mapato ya madini ya Fedha yalikuwa ni $10,500,000
_______________
Jumla $2,152,720,000

Katika ripoti hiyo inaonyesha Tanzania iliambulia mapato ya $71,100,000 million tu ambayo ni sawa na 3.3% kama mapato hayo ya$2,152,720,000 yangetozwa kodi ya 30% basi Tanzania ingeongeza mapato yake na kufikia $645,816,000 kodi plus royalties income of $71,100,000 total income kwa mwaka mmoja tu wa 2012 ingekuwa ni $716,916,000 badala ya $71,100,000 tu huu kama SI WIZI sijui ni kitu gani!!!!

Kama nchi ya dunia ya kwanza Australia inaweza kuyatoza makampuni ya uchimbaji wa madini kodi ya 30% sioni sababu ya Tanzania nayo kushindwa kufanya hivyo.

UPDATE 2-Australia's mining tax passes biggest political hurdle | Reuters

Wakati umefika wa kuhakikisha mikataba yote ya rasilimali za Tanzania inawekwa wazi ili kuona kama mikataba hiyo ina manufaa yoyote kwa Watanzania au ni wizi tu unaowatajirisha shareholders wa makampuni ya nje na makampuni hayo na mafisadi wachache ndani ya Serikali.

Tuache kukurupuka tuwe tunachambua vitu kwa kina kwa maslahi ya nchi yetu ili kujua hali halisi ya kile kinachoongelewa.

Back
Top Bottom