Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,051
- 23,499
Na kamarada Sebastian Emmanuel jr, MAFINGA
(Uchunguzi wa mwandishi wa habari hizi umebaini madudu Mengi ikiwa pamoja hata viongozi waandamizi wa Serikali ya JK kudanganywa na mwekezaji huyo pamoja na kupewa takwimu zisizo sahihi, kwa lengo la kujinufaisha kibiashara)
Kiwanda cha karatasicha Mufindi paper mills LTD (MPM) zamani Southern Paper Mills (SPM) kilichokuwa kinamilikiwa na serikali ya jamhuri ya Tanzania, chini ya shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kilichopo wilaya ya Mufindi, mkoa wa Iringa kinacho milikiwa na kampuni ya RAI GROUP LIMITED.
Kiwanda hiki cha mgololo kilianzishwa rasmi na kuzinduliwa na Rais wa kwanza wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, hayati Mwl. JULIUS. K. NYERERE mwaka 1985, kikiwa na jukumu la kuzalisha karatasi kwa kutumia malighafi za ndani na nje ya nchi kwa uchache, lengo ilikuwa ni kufanya biashara na kuongeza wigo wa ajira kwa watanzania.
Huko nyuma kabla ya kuuzwa Kiwanda kilikuwa chini ya shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) ambapo Tarehe 24/01/1997 kwa waraka wa serikali (Government Notes) namba 33, Serikali ili-specify Kiwanda na kukiweka chini ya tume ya kurekebisha mashirika ya umma (PSRC) iliyopewa jukumu la kusimamia shughuri za Kiwanda zikiwemo huduma kwa wafanyakazi wanaotunza kiwanda kwa kufanya uzalishaji mdogo mdogo (mill warming) na pia kukinadi hatimaye kukiuzwa kiwanda.
Leo sitaelezea historia ya Kiwanda hicho ila kupitia toleo lijalo utapata kujua mengi yanayo husu Kiwanda hicho. Ila leo tutaangalia namna ambavyo wamiliki wa Kiwanda wakitumika kuwanyanyasa wananchi wasio na hatia hasa wafanyakazi walio nje ya kazi tangu mwaka 2005 mpaka sasa huu ni mwaka wa 11 na hawajalipwa stahiki zao.
Chanzo chetu cha habari kinasema kuwa, tangu kipindi chote hicho aliyekuwa waziri wa viwanda na Biashara alikuwa ni Dr Juma Ngasongwa,ndiye aliyekuwa mhusika mkubwa kwenye kunadi na kuuzwa kwa Kiwanda hicho, chini ya Rais wa awamu ya tatu ya Mh Benjamini Willium Mkapa na waziri mkuu wa kipindi hicho alikuwa ni Fredirick Sumaye.
Tarehe 24.01. 1997 kwa mjibu wa waraka wa serikali ( Government Notes) namba 33, serikali ili specify Kiwanda na kukiweka chini ya tume ya kurekebisha mashirika ya umma (PSRC) iliyopewa jukumu la kusimamia Kiwanda zikiwemo huduma kwa wafanyakazi wanaotunza Kiwanda kwa kufanya uzalishaji mdogo mdogo (mill warming) na pia kukinadi na hatimae kukiuza Kiwanda.
Aidha taarifa tulizo nazo zinasema kuwa, Siku moja kabla ya makabidhiano ya mali (assets) kwa mwekezaji- yaani tarehe 12/2/2004, maafisa wa serikali kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara wakati huo (mrs Palyango) na kutoka PSRC (Mr Nsoya N. Magoti) waliitisha kikao na waliokuwa wafanyakazi wa SPM na kuwadanganya kuwa ajira na utumishi wao ungeendelezwa na kuboreshwa. Lengo la udanganyifu huo ulibainika baadaye kuwa walidhani ingepatikana endapo makabidhiano yangeshindikana.
Kwa mjibu wa taarifa tulizo nazo, zinasema kuwa, Mchakato wa uuzaji wa Kiwanda hicho ulifanywa kwa siri kubwa ambapo hata wafanyakazi ambao ndiyo wazalishaji wa bidha hiyo adimu barani Afrika hawakuhusishwa kwa lolote hasa kuhusu suala la masilahi yao na hatima yao. Hata kupatikana kwa mnunuzi, wafanyakazi waliona kupitia gazeti la serikali la Daily news la tarehe 16.10.2003.
Chanzo kimoja wapo cha taarifa hizi zinasema kuwa, Tarehe 13/02/2004 kiwanda kilikabidhiwa rasmi kwa Rai Group ya Kenya kwa maelezo ya kuwa wao ndio wanunuzi wa Kiwanda hicho adimu barani Afrika, ambaye naye katika hotuba yake siku hiyo aliwasifu sana wafanyakazi kwa kukitunza Kiwanda na kuwa kilikuwa na katika hali nzuri nay a kuendelesheka.
Taarifa inaendelea kusema kuwa, ilipofika tarehe 10/05/2004 uongozi wa MPM ltd ulianza zoezi la kuwaachisha kazi baadhi ya wafanyakazi wakiwamo wa ngazi za juu (menejiment) na wa chini kwa kigezo cha muda wa matazamio anaesema kuwa hii ilikuwa ni kinyume na makubaliano ya awali kuwa wangebaki kufanya kazi kama awali.
Mtoa taarifa mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe humu kwa kuhofia usalama wake (jina tunalo) ambaye ni mmoja wapo wa walioachishwa kazi, anasema kuwa, Tarehee 14/02/2014 wafanyakzi walianza kupata barua mpya za ajira kimyume na walivyoahidiwa na maafisa wa serikali waliotajwa hapo juu. Barua walizopewa zilikuwa na mda wa matazamio (probation Period) wa miezi sita, zenye mzunguko mpya wa likizo ( annual leave cycle) na ndani ya kampuni mpya ya Mufindi Paper Mills (MPM).
Aidha kwa upande mwingine, Taarifa hizo zinadai kuwa Katika hili la mnunuzi/ mwekezaji na PSRC walikuwa wakikana kwa kutupiana mpira kila mmoja akimsukuma mwenzake kuwa ndiye mwenye kuwajibika kulipa stahiki za wafanyakazi hao. Baada ya kukabidhiwa Kiwanda, mwekezaji aliwatumia wafanyakazi hao waliokuwepo kukarabati na hatimaye kuendesha Kiwanda huku akiendelea kuweka mazingira magumu ya kazi tafauti na hapo awali ilivyokuwa chini ya serikali kama ifuatavyo.
Aidha inadaiwa kuwa, baada ya kugundua udanganyifu huo, wafanyakazi wa Kiwanda hicho walijitahidi kufanya mambo kadhaa yaliyokuwa na nia ya kujua ukweli kwa kuwasiliana na uongozi wa Kiwanda na mamlaka husika. Hata hivyo huko nyuma baada ya kupata taarifa za ununuzi wa Kiwanda hicho kupitia magazeti, wafanyakazi 760 walifungua kesi ya madai kwa afisa kazi wa wilaya ya Mufindi, kulalamikia namna ambavyo mfumo wa ufukuzaji kazi wafanyakazi haukuzingatiwa. Taafifa zinaeleza kuwa Afisa kazi alimua kupeleka kesi hiyo kwenye mahakama ya kazi dhidi ya serikali, mnunuzi kwa kudai haki za wafanya kazi hao, mahamaka hiyo iliendesha kesi hiyo kwa miaka miliwi (2) tarehe 30/11/2007 wafanyakazi walishinda kesi kwa asilimia sabini 70%. kesi ambayo wafanyakazi hao wameshinda mara mbili na mwekezaji amekata rufaa mahakama kuu mpaka leo ni mwaka wa 11 (kumi na moja) haijamalizika licha ya juhudi kadhaa za viongozi wa kiserikali kuonesha nia ya kulishughurikia suala hilo lakini inaonekana kugonga mwamba.
• Kuwafanyisha kazi wafanyakazi masaa ya ziada bila malipo kinyume na utaratibu wa kazi na ajira.
• Kuongeza masaa ya kufanya kazi bila makubaliano na wafanyakazi.
• Kuondoa huduma za malipo kama ilivyokuwa awali
• Kufuta huduma ya chakula kwa wafanyakazi wakati wa kazi.
• Kutumia lugha chafu naya kibaguzi hadi kufikia kuwaita wafanyakazi wazalendo mbwa (ushahidi wa kimaandishi upo aliouandika mwajili mwenyewe)
Mtoa taarifa huyo anaelendelea kusema kuwa, Nguvu nyingi na vitisho vilitumika dhidi ya wafanyakazi hao na watendaji wa serikali hasa Dr Juma ngasongwa (mb) na mwekezaji, waliotafuta mbinu haramu ya kutaka waondoke kwenye nyumba za kiajira bila malipo, lakini wafanyakazi hao walipata afueni kutoka katika amri ya mahakama ya kazi kunusuru hali hiyo kwa shida sana hadi leo wafanyakazi hao wanaishi maisha ya taabu kama mtende katika jangwa.
Taarifa hizo zinaendelea kusema kuwa, Mchanganyiko wa matukio hayo na mengine mengi ulipelekea kuwepo kwa mgogolo mkubwa wa kikazi ambapo serikali (Dr Ngasongwa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara) akiwakilishwa na Mh. Pascal Mhongole ( aliyekuwa mkuuu wa wilaya ya Mufindi) ilileta askari wa kutuliza ghasia 150 (F.F.U) na wavurumisha /kuwaondoa kwa nguvu wafanyakazi nje ya Kiwanda ilikuwa ni tarehe 16/08/2005. Wakati huohuo serikali kupitia mkuu huyo wa wilaya alisoma tamko kuwa “wafanyakazi wote waondoke eneo la kiwanda na kwenda majumbani kwao au makambini (kwa waliokaa nyumba za kiajira) na kusubiri mpaka serikali itakapotafuta umbuzi wa matatizo yaliyokuwepo” mpaka sasa ni zaidi ya miaka 11 (kumina moja) serikali haijapata ufumbuzi wowote licha ya juhudi kadhaa kuchukuliwa bila ya muafaka wowote.
Kwa mjibu wa mtoa taarifa mwingine ambaye pia hakutaka jina lake litajwe humu kwa sababu za kiusalama anasema kuwa, Katika kipindi hicho chote cha subira, mwekezaji aliwagawa wafanyakazi katika makundi kama ifuatavyo;
Kuna waliofukuzwa kazi ambao walikuwa ni 119 wakiwamo viongozi wa chama cha wafanyakazi mahala pa kazi, waliotelekezwa na waliorudishwa kazini mpaka leo lakini nao wanalalamikia mishahala kucheleweshwa kinyume na sheria/ utaratibu wa kazi na mazingira magumu ya kufanyia kazi.
Taarifa za ndani zinaonesha kuwa, Tangu serikali ilipotoa tamko lake la wafanyakazi kutimuliwa na askari wa kutuliza ghasia (F.F.U) tarehe hiyo ya 16.08.2005. ambapo mpaka leo askari hao wa kutuliza ghasiabaadhi bado wapo, hakuna mtendaji yeyote aliyerudi pale kiwandani kwenda kuangalia au kujua hatima za wafanyakazi wale, (hata wanaokwenda wanaishia mikononi mwa mwekezaji kwa kupewa taarifa zisizo sahihi juu ya kiwanda hicho mpaka waandishi wa habari nao waliingia katika mkumbo huo) pamoja na hayo yote wafanyakazi hao bado waliendelea kuishi kwa shida na dhiki kubwa ndani ya nchi yao kuliko hata wakimbizi.
Aidha taarifa zinaonesha kuwa, Wafanyakazi hao hawakuwahi kupata ujira wowote tangu julai 2005. Licha ya mahakama ya kazi kuamuru wapatiwe huduma za kibinadamu wakati kesi yao ilipokuwa inaendelea lakini mwekezaji alidiriki hata kuwakatia hata huduma za umeme tangu mwezi October 2005 mpaka sasa.
Suala jingine alilofanikiwa kulitolea ufafanuzi ni suala la wafanyakazi walipo kazini wanaonyanyaswa anasema kuwa si kweli kwa kuwa hata wakiwahishiwa mishahara yao wanalalamika. Kwa hiyo wanalazimika kuchelewesha kwa makubaliano na wafanyakazi hao. Kitu ambacho wafanyakazi wanapinga vikali kuwa si kweli ila kuna wenzao wa chama cha wafanyakazi TUICO waliowasaliti kwa kushirikiana na chama cha mwajiri kinachoitwa MPETU. Kuwa kuna inasadikika kuna siku waliandika barua kwa waziri wa viwanda na biashara kuwa wanataka walipwe mishahara kuanzia tarehe 20 ya mwezi unaofuata.
Mtoa taarifa huyo anasema kuwa “Wafanyakazi wamezuiliwa na kunyanyaswa pia kupata huduma zozote eneo hilo kama vile kuzuiliwa kukata wala kuokota walau hata kuni za kupikia eneo hilo, mwekezaji alithubutu kufyeka mazao ya wafanyakazi kwenye mashamba waliyokuwa wakilima ili kujipatia walau chakula chao na badala yake yeye akapanda miti. Lakini pamoja na zambi zote hizo hapo juu, mwekezaji alikataa kujaza fomu za malipo halali ya mafao ya pensheni (PPF) tangu 2005 kwa baadhi ya wafanyakazi bila kuwa na sababu za msingi ingawa kuna taarifa zinadai kuwa serikali ilipeleka makato ya wafanyakazi hao katika mfuko huo (PPF) pamoja na kufanya mawasiliano mengi pande zinazohusika, wakuu wa mkoa (Iringa) na wa Wilaya (Mufindi) walikuwa wanalijua hilo” alisema mtoa taarifa wetu alipozungumza na mwandishi wa taarifa hizi huko mgololo.
Madhara ya ucheleweshaji wa kesi hiyo.
Kuna baadhi ya wahanga wa tukio hilo wapatao 87 mpaka sasa wamefariki dunia bila kujua hatima yao hivyo wamewaacha watoto katika makambi hayo wakiwa hawajui ni lini wataondoka na watakwenda wapi kwani hata ndugu zao wamewatenga, wengine wamerudi kwenye wimbi la umaskini na kukosa cha kufanya wamebaki omba omba kwa wenzao wanaoendelea na kazi, wengine ni wagonjwa na hawana msaada wowote ule nje ya wenzao ambao ni wazima wanaokwenda kuomba huku na kule ili wenzao wapone.
Wahusika (MUFINDI PAPER MILLS) wanasemaje?
Tulibahatika kukutana na meneja wa Kiwanda Ndg. Grerory Chogo pamoja na Afisa utumishi wa Kiwanda hicho aliyefahamika kwa jina moja ambaye pia anafahamika kama mwanasheria Ndg. Hery na kufanikiwa kuzungumza naye mazungumzo yaliyochukua takribani masaa mawili. Meneja anasema kuwa ni kweli kesi hiyo ipo mahakamani na wao pia wanaomba iishe ili wapate nyumba zao ambazo zinakaliwa na wafanyakazi hao waliopo nje ya kazi kwa amri ya mahakama kitu ambacho kinawafanya wafanyakazi wa sasa kukosa pahala pa kujisitili wakati wakiwa kazini, anasema kuwa “tumekuwa tukitafuta suruhu hata nje ya mahakama ili suala hili liishe ila cha kusikitisha ni kuwa kuna utata wa malipo je ninani anayetakiwa kulipa na tunalipa nini?” alisikika meneja huyo kwenye moja ya maswali aliyoulizwa na mwandishi.
Iadha meneja huyo anadai kuwa yaliyoelezwa na wahanga hao si ya kweli kwa kuwa wanawasaidia kama ndugu zao, na hata panapotokea msiba hujitokeza kuwasaidia.
Uchunguzi wa kina tena ukafanyika kubaini ukweli huo.
Mwandishi wa habari hizi alilazimika kuingia tena kazini kubaini ukweli wa taarifa hizi, kuwa si kweli kwa kuwa waandishi, wataalamu, viongozi wa serikali na watu wa kada mbalimbali wakifika kuthibitisha ukweli huo hudanganywa na viongozi wa Kiwanda hicho ila tayari mwandishi alibaini uongo huo kwa kuwa unakinzana na taarifa/ nyaraka mbalimbali kutoka ndani ya Kiwanda hicho ambazo zimenaswa kwa usiri mkubwa.
Angalizo likatolewa.
Itaendelea toleo lijalo.
Mmoja wa wadau wa maendeleo wilayani Mufindi,bwana Gwamaka Gwakisa anasema kuwa, Kwa manufaa ya Taifa letu,mwelekeo sahihi na Bora wa maongozi ya serikali yetu ya HAPA KAZI TUU na utawala bora, sii tuu itume tena jopo la wataalamu, kwa kuwa tayari zaidi za tume nane zimefika kiwandani hapo wakiwamo waandishi wa habari lakini wote waliishia mikononi mwa mwekezaji na kurudi bila ama habari za kupotoshwa. Bali serikali itazame upya kesi hii iliyochukua miaka 11 (kumi na moja), pili Rai yangu kwa mtendaji mkuu wa serikali yaani waziri mkuu alitazame upya mikataba na namna mchakato mzima wa uuzwaji na ubinafsishaji wa kiwanda hiki ulivyo fanyika. Tatu kituo cha uwekezaji yaani Tanzania Investment Center pia nao wachunguzwe kwa umakini kujua nini kilifanyika wakati wa mchakato huo.