Ripoti: Dereva aliyefia POLISI Chang'ombe alikabwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti: Dereva aliyefia POLISI Chang'ombe alikabwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, May 14, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,333
  Likes Received: 22,181
  Trophy Points: 280
  TUKIO la dereva teksi kufia kwenye Kituo cha Polisi cha Chang'ombe jijini Dar es Salaam limeingia sura mpya baada ya taarifa iliyoko kwenye kibali cha mazishi kilichotolewa na Idara ya Msajili wa Vizazi na Vifo kueleza kuwa alikufa kwa kukabwa na kukosa hewa.

  Taarifa hiyo imekuja wakati ndugu wa Marehemu Musa Juma (28) wakilalamika kuwa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limezuia ripoti ya uchunguzi wa kifo hicho kilichotokea mwezi Machi mwaka huu.

  Hati hiyo ya Msajili wa Vizazi na Vifo namba BD 0032825 iliyotolewa Machi 15 mwaka huu, pia imetofautiana na maelezo ya polisi kuhusu siku ambayo marehemu alikufa na sababu za kifo hicho.

  Wakati Machi 12 mwaka huu polisi ilisema kuwa marehemu alifariki Machi 10 katika Hospitali ya Temeke alikopelekwa kwa matibabu muda mfupi baada ya kukamatwa, Msajili wa Vizazi na Vifo amesema kifo hicho kilitokea Machi 9 kwa sababu ya kukabwa na kukosa hewa.

  “Juma alifariki hospitali muda mfupi baada ya kukamatwa na askari kwa ajili ya mahojiano Machi 10 mwaka huu, aliwaambia askari hao kuwa anajisikia vibaya ndipo alipochukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Temeke na kufariki dunia," Kamanda wa polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari.

  Kwa mjibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na msaidizi usajili wa kituo cha (MK71), marehemu huyo alifariki dunia kwa kukosa hewa ya kutosha.

  “Baada ya kuchunguza na kuthibitisha sababu ya kifo cha marehemu, natoa kibali cha mazishi", inasema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza, " sababu za kifo hicho ni ASPHYXIA,"kukosa hewa ya kutosha".

  Huu ni utata mwingine katika kifo hicho kilichovuta hisia kubwa kwa jamii baada ya awali ndugu zake kudai kuwa walikuta mwili wa marehemu una tundu sehemu ya mguu wa kushoti, uvimbe kichwani na kubabuka sehemu za siri.

  Juzi Msemaji wa familia hiyo Mwinjuma Mzee alilimbia gazeti hili kuwa familia ya marehemu imekuwa ikitafuta na kufuatilia ripoti ya daktari kuhusu uchunguzi huo siku zote bila ya mafanikio.

  “Tumekuwa tukifuatilia ripoti hiyo ili tuweze kuchukua hatua za kisheria, lakini wenzetu polisi wameshindwa kutupa ushirikiano. Mawakili wetu M$B LAW CHEMBERS nao wameandika barua polisi kuitaka ripoti hiyo, lakini pia hawajajibiwa,"alisema Mzee.

  Mzee alifafanua kuwa familia inafuatilia ripoti kamili ya kifo hicho ili iwe moja ya vielelezo itakavyotumia kuendesha kesi mahakamani dhidi ya wahusika wa tukio hilo.

  “Taarifa za awali tulizozipata kutoka kwenye kibali cha mazishi zinaonyesha kuwa kifo cha kijana wetu kimetokea katika mazingira yasiyo ya kawaida. Marehemu alikufa kwa kukosa hewa tumekuwa tukifuatilia, tunaitaka ripoti kamili ya uchunguzi ili tuweze kuchukua hatua za kisheria,"alisema Mzee.

  Alisema katika kufuatilia ripoti hiyo walikwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na kuthibitishiwa kwa mudomo kuwa ripoti hiyo iko tayari na kwamba imekabidhiwa polisi.

  Kova aliliambia gazeti hili kuwa hawezi kuzungumzia ripoti hiyo ya mazishi kwa kuwa ni ya kitaalamu zaidi.

  Alisema anachojua polisi imemaliza kazi ya kuchunguza suala hilo na sasa inasubiri ripoti ya daktari ili iweze kuwasilisha faili ya kesi hiyo kwa wakili wa serikali.

  Hata hivyo, alifafanua kuwa hadi sasa polisi wanne waliokuwapo siku siku ya tukio wametiwa mbaroni na kuhojiwa kuhusu kifo hicho.

  "Hilo ni suala la daktari, ninachoweza kusema uchunguzi wa kipolisi tumeshaukamilisha na tunachosubiri ni ripoti ya daktari ili tuweze kuiambatanisha kwenye faili na kulikabidhi kwa mwanasheria wa serikali," alisema Kamanda Kova.

  Siku chache baada ya dereva huyo kufariki dunia, jopo la madaktari walioshiriki kuufanyia uchunguzi mwili wake, walikubaliana kupeleka vimelea kwa Mkemea Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
   
 2. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  A very sad story; Yataisha lini haya?:angry:
   
 3. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ubabe huu wa polisi sijui utaisha lini jamani.,raia kufia mikononi mwa polisi ni jambo la kustaabisha sana.
   
 4. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Very sad, cjui lini police wataacha huu uuaji?
   
Loading...