John kisomo
Member
- Jan 21, 2019
- 22
- 40
Rafael 'Rafi' Eitan amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92.
Huyu na wenzake wachache ndiwo waanzilishi wa jumuia ya intelijensia ya Israel, Desemba 13, 1949.
Amewahi kuitumikia 'ShinBet' ambayo ni intelijensia ya ndani ya Israel mfano wa FBI ya marekani, kisha akaitumikia na kuiogoza Mossad, intelijensia ya kimataifa ya Israel.
Amefanya mengi ya kustaabisha ambayo yanaweza kuigwa na watu wema na waovu, katika kufanikisha malengo yao.
Moja ya misheni ya kustaajabisha alilowahi kutekeleza ni kumtafuta na kumkamata Adolf Einchman aliyekuwa kiongozi wa Nazi ya Ujerumani. Einchman alikamatwa siku ya Mei 11, 1960 huko Buenos Aires nchini Argentina na alitoroshwa hadi nchini Israel kupitia Senegal bila mamlaka za Argentina kujua.
Alishitakiwa nchini Israel na kuhukumiwa kunyongwa kwa kosa la mauaji ya halaiki ya waisrel, aliyofanya miaka ya 1940 wakati wa vita kuu ya pili ya dunia.
Jambo lingine la kumkumbuka Eitan ni namna alivyotumia utaalamu wake wa saikolojia ya tabia za wanadamu kwa kuwasajili mashushushu wa mataifa mengine ili wavujishe siri za mataifa yao kwa Israel, mfano mzuri ni shushushu
Jonathan Pollard wa Marekani aliyevujisha taarifa nyingi za sayansi ya nyuklia kwa Israel zilizosaidia uwezo wa Israel kutengeneza silaha za Nyuklia.
Jonathan Pollard aliishia jela huko Marekani kwa kosa la kuvujisha siri nyeti kwa taifa rafiki. La, ingelikuwa Israel na Marekani ni maadui, pengine Pollard angehukumiwa kifo.
Rafi Eitan alikuwa muuaji, mwenyewe aiwahi kukiri kufurahia rangi nyeupe ya macho ya mtu anayekata roho. Aliua kwa ajili ya Israel, hakusita kuua kwani naye alishuhudia mauaji ya halaiki ya nduguze wayahudi katika nchi mbalimbali za ulaya mashariki na magharibi.
Mathalani nchini Romania wayahudi walikusanywa viwanjani na kuchinjwa kama kuku, huko Ujerumani wayahudi walifungiwa kwenye vyumba vyenye gesi ya sumu na kuuawa kwa mamilioni. Adolf Einchman, akiwa chini ya Adolf Hiter aliratibu mauaji ya wayahudi takribani milioni sita wakati wa vita kuu ya pili ya dunia.
Roho ya kisasi ilibaki katika mioyo ya wayahudi wengi, lakini wachache waliamua kulipiza kwa vitendo, mmojawapo ni Rafael 'Rafi' Eitan, 'The master Kidnapper'.
Tukijaaliwa tutazungumzia zaidi misheni za huyu jamaa, ikiwemo 'Operation Finale' iliyohusu kumkamata mnazi Adolf Einchman.
Malaika wa mbinguni wamuongoze Rafi Eitan katika malango anayostahili kuingia.
Pata nakala ya kitabu; HISTORIA YA Israel
Post#71. Softcopy 1000 tuu.kufurahia Tz kufuzu Afcon. Vitabu vyote vyangu nauza elfu moja kwa siku tatu.
Whatsapp 0746609032