Ridhiwani Kikwete kachukizwa na kitendo cha Nape kumpa bendera Diamond Platnumz?

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,878
5,431
TFF nadhani mnajua kuwa Mungu wa Watanzania anawaona. Tumefika hapa baada ya Mpira kutushinda kabisa. Sasa tunatoa Bendera kwa wanaokwenda Kuburudisha na sio wanamichezo tena........ Ngashindwa mie. @dstvtanzania @mwigulunchemba @waziri_habari @sheila_simba @simbasctanzania @jerrymuro1980

9f3989c1d544f24d181a8d479bbcb7a4.jpg


Kayasema Hayo Kwenye Account Yake Ya Instagram...

Je Ni chuki?.... Kutomkubali Nape ?.. kutomkubali Diamond au Basi Tu
 
Jamaaa riz yuko sahihi kabisa unajua inauma sana badala ya timu yetu kupewa bendera ikatuwakilishe (IMESHINDWA) ndio maana anaumia kupewa msanii wa muziki.... Tena tunajitangazia kwa furaha.... Ni aibu jamani NEXT TIME tujitahidi...
Kama timu zetu zinafanya mbofumbofu, zinafanya ouvyoouvyo, kwanini tusijiliwaze kwa burudani mbadala?
Hauwezi kushangilia ama kuunga mkono kitu kisichokuridhisha bana!
 
Hilo neno "Ngashindwa" pia kaliandika Mh.Mbunge? Yule Mzee kifimbo cheza inabidi arudi maana wachafuzi wa lugha wanazidi kuongezeka
 
>>>>>Diamond anaenda kuiwakilisha Tanzania ipi??

Nyimbo zake zenyewe hazina mahadhi ya Kitanzania..... Ukiangalia video ya Diamond huwezi jua kuwa ni Mtanzania.


Ni aibu kubwa kwa TFF na Nape..
 
Back
Top Bottom