Ridhiwani abariki Takukuru wamchunguze!

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
51,614
68,543
Aliyasema hayo mjini bagamoyo kwamba amechoka kuchafuliwa na vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ameomba vyombo usika kumchunguza mali zake.





Inputs zetu.

Haya haya Takukuru anzeni na machimbo ya mawe na mchanga iringa,kisha njooni kwenye kiwanda cha cement(mkuranga),mkimaliza njooni buyuni kwenye heka 15 baharini,kisha njooni mbezi kwenye ikulu ndogo,mkimaliza chunguzeni maroli yale 200,pia njooni big bon sinza,pia ile bil64 ya epa ichunguzwe iliyorudishwa.

Source:Jambo Leo
attachment.php
 
Takukuru ya Tanzania au Scotland Yard? Kama ni hii takukuru ya Hosea bora yaishe hivi hivi kwani mshindi anafahamika kabla ya mechi.
Niwape mfano halisi, hapa Mwanza hiyo 'sakosi'inayoitwa takukuru wanafanya komedi moja ya uchunguzi kwa mfamasia wa jiji, wameshindwa na juzi nilisikia wamekamata magari yake(mitumba). Kwa aina yao ya utendaji ndio maana hatuwezi kutofautisha vishoka wanaojiita takukuru na takukuru 'orijino'.
 
Muda huu hatuhangaiki naye maana tunajua anaongea kwakujipambanua sana, na hata kazi ya mkewe ichunguzwe maana nasikia hakufanya hata interview bali alichomekwa wakati watu walipigishwa interview na kijana mmoja akapata baadae akaambiwa asubiri ataitwa ikawa ataitwa mama wawatu akajianzia kazi
 
Angefanya hivyo tangia mwanzo wa tuhuma na siyo kuwa kimya na baada ya kuficha vilivyokuwa vikilalamikiwa ndo anatoa ruhusa sidhani kama itasaidia
 
Wachunguze na mkopo wa elimu ya juu aliopatiwa mkewe ilihali hakustahili
 
Siku chache zilizopita niliandika habari juu ya TAKUKURU. Hii tume imeoza and they are not fair at all. Tume gani inakamata walalahoi na kuacha wezi walio kubuhu katika kuibia serikali? Hapa mechi imekwisha na matokeo yameshabandikwa ikulu. Hata iweje TAKUKURU haimchunguzi Ridh wala nini, wao watakula posho tu na kutapatapa vijiweni na nyumba ndogo zao pamoja na kutishia watu ili waachwe wafanye porojo zao. Kweli rais, YOU ARE NOT FAIR yourself, what is the point of this TAKUKURU? Hapa TZ viongozi wengi tu wezi na wala rushwa mbona hatusikii wanakamatwa? What are you really doing to us?
 
View attachment 55713

Waingereza wana kitu kinaitwa "Common Law," yani sheria za nchi yao ambazo hazijaandikwa na Bunge na huwezi kutajiwa kifungu na namba na kadhalika lakini zipo na zinajulikana na zina nguvu kama legislation iliyoandikwa na Bunge na jaji lazima azifuate. Zimejengeka kwa mazoea lakini zina nguvu ya sheria za dola!

Common Law yetu sisi Tanzania inatamka wazi kuwa Kinga ya Rais inatandaa ukoo mzima wa Rais! Kwa hiyo hata Ridhituu, yani uzao wa kuume wa Ridhiwani, achana na Ridhiwani, mtoto wa Ridhiwani ambae atarithi hayo ma Big Bon na malori 200, hatahojiwa na mahakama yeyote ya sheria kwa vitendo na maamuzi yeyote atakayofanya akiwa amebeba ubini wa Rais na kadi ya Chama Cha Mapinduzi.
 
Angefanya hivyo tangia mwanzo wa tuhuma na siyo kuwa kimya na baada ya kuficha vilivyokuwa vikilalamikiwa ndo anatoa ruhusa sidhani kama itasaidia
awe na subira tu kidogo, nina imani baada ya miaka kama miwili au mitatu hivi kuanzia sasa tutakuwa na TAKUKURU mpya na imara!
 
Kama anauwezo mkubwa hivyo kwanini asilipe mkopo wa bodi wakapata na wengine?
 
Ah atupishe nae huyo hana mpya anajificha kwenye kivuli cha babake asubiri babake ashuke kwenye kiti atakiona kilicho mtoa kanga manyoya.
 
awe na subira tu kidogo, nina imani baada ya miaka kama miwili au mitatu hivi kuanzia sasa tutakuwa na TAKUKURU mpya na imara!

Teh teh teh.
Watu mna mambo!
Hivi Takukuru anayo refer huyu dogo ni hii hii inayoongozwa na Eddy Hosea ama nyingine?
 
Ahaaaaaaaaaaaa ...kumbe takukuru mpaka awaruhusu ndipo waende kumtembelea Etieee.
 
Ridhiwani endelea kula maisha tu siku ikifika hutawakumbusha takukuru kufanya kazi yao.!
 
Back
Top Bottom