Mantombazane
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 579
- 367
Jana 18/06/2015 kwenye muda wa saa 3.30 kuelekea saa 4.00 asubuhi kulikuwa na kipindi RFA ambacho sikikumbuki jina lake lakini watangazaji walikuwa wa kike wakipokea wakizungumza na kupokea sms kutoka kwa wasikilizaji na kuzungumza mambo mbali mbali yanayo husu matukio yaliyowatukia watu walipokuwa wanasoma shule za msingi na hasa kuhusiana na walimu mbali mbali jinsi walivyokuwa wanawachapa viboko kwa makosa mbali mbali.
Ambacho sikukipenda ni ile tabia ya kutaja majina ya walimu redioni kuwa eti waliwachapa viboko wengine wakisema viboko vinne, wengine sita na wengine tisa. Cha ajabu na watangazaji nao wakawa wanataja majina ya walimu waliowachapa wakati wakiwa shule za msingi.
Sijui wengine wataonaje lakini mimi naona huo sio ungwana kuanza kuwaanika redioni walimu waliowaadabisha nyakati hizo. Historia kama hizo zinapaswa kuzizungumzwa watu wakikutana au bila kutaja majina ya wahusika hadharani kwani ni kama kutaka kuonesha kuwa walimu fulani walikuwa wakorofi, wakali, waonezi nk wakati wao walikuwa wanatimiza wajibu wao wa kusimamia nidhamu ya wanafunzi kwa mujibu wa sheria na ndio maana baadhi ya wanaowaanika walimu wao redioni wako katika nafasi mbali mbali za kiutendaji. Kama wangewaacha bila kuwaadabisha huenda nao wasingefanikiwa kimaisha kwani wangeharibika.
Mimi nashauri mtindo huo uachwe kwani unakera walimu wenyewe ambao wengine wameshatangulia mbele za haki, wengine kustaafu, wengine bado wako kazini na wengine wako katika nyadhifa mbali mbali.
Hao akina dada walikuwa wanaongoza hicho kipindi kama wanaona raha kuanika redioni majina ya walimu wao waliowaadhibu basi wangeanika na majina ya wavulana waliowavunja bikira kama kwao halitakuwa jambo la kuwefedhehesha.
RFA rekebisheni ujinga huo.