Review: Magufuli Elimu bure ni ndoto ila Elimu bora inawezekana, tukubali kuchangia elimu

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,595
Dhana ya elimu bure ni nzuri kwa kuwa ina lengo la kumpunguzia mwananchi gharama na kuhakikisha elimu inapatikama kwa kila mtoto. Changamoto ni nyingi

Kwa kawaida shule nyingi za serikali zina wastani wa wanafunzi kati ya 800 hadi 1300 hivyo uwezo wa serikali kuzihudumia kwa 100% na kuleta matokeo chanya ni mdogo!

Hivyo ni muhimu kurudisha dhana ya wananchi KUCHANGIA ELIMU ila ikiwa katika maboresho zaidi! Ambapo ada itakuwa lets say elfu 40 kwa kila mwafunzi na PASIWEPO NA MICHANGO MINGINE! Fedha hizo ziwekwe kwenye account ya shule husika na zitumike kwa nahitaji muhimu kama vile Kununulia CHAKI, KARATASI, KULIPA MLINZI, KUCHAPISHIA MITIHANI, NA KUNUNULIA VIFAA VINGINE!

Jukumu la serekali likabaki kulipa mishahara, kuboresha miundombinu kama madawati, maabara, maktaba, ukaguzi kusimamia mitaala na kulipa fedha za ziada zitazohitajika

CALCULATION
Tufanye wastani wa Wanafunzi ni 1000 so kila mwanafunzi alipe 40,000= 40,000,000 kwa mwaka
...shule zenye wanafunzi wachache kama 500 itakuwa 20,000,000 kwa mwaka
Endapo mfumo huu utasimamiwa vizuri utakuwa na matokeo mazuri kwa elimu yetu

Updates
Elimu bure kaa la moto D’ salaam
Wakati Serikali ya Awamu ya Tano ikisisitiza kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari,
Wanafunzi wa darasa la pili wa Shule ya Msingi Mbezi Ndumbwi wakiwa darasani huku wengine wamekaa chini kutokana na upungufu wa madawati shuleni hapo, Dar es Salaam jana. Picha na Herieth Makwetta
Dar es Salaam. Wakati Serikali ya Awamu ya Tano ikisisitiza kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari, mpango huo umesababisha adha kwa baadhi ya shule ikiwamo kukosekana walimu wa ziada, kuibwa vifaa vya kufundishia na ongezeko la wanafunzi.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika shule za msingi na sekondari katika wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke, umebaini kuwa mpango huo badala ya kuwa msaada kwa walimu umekuwa mzigo unaowapasua kichwa.
Fedha za ruzuku zinazopelekwa katika shule kwa mchanganuo maalumu kulingana na idadi ya wanafunzi, hazikidhi matumizi ya shule hizo hata kwa wiki mbili.
Mchanganuo wa fedha za ruzuku Wilaya ya Kinondoni, unaonyesha kuwa ni shule tano pekee ambazo zimepewa fedha ya chakula ni Kawe A, Mbuyuni, Msasani A, Msewe na Sinza Maalumu, huku nyingine zote zikiwa hazina fedha za kulipa walinzi, bili ya maji, umeme, ukarabati wa madawati, madarasa na vyoo.
Katika Wilaya ya Temeke, shule kadhaa zimevunjiwa madarasa, ofisi za walimu na kuibwa vifaa vya kufundishia, meza, viti kutokana na kukosekana walinzi ambao walikuwa wakilipwa kwa ushirikiano wa shule na wazazi. Mlinzi mmoja hulipwa kati ya Sh150,000 hadi 200,000.
Mpango huo umekuwa mwiba mchungu kwa walimu wa shule hasa za sekondari ambao walitakiwa kuwa wabunifu kwa kutafuta jinsi ya kuongeza ufaulu wa wanafunzi na kushirikiana na wazazi kulipa walimu wa ziada hasa wa masomo ya sayansi.
“Nimeajiri walimu sita wa masomo ya sayansi kwa kushirikiana na wazazi, ambao hapa kwangu nina mahitaji makubwa huku akiwapo mmoja aliyeajiriwa na Serikali. Kwa mwezi nawalipa Sh300,000 hadi 350,000, najiuliza nitawalipa nini na fedha ya ruzuku haina fungu hilo? Bado mlinzi, bado maji, bado umeme, nimechanganyikiwa natamani kurudi kijijini nikalime kuliko fedheha hii, ”alisema mmoja wakuu wa shule ya sekondari wilayani Temeke ambaye hakuwa tayari jina lake liandikwe gazetini.
Alisema mwaka huwa ana mitihani minne wa Machi, Juni, Septemba na Desemba, ambayo kila mmoja hadi unamalizika humgharimu Sh1.5 milioni, kwa bahati mbaya fedha ya ruzuku aliyopata kwa mchanganuo wote ni Sh4.8 milioni hivyo kwa mitihani pekee anatumia Sh6 milioni ambazo hafahamu atazitoa wapi huku fedha za ruzuku zikiacha hayo yote bila majibu wala ufafanuzi.
“...Wazazi wametangaziwa elimu bure kwa kishindo, sielewi itakuwaje na waliendelea kufundisha mwezi uliopita wananidai na sifahamu mwezi huu nitawapa nini,” alisema mwalimu mwingine.
Katika shule za msingi, tatizo kuu lililojitokeza ni wanafunzi kuwa wengi kuliko uwezo wa shule.
“Mwaka jana na mwaka juzi, wiki ya kwanza shuleni nilikuwa nimekadiria kuandikisha wanafunzi 250, wakaongezeka hadi 300, lakini hadi asubuhi ya leo (jana) nimeandikisha wanafunzi 600, ” alisema mwalimu mkuu wa shule moja wilayani Temeke ambaye pia aliomba jina lake lisiandikwe gazetini.
Alisema kwa ongezeko hilo kila darasa watakaa wanafunzi 150 badala ya 50 waliokuwa wanakaa awali.
“Hatuwezi kuwakataa tutaambiwa tunakataa wanafunzi, bado wanakuja hadi Machi, sijui itakuwaje,” alisema mwalimu mwingine wa shule ya msingi wilayani humo.
Alisema mbali ya hilo wamelazimika kutoa elimu ya ziada kwa wazazi, kutokana na wengi wao kuwaleta wanafunzi wakiwa hawana kitu chochote hadi begi la kubebea madaftari.
“Ukiwauliza wazazi mbona mtoto hana kitu zaidi ya sare alizovaa anakuambia wametangaziwa elimu bure, kibaya zaidi hata nembo hawana, tunashindwa kuwaambia walipe Sh500 au 1,000 ya nembo watasema tunawalipisha,” alisema.
Alifafanua ikitokea wanafunzi wamepata matatizo itakuwa ngumu kuwatambua, kutokana na kutokuwa na nembo,” alisema.
Akizungumzia changamoto ya ruzuku, Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda alisema shule zinazopata tabu ya ruzuku ni zenye wanafunzi wachache kwani zilizo na wengi hazipati adha hiyo kwa kuwa zinapata fedha nyingi.
Alisema Serikali imepanga kila mwanafunzi kwa mwaka atumie Sh10,000 hivyo zitatolewa kidogokidogo hadi zitimie: “Hizo changamoto zilizopo zitafanyiwa kazi taratibu lakini fedha iliyopo itumike kulingana na maelekezo yaliyotolewa.”
 
Last edited:
Dhana ya elimu bure ni nzuri kwa kuwa ina lengo la kumpunguzia mwananchi gharama na kuhakikisha elimu inapatikama kwa kila mtoto. Changamoto ni nyingi

Kwa kawaida shule nyingi za serekali zina wastani wa wanafunzi kati ya 800 hadi 1300 hivyo uwezo wa serekali kuzihudumia kwa 100% a kuleta matokeo chanya ni mdogo!

Hivyo ni muhimu kurudisha dhana ya wananchi KUCHANGIA ELIMU ila ikiwa katika maboresho zaidi! Ambapo ada itakuwa lets say elfu 40 kwa kila mwafunzi na PASIWEPO NA MICHANGO MINGINE! Fedha hizo ziwekwe kwenye account ya shule husika na zitumike kwa nahitaji muhimu kama vile Kununulia CHAKI, KARATASI, KULIPA MLINZI, KUCHAPISHIA MITIHANI, NA KUNUNULIA VIFAA VINGINE!

Jukumu la serekali likabaki kulipa mishahara, kuboresha miundombinu kama madawati, maabara, maktaba, ukaguzi kusimamia mitaala na kulipa fedha za ziada zitazohitajika

CALCULATION
Tufanye wastani wa Wanafunzi ni 1000 so kila mwanafunzi alipe 40,000= 40,000,000 kwa mwaka
...shule zenye wa afunzi wachache kama 500 itakuwa 20,000,000 kwa mwaka
Endapo mfumo huu utasimamiwa vizuri utakuwa na mahoteo mazur kwa elimu yetu

Let say, shule ina walinzi watatu na muhudum mmoja wa ofisi(PC) na wanalipwa 200,000/ kwa mwezi kila mmoja = 9,600,000/=kwa mwaka, kutoa copy mitihani sh.50 per page(mtihani ni zaidi ya page moja) kwa masomo 11, monthly test, midterm test, terminal na annual(kumbuka shule nyingi hazina umeme wala vifaa vya kutolea copy), kununua kemikali za maabara kwa ajili ya practical (pita madukani kaulize bei zake), vifaa vya kufundishia na kujifunzia mf. kalamu, maandalio, madaftari, chaki, manila n.k n.k kwa mwaka mzima, unadhani hizo mil.10.4 kwa wanafunzi 500 au mil.30.4 kwa wanafunzi 1000 zinatosha!? kabla hamjalijadili hili watafuteni wakuu wa shule na maafisa elimu wilaya au mkoa muwaulize kwanini walikubali michango ya pembeni kama ya ulinzi, taaluma, na ukarabati walibariki itozwe!
 
Me nasubiri kuona how it will work,hadi february ntakua na mchango mujarabu,maana jamaa watakua wameshatumia za January
 
Let say, shule ina walinzi watatu na muhudum mmoja wa ofisi(PC) na wanalipwa 200,000/ kwa mwezi kila mmoja = 9,600,000/=kwa mwaka, kutoa copy mitihani sh.50 per page(mtihani ni zaidi ya page moja) kwa masomo 11, monthly test, midterm test, terminal na annual(kumbuka shule nyingi hazina umeme wala vifaa vya kutolea copy), kununua kemikali za maabara kwa ajili ya practical (pita madukani kaulize bei zake), vifaa vya kufundishia na kujifunzia mf. kalamu, maandalio, madaftari, chaki, manila n.k n.k kwa mwaka mzima, unadhani hizo mil.10.4 kwa wanafunzi 500 au mil.30.4 kwa wanafunzi 1000 zinatosha!? kabla hamjalijadili hili watafuteni wakuu wa shule na maafisa elimu wilaya au mkoa muwaulize kwanini walikubali michango ya pembeni kama ya ulinzi, taaluma, na ukarabati walibariki itozwe!
Mkuu nakubali kuwa garama ni kubwa kwa serekali kumudu ndo maana nikaja a concept ya cost sharing kwa maana mzazi anachangia pia serekali inachangia! Mil 40 kwa wanafunzi 1000 hazitoshi ndo hapo serekali itatoa fungu lake kufidia hela iliyopungua
 
Last edited:
Wewe utakuwa mwalimu nadhani. Hakuna cha bure kama hewa isipokuwa ni kwamba serekali inalipia hiyo elimu. C umesikia mabilioni yanapelekwa mashuleni?? Chamsingi ni serekali kuhakikisha fungu lakutosha halikosekani.
 
Mabilioni yameshapelekwa tusubiri tuone how it works. Naamini calculations zilizofanywa na wataalam ni accurate.
 
Dhana ya elimu bure ni nzuri kwa kuwa ina lengo la kumpunguzia mwananchi gharama na kuhakikisha elimu inapatikama kwa kila mtoto. Changamoto ni nyingi

Kwa kawaida shule nyingi za serekali zina wastani wa wanafunzi kati ya 800 hadi 1300 hivyo uwezo wa serekali kuzihudumia kwa 100% a kuleta matokeo chanya ni mdogo!

Hivyo ni muhimu kurudisha dhana ya wananchi KUCHANGIA ELIMU ila ikiwa katika maboresho zaidi! Ambapo ada itakuwa lets say elfu 40 kwa kila mwafunzi na PASIWEPO NA MICHANGO MINGINE! Fedha hizo ziwekwe kwenye account ya shule husika na zitumike kwa nahitaji muhimu kama vile Kununulia CHAKI, KARATASI, KULIPA MLINZI, KUCHAPISHIA MITIHANI, NA KUNUNULIA VIFAA VINGINE!

Jukumu la serekali likabaki kulipa mishahara, kuboresha miundombinu kama madawati, maabara, maktaba, ukaguzi kusimamia mitaala na kulipa fedha za ziada zitazohitajika

CALCULATION
Tufanye wastani wa Wanafunzi ni 1000 so kila mwanafunzi alipe 40,000= 40,000,000 kwa mwaka
...shule zenye wa afunzi wachache kama 500 itakuwa 20,000,000 kwa mwaka
Endapo mfumo huu utasimamiwa vizuri utakuwa na matokeo mazur kwa elimu yetu
Hata mm nilikua nafikiria kuboresha elimu kwanza ili baadae waangalie uwezekano wa kuwa bure wakati tayar elimu inayotolewa ni bora. Kwa mfano umegusa masuala ya miundo mbinu. Ni kweli. Serikali kwa Bajeti yake haitaweza kukidhi mahitaji yote ikiwa no pamoja na kuwasomesha bure. Ni bora wangeboresha kwanza
 
Ila ukiangalia haya masuala yanafanywa kisiasa
 
Hata mm nilikua nafikiria kuboresha elimu kwanza ili baadae waangalie uwezekano wa kuwa bure wakati tayar elimu inayotolewa ni bora. Kwa mfano umegusa masuala ya miundo mbinu. Ni kweli. Serikali kwa Bajeti yake haitaweza kukidhi mahitaji yote ikiwa no pamoja na kuwasomesha bure. Ni bora wangeboresha kwanza

Nadhani umenielewa lengo langu! Serekali iboreshe miundombinu wakati huo wananchi wanachangia elimu! Hii itaipu guzia garama serekali hivyo kutoa fursa ya ukuaji wa elimu
 
Wewe utakuwa mwalimu nadhani. Hakuna cha bure kama hewa isipokuwa ni kwamba serekali inalipia hiyo elimu. C umesikia mabilioni yanapelekwa mashuleni?? Chamsingi ni serekali kuhakikisha fungu lakutosha halikosekani.
Mm sio mwalimu ni mwananchi wa kawaida..... Lengo ni kuwa wananchi wachangie elimu huku serekali kuu ikiboresha mazingira kama nadawati, nadarasa, maabara, nyumba za waalimu, na maktaba.

Nikatoa mfano sbule yenye wanafunzi 1000 kila mwanafunzi akilipa 40,000 ni sawa na 40,000,000 ambazo zitasaidia garama za uendeshaji huku serekali ikiongezea pale inapolazimu.
Ni kweli ni ngumu kwa serekali kumudu garama za uboreshaji pamoja na uendeshaji
 
mwenyewe naona serikikali ingehakikisha kunakua na maabara nzuri, madawati na vitabu kabla ya kusema bure
 
Nikwelj mkuu kusema elimu bure wakati hakuna madawati, maabara na maktaba ni matatizo...... Bora serekali ijidhatiti kuboresha miundombinu wakati huo wananchi wanachangia gharana za uendeshaji!
Baada ya hapo tuendelee na dhana ya elimu bure
 
Elimu bure tena bora inawezekana serikali iongoze mikakati ktk kukusanya mapato tukifikia trillion 2.5 elimu na inchi itakuwa imekaa vizuri
 
Back
Top Bottom