Revealed: NASA’s grand plan to bag 9 million votes

kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,092
2,128
By Nzau Musau and Jacob Ng’etich | Updated Sun, April 30th 2017

In an elaborate plan seen by Sunday Standard, the emboldened opposition grouping projects to score 9,109,344 votes against Jubilee’s 7,297,800 votes.

They project 85 per cent voter turn-out in the country —16,407,144 voters out of the estimated 19,302,522 registered voters.

From its core support base of the Luhya, Kamba and Luo communities, NASA approximates that it will bag a total of 5.6 million votes — 1.7 million from Kambas, 1.7 million from the Luo and 2.2 million from the Luhya community.

From the document, Jubilee will score zero votes from the Luhya community it has worked fl at out to impress. It will also score zero votes among the Luo and Kamba.

Modest figures

Saturday, NASA Pentagon member Musalia Mudvadi projected that they would get more votes than these “modest figures” when they launch massive campaigns in the next few weeks.

He said they intend to knock on every door and ensure they win the presidential vote in the first round. Another Pentagon member Moses Wetang’ula said they would penetrate the Jubilee stronghold and win over more voters.

From the NASA document, the opposition expects to top up their votes from the Maasai (256,118), Kisii (660,000), Somali (660,000), Mijikenda (680,000), Meru (74,000), Turukana (300,000),Teso (124,000) and Kuria (81,000) among others.

The party is counting on its newly-minted principal Isaac Ruto to deliver at least 205,000 votes from the Kalenjin nation. In contrast, the analysis approximates that Jubilee will bag 4.8 million votes from its core support base of Kikuyu and Kalenjin communities.

In 2013 election, the two communities voted Jubilee man-to-man. From the Kikuyu’s, Jubilee will scoop the entire 3,035,621 of the voters who will turn out to vote. And from the Kalenjin Jubilee will get 1,845,162 votes.

The document says the total number of registered Kikuyu voters is 3.5 million but projects that only three million will turn out to vote.

Similarly, the Kalenjin vote stands at 2.4 million according to NASA strategists, but only two million will turn out on Election Day.

To add up to their 7.2 million votes, NASA believes Jubilee will get 64,000 votes from the Maasai, 283,000 from the Kisii, 440,000 from Somalis, 667,000 from the Merus, 128,000 from the Turkana, and 297,000 from the Embu among others.

In Nairobi, NASA approximates that the Kikuyu vote to stand at 706,000 followed by Kamba (381,000), Luhya (338,000) and Luo (324,000). The calculations done by a group of consultants engaged by the NASA principals ignores the impact of Jubilee inroads in Coast, lower Eastern and Western. Presidential line-up.

Jubilee for supper

In the 2013 polls and according to the official figures, President Uhuru Kenyatta beat Raila Odinga, the main opposition candidate by 832,887 votes. Kenyatta scored 6,173,433 against Raila’s 5,340,546. On Thursday, NASA announced its presidential line-up with Raila at the top and his 2013 running mate Kalonzo Musyoka as his deputy.

“This time, we are ahead of them in this game. We have done our mathematics and we have the fi gures ready with us. Trust me, on August 8, we will have Jubilee for supper,” ODM Director of Elections Junet Mohamed told Sunday Standard.
Revealed: NASA’s grand plan to bag 9 million votes
 
That will be a decisive victory, but the analysis seems to err on some assumptions that Jubilee will get zero from Kamba and Luhya land. Such assumption would have been valid had NASA opted for Mudavadi with Kalonzo as DP or vice versa.
 
Huwa natamani sana waanzilishi wetu wangaliweka mfumo tofauti wa siasa,labda sera ama hata siasa za uchumi kuliko ukabila.
Ikiwa tutapona huu ugonjwa na tutoke salama Kenya hilo ni Maulana tuu atatusaidia tuondokane na janga hili.
Kila jamii huwa na wasiwasi juu ya jamii nyengine ,ndani kwa ndani,na kuogopana bure tu! kutokana na mbegu za siasa za kikabila na kishetani.
Trust me wakenya inside the machismo and the bravado of whatever community lies fear and hope that all of us will be one Kenya one day,tunachonganishwa na kuogopeshwanisha(for lack of a better word) ,hata Mungu analijua hili.
 
NASA ilivyo kaa
sijui wacha tuendelee kufuatilia kabla ya mwezi 8
Kuna vituko vingi vitatokea
 
Huwa natamani sana waanzilishi wetu wangaliweka mfumo tofauti wa siasa,labda sera ama hata siasa za uchumi kuliko ukabila.
Ikiwa tutapona huu uganjwa na tutoke salama Kenya hio ni Maulana tuu atatuokoa na janga hili.
Kila jamii huwa na wasiwasi juu ya jamii nyengine ndani kutokana na mbegu za siasa za kikabila na kishetani.
Trust me wakenya inside the machismo and the bravado of whatever community lies fear and hope that all of us will be one Kenya one day,tunachonganishwa na kuogopeshwanisha(for lack of a better word) ,hata Mungu analijua hili.
.Linawezekana
kama mnaweza kuunganisha Muungano wa Wagombea
mnapaswa kila upande uwe na Kila kabila.
Lakini mkiacha hivyo hali itazidi kuwa mbaya,
Kumeanza kuzuka Vitu vya hovyo hata kabla ya Kampeni halisi
 
Ninyi mmewezaje kuondokana na hili utata kwenye maswala yenu ya kisiasa mkuu?
Kwasababu sidhani kua ukabila ni mfumo,hilo siamini abadan!..ni sera tu tena bovu sana.
 
Mtu wa kulaumiwa kwa Kenya nadhani ni Jomo Kenyatta, alitengeneza taifa lenye kupendelea watu wake na kubagua makabila mengine. Pia, hata vijana wa Kenya nao wanaendekeza ukabila kwa hiyo kubadilisha hali hii inakuwa ngumu.
Sisi tulibahatika kupata Rais wa kwanza ambaye hakupandikiza sumu hii ya ukabila na ubaguzi mwingine.
 
Kwa hili la Hayati Mhe. Mwalimu, mlineemeka!
Mungu husitupite jamani.....:confused:(kwa sauti yake C. Shusho)
 
Kwahiyo NASA wameona hawapati kitu KIKUYU?

Siasa za Ukabila mbaya sana.
 
Mtu wa kulaumiwa kwa Kenya nadhani ni Jomo Kenyatta, alitengeneza taifa lenye kupendelea watu wake na kubagua makabila mengine. Pia, hata vijana wa Kenya nao wanaendekeza ukabila kwa hiyo kubadilisha hali hii inakuwa ngumu.
Sisi tulibahatika kupata Rais wa kwanza ambaye hakupandikiza sumu hii ya ukabila na ubaguzi mwingine.

Miaka yote nilikua naamini hivyo, kwamba nchi ilianza ukabila baada ya Kenyatta kuwa rais, lakini baadaye nikaanza kusoma historia ya Kenya taratibu na kuona taharuki za kikabila zilikuwepo hata kabla nchi haijapata uhuru.
Pia punde baada ya kupata uhuru kulikua na miungano na mahesabu ya kikabila, haya mambo ya ukabila yalianzishwa awali sana. Mzungu alitugawa kwenye divide and rule, hata wakati anaondoka nchi alikua na mahesabu aachie uongozi wa nchi kwenye kabila lipi.

Muingereza hakua na haja ya kuwatenganisha Watanganyika maana nchi yenu alihodhi kutoka kwa Mjerumani na alijua ataachia tu, hivyo hakua na nia ya kung'ang'ania. Kuna mzee fulani alinipa historia ya Tanganyika pale nilipoanza kumsifia Nyerere kwamba ndiye kazuia ukabila Tanzania, mzee aliniweka sawa kabisa kwamba Nyerere alikuta Watanganyika wameungana tayari wakati anatokea kwa Butiama.

Tatizo kubwa Kenya ni kwamba kila mmoja anataka kuelekeza kidole cha lawama kwa mwnezie ilhali yeye hapo alipo anaendekeza ukabila. Unakuta wanasiasa wanaunda muungano wa tribal lords halafu wanaelekeza kidole cha lawama kwa mlengo wa pili. Hadi wote tukubali tuna uchafu, hamna hatua tutakaypiga maana mkiunda muungano wa kikabila, upande wa pili nao wanajikusanya kikabila ili kukabana nanyi.
 
Ahsante mkuu!

Lakini kama MWANZILISHI ,Kenyatta angeliona hili kwa mbali na kulishughulikia upesi.
Nafahamu kama taifa changa kulikua na changamoto nyingi zaidi, kama uvamizi wa ghafla uliokusudiwa toka Somalia.
Pia nilisoma pahali Muingereza alihofia uvamizi wa Ethiopia chini ya dikteta Mussolini wa Italia dhidhi ya koloni lake Kenya.
Nafikiri nguvu zote zilielekezwa kule.
 
Miaka yote nilikua naamini hivyo, kwamba nchi ilianza ukabila baada ya Kenyatta kuwa rais, lakini baadaye nikaanza kusoma historia ya Kenya taratibu na kuona taharuki za kikabila zilikuwepo hata kabla nchi haijapata uhuru.
Pia punde baada ya kupata uhuru kulikua na miungano na mahesabu ya kikabila, haya mambo ya ukabila yalianzishwa awali sana. Mzungu alitugawa kwenye divide and rule, hata wakati anaondoka nchi alikua na mahesabu aachie uongozi wa nchi kwenye kabila lipi.

Muingereza hakua na haja ya kuwatenganisha Watanganyika maana nchi yenu alihodhi kutoka kwa Mjerumani na alijua ataachia tu, hivyo hakua na nia ya kung'ang'ania. Kuna mzee fulani alinipa historia ya Tanganyika pale nilipoanza kumsifia Nyerere kwamba ndiye kazuia ukabila Tanzania, mzee aliniweka sawa kabisa kwamba Nyerere alikuta Watanganyika wameungana tayari wakati anatokea kwa Butiama.

Tatizo kubwa Kenya ni kwamba kila mmoja anataka kuelekeza kidole cha lawama kwa mwnezie ilhali yeye hapo alipo anaendekeza ukabila. Unakuta wanasiasa wanaunda muungano wa tribal lords halafu wanaelekeza kidole cha lawama kwa mlengo wa pili. Hadi wote tukubali tuna uchafu, hamna hatua tutakaypiga maana mkiunda muungano wa kikabila, upande wa pili nao wanajikusanya kikabila ili kukabana nanyi.

Mzizi mkuu wa tatizo hili ni Wakoloni walipojaribu kulazimisha makabila tofauti yaishi pamoja. Kila kabila lina mila na desturi zake kwa hiyo kuwaweka pamoja watu tofauti kama hawa haiwezekani.

Kuhusu Mwalimu na Tanzania, kama Mwalimu angefanya kama Jomo kuvamia maeneo ya makabila mengine na kuwaweka Wazanaki wenzake hali ingekuwa mbaya kama Kenya. Mwalimu hakuwa mbinafsi na mkabila kama Jomo ndio maana hakumuibia mtu ardhi yake wala hakujilimbikizia mali.
 
Kilam Mkuu!

Ushabik kando, Muingereza alitawala kwa formula liitwalo DIVIDE AND RULE, aliwaadhibu makabila yaliyokuwa yakipambana kujinyakulia uhuru ,akawatenga kama mahasidi huku akijaribu kupandikiza chuki na kujaribu kuwatenganisha na wale waliokua hawana harakati za mapambano hadharani.
Loyals and rebels.
Mfaransa naye alikua na formula liitwalo ASSIMILATION POLICY. Kwa hiyo MK254 ana hoja kuu.
Haya yote yapo kwenye somo la Historia ya (scramble for Africa),sijui huwa mnaenda kusomea ujinga hizo shule ama ndio ma saint Kayumbaz!
 
Hehe nimekuja humu najiuliza NASA space agency wanatafuta tena votes zq nini, nakuta ni politics za Kenya, hehe Kenyans nimewanyanyulia mikono, hilo jina tu lazima wabebe votes.
 
Kilam Mkuu!

Ushabik kando, Muingereza alitawala kwa formula liitwalo DIVIDE AND RULE, aliwaadhibu makabila yaliyokuwa yakipambana kujinyakulia uhuru ,akawatenga kama mahasidi huku akijaribu kupandikiza chuki na kujaribu kuwatenganisha na wale waliokua hawana harakati za mapambano hadharani.
Loyals and rebels.
Mfaransa naye alikua na formula liitwalo ASSIMILATION POLICY. Kwa hiyo MK254 ana hoja kuu.
Haya yote yapo kwenye somo la Historia ya (scramble for Africa),sijui huwa mnaenda kusomea ujinga hizo shule ama ndio ma saint Kayumbaz!

Hiyo 'divide and rule' ni upuuzi ambao hauna maana. Wakikuyu, Wakalenjini, Wajaluo na wengineo hawakuwa wakiishi pamoja kabla ya Wazungu. Kosa kubwa ni kulazimisha Wajaluo, Wakikuyu, Wakisii, Waluhya na wengineo waishi pamoja.

Sasa hivi ingekuwa Raila kiongozi wa Wajaluo na Uhuru kiongozi wa Wakikuyu kusingekuwa na shida. Kila kabila ilitakiwa liishi peke yake na siyo kuchanganyikana.
 
Mzizi mkuu wa tatizo hili ni Wakoloni walipojaribu kulazimisha makabila tofauti yaishi pamoja. Kila kabila lina mila na desturi zake kwa hiyo kuwaweka pamoja watu tofauti kama hawa haiwezekani.

Kuhusu Mwalimu na Tanzania, kama Mwalimu angefanya kama Jomo kuvamia maeneo ya makabila mengine na kuwaweka Wazanaki wenzake hali ingekuwa mbaya kama Kenya. Mwalimu hakuwa mbinafsi na mkabila kama Jomo ndio maana hakumuibia mtu ardhi yake wala hakujilimbikizia mali.

Jomo Kenyatta anazo lawama pia, maana yeye kazidisha uchafu wa muingereza badala ya kutafuta mbinu za kupunguza. Japo aliridhi nchi ikiwa na tension kibao za masuala ya ardhi, kuna watu walikwenda kupigana na mzungu mbugani almaarufu kama maumau, waliporudi na kupata ardhi zao zimenyakuliwa, akawasogesha kuishi kwengine.
Pia naye akajilimbikizia kijisehemu ambacho kimetumika kama propaganda dhidi ya hata wale walinunua ardhi kihalali. Sio kila Mkikuyu anayeishi bonde la Ufa kwamba alinyakua ardhi wala nini.

Hapo pa Nyerere kutowasaidia Wazanaki, wale ni kabila ndogo sana hata waliopo Dar ni wa kuhesabu. Hiyo nchi yenu uongozi ungepewa kabila kubwa au hata makabila ya kutajika kama Wachagga, basi mngekua na tension za kiaina japo hazingekua kubwa kama Kenya maana nchi yenu ni kubwa kiasi hata ukijilimbikizia ardhi hutoimaliza. Wazanaki ni kabila ndogo ambao sio aggressive sana, leo hii Wachagga hata ukienda maeneo ambapo yeye ni mkurungezi lazima utakuta amewajaza jaza Wachagga humo humo, hilo lipo hata kwa Wahaya, nakumbuka kile kisa cha ufisadi wa Rugemalira alivyokula na Wahaya wenzake.
 
Hiyo 'divide and rule' ni upuuzi ambao hauna maana. Wakikuyu, Wakalenjini, Wajaluo na wengineo hawakuwa wakiishi pamoja kabla ya Wazungu. Kosa kubwa ni kulazimisha Wajaluo, Wakikuyu, Wakisii, Waluhya na wengineo waishi pamoja.

Sasa hivi ingekuwa Raila kiongozi wa Wajaluo na Uhuru kiongozi wa Wakikuyu kusingekuwa na shida. Kila kabila ilitakiwa liishi peke yake na siyo kuchanganyikana.

Oya!..wanyantuzu,wasukuma pamoja na wamaasai walikua wakishi pamoja na waarabu na waunguja pamoja na wazaramo?
 
Back
Top Bottom