Kwa Tanzania sheria inasema kile mlicho chuma mkiwa pamoja ndo kinagawanywa sawa kwa sawa kama hamna watoto, lakini kama mna watoto yule anayekaa/kutunza watoto ndo anapewa robo tatu ya mali. Hii inamaanisha watoto nusu ya mali, baba robo na mama robo.
Na hii haiangalii nani anazalisha zaidi ilimradi tu mali hizo mmezipata mkiwa pamoja. Nadhani wanaoachana baada ya miezi hawastahili hata kuwa na kesi yoyote kwa sababu kila mtu anaweza kuondoka na alichokuja nacho. Ikiwa mmoja atamkataa mwenziwe basi asidai chochote, na yule anayekataliwa ana haki ya kushitaki ili alipwe fidia na yule anaye mkataa, na sheria zipo (za madai)