Report ya kamati ndogo ya bunge-sector ya gas

TzPride

JF-Expert Member
Nov 2, 2006
2,616
1,167
Habari za asubuhi waheshimiwa. Ninaomba kama kuna mtu anaweza kuweka copy ya report kamati ndogo ya bunge iliyoundwa kuchunguza sector ya gas.
Nitashukuru kwa msaada huo.
 
Asante mkuu PhD. Ingekuwa vizuri tukaipitia kabla ya kuwa tabled, ili tuweze kuona relevance ya michango ya waheshimiwa wa mjengoni.
 
TAARIFA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI ILIYOSHUGHULIKIA UENDESHAJI WA SEKTA NDOGO YA GESI NCHINI


Mheshimiwa Spika, awali ya yote naomba kuchukua fursa hii kwa niaba ya wajumbe wenzangu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Nishati na Madini kukushukuru wewe binafsi kwa kutoa kibali ili Kamati ya Nishati na Madini kupitia Kamati yake Ndogo kufanya kazi
kwa lengo la kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya kikatiba ya Bunge katika kuisimamia na kuishauri Serikali na vyombo vyake kwa
niaba ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


View attachment kamati gesi new 2 Ammended.pdf 2.pdf
 
Wadau natafuta ile ripoti ya Tume ya Kamati ya Nishati na Madini iliyoongozwa na Januari Makamba kufuatilia hali ya uzalishaji Gesi Tanzania.

Tunaomba iwekwe hapa ili wachambuzi tuisome kwa undani...!

Asanteni
 
Naunga mkono hoja unajua tulikuwa busy na masuala ya akina Jairo tukasahau mambo muhimu sana.


Wadau natafuta ile ripoti ya Tume ya Kamati ya Nishati na Madini iliyoongozwa na Januari Makamba kufuatilia hali ya uzalishaji Gesi Tanzania.

Tunaomba iwekwe hapa ili wachambuzi tuisome kwa undani...!

Asanteni
 
Hii ripoti ni nzuri sana...! Hawa jamaa walifanya uchambuzi wa kina kuhusu upataikanaji na uzalishaji wa Gesi Tanzania. Walionyesha pia ni kwa kiasi gani Serikali yetu imekua ikiibiwa na kupoteza fedha kwenye masuala ya Gesi Tanzania...!

Tafadhali mwenye nayo naomba taupatie hapa...!
 
Nedha kwenye jukwaa la jamii inteligency utafute bandiko " tanzania gas" ndo utajua maana ya January Makamba. Na utajua pia kuwa bunge linaendeshwa nje ya bunge.
 
Na Zitto Kabwe,

Mkutano wa Tano wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
pamoja na mambo mengine ulijadili
Taarifa ya Kamati ya Bunge ya
Nishati na Madini kuhusu Sekta
ndogo ya Gesi nchini. Taarifa hii ilitokana na kazi iliyofanywa na
Kamati ndogo iliyoundwa na Kamati
ya Nishati na Madini chini ya
uongozi wa Mbunge wa Bumbuli
ndugu Januari Makamba. Miongoni
mwa Hadidu rejea za Kamati ndogo zilikuwa ni kubainisha kama
Mikataba, taratibu na Kanuni
zinazotawala shughuli za gesi
zinazingatia maslahi ya Taifa na
hazitiliwi shaka na wadauna
Kubainisha kama maamuzi yanayoendesha shughuli za gesi
kama vile gharama za ujenzi,
uendeshaji na mambo mengine
yanayoweza kuathiri gharama na
usalama wa shughuli yanafikiwa
kwa ufanisi na yanazingatia maslahi ya Taifa. Taarifa ya Kamati iliwasilishwa
Bungeni na kupitishwa na Bunge ili
Serikali iweze kutekeleza maazimio
zaidi ya ishirini na Sita
yaliyopendekezwa. Miongoni mwa
Maazimio hayo ni Azimio namba mbili ambalo linasema ‘Kamati
imejiridhisha bila shaka kwamba
kwa kipindi cha 2004 hadi 2009
Kampuni ya Pan African Energy
Tanzania Ltd (PAT) imejirudishia
isivyo halali gharama zinazofikia jumla ya dola za kimarekani milioni
28.1 sawa na fedha za kitanzania
bilioni 46.3. Kutokana na kujirudishia
fedha hizo isivyo halali kumefanya
Serikali kukosa gawio lake linalofikia
dola za kimarekani milioni 20.1. Aidha, mpaka wakati Kamati
inaandaa ripoti hii, Kampuni ya Pan
African Energy Tanzania Ltd (PAT)
imeshindwa kuwasilisha uthibitisho
wa uhalali wa kujirudishia gharama
nyingine zinazofikia jumla ya dola za kimarekani milioni 36. Hali hii
inaonyesha mashaka makubwa
katika uendeshaji wa sekta hii
muhimu ya gesi’. Azimio hili ni moja ya Azimio
linalopaswa kuangaliwa kwa makini
sana tunapojadili namna Tanzania
inavyosimamia na kufaidika na
Sekta ya Mafuta na Gesi. Taifa
linafaidika kwa kiwango gani na Wawekezaji wanafaidika kwa
kiwango gani ndio msingi wa
Mikataba ya Mafuta na Gesi nchini.
Hapajawa na mijadala mikali katika
eneo hili kama ilivyo kwenye sekta
ya Madini na hivyo kuachia kila kukicha Shirika la Maendeleo ya
Mafuta Nchini (TPDC) likisaini
Mikataba ya Kutafuta na kuchimba
Mafuta na Gesi (Production Sharing
Agreements – PSAs) bila Watanzania
kujua haswa ni jambo gani linasainiwa. Hivi sasa kuna Mikataba
hii 23 hapa nchini. Duniani kote kuna familia mbili za
mikataba ya Mafuta na Gesi. Familia
ya kwanza inaitwa ‘concessionery’
ambapo Kampuni ya Mafuta ya
Binafsi inapewa haki zote za
mchakato mzima wa kutafuta, kuchimba, kusafirisha na kuuza
Mafuta au Gesi. Umiliki wa Mafuta
(rights) unakuwa ni wa Kampuni
Binafsi na sio Serikali. Katika mfumo
huu Kampuni hulipa mrahaba
Serikalini na kodi zinazopaswa. Nchi kama Marekani, Uingereza na Canada
hutumia mfumo huu. Familia ya pili ni Mikataba ya
Uzalishaji au kwa Kiingereza
Production Sharing Agreements
(PSAs). Katika mfumo huu Haki
(right) inabakia kuwa mali ya Taifa
husika na Kampuni ya Mafuta huwa ni kama mkandarasi tu wa kutafuta
na kuchimba mafuta. Akipata
mafuta, anaondoa gharama za
kuzalisha na faida inagawiwa kati ya
Kampuni hiyo na nchi husika kupitia
Shirika la Mafuta. Huu ndio mfumo unaotumika hapa Tanzania na
ulianzia huko Indonesia na
Venezuela miaka ya sitini.
Kutokanana mfumo huu ndio
tunapata masuala haya ambayo
Kamati ya Nishati na Madini imegundua kama nitakavyofafanua
kwa ufupi hapa chini. Mkataba wowote wa Mafuta na Gesi
ni lazima uzingatie Uzalishaji na
Mapato kwa ujumla, mrahaba kwa
nchi, urejeshaji wa gharama za
uzalishaji na kodi mbalimbali na
namna faida inavyogawanywa. Kampuni ya Pan Africa Energy
kujirejeshea gharama isizostahili za
zaidi ya shilingi 46 bilioni ni sehemu
ya mianya iliyopo katika mikataba
yetu. Jumla ya shilingi 110 bilioni
zimeonekana kuwa na mashaka makubwa katika mahesabu ya
Kampuni hii. Taarifa inaonyesha kwamba
Kampuni hii imeweka pia Gharama
zao za uzalishaji kwa miradi ya nje
ya Tanzania. Kwa kuwa Kampuni ya
Pan Africa Energy Tanzania Limited
ni Kampuni Tanzu ya Pan Africa Energy iliyosajiliwa ‘offshore’
Mauritius ambayo nayo ni Kampuni
tanzu ya Orca ambayo pia
imesajiliwa visiwa vya Jersey,
Tanzania isingekwepa kubambikiwa
gharama ambazo si zake ili kupunguza mapato ya Serikali ya
Tanzania. Imewahi kuelezwa huko
nyuma kwamba hizi njia za
kukwepa kodi zimeshamiri sana
kutokana na Makampuni makubwa
yanayofanya biashara hapa nchini kufanya ‘tax planning’ na hivyo
kuhamisha mapato yao kwenda nchi
zisizo na kodi kubwa kama
Mauritius, Isle of Man, Jersey au hata
City of London. Mwaka 2009 mwezi Aprili katika
Taarifa yake ya mwaka, Kamati ya
Hesabu za Mashirika ya Umma
ililiambia Bunge kwamba Mkataba
kati ya TPDC na Pan Africa Energy ni
moja ya mikataba mibovu kuliko yote nchini. Hii ilitokana na ukweli
kwamba kwa mujibu wa PSA kati ya
TPDC na Pan Africa Tanzania,
mrahaba wa mafuta wa asilimia 12
unalipwa na TPDC na pia Kodi ya
Mapato inakokotolewa kutoka katika mrahaba huo. Kwa maana
hiyo Kampuni hii hailipi Mrahaba na
pia hailipi kodi ya Makampuni
(corporate tax) kwa mujibu wa
Mkataba. Suala hili Kamati ya Nishati
na Madini haikuliangalia (labda kwa kuwa ni la kimahesabu). Kamati ya
POAC ilitaka mikataba yote ya
Mafuta iangaliwe upya ili kuondoa
mazonge haya yanayokosesha Taifa
mapato makubwa sana. Uwezo wa TPDC kukagua mahesabu
ya Kampuni za utafutaji mafuta ni
mdogo au haupo kabisa. Kama TPDC
wangekuwa na uwezo huu leo
Kamati ya Nishati na Madini
isingekuta madudu haya katika kampuni. Pia kama Kamati ya
Nishati na Madini ingeangalia
mikataba ya kampuni zote za
kutafuta mafuta wangekuta madudu
mengi zaidi. Kuna kampuni moja
yenye kisima pale Mkuranga, wamesema gharama za kuchimba
visima vile ni dola za Kimarekani
240 milioni ilhali gharama halisi ni
dola za kimarekani 60 milioni tu.
Hivyo Gesi ikianza kuchimbwa
itabidi warejeshe gharama zao kwanza. Tanzania haitapata lolote
mpaka Gesi ile itakwisha. Kuna haja ya kufanya marekebisho
makubwa sana katika uendeshaji na
usimamizi wa sekta ya Gesi
Tanzania. Shirika la TPDC
lirekebishwe kwa kuanzisha
Mamlaka ya Mafuta na Gesi yenye uwezo na nguvu ya kusimamia
uwekezaji katika sekta hii. Vilevile
kuwepo na Shirika la Mafuta na Gesi
(PetroTan –National Oil and Gas
Company) ambalo litashiriki katika
uwekezaji kikamilifu na kampuni binafsi. Tusiposimamia vema sekta
hii Taifa letu litaingia kwenye
matatizo makubwa sana huko siku
za usoni. Maneno ya Mwana Uchumi Gwiji
Joseph Stiglitz ni ya kuzingatia sana.
Anasema, Mara zote nchi
zinazoendelea zijue,
wanapojadiliana na Kampuni kubwa
za Mafuta, Kampuni hizi hufikiria jambo moja tu. Jambo hilo ni
kuongeza mapato yao kwa
kupunguza mapato ya mataifa
husika. Tanzania ni lazima ihakikishe
kwamba inapangua mbinu zote za
Makampuni makubwa kwa kujenga uwezo wa Wananchi wake kupitia
Shirika la Mafuta na Gesi kuweza
kuwa na mikataba yenye kujali faida
kwa nchi. Hili la Pan Africa Energy
litufumbue macho.
 
Safi sana mh zitto.....hivi ndivyo tubategemea wabunge wetu wote wafanye.
 
Back
Top Bottom