Report: Iranians use Israeli-made app during protests

FACTS Kwa Uturuki Labda Abadilike Sana Aseee Turkey kaishakaliwa hana athari yoyote kwa Israel, rejea habari za Kargil war kati ya India na Pakistan utafahamu nguvu ya Israel mdogo wangu
 
Labda wabadilike Sana Maana IRAN Anaweza Asimame Apambane na ISRAEL Anamuweza Kabisa Ila Jirani Zake Wataungana Kuwa AGAINST Nae Kama watakaa wao kwa wao ISRAEL Anakalishwa
Kid jifunze kuandika vizuri kwanza ndivyo uniite hivyo!
No any Muslim country can beat Israel.

Don't swell up your head sycophantic again
No any Muslim country can beat Israel.

Don't swell up your head sycophantic again
 
Saudi Arabia au
 
Siku zote hawa jamaa waturuki mimi huwa siwaelewi kabisa,hafadhali Iran anayejionyesha waziwazi...Turkey the sleeping Lion.
Maangamizi la taifa la Israeli li mkononi mwa uturuki, tunasubiri tu siku ziongee
 
Una uhakika gani ya kwamba mimi ni mdogo kwako?
Una miaka 23 tu, hata hadhi ya kuwa mdogo wangu hauna kwa hakika maana mdogo wangu wa mwisho ana miaka 25
 
Siku zote hawa jamaa Waturuki mimi huwa siwaelewi kabisa,hafadhali Iran anayejionyesha waziwazi...Turkey the sleeping Lion.
Mkuu SirChief, muda huwa ni mwalimu mzuri mno. Huwa tunabishana hapa na kupeana kejeli nyingi, lakini nadhani mwaka 2023 tumepata uzima ni vema tena tukaupitia huu mjadala kuhusu taifa la Uturuki.

Migogoro mikubwa duniani imethibitisha jinsi Uturuki ilivyojijenga kidiplomasia, kijeshi na kiuchumi. Hakuna mgogoro wowote ule mkubwa uliotokea Ulaya na Mashariki ya Kati ndani ya 2020-2022, taifa la Uturuki halijahusika.

Migogoro ya Nogorno-Karabakh, Ukraine, Iraq, Syria na Serbia serikali ya Uturuki imekuwa na ushawishi mkubwa kidiplomasia kuliko taifa lolote lile la NATO kwasababu za kijiografia, kihistoria na kitamaduni.

Dola la Ottoman lilifika eneo lote la Transcaucasia na Balkans, na miaka mia-moja baada ya kuanguka jamii za kituruki (Turkic People) ambazo ni waislamu utazikuta kwenye nchi kama Georgia, Azerbaijan, Armenia na Serbia/Kosovo. Taifa la Uturuki lina ushawishi mkubwa mno juu ya hizi jamii mpaka leo.

Kwenye mgogoro wa Ukraine, Uturuki kama taifa lisilofungamana na upande wowote (A Neutral State) limetumika na Urusi na NATO kama kitovu cha usafirishaji wa gesi kwenda Ulaya. Urusi siyo rafiki wa Uturuki, lakini anafahamu fika kwamba ni lazima ashirikiane naye, hasa kiuchumi kwa kuwekeza miundo-mbinu ya gesi nchini kwake ili kutanua uwanja wake wa usambazaji.

Nchi za Magharibi nazo zimefahamu kwamba Uturuki ndani ya NATO amekuwa na nguvu kubwa siyo kwasababu ni mwanachama. Lakini kwasababu za kihistoria na kijiografia ambazo ziko nje ya uwezo wa NATO, lakini bila hivyo Uturuki ingeshashughulikiwa na ingeshatolewa NATO kitambo mno.

Huu udhaifu NATO anaufahamu na Uturuki ameutumia kujipa manufaa kidiplomasia, kwa kula chakula Urusi na kulala Brussels. Muhimu pia ni kwamba Umoja wa Ulaya (EU) hauwezi kutatua migogoro mikubwa barani humo bila Uturuki, hata kama siyo mwanachama.

Ila pia tatizo la wahamiaji haramu kutoka Afrika na Mashariki ya Kati, ambako kuna migogoro mikubwa lango lake kubwa ni Uturuki.

Kule Mashariki ya Kati, nchi zenye nguvu kubwa kiushawishi ni Israel, Saudi-Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Iran na Uturuki. Kiufupi ukitaka kufanikisha chochote kwenye huu ukanda ambao umejaa mataifa ya kiislamu ni lazima uongee vizuri na ushirikiane na Iran, Saudi-Arabia, Uturuki na UAE.

Hili halijalishi wewe ni Marekani, Umoja wa Ulaya au Uchina. Huwezi kufanya lolote bila kuyashirikisha haya mataifa niliyoyataja. Ila sasa, Uturuki ni tofauti kidogo na mataifa mengine kama Iran, Saudi na UAE, kwasababu yeye ana kitu ambacho Israeli anacho: NGUVU KUBWA YA KIUSHAWISHI BARANI ULAYA kwasababu yeye ni taifa ambalo liko Mashariki ya Kati na Ulaya.

Wanazuoni wa sayansi na siasa, na mahusiano ya kimataifa kama Prof Graham T Alison, kutoka chuo cha Harvard wanasema kwenye ukanda wowote ule, yanapokuwepo mataifa mawili yenye nguvu basi tegemea mtafaruku mkubwa mno. Hili analiita The Thucydides-Trap.

Mashariki ya kati, wenye nguvu kubwa ni Uturuki na Israel. Hawa wawili watakuja kushindana mno huko mbeleni, tena katika kiwango kisicho cha kawaida. Siyo lazima wapigane kijeshi, lakini watafanyiana hujuma nyingi mno.

Mengine sitayasema, lakini miaka mingi ijayo tutashuhudia mengi mno. Tuombe uzima...

Mkuu Consigliere tunaupitia huu uzi tena mwaka 2023, ili tujisahihishe pale ambapo tafakuri zetu zilijikwaa katika kuangalia mambo...
 
Unaamanisha Turkey mkuu? Alipowekewa kikwazo kauchumi kidogo tu akaanza kujamber nakukimbilia Kwa Althan Qatar nakumpigia magoti nakuomba msaada nakupewa 14 billion dollars akapumua
Bwana Copenhagen, muda huwa ni mwalimu mzuri mno. Hii hoja uliitoa mwaka 2019 kwa ujasiri mno. Ukiangalia kinachoendelea leo hii duniani, bado unaamini Uturuki ni taifa la kupuuzwa ???
 
Uturuki kwa juujuu linaonekana ni taifa la kawaida sana lakini ni tofauti na wengi wanavyo dhani.
 
Kihistoria inaonesha kuwa kuanguka kwa ottoman empire wayahudi walichangia saana pia haohao wayahudi walichelewesha kuanguka kwa ottoman empire
Ottoman Empire lilianza kudorora muda mrefu mno na kuna sababu nyingi. Hasahasa, Arab Nationalism ambayo ilichangiwa na Waingereza. Hayo mengine mtawasingizia tu Wayahudi.
 
Muda tu ndiyo utasema yote...
Tunahitaji mchango wako sana kwenye hii vita ya Ukraine na geopolitics za sasa, yaani pale unapohitajika wewe ndo unapotea, kwa nini lakini? BTW kwa nini 2023 ni mwaka wa maajabu?
 
Kwa hiyo msomi wa Cambridge akisema jambo,linakua sahihi.?
 
Kama ni Uturuki huenda upo sahihi ila sio sahihi Sana.....

Uturuki ambayo inahamu ya kujiunga na EU itaweza vipi kuivimbia Israel ambaye ni mshirika muhimu wa EU ?... Uturuki bado pia ni mnunuzi mkubwa wa silaha kutoka US na nchi za NATO.

Isitoshe kujiingiza kwa Uturuki kijeshi kwenye nchi za kiarabu kama Syria, Libya kutaleta matatizo huko mbeleni na jambo hili haliwafurahishi nchi kama Saudia na umoja wa nchi za Ghuba.
 
Uturuki ambayo iko NATO ambako Marekani ndio kinara wa huo umoja iwe na vita na Israel maajabu hayo una maono ya ajabu sana.
Bado unaamini kuna kwamba haiwezekani ???
😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…