Rematch Floyd Mayweather Vs Canelo Alvarez.

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,464
21,195
Wakati ulimwengu ukijiandaa kuangalia pambano la kukata na shoka kati ya Floyd Mayweather(The Pretty Boy) na Conor McGregor mnamo tarehe 26 August pamoja na lile la Canelo Alvarez na Gennady Golovkin mnamo September.


Wadau wengi wa ngumi pamoja na ma boxer's wengi wamekuwa na mtazamo tofauti hasa pambano la Floyd na McGregor.


Miongoni mwa mabondia wanaolipinga kwa vikali pambano ni pamoja na Manny Pacquiao au mzee wa cherehani kama vijana wengi wa mtaani wanavyopenda kumuita kutokana na kasi na ngumi zake nyingi za mfululizo kwa wakati mmoja .

Pacquiao amekuwa akiliponda mara kwa mara pambano hilo akidai kuwa McGregor hana uwezo hata kidogo wa kumkalisha Floyd hivyo kitendo cha kumpanga Floyd na McGregor ni kitendo cha kumuonea sana McGregor na kumuongezea idadi ya mapambano ya ushindi Floyd



View attachment 552843


Mbali na Pac,bondia mwengine ambaye aliwahi kutamba miaka ya nyuma kidogo aitwae Sugar ray Leonard naye amekuwa akikosoa vikali pambano hilo ,hata hivyo kadri hili pambano linavyozidi kukosolewa ndivyo hamu ya kutazama pambano hili linazidi kuzidi na wadhamini wengi ndivyo wanavyozidi kumiminika.


Katika pambano hilo Floyd ataondoka na dola za kimarekani 250Million wakati Conor atapata us dollars 75Million ingawaje kwa Conor hili ndilo pambano alilopata pesa kubwa zaidi.


Floyd amedai kuwa hili ndilo pambano lake la mwisho na hatopigana tena.

Lakini wapenzi wa mchezo wa boxing wamemtaka Floyd kabla hajastafu apande ulingoni arudiane na Canelo Alvarez.

Santos Saul Alvarez au jina la utani Canelo Alvarez amepigana mapambano 51 na kati ya hayo ameshinda 49 ametoka sare pambano moja na amepigwa pambano moja na Floyd Mayweather .


Mashabiki wa Canelo wanadai Floyd alimpiga Canelo kipindi kile kwa sababu Canelo hakuwa na uzoefu wa kutosha kipindi hicho ila kwa sasa wanaimani kubwa Floyd hawezi kumaliza hata round tano akizipiga na Canelo Alvarez.


View attachment 552855Santos Saul Alvarez(Canelo Alvarez)


View attachment 552856
Unbeaten man Floyd Mayweather.


Nikiwa kama shabiki nguli wa Floyd nasemaje Floyd ataendelea kuwa bora karne na karne hatotokea mtu wa kumkalisha dunia hii hata warudiane mara mia huyu dogo bado ataendelea kupokea kichapo tu.
 
Screenshot_2017-07-28-18-58-50_1.jpg
Unbeaten man Floyd Mayweather

Screenshot_2017-07-28-18-57-12_1.jpg
Canelo Alvarez


Screenshot_2017-06-30-02-08-18_1.jpg
Pacquiao
 
Tayari mipango ya chinichini ya kumshawishi.Floyd apande ulingoni ili achapane na Canelo imeshaanza kusukwa kwa kumuandalia donge nono ili kumshawishi Floyd akubali kuzipiga na Canelo
 
mkuu mimi ni mshabiki mkubwa sana wa pretty boy jinsi alivyo na mchezo mgumu na pia anajua kucheza na kila bondia kutokan na anavyo kuja na conor nina kuhakikishia hawezi hata kumgusa Floyd ambaye ana good target na good defense, lakini pia mm ni mshabiki mzuri wa canelo Alvarez kijana ameanza pro katika umri mdogo na ana improve day by day ila sitaki aje kupigana na maywether kipindi hiki may akiwa katika kipindi cha mwisho kabisa wa career yake lakini naamini hata kama wakipigana naamini kama canelo atakaza msuli atatoa dro ila sio kumpiga Floyd.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu mimi ni mshabiki mkubwa sana wa pretty boy jinsi alivyo na mchezo mgumu na pia anajua kucheza na kila bondia kutokan na anavyo kuja na conor nina kuhakikishia hawezi hata kumgusa Floyd ambaye ana good target na good defense, lakini pia mm ni mshabiki mzuri wa canelo Alvarez kijana ameanza pro katika umri mdogo na ana improve day by day ila sitaki aje kupigana na maywether kipindi hiki may akiwa katika kipindi cha mwisho kabisa wa career yake lakini naamini hata kama wakipigana naamini kama canelo atakaza msuli atatoa dro ila sio kumpiga Floyd.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sema ki Canelo nacho kipo vizuri.

Kingekaza kidogo nacho kingekuwa na rekodi sawa na Floyd .

We mtu amepambana mapambano 51 49 yote kashinda na kati ya hayo 34 ameshinda kwa K.O na ametoa sare pambano moja tu ,ni kitu kikubwa sana kwa kweli .

Ila kiukweli Floyd atabaki kuwa Unbeaten tu huyu kinsman hili pambano likikubaliwa atapigwa kwa mara nyingine tena.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom