Nakuunga mkono mimi nilipoteza siku 5 hapo. Wiki mbili zilizopita mzee wangu alikuwepo hapa mjini akilalalmika kuugua na akashauri twende Regency kwa sababu anazozijua yeye.
Tulifika mida ya saa tatu asbuhi, show ikaanza tukaelekezwa kwa dk yupo room namba 21 nurse wake anaitwa Ngeta kama sijakosea jina., hapo tulikaa sana hadi tunafanikiwa kumuona dk ilikua saa saba mchana. Akatuandikia vipimo vinne; Ultrasound, tezi dume, moyo na kingine nimekisahau jina ambacho unakojolea kipimo fulani.
Show ikaanza; siku hiyo tukaenda kwenye kipimo cha kukojolea, ambapo hadi tunahudumiwa ilikua saa kumi jioni, baada ya hapo tukaenda mionzi tukaambiwa mashine ni mbovu hivyo daktari akatuandikie form maalum ya kwenda kupata kipimo nje.
Tukaenda maabara kupima vipimo vingine vya Tezidume na moyo. Huko maabara tukaambiwa watapima tu tezi dume ila moyo hadi room namba 28 halafu tukaambiwa kipimo cha tezi dume majibu hadi baada ya masaa matatu.
Hapo siku ikawa imeisha tukarudi home.
DAY 2.
Tukawahi hospital kama kawaida, tukafikia maabara tukaambiwa majibu ya tezi dume ni hadi baada ya siku 5 tukaenda kuchukua barua kwa ajili ya kwenda kupata kipimo cha ultrasound tukakuta daktari yupo theater tumsubirie, hapo tukaambiwa kuhusu moyo inabidi tukamuone kwanza dk Khan room namba 5 kama sijakosea. Ikabidi tumngoje huyu wa barua ambaye hadi yule nurse alitusaidia kumfuata theater basi tukapewa barua tukaenda TMJ, kufika huko wakatugomea kuwa hakuna historogy ya mgonjwa dk wetu hajatuandikia😂😂😂😂😂 hiyo ni mchana tayari, tukarudi Regency tukaandikiwa na samahani nyingi tukarudi TMJ tukapiga ultrasound tukapata majibu baada ya 30mins. Siku ikaisha.
DAY 3
Tukaenda kuonana na dk wa kwanza kabusa kurudisha majibu akatutafsiria na kurecomend tiba husika.
Tukaenda kumuona dk Khan tukakuta ameenda ward round, aliporudi akatusikiliza na kutuandikia kipimo ambapo tukafanikiwa kupima siku hiyo na majibu tukapewa ila kurudisha majibu huyo dk alikua ameenda theater, siku ikaisha. Tukachukua dawa tulizoandikiwa na dk wa mwanzo tukaondoka.
DAY 4
Tukawahi, as usual tukahudumiwa na kupewa matibabu yanayostahili.
DAY 5.
Tukapewa majibu ya vipimo vya tezi dume na kupewa matibabu.
Hiyo ndio hali iliyonikuta hapo, sijui kama ilikua bahati yangu tu au lah