Reformation ni muhimu CWT

Reformation ni muhimu CWT

tatamajuva

Member
Joined
Sep 11, 2019
Posts
74
Reaction score
84
REFORMATION NI MUHIMU CWT

Wiki Jana 15 may 2020 kulikuwa na uchaguzi wa viongozi cwt ngazi ya wilaya shinyanga DC. Kwakweli CWT kimekuwa siyo chama cha kutetea maslahi ya walimu bali ni cha wachumia tumbo kutokana na mchakato wako ulivyoendeshwa. It's shame! Uchaguzi uliojaa rushwa, uchaguzi ambao uongozi uliokuwepo ulipanga nani awe kiongozi wa chama hicho, haiwezekani viongozi wa CWT waandae malazi ya wapiga kura, chakula, vinywaji for 2 days. Hivi unataraji tutapata viongozi wazuri katika chama hiki?

CWT shinyanga DC ni uozo mtupu, haijawahi kushuhudiwa hali hii, baada ya uchaguzi kuna kiongozi aligombea nafasi ya mkoa na kwa njia ileile aliyotumia alishinda lakini nafasi ya ngazi ya wilaya tayari aliandaliwa mtu ambaye kamati imekubaliana awe huyo headmaster wa shule fulani, je, tutafika?

CWT ni jipu linalosubiri kutumbuliwa, na mtumbuaji ni mkuu wa nchi.

CWT wanagawa T-shirt siku 10 baada ya sherehe za Mei Mosi? Hii syndicate ya baadhi ya watu, na kwa manufaa yao ya kulindana ili kuchumia tumbo.

Mwakilishi wa shule moja ya msingi aliandikiwa barua ya kutenguliwa kushiriki mkutano mkuu kwa kukosa sifa siku 1 kabla ya uchaguzi CWT Shy DC na hii ilitokana na mwakilishi huyu kuwa na msimamo thabiti alipoambiwa awasilishe salary slip 3 na barua iliyoandikwa kwake ni kupitia kwa mkuu wa shule ambapo ni kinyume na katiba, pia mkuu wa shule aliteua mwakilishi mwingine kinyume na katiba, hivyo uchaguzi kukiukwa kwa kiwango cha hali ya juu.

Mwakilishi huyo alirusha barua hiyo kwenye group fulani la WhatsApp na ndipo taarifa hii ilipothibitika na huu ni uonevu mkubwa, kwani anastahili kulipwa stahiki zake kama mwakilishi halali, pili mwakilishi aliyeteuliwa. Na mkuu wa shule alipiga kura kinyume na katiba inayotaka mwakilishi achaguliwe na wanachama katika kituo cha kazi.

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makato ya cwt ni makubwa mno wakati msaada wao kwa walimu ni mdogo sana.
Niliwahi kuunga mkono hoja ya makato ya walimu kukatwa na cwt yasitishwe. Nilileta hoja kwamba Walimu wakubaliane na vyama kwa hiari yao na si kukatwa bila ridhaa yao.
 
Mkuu samahani natoka nje ya mada kidogo

Hivi wale TTN au UMET walioanzishaga hoja ya walimu wasikatwe mishahara yao ya 2% na CWT wako wapi hivi sasa?

Mimi nadhani Tatizo ni kubwa kuliko wengi tunavyofikiri. Mara nyingi vyama vinavyoibuka na kuja na makato madogo huwa ni mapandikizi ya watu wachache na havina lengo la kumtetea mfanyakazi kwa sababu utetezi ni gharama sana. Kuchangia asilimia 1 au chini ya hapo ni hadaa ya vyama vya kitapeli.

Binafsi ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya vyama hivi ni kiwa mimi ni mwanachama wa THTU (UDSM), najua ili chama kitoe utetezi mwafaka lazima kiwe na waajiriwa ambao lazima walipwe maslahi yao kutokana na michango ya wanachama sasa huyo anayedai atakata 0.2% kimsingi hizo watakuwa wanatumia viongozi na kutofanya chochote.

Mfano kuna katika kupigania maslahi ya wafanyakazi kuna kamati ya utatu ambayo inajumuisha serikali, vyama vya wafanyakazi chini ya TUCTA na chama cha waajiri. Vyama vingi vinavyoibuka hivi sasa haviko TUCTA kwa hiyo havishiriki utetezi au kupigania maslahi, hayo wanapigania wengine vyenyewe vinanufaika na michango ya wafanyakazi wachache wasio na uelewa wa masuala haya.

Sasa inawezekana CWT wana makosa lakini mimi nadhani ni vema kutatua matatizo yaliyopo kuliko kuua CWT kumbuka atakayenufaika ni serkali na hapo tunakoleza suala la wagawe ili uwatawale (Divide and rule) na pia umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
 
Unasema mtumbuaji ni Mkuu wa Nchi...Nchi ipi hiyo unayoiongelea Mkuu au unamaanisha Tanzania, ambayo kila siku inahonga na kuwanunua wapinzani? na sasa tumeingia kuhonga hata viongozi wa Dini?

It seems you are NOT serious !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbinu zilizotumika kwenye uchaguzi CWT wilaya ya shinyanga vijijini ili viongozi walewale waendelee kuongoza na kuchumia tumbo ni kuwaandikia barua za kutengua uwakilishi sehemu za kazi kwa wawakilishi walioonekana wanakaidi/hawaungi mkono viongozi hao kwa kutengua uwakilishi wao mahala pa kazi,
Soma document hiyo hapo chini kwa uthibitisho zaidi
IMG-20200517-WA0003.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom