Refa ameruhusu timu zote ziingie Uwanjani, UVCCM na Wana CCM wote sasa ni muda wakuwa field kusimamia na kuelezea Serikali inavyotekeleza miradi

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,161
1,493
Kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameruhusu vyama vyote vya siasa vinaruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara, ruhusa hii inahusu Chama Tawala pia. Kwa namana yeyote ile vijana wa UVCCM na Wana CCM wote kwa ujumla ni muda sahihi ya kuingia field kuwaelezea Watanzania namna Serikali yao ya awamu ya sita chini ya Mh. Samia Suluhu Hassan inavyotekeleza miradi ya maendeleo na kutoa huduma nyingine muhimu kwa Jamii.

UVCCM, tumepata uongozi mpya hivi karibuni, ni Vijana wenye nguvu, ari na utashi mkubwa, tegemeeni vyama vya upinzani sasa agenda yao kubwa itakuwa ni kukosoa mambo yaliyofanywa na Serikali, hakutakuwa na agenda nyingine, maana ile kuu ya Katiba Mh. Rais amesema inafanyiwa kazi. Sasa vijana wa CCM nendeni kwa Watanzania mkawaambie ukweli kwa namna miradi in zipo, twendeni tukawaaambie Watanzania kwa miezi mitatu tu iliyopita Serikali yenu imejenga vyumba vya madarasa 8000 na ndio maana hakuna mtoto mwenye sifa za kwenda shule hataenda shule kwa sababu yeyote ile, Ilani ya CCM inataka watoto wote wapate elimu iliyo bora, tukaseemee utekelezaji wa ujenzi wa shule mpya kila mkoa, kila Wilaya, Kata na Vijiji, tukasemee utekelezaji wa ujenzi wa vituo vya Afya kuanzia hospital za Rufaa, Mikoa, Wilaya, Ujenzi wa Vituo vya Afya kwa kila kata, tukasemee ujenzi wa Zahanati kwa kila Kijiji, tukasemee upatikanaji wa vifaa tiba na dawa kwenye kila kituo cha kutolea huduma. Tukasemee upatikanaji wa huduma za maji, ujenzi wa barabara, mbolea za ruzuku etc.

Comrade Mohamed Ali Mohamed Kawaida na Comrade Kenani Kihongosi, Vijana wenu huko Wilayani wana Taarifa zote za utekelezaji wa Ilani ya Ccm 2020 - 2025, ni jukumu lao sasa kuwaelezea Watanzania utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao. Wataalamu wakuwapa taarifa sahihi wapo huko Halmashauri, wawatumie vizuri Maafisa Mipango wa Halmashauri ili kupata Taarifa za kujitosheleza pale inapotakiwa.

Inaweza isiwe rahisi saana, Wapinzani watataka kuaminika kwa Watanzania, lakini CCM ni chama bobevu, CCM itaendelea kuaminika kama kila Mwana CCM atatekeleza wajibu wake.

Mungu ibariki Tanzania.

Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
 
Kwani cha ajabu nini kwa CCM na hata kwa Wapinzani mikutano ilikuwepo miaka yote ya demokrasia ya vyama vingi kuanzia miaka ya 90, hiyo ndiyo value ya political pluralism. chawa wasifundishe watu kazi za siasa kwa pande zote mbili. Wacha mpira uchezwe Rais karuhusu wacha mhemuko.
 
Kwani cha ajabu nini kwa CCM na hata kwa Wapinzani mikutano ilikuwepo miaka yote ya demokrasia ya vyama vingi kuanzia miaka ya 90,hiyo ndiyo value ya political pluralism. chawa wasifundishe watu kazi za siasa kwa pande zote mbili. Wacha mpira uchezwe Rais karuhusu wacha panick.
Hakuna aliye panic dndagula kuwaambia UVCCM wakawaambie ukweli dhidi ya upotoshaji unaokuja wala sio kupanic, itakuwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yao. Yes wacha mpira uchezwe
 
Kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan ameruhusu vyama vyote vya siasa vinaruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara...
Kama wajenga hoja, watetezi wa hoja ndio kama wewe unayemwita mwenyekiti wa chama "refarii", basi tutegemee vihoja na viroja toka kwa CCM na UVCCM yake.
 
Kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameruhusu vyama vyote vya siasa vinaruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara, ruhusa hii inahusu Chama Tawala pia. Kwa namana yeyote ile vijana wa UVCCM na Wana CCM wote kwa ujumla ni muda sahihi ya kuingia field kuwaelezea Watanzania namna Serikali yao ya awamu ya sita chini ya Mh. Samia Suluhu Hassan inavyotekeleza miradi ya maendeleo na kutoa huduma nyingine muhimu kwa Jamii.

UVCCM, tumepata uongozi mpya hivi karibuni, ni Vijana wenye nguvu, ari na utashi mkubwa, tegemeeni vyama vya upinzani sasa agenda yao kubwa itakuwa ni kukosoa mambo yaliyofanywa na Serikali, hakutakuwa na agenda nyingine, maana ile kuu ya Katiba Mh. Rais amesema inafanyiwa kazi. Sasa vijana wa CCM nendeni kwa Watanzania mkawaambie ukweli kwa namna miradi in zipo, twendeni tukawaaambie Watanzania kwa miezi mitatu tu iliyopita Serikali yenu imejenga vyumba vya madarasa 8000 na ndio maana hakuna mtoto mwenye sifa za kwenda shule hataenda shule kwa sababu yeyote ile, Ilani ya CCM inataka watoto wote wapate elimu iliyo bora, tukaseemee utekelezaji wa ujenzi wa shule mpya kila mkoa, kila Wilaya, Kata na Vijiji, tukasemee utekelezaji wa ujenzi wa vituo vya Afya kuanzia hospital za Rufaa, Mikoa, Wilaya, Ujenzi wa Vituo vya Afya kwa kila kata, tukasemee ujenzi wa Zahanati kwa kila Kijiji, tukasemee upatikanaji wa vifaa tiba na dawa kwenye kila kituo cha kutolea huduma. Tukasemee upatikanaji wa huduma za maji, ujenzi wa barabara, mbolea za ruzuku etc.

Comrade Mohamed Ali Mohamed Kawaida na Comrade Kenani Kihongosi, Vijana wenu huko Wilayani wana Taarifa zote za utekelezaji wa Ilani ya Ccm 2020 - 2025, ni jukumu lao sasa kuwaelezea Watanzania utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao. Wataalamu wakuwapa taarifa sahihi wapo huko Halmashauri, wawatumie vizuri Maafisa Mipango wa Halmashauri ili kupata Taarifa za kujitosheleza pale inapotakiwa.

Inaweza isiwe rahisi saana, Wapinzani watataka kuaminika kwa Watanzania, lakini CCM ni chama bobevu, CCM itaendelea kuaminika kama kila Mwana CCM atatekeleza wajibu wake.

Mungu ibariki Tanzania.

Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Ikili za kisoda ...muda wote mlikuwa wapi akili zenu ziko mfukoni mwa Chadema
 
Kwa kuwa mnategemea Polisi na Usalama wa Taifa, bila hao, mapema asubuhi tu CCM hawapo.
Mkuu @eliasimisinzo hao wanatoka wapi tena? Si vyama vyote vimeruhusiwa vikaongee na Wananchi? Waende wakawaelezee Watanzania watawafanyia nini
 
Back
Top Bottom