Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 638
- 1,038
Habari zenu mabingwa wa mahekalu ya ghorofa, mabepari wa Instagram, na ma celebrity wa maokoto group,
Twende kazi……………!
Mmejenga nyumba za kupendeza hadi ukipita sakafu inafanya screenshot. Mmeseti vibanda vya mbwa vya kisasa kuliko bedroom ya bibi yangu kijijini matemanga. Mmeweka ring light hadi kabati linapiga pose. Ila Biblia iko pale juu ya friji, ikifuga vumbi na maneno ya uzima.
Yaani wardrobe yenu ina rangi zote za rainbow, lakini hamjui hata kama Warumi walikuwa watu au wimbo wa Aslay.
Kila siku mnachapisha…!
"Hustle hard, sleep later."
"Secure the bag."
"Catch flights not feelings."
Lakini hata mstari mmoja wa Zaburi 23 mnausoma kama ni bio ya mtu mwingine.
Sawa jamani, mafanikio ni baraka. Lakini sasa hadi Mungu anabisha hodi anasema …….
"Hodi? Au ndo nime unfollowiwa?"
Tusome kidogo Biblia (usipate pressure, hata app ni sawa)…..!
“Maana mwanadamu atafaidi nini akiupata ulimwengu wote, lakini akapoteza roho yake?” Marko 8:36
Wewe kila siku unapiga “manifesting mansion, manifesting Maldives”, lakini hujawahi manifest sala hata ya dakika mbili. Umejaa wishlists lakini huna prayer list.
Yesu alisema……!
“Tafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, na hayo mengine mtazidishiwa.” Mathayo 6:33
Lakini nyinyi mmepanga hivi……!
“Kuna wakati kwa kila jambo chini ya jua...” Mhubiri 3:1
Lakini pia kuna mwisho wa kila kitu. Hiyo deadline ya roho haina snooze button.
Basi ndugu zang kabla hujanunua Tesla ya kuonyesha kwa ex, nunua muda wa kukumbuka Muumba wako. Ukinunua iPhone 39 Pro Max Ultra AI Edition, pakua pia Bible App. Usisahau kupiga update ya kiroho.
Na mwisho kabisa, kama una t shirt 80 na jirani hana hata moja ya kujifunika, hiyo si fashion hiyo ni kufunga macho kwa maumivu ya binadamu.
“Yeyote mwenye kanzu mbili na amgawie asiye na yoyote.” Luka 3:11
Kwa hiyo kabla hujapost “2025 Goals, Soft life only”, tafadhali andika hii kwanza….!
“Goal #1: Kumbuka una roho.”
Wasalaam kwa upendo, hekima na kawarning ka upole,
Mtumishi asiye verified
~mwanenu Chavalikungu!

- Tafuta followers
- Tafuta Pesa au maokoto
- Tafuta Mwanaume au Mwanamke wa ndoto
- Halafu maybe Mungu akitokea, mpe Sunday 10:30 - 12:00 (kama hakuna EPL)