Redet: Kikwete soma alama za nyakati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Redet: Kikwete soma alama za nyakati

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mzambia, Jan 2, 2011.

 1. m

  mzambia JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Redet: JK soma alama za nyakati Send to a friend Friday, 31 December 2010 20:48 0diggsdigg

  Salim Said
  MWENYEKITI Mwenza wa Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (Redet), Dk Benson Bana, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kusoma alama za nyakati na kubeba ajenda ya katiba mpya ili kuweka vipaumbele vyake na kujijengea heshima baada ya kustaafu kwake.
  Akizungumza na Mwananchi kwa simu jijini Dar es Salaam jana, Dk Bana alimtaka Rais Kikwete kuwapa Watanzania salamu bora za mwaka mpya kwa kuwaahidi katiba mpya kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji mwaka 2014.

  “Kama napata fursa ya kukutana na rais leo (jana), kabla hajaanza kuwahutubia Watanzania, ningemshauri na kumuomba kabisa asome alama za nyakati, ni aibu ajenda ya katiba mpya kuongozwa na wapinzani, wanaharakati na watu wengine wakati serikali ipo,” alisema Dk Bana na kuongeza:
  “Mifano ipo ya kutosha, wenzetu wa Kenya na Uganda wameachana kabisa na katiba hizi za watu waliojifungia vyumbani na kutunga katiba bila ya kushirikisha jamii husika.”

  Dk Bana anaungana na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Jaji Omar Makungu, Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mawaziri wakuu wa zamani, Joseph Warioba na Frederick Sumaye na Jaji Mkuu mstaafu Augostino Ramadhan kuunga mkono hoja ya kuundwa katiba mpya.

  Madai ya Katiba mpya, pia yamewahi kutolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, ambaye alisema bayana kuwa katiba mpya iandikwe mapema kabla ya mambo kuharibika.
  Dk Bana anapingana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, aliyetaka katiba iliyopo iwekewe viraka.

  “Suala la katiba mpya halitaki mjadala mrefu na wala sio la kuweka viraka, haya tumeweka viraka halafu iweje? Itasaidia nini? Hivyo viraka tumeweka mpaka tumechoka, lakini hakuna mabadiliko matatizo yanaendelea kuzidi,” Dk Bana alipinga vikali kauli ya Jaji Werema.

  Alisema katiba mpya ni msingi kwa Tanzania ya sasa na kwamba, serikali haipaswi kupata kigugumizi katika kuchukua ajenda hiyo ya kuanzisha mchakato wa kuipata haraka.
  Dk Bana ambaye pia ni Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema katiba iliyopo haijibu maswali ya msingi ya Watanzania kuhusu mustakbali.

  “Katiba ndio msingi wa taifa kwa kila kitu, hivyo pamoja na mambo mengine, lazima ijibu maswali ya msingi ya Watanzania, mambo ya Tume huru ya uchaguzi, nguvu ya rais, viongozi wa umma wawajibike kwa nani, katiba lazima iweke wazi mambo haya mazito,” alisema Dk Bana.

  Alifafanua kuwa, katiba mpya lazima iwe na fikra na mawazo shirikishi sio suala la mtu au kikundi cha watu kujifungia ofisini na kuandika katiba kwa niaba ya Watanzania.
  Madai ya katiba mpya yalizidi kupamba moto baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010 ambapo Rais Kikwete alitangazwa mshindi kupitia CCM.

  Pia, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, tayari amewasilisha hoja binafsi ofisi za Bunge ili iweze kujadiliwa katika kikao kijacho cha bunge na CUF wamewasilisha mapendekezo yao ya katiba mpya kwa Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani.
  SOURCE: MWANANCHI DEC31
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kusije kukawa na tume kama ile ya EPA yenye maslahi maalum kwa anayeiunda!
   
 4. m

  mams JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2011
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Bana, hapa kidogo kaongea.
   
Loading...