Recruiters agences: Serikali simamia hili

Recruiters agences: Serikali simamia hili

Miwatamu

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2012
Posts
1,450
Reaction score
492
Kwa kiasi fulani uwepo wa makampuni haya haukatazwi ila kinachotokea ni kwamba serikali imewaacha huru mno na kunesha kama vile watu wanaopata ajira kupitia kampuni hizo serikali haihusiki nao kwa lolote! Nao kwa kutumia mwanya huo wa upofu wa serikali ndio maana wanafanya wanachokifanya ikiwa ni pamoja na kutolipa kodi ya mishahara {pay as u ean} kwa kuwa wao wamesajiliwa kama COMPANY LMT!

Kwa maana nyingine wao wanalipia kodi ya kampuni na si kodi itokanayo na mshahara wa mfanyakazi. Lakini kitu kingine ni danadana zinazotokea kwa mwajiriwa hasa wakati wa kuhitaji kusoma au akipatwa na matatizo ya kifamilia na kushindwa kuelewa yeye anamilikiwa na nani?

Mara utaambiwa na kampuni unayofanyia kazi kwamba mimi sikutambui kwakuwa sio mwajiri wako! na ukirudi kwa aliyekusainisha mkataba atakwambia kuwa kazi yangu ni kukutafutia kazi tu! Hayo matatizo yako mwambie unayemfanyia kazi.

Sasa katika hali hii hawa watu wamesimama wapi na sheria ya kazi inasemaje??!! Najua ninawachosha! Sasa naomba serikali ifanye hivi. Haya makampuni yaendelee kuwepo na yaendelee kuwatafutia ajira watu, ila pindi wawapatiapo ajira hiyo wasiwamiliki zaidi ya miezi 6 tu. {yaani mtu anapokuwa under probation}na baada ya hapo mtu amilikiwe na kampuni anayofanyia kazi.

TAFAKARINI SANA KWANI VIJANA WENU WANATUMIKISHWA KAMA MANAMBA.
 
mkuu jifunze kutumia Aya katika Uandishi.Ni watu wachache sana wenye kuweza kusoma habari hii waimalize.
 
Erolink spanco na wengineyo ni janga la taifa Nasubiri utekrlezaji wa hili suala kwa hamu....
 
Kweli serikali inatakiwa kuonesha kama kweli inameno au iko mifukoni kwa watu vijana wameteseka sana tunasubili utekelezaji Wa hili tuone
 
Sikuelewa unachoongelea ni kama tunalijua wote hebu edit kwanza ueleweke,
 
Back
Top Bottom