Rebeca Gyumi anastahili recognition

chuchunge

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2007
Posts
225
Reaction score
174
Rebeca ni mwanamke wa kitanzania na mwenye umri mdogo kulinganisha na mambo aliyoyafanya kwa ustawi wa wasichana wa tanzania kupitia shitika lake la msichana initiatives.

Aliweza kuchallenge serikali kipengele cha ndoa kwa msichana katika umri wa miaka 15, amepata UN awards usiku huu na amekua akipata other awards kutoka mashirika na mabalozi mbalimbali.

Kinachonishangaza hakuna siku Rais amerecognise efforts zake na kumpongeza hata waziri wa wizara husika!!!

Something is wrong somewhere!
 
Sasa ana challenge nini? Anaona heri kuzaa za nje halafu kujaza watoto wa mitaani kuliko kuolewa?

Unajuwa Tanzania jinsi watoto wa mitaani walivyojaa mpaka tumechukuwa kombe la dunia la watoto wa mitaani. Halafu tunashangilia! Ajiiib.
 
Hatumtambui kwasababu anaandaliwa kutumika na watetea ushoga.
 
Tukisha m' recognise wananchi inatosha.....rais yuko bize na kuua demokrasia na uchumi wa Nchi yake pendwa.......acha amalize kwanza huo mkakati wake then mengine yatafata
 
Sasa ana challenge nini? Anaona heri kuzaa za nje halafu kujaza watoto wa mitaani kuliko kuolewa?

Unajuwa Tanzania jinsi watoto wa mitaani walivyojaa mpaka tumechukuwa kombe la dunia la watoto wa mitaani. Halafu tunashangilia! Ajiiib.

Mtazamo wako umenishangaza sana. Kwa hiyo mtoto kuolewa akiwa na umri wa miaka kumi na mitano ndio suluhu la tatizo la watoto wa mitaani?!! Unadhani kweli watoto wa mitaani wengi wao ni kwakuwa mama zao wamenyimwa kuolewa wakiwa wadogo?

Tatizo la tabia au hulka hurekebishwa kwanza kiakili au kimtazamo, kisha au/na wakati huohuo kuhakikisha mazingira rafiki kwa mtoto wakike na wakiume.
 
Natambua mchango wako Rebecca, Hongera sana na uendelee hivo hivo!!
 
You have said it all!Kudos!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…