Real Madrid waliuza Punda wakanunua Farasi enzi za mwanzo kabisa wa GALACTICOS

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Warren buffet ambaye ni mmoja wa matajiri ambao wamedumu katika tano bora ya matajiri dunia katika kipindi cha miaka kumi na tano, aliwahi kusema “siku zote ukinunua usicho kiihitaji utapoteza chenye thamani kwako”aliongea hivyo wakati akiwapa nasaha vijana huko Marekani.

Mwanzoni mwa miaka ya 2000 wakati rais wa Real Madrid Florentino Perez Rodriguez anaingia pale madarakani Madrid alikuja kutimiza agenda yake ya uchaguzi ya kusajili wachezaji wenye majina na viwango vikubwa “Galacticos”

Akianza na kumsajili Luis Figo kutoka mahasimu wao wakuu Barcelona mwaka 2000,

2001 alivunja rekodi ya dunia kwa kumsajili Zinedine Zidane kutoka Juventus kwa ada ya euro million 77.5,

2002 akafuata Ronaldo de Lima, 2003 David Beckham kutoka Manchester united, 2004 Michael Owen kutoka Liverpool na 2005 Mbrazil Robinho.

Mwanzoni sera hii ya Galacticos ilifanya kazi na kuisadia Madrid kushinda mataji ya Hispania na ulaya chini ya kocha Vinte del Bosque.

Ubora huo ulifanya mpaka kocha Del Bosque kuja na kauli kuwa kitu pekee Barcelona walichokuwa wakisheherekea ni siku ya kuzaliwa kwa klabu yao tu kipindi yeye akiwa kocha wa Madrid.

Baada ya kusajiliwa kwa Beckham Real Madrid walimuuza kiungo mwenye mapafu ya mbwa mfaransa Claudie Makelele kama sehemu ya kupunguza gharama za uendeshaji.

Makele alitimkia Chelsea chini ya Jose Mourinho msimu wa 2003/2004. baadae Del Bosque aliondoka Blancos likafuata anguko la Real madrid yenye mastaa,

2004 Real Madrid walimaliza la liga wakiwa nafasi ya 4 na walishindwa kufanya vizuri UCL kuanzia 2003-2007

27/02/2006 Florentino Perez alijiuzuru wadhifa wake kabla ya kurejea tena mwaka 2009

Usajili wa Bechkam ulikuwa ni kulipaka gari la Rolls Royce dhahabu na kumuuza Makelele ilikuwa kama kuondoa injini kwenye gari.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom