Real Madrid VS Barcelona- toka Santiago Bernabeu

Real Madrid VS Barcelona- toka Santiago Bernabeu

SG8

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2009
Posts
3,955
Reaction score
2,135
Leo tena!!!! Wababe wawili wa Ligi Kuu nchi Hispania wanakutana tena katika mechi ya Marudiano ya La Liga ikiwa ni siku chache tangu Real Madrid walipoifunga Barcelona magoli 3-1 kwenye nusu fainali ya Kombe la Mfalme.

Mechi ya leo itazikutanisha timu hizi wakati Barca ikiwa juu ya Real Madrid kwa pointi 16. Aidha Barca itaingia uwanjani bila kiungo wake tegemeo Xavi huku Real Madrid ikitarajiwa kuwapumzisha nyota wake wengi ili kujiandaa na mechi ya marudiano ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Manchester United mapema wiki ijayo. Huenda Christiano Ronaldo, Mesut Ozil, Xabi Alonso, Angel Di Maria na Sergio Ramos wakapumzishwa ili kujiandaa na mechi kali itakayopigwa kwenye uwanja wa Old trafford
 
Full time Los Blancos 2 Barcelona 1! Hala Madrid..
 
Back
Top Bottom