Moja ya makosa makubwa tunayoyafanya miaka nenda rudi ni kwenye uchaguzi wa makocha.
Ancelloti alikuwa kocha mzuri lakini amepitwa na wakati na hilo lilionekana tangu awamu yake ya kwanza na kwenye timu alizoenda kufundisha baada ya pale. Timu anazofundisha zinakuwa si mbaya lakini pia si nzuri sana.
Same kwa Zidane ingawa alichukua makombe mengi ila bahati ilikuwa upande wake kwa kiwango kikubwa, mpira tuliokuwa tunacheza ni wa kawaida tu huyu me nilifurahi kuondoka kwake.
Mourinho alijitahidi sana misimu yake miwili ya mwanzo shida ni kwamba Barca nao walikuwa vizuri kutuzidi ila ndio kocha alierudisha nidhamu na morali ya kushindana. Ni bahati mbaya akavuruga timu aliyotumia nguvu kubwa kuijenga, nae kwa sasa ni kama Ancelloti tu.
Lopetegui na Benitezi wamefeli kabla ya kuanza.
Liverpool walikuwa na tatizo kama letu kila siku wanabadilisha waalimu ila walipompata kocha anaeendana na mpira wa kisasa wametulia. Tuchel pia unaona timu alivyoigeuza. Timu inayofanya homework kwenye uchaguzi wa makocha ni Bayern Munich hawa jamaa ni mara chache wanakuwa na makocha wabovu. Hata Ajax unaona wanavyoelewana na walivyo wagumu kucheza nao.
Ni wakati sasa Perez akune kichwa alete kocha ambae atafanya wachezaji kuhangaika sana uwanjani na kuogopeka na wapinzani endapo huyu wa sasa hatoleta matokeo chanya mwishoni mwa msimu.