Tissaphernes
JF-Expert Member
- Mar 27, 2018
- 2,902
- 3,566
Ni mpumbavu pekee ndie atakayeamini kuwa Salah atamsunbua Marcelo, ni Messi pekee ndie anayeweza kumsumbua jamaa tena wakiwa face to face.Nimeangalia na nimesoma wachambuzi wengi wana point upande wa Marcelo kama ndio unapitika zaidi, kisa ni kwamba jamaa anapanda sana kufanya mashambulizi huku akiacha gap kubwa upande wake, lakini ninachokijua ni kuwa Marcelo hajawahi kubadili style yake ya uchezaji na bado hilo gap wapinzani wameshindwa kulitumia, sasa ngoja tuone hiyo kesho itakuwaje,..., [HASHTAG]#HalaMadrid[/HASHTAG].., [HASHTAG]#AporLa13[/HASHTAG]!!
Live streaming mwenye link atupie mpira ukianza
Nipo kutztown pennsylvania hapa states, hapa ningekuwa na muda ningeenda golazo pub betrehem ndo kuna shangwe la soka but nipo job mpaka saa 11 jioni ya huku
There you are again!Kila mmoja atatarajia mashambulizi makali zaid kutoka Liverpool wakati wa fainali la klabu bingwa Ulaya lakini kile hatufahamu ni jinsi Real Madri itakabiliana na hali hiyo.
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp hana nia ya kubadilsha mbinu za kikosi chake cha 4-3-3 kwenye mechi ya leo Jumamosi na kama kutakuwepo na majeraha inamaanisha kuwa hatakuwa na mbinu tofauti pia wa wachezaji.
Kwa upande mwingine meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane ana maauzi makubwa ya kufanya kuhusu ni yupi anayamweka kwenye kikosi cha mechi ya Kiev.
Zidane amekuwa na nyakati msimu huu ambapo kikosi chake kimekuwa na wakati mgumu hasa Ulaya lakini licha ya hilo amefanikiwa.
Ameifikisha Real fainali sio kwa kuangazia pande moja lakini kwa kuwasoma sana wapinzani.
Kwa kufanya hilo na kubadilisha jinsi Real wanacheza kutokana na ni nani wanacheza naye, ameonyesha kuwa sio kocha anayetuma kikosi chake na kukiambia kucheza vile wanacheza licha ya wachezaji wazuri alio nao.
Real lazima iwakabili vilivyo washambuliaji watatu wa Liverpool
Moja ya vita vikali zaid vitakuwa kutoka Mohamed Salah ambaye ni mshambuliaji hatari zaidi duniani dhidi ya mlinzi wa Real Mbrazil Marcelo.
Marcelo ni muhimu sana kwa Real lakini kumwezesha kucheza vizuri zaidi bila ya kuiacha safu ya ulinzi na hatarai kutoka Liverpol ni jamboa litasababisha Zinade kuamua mfumo ambao atautumia.
Amekuwa mwangalifu akicheza na timu ambayo hucheza kwa kushambulia kwa ghafla kama Liverpool na huenda akaitumia mbinu sawa na hiyo.
Zinade pia huenda akafikiria kuwa ikiwa Marcelo atacheza mbele ataupa upande wake ulinzi zaidi akisaidiana na safu ya kati kama Mateo Kovacic na katika mfumo wa 4-4-2 sawa na alivyofanya wakati wa duru ya pili ya ushindi wake dhidi ya PSG.